I WILL BE BACK SEHEMU YA 12 | BongoLife

I WILL BE BACK SEHEMU YA 12

I WILL BE BACK 12

Ilipoishia.

Sikutaka kuamini kama kweli mtu niliyemuona amesimama mbele yangu baada ya mimi kugeuka nyuma alikua ni.  
         
Songa nayo.
                 
Alikua ni Slyvester mdogo wake na yule rafiki yangu James niliyekutana nae pale Canning airport jijini Beijing nchini China siku nilipokua nikiianza ile safari yangu ndefu ya kurejea nyumbani nchini Tanzania baada tu ya kuhitimu masomo nchini humo.
Nilipigwa na butwaa, sikutaka kuamini kama Slyvester niliyesafiri nae kwa ndege moja kutoka nchini China na kutengana nchini Kenya alipomaliza yake na kuniacha mimi nikiendelea na safari mpaka nyumbani nchini Tanzania ndiye aliyekuwa ameniita na kusimama mbele yangu huku akionyesha tabasamu lililofukuza hofu kubwa niliyokua nayo.

“Oh Slyvester, I never thought to see you here.” (Oh Slyvester, sikutegemea kukuona hapa) nilimwambia huku nikimpa mkono kumsalimu, kwa kiasi fulani hofu ilipungua.

“Mr. Davis I knew you will be here today and that why I’m here”(nilifahamu utakuepo hapa leo ndio maana nipo hapa)

Kauli ya Slyvester kua alifahamu nitakuwepo hapo siku hiyo ilizidi kunichangaya, maswali mfululizo yalikosa majibu yalizalijazana kichwani mwangu, ilikua kama picha la kihindi steringi kufa kwenye maua, nilishindwa kupambanua kipi ni kipi, uvumilivu ulinishinda kama nisingesema neno basi ningekufa kwa mzigo wa sintofahamu niliokua nimeubeba. 

“Who told you?”(nani aliyekuambia)

“No time for stupid questions”(hakuna muda wa maswali ya kipumbavu) 

Joel aliingilia kati, alinizuia kuuliza maswali huku akisalimiana Slyvester. Kumbe wote walikua wanafahamiana maongezi yao mafupi na kuulizana habari za siku mbili tatu vilikua ushahidi tosha kua walikua ni marafiki wa muda mrefu.

Muda wa kuingia kwenye ile nyumba ya maajabu ulifika, sikuona mlango wala dirisha hata moja lakini uwepo wa Joel na Sylvester ulimanisha ni lazima tungeingia ndani. Tulipofika karibu kabisa na ukuta Slyvester alitoa kitu kama rimoti akabofya kitufe ghafla ukuta ukajitenga katikati, tukakutana na geti kubwa la chuma lililokua na maneno FBI katikati.                                            
Ni kama nilikua nje dunia nyingine kumbe nilikua tu jirani nchini Kenya, kila kitu kilichokua kikifanyika hapo kilikua kigeni kwangu vichache sana ndivyo nilivyo bahatika kuviona kwenye filamu za kijasusi.            
                   
Getini Slyvester alibofya tena kitufe kingine ghafla mwanga mdogo wa kijani ukammulika usoni, kompyuta ndogo pembeni ya geti ika u scan uso wake kama nusu dakika kisha geti likafunguka lenyewe tulivyoingia likajifunga.   
 Mle ndani nilikaguliwa peke yangu na kifaa maalumu kuona kama nilikua na silaha au device yoyote tofauti na simu, Joel na Slyvester walinisubiri pembeni. 
Begi langu pia lilikaguliwa baada ya kua salama niliruhusiwa kuingia mlango unaofuata. Kama kawaida niliongozana na wenyeji wangu Joel na Sylvester.         
        
 Sikuamini nilichokiona ndugu zangu acheni tu Marekani iitawale dunia. Ilikua mara yangu ya kwanza kuingia kituo cha FBI ambacho asili na makao makuu yake yapo nchini Marekani. Vituo hivyo nje ya nchi ya Marekani huwa vichache sana tena vinawekwa kwa siri kubwa hasa kama kuna shughuli ya kumtafuta mhalifu mkubwa ama virus kama wanavyopenda kuita wao.

Ndani ya kituo hicho nilikutana na kompyuta aina zote ambazo sikuwahi kuziona kabla, nyingi zilikua kubwa na nyingine zilikua kama vioo vya kunyolea saluni zilikua ni za kupangusa tu hazikua na kitufe chochote cha kuingizia data. Kamera za cctv zilizagaa kila kona ya ukuta, tv kubwa zilizounganishwa na programu za kompyuta (smart tv) zilining'inia ukutani, aina zote za simu unazozijua wewe zilikuwepo mezani, drones, projekta, kila kitu kilikuwepo humo ndani.
Nje ilikua nyumba ya maajabu lakini ndani palikua pasafi kupita maelezo, palikua pazuri kila kitu kilipangaliwa vizuri mahala pake.   
                                                                                                    Kiukweli niliduwaa, wakati nikiwa katika kushangaa ili nipate kitu cha kuja ku kuwatambia watu ghafla nilishangaa kumuona yule rafiki yangu James niliyemuacha kule nchini China pamoja na mpenzi wake na Joel ambaye muda wote huo nilijua yupo sun rise hotel chini Tanzania anasubiri kwenda kutalii. Wote walisimama mbele yangu huku wakiwa wamevalia bullet proof nyeusi zilizokua na maneno FBI mbele na nyuma. 
Kichwa kiliwaka moto sikuelewa kitu gani kilikua kinaendelea, safari hii ule mzigo wa sintofahamu ulikua unaniua sababu ulizalisha maswali mfululizo yasiyokua na majibu, kama isingekua Joel kuniwahi basi ningepoteza fahamu kama sio kufa kabisa kwa kuchanganyikiwa.

