I WILL BE BACK SEHEMU YA 11

I WILL BE BACK 11

Joel aligeuka nyuma na kunipigia saluti kisha akaendelea na safari yake fupi kurudi hotelini. Nilimuangalia kwa makini mpaka alipoingia mlangoni ndipo niliwasha gari kurudi Mbezi beach nyumbani kwa Mzee Ambrosi yalipokuepo makazi yangu ya muda. 
Joel alikua kijana wa makamo lakini mwenye akili sana muda mfupi niliofahamiana nae niligundua kua alikua ni mtu mwenye umakini mkubwa asiye na masihara hata kidogo.                         
                                                                                                        Imani aliyoionyesha juu yangu ilinipa hali fulani ya kujiamini, bila shaka kuna kitu fulani alikiona kwangu ndio maana akaniamini mapema kitu kilichonizidishia hali ya kujiamini zaidi.

Barabarani niliendesha gari kama mwehu, saluti ya Joel ilifanya nijione steringi dakika kumi na tano zilitosha kunifikisha kwa Mzee Ambrosi. Nilipiga hodi haikupita muda niifunguliwa geti maongezi machache yalifuata kisha tukaenda kulala.
Niliamka asubuhi mapema sana ilikua karibu saa kumi na moja afrajili. Nilioga kisha nikaandaa nguo chache za kubeba kwenye ile safari ya kwenda nchini Kenya. Nilivuta subira kidogo jua lilipoanza kuchomoza nilimgongea mlango Mzee Ambrosi nilimdanganya nimepata simu ya dharura hivyo naenda nyumbani Morogoro kuwasalimu wazee pamoja na ndugu zangu nilijua wazi kama ningesema ukweli lazima angenizuia kuhofia usalama wangu. Wazazi ni Mungu wa pili duniani, unaanzae kumzuia mtu kwenda kuwatazama?, Mzee Ambosi hakua na jinsi zaidi ya kupokea taarifa na kukubali.

“Nashukuru sana” nilimwambia.

“Usijali ngoja nikusindikize” alinijibu.

 “Hapana hapana nitafika”

Nilikataa katakata Mzee Ambrosi kunisindikiza maana ingemrahisishia kugundua kua nimemdanganya jambo ambalo lingefanya aache kuniamini kama sio kujisikia vibaya. 
Niilichukua usafiri wa tax mpaka sun rise hotelini. Nilimpigia Joel simu ndani ya dakika moja alitoka na kila kitu kasoro mpenzi wake.

“Let’s go”(twende) aliniambia bila hata salamu.

Tulitumia lile lile tax kuelekea airport. Muda wote huo nilijiuliza kuhusu mpenzi wake nilitamani kujua uongo alioutumia mpaka kufanikiwa kuondoka lakini hata ningemuuliza ningeambulia jibu lile lile marehemu baba yangu ni bora kuliko yeye, ilinibidi niwe mpole.          
                                  
“Take your ticket”(chukua tiketi yako) Joel aliuvunja ukimya mdogo uliokua umetawala na kunikabidhi tiketi ya ndege ya shirika la Fly Emirates iliyokua inaenda Dubai kupitia Kenya.

Tiketi ilikua na majina yangu kamili pamoja na jina la katikati na yote yalikua sahihi jambo hili lilinishangaza sana. Nilijaribu kukumbuka lakini wapi kichwa kiligoma hata siku moja sikua nimewahi kumtajia Joel majina yangu yote. Nani aliyekata zile tiketi ikiwa tu hata mpenzi wake hakujua kuhusu ile safari yetu lilikua swali lingine zito lililonimaliza nguvu. Au labda aliliona facebook? Nilijiuliza lakini hapana facebook nilitumia majina mawili tu hili la katikati kalitoa wapi maana ndilo lililokuwepo kwenye passport yangu na hakuwahi kuishika hata mara moja.
Niliamua kukata kiu ya kutaka kufahamu majibu ya yale maswali yangu yote, uvumilivu ulinishinda nilimuuliza lakini hata kabla sijamaliza sentesi alinikatisha.

“Davis I know you more than you think”(Davis nakufahamu zaidi ya unavyofikiria) 

Hata angekua Francis Cheka angeshtuka sembuse mimi mifupa ya njiwa. Nilishtuka sana kwa mara nyingine tena niliamini kua Joel hakua binadamu wa kawaida, ilinibidi niwe mpole sikutaka hata kujua ananifahamu vipi maana kama ningejua huenda ningehairisha hata safari yenyewe.
Airport tulikaguliwa mizigo tulipanda ndani ya ndege bila kuchelewa magurudumu yakaiacha ardhi ya Tanzania safari ya kwenda nchini Kenya ikaanza. Muda wote wa safari hofu kubwa ilinijaa kama mpagani imani iilinishuka nikashindwa kuamini kweli Joel ni rafiki au adui. Nilimtazama Joel lakini alionekana hana habari uso wake ulikua kawaida ulionyesha tabasamu hafifu. Pengine anafurahia kuninasa katika mtego wake mmh lakini hapana, nilikua kama chizi nilijiuliza maswali nilijipa majibu na kuyakataa mwenyewe.   
                                     
Kama alivyowahi kusema Pablo Escober muuza madawa ya kulevya maarufu kuwahi kutokea katika uso wa dunia jamaa alikua na pesa na kila kitu kuna siku binti yake mdogo alikua anasikia baridi Pablo alichoma noti usiku kucha ili binti yake aote moto karibu bilioni mbili ziliteketea usiku huo mmoja acha mabilioni mengine yaliyoliwa na panya kila siku (tafuta series inaitwa Narcos inaelezea kisa chote cha huyu jamaa). Wakati anatafutwa na serikali yake ya Kolombia kwa msaada mkubwa wa serikali ya Marekani Pablo alisema ni heri kua kaburini Kolombia kuliko kua jela Marekani.
 Kwangu pia Tanzania ilikua ni kama kua jela Marekani na Kenya ilikua ni kama kua kaburini Kolombia. Nilikata kauli kama Davis ni mtu mbaya ni bora nife kishujaa nchini Kenya (Kolombia kaburini) kuliko kuishi kitumwa hapa Tanzania (Jela Marekani) kulala kwenye chumba cha kupewa na kumuona yule mwanaharamu akimsosomola mke wangu kipenzi na mali zangu huku mimi nikiishia kukumbatia mito usiku kucha. 

Tulitua salama jijini Nairobi abiria wote tulishuka pamoja na mizigo yetu. Ilikua saa nne kuelekea saa tano usiku. Kama isingekua taa za kisasa basi pale uwanjani pangejaa giza tupu kiasi cha watu kushindwa kuonana hata sura.                                                      
Baada ya kutua macho na kila kitu changu kilikua kwa Joel nilitazama kila kitu alichokifanya. Muda huu Joel hakua muongeaji sana kama kule Tanzania. Tuliposhuka tu tulichua tax safari Joel alionekana kua mwenyeji kuliko mimi, alitoa maelekezo dereva alitupeleka nje ya mji hapo tena hofu yangu ikazidi kuongezeka kila nikiangalia ukimya wa Joel na umbali tulioutumia kwenda alipotoa maelekezo nilipata jibu moja kua I’m fucked up.

Tulifika mpaka mahali penye msitu mnene miti ilikua mingi kuliko idadi ya taa zilizowaka na kutoa mwanga kwa mbali. Dereva tax aliondoka na sisi tukaanza kuingia katikati ya msitu huo. Wasiwasi ulinijaa zaidi. Ghafla hata kabla sijapiga hatua tatu mbele Joel alinisimamisha bila kunisemesha neno alinifunga kitambaa cheusi usoni ukijumlisha na lile giza ni kama nilikua kuzimu nikisubiri kupigwa makofi na shetani. Nilivaa begi langu mgongoni, kama mtoto mdogo Joel akanishika mkono kisha safari ya kuingia msituni ikaanza.Tulitembea karibu nusu saa na zaidi, njia nzima ilijaa milima na mabonde mpaka tulipofika. Joel alinifungua kitambaa, tulikua tumesimama mbele ya nyumba ya ajabu niliona tu taa zikiwaka lakini sikuona dirisha wala mlango hata mmoja, Nilitoa macho kama mayai kushangaa mazingira ya pale jinsi yalivyokua ya kutisha. Ghafla katika kushangaa kuna mtu aliniita jina langu.                                           
 Kwa hofu kubwa niligeuka nyuma kumtazama. Japo alitokea gizani lakini niliiona vyema sura yake. 
                     
“Jesus Christ”(Yesu kristu) nilipigwa na mshangao.

Sikutaka kuamini kama kweli mtu niliyemuona amesimama mbele yangu baada ya mimi kugeuka nyuma alikua ni.                            
                                   
   …. ITAENDELEA…
Tukutane jumatatu.
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni
close