I WILL BE BACK SEHEMU YA 10

I WILL BE BACK 10

Kama mlinzi anavyoisubiria asubuhi kwa hamu, ndivyo Joel alivyokua na hamu ya kumtia mikononi Motemapembe. Kitendo cha wazungu kujali muda kilifanya Joel aniharakishe kwenda kwa yule mtu niliyemuambia huenda angetusaidia kupata mahala pa kuanzia kumsaka huyo mshenzi Motemapembe.

“What about your girl” (Vipi kuhusu msichana wako) nilimuuliza.

“My late father is more important than her” (Marehemu baba yangu ni muhimu kuliko yeye) alinijibu.

Sikua na swali tena wala pingamizi lolote. Bila kupoteza muda tulitoka pamoja ndani ya ile bar na kuelekea sehemu yalipokuwepo maegesho ya magari. Tulitumia lile lile gari nililoenda nalo, niliungurumisha injini nikaingiza gia kisha safari ya kuelekea kwa yule mtu niliedhani angeweza kutusaidia mimi na Joel kupata mahala pa kuanzia kumtafuta yule mwanaharamu kutoka Kongo .
Ilikua kama muvi ya kutisha, ndani ya gari hakuna aliyemuongelesha mwenzake, Joel alikua bize kuichunguza Dar es salaam na mimi nilikua bize kuendesha chombo, mikono ilicheza na gia na usukani wakati miguu ilicheza na breki na mafuta.

 Speed niliyoondoka haikua ya kawaidia, ilikua kama picha la kutisha kama ungetuona ungesema hollywood imehamia bongo maana mwendo ulikua mkali kama majambazi waliopora bank na kuanza kufukuzana na ma askari.              
Tulikua tunarudi nilipotoka, mbezi beach kwa Mzee Ambrosi yule jirani yangu mkubwa aliyekuepo karibu kabisa na ile nyumba yangu ya kifahari ambayo Tressy alikua ameiuza.         
   
Tofauti na Mzee Ambrosi sikuona mtu mwingine ambaye angeweza kutusaidia ndio maana niliamua kwenda kwake pamoja na Joel, niliamini kitendo cha yeye kuwepo pale karibu na nyumbani kwangu kwa muda mrefu lazima kuna jambo lolote ambalo angekua analifahamu na lingeweza kutusaidia katika kuianza ile mission yetu nzito ya kumtafuta na kumsaka yule wanaharamu na kuhakikisha anapatikana kwa gharama yoyote ile akiwa hai au amekufa.

Tulifika mpaka kwa Mzee Ambrosi, kabla ya kuingia ndani nilimuonyesha Joel ile nyumba yangu, alisimama kwa muda kisha akaitazama kwa makini. Alitumia sekunde kazaa kuitazama pande zote hakusema neno alitoa kalamu mfukoni na kuandika vitu nisivovijua kwenye notebook kisha akaishia kushusha pumzi.
Ilikua inaelekea karibu 3 na robo usiku wakati tulipoingia kwa Mzee Ambrosi na kumkuta akiwa sebuleni akinisubiri kwa hamu.                                                                        

 Mzee Ambrosi alikua mkarimu sana, japo alipata hofu kidogo kuona sura ya kigeni lakini alimkaribisha Joel kwa uchangamfu mkubwa kana kwamba walikua wanafamiana kwa muda mrefu.                                              
Nilijipa jukumu la kua msemaji, kwanza nilimuomba radhi Mzee Ambrosi kwa kumpeleka Joel usiku tena bila taarifa wakati mimi mwenyewe nilikua nimekaribishwa.  
                    
“Hata usijali kua huru” Mzee Ambrosi aliniambia.                        
  
 Kwa kuujali muda nilimwambia Mzee Ambrosi kila kitu na sababu ya Joel kuja Tanzania mpaka kuwepo sebuleni kwake muda huo. Nilimueleza maovu yote ambayo mwanaharamu huyo alikua ameyatenda kwa marehemu baba yake na Joel. Niliweka wazi kila kitu kua mwanaharamu huyo alikua amemuua baba yake na Joel na kupora mali zote pamoja na pesa taslimu shilingi Bilioni 3 na milioni 200. Kama haitoshi nikamwambia lengo kubwa la Joel kuja nchini Tanzania kua ni kumkamata Motemapembe na kurudisha utajiri wa marehemu baba yake mikononi mwa familia yao.
Nilifanya hivyo kucheza na saikolojia ya Mzee Ambrosi ili awe tayari kutuambia kila kitu alichokifahamu. Nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa, Mzee Ambrosi aliguswa sana kiasi cha macho yake kuruhusu machozi ya huzuni yamtoke kidogo. 

“Sijui niwasaidie vipi” Mzee Ambrosi alisema.

Nilimsihi sana Mzee Ambrosi huku nikimuomba atusaidie kutuambia matukio yote ambayo alikua ameyaona na ambayo huwa anayashuhudia mara kwa mara katika ile nyumba yangu aliyoiuza Tressy mke mtarajiwa wa Motemapembe ambaye ndo kwanza tulikua tunainza mission nzito ya kumtafuta na kumsaka kwa hudi na uvumba.

“Mgghrrrh” Mzee Ambrosi alisafisha koo lake. “Ngoja niwaeleze yote niliyoyaona kwa macho yangu” alisema.