Joel alisogea katikati yao na kuanza kuniambia kua alikua amekuja nchini Tanzania kumkamata yule mwanaharamu Motemapembe ambae jina lake halisi ni Abrahamu Odhiambo na hakua amemuua baba yake kama alivyoniambia awali bali alikua ni kiongozi mkubwa wa kikundi cha M23 na alikua anahusika na mauaji ya wamarekani 57, 40 walikua wanafunzi huku 17 walikua ni madaktari wa shirika la msalaba mwekundu waliojitolea kwenda kufanya huduma za kitabibu nchini Kongo miaka mitano iliyopita.     

Hakuna asiyeijua nchi ya Marekani, achana na wema wake wa kutoa misaada na kuzikopesha nchi masikini za Afrika, achana na uzuri wa nchi hio na ukubwa wa teknolojia iliyosambaa kila mahali nchi nzima. Lilipokuja suala lolote kuhusu raia wake Marekani haikua na masihara hata kidogo, haikujali idadi, sura, rangi, kabila la raia husika, wala muda wa tukio kufanyika walichojali ni mtu huyo kua raia wa Marekani, hicho ndicho walichokithamini. Ilikua rahisi kwa Marekani kutuma ndege za kivita, vifaru na wanajeshi ili kumuokoa hata raia mmoja ambae alikua mikononi mwa adui, mfano mzuri ilivokua kwa Marcus Luttrell mwanajeshi wa operation of red wings, mlioiona movie ya Lone survivor mtakua mashahidi wa hili, helicopter mbili, ndege ya kutupa makombora, pamoja na wanajeshi karibu 15, walienda kumuokoa Marcus Luttrell, mnusurika pekee katika mission hiyo ya red wings iliyotokea mwaka 2007, katika milima ya Taliban. 
Hivyo ilikua ni lazima Abraham Odhiambo maarufu kama Motemapembe akamatwe, akiwa hai au amekufa.
Nilibaki nimeduwaa, nilimuonea sana huruma mke wangu Tressy nilijua maovu aliloyoyafanya Motemapembe ni lazima yangemtia matatani.

Joel aliendelea kuniambia, maelezo yake yalizidi kunishangaza hasa pale aliponiambia kua yule mwanamke mzungu mbele yangu hakua mpenzi wake bali alikua ni mfanyakazi mwenzake wa FBI yeye ndiye aliyetukatia tiketi ya ndege kisha akaondoka jana yake usiku hadi ule muda niliomrudisha Joel hotelini yeye hakuepo nchini Tanzania pia Joel aliniambia muda mfupi ujao nitafahamu sehemu alipoyatoa majina yangu yote matatu.
Kama maji ya mto Joel alizidi kutiririka kuwa James nae hakua mfanyabiashara kama nilivyoamini kua alikua mteja wangu mzuri. Alikua ni mpelelezi wa FBI alikuja nchini Tanzania akitokea Kongo kutafuta na kupeleleza habari za Abraham Odhiambo pia akaniambia siku ile nilipomuacha nchini China yeye alikuja kesho yake na vifaa vitakavyotumika katika ile mission.           
        
Mwisho ya Joel alimaliza kuniambia Slyvester nae hakua mdogo wake na James kama nilivyodhani bali alikua mtaalamu wa kompyuta na mawasilano FBI na siku ile aliposhuka nchini Kenya alienda moja kwa moja pale kituoni kuhakikisha mambo ya mawasiliano yanakua sawa.
Maelezo Joel yaliniacha mdomo wazi, niligundua kumbe siku ile kwenye ndege yule mwanamke wa kizungu hakua amelala alikua macho akiyasikiliza maongezi yetu yote. Mbembwe zote za kuigiza usingizi na kukoroma kumbe alikua ananichora, jamani narudia tena kwa kweli acheni tu Marekani waitawale dunia. 

  “So why I’m included in this mission?”(kwanini nahusishwa katika hii mission) nilimuuliza Joel baada ya kumaliza kunielezea.

“Worry out very soon you will know everything”(ondoa shaka muda si mrefu utafahamu kila kitu)

…..ITAENDELEA….

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,156,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,13,biashara mtandaoni,3,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,209,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,118,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,229,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : I WILL BE BACK SEHEMU YA 12
I WILL BE BACK SEHEMU YA 12
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/i-will-be-back-sehemu-ya-12.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/i-will-be-back-sehemu-ya-12.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content