Tulikaa mkao wa kula, tulimtazama na kumsikiliza kwa makini sana kana kwamba angetupatia mtihani baada ya maelezo yake. Kama cherehani mbovu ya urithi Mzee Ambrosi alianza kutiririka.

“Davis ninavyohisi mkeo Tressy hajaiuza hiyo nyumba yako kama sikosei lazima atakua anaishi mule ndani na huyo Motemapembe”

Mzee Ambrosi aliniambia huku mimi nikimtafsiria yule Joel kwa lugha ya kingereza kwa sababu hakua akikijua kiswahili. Kisha yule jirani yangu aliendelea kuniambia kua sababu kubwa inayofanya aamini hivyo ni kitendo cha pedeshee huyo kuja nyumbani hapo kila baada ya wiki mbili au mwezi mmoja wakiwa wote wawili na Tressy mke wake mpya. Kupitia dirisha la chumba cha juu usawa ya jengo la ghorofa moja hua naona wakibadilishana mabegi na kisha kuwaachia pesa nyingi wafanyakazi wachache wanaoishi hapo.
Baada ya kutuambia hayo alituambia tena kuwa anahisi pedeshee huyo anamiliki genge kubwa la majambazi waliobobea katika utumiaji wa silaha za moto ambao huwa wakimsaidia sana katika kuilinda kambi yake iliyopo katika msitu wa Magopande ambayo hutumika sana kwa kufanya biashara zake haramu za madawa ya kulevya iliyomuingizia utajiri mkubwa uliofanya aogopeke mpaka na polisi.
Saa 5 kamili usiku ilitukutia sebuleni kwa Mzee Ambrosi. Umuhimu wa maongezi hayo ulifanya muda wote tulioutumia uonekane kama dakika mbili.  
                                                                                                     Waswahili walisema muda ni ukuta ukishindana nao utaumia, tulimani tuendelee kuongea hadi asubuhi lakini haiwezekani hatukua na jinsi ilitakiwa Joel arudi hotelini. 
Joel aliaga niliondoka nae ili kumrudisha hotelini maana hakua na usafiri pia hata kama angekua nao lazima njia ya kufika Sun rise hotel ingemchanganya hasa ukizingatia usiku ulikua umeingia. Tulipotoka getini Joel aliomba kuitazama tena ili nyumba yangu. Aliitazama kwa makini kisha akanigeukia.

“Do you have it’s map? I think our mission will start here” (unayo ramani yake? nadhani mission yetu itaanzia hapa) Joel aliniuliza huku akiingia kwenye gari.
“No”(hapana)

Sikua na ramani kama nilikua nayo basi itakua ilibaki humo ndani wakati nikienda masomoni. Nilivuta kumbukumbu wapi nilipoinunua lakina sikukumbuka. Nilimuahidi kumchorea Joel kama atahitaji maana nyumba nzima ilikua kichwani kwangu.
Nilimfikisha Joel mpaka hotelini nilitamani kumuuliza uongo atakaotumia kumdanganya mpenzi wake lakini nilijizuia maana mahusiano yao hayakunihusu. Tuluiagana ndani ya gari na kabla sijaondoka kurudi mbezi beach Joel aliniambia. 

“As I told you on plane I’m sniper tomorrow we will fly to Nairobi Kenya to take all sniper stuffs, and few techniques before we come back to complete this mission” (Kama nilivyokwambia kwenye ndege mimi ni sniper kesho tutapaa Nairobi Kenya kuchukua vifaaa tayari na mbinu chache kabla ya kurudi kumaliza hii mission)  

Joel aliniambia, alikua serious, maneno yake na sura yake havikua na masihara hata kidogo. Toka nimekua na akili sikuwahi kumuona mtu yoyote katika hali hiyo ya u serious na umakini mkubwa kama alivyokua Joel muda huo, vitu hivyo niliishia kuviona kwenye muvi za kijasusi.

   “What about your girlfriend” (vipi kuhusu mpenzi wako) safari hii nilishindwa kujizuia.

 “I already told you that ,My late father is more important than her” (nilishakwambia marehemu baba yangu ni bora kuliko yeye)
Joel aliniambia huku akishuka kwenye gari na kuelekea hotelini.                    
 Kabla hajafika mbali nilimuita, alipogeuka nikamwambia 

“Joel after arriving to Nairobi, I can’t wait to come back to complete this mission” (Joel kama tukifika Nairobi nitashindwa kuvumilia kurudi kuimaliza hii mission)

“Don’t worry you will be back” (Ondoa shaka utarudi tu) Joel aliniambia huku akianza kupiga tena hatua zake kuelekea hotelini.

Userious, maneno na mipango yake vilinipa ujasiri, nilijikuta ninja akilini mwangu nilijiona kama Bluce Lee au Steringi kichaa. Nilikua na hamu ya kumsaka Motemapembe nakumbuka hata kabla Joel hajafika mbali zaidi niliongea na kupaza sauti kubwa kiasi.

“yah sure I will be back” (kweli nitarudi) 
 kiasi cha kumfanya Joel ageuke nyuma na kunipigia saluti kisha akaendelea na safari yake kuelekea hotelini.

Je nini kitaendelea……?
 Tukutane alhamisi. Usisahau ku like na ku share iwafikie wengi zaidi.

            ……… ITAENDELEA……..
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni