I WILL BE BACK SEHEMU YA 05

I WILL BE BACK 5

Ilikua ni majira ya saa 7 na nusu usiku wakati sauti za vishindo na minong’ono zilionekana kusikika kwa mbali na kuuvunja ule ukimya uliokua umetawala katika eneo la uwanja wa ndege wa Nanning jijini Beijing nchini China.
vilikua ni vishindo na minong’ono ya baadhi ya watu waliokua wakimalizia kuuingia ndani ya ndege iliyokua mali ya shirika la ndege la serikali ya Ethiopia .
wakati watu hao wakionekana kumalizika kuingia ndani ya ndege hiyo mimi pamoja na Slyvester mdogo wake na yule rafiki yangu wa kizungu Mr.James tulikua tumeshaingia ndani ya ndege na hivyo tulikua tukiwasubiria abiria wengine wamalizike kuingia ndipo safari yetu ndefu ya kutoka katika bara la Asia na kwenda katika bara la Afrika ianze.
Rafiki yangu kipenzi Mr.James alikua amenikabidhi mdogo wake huyo Sylvester ambaye kwa mara ya kwanza ndio alikua anakwenda kuikanyaga ardhi ya bara la Afrika ili nimtazame na kuhakikisha anafika salama mpaka mwisho wa safari yake iliyokua inaishia nchini Kenya.
Lakini licha ya rafiki yangu Mr.James kuniomba na kunikabidhi jukumu hilo la kumtazama mdogo wake Slyvester aliyekua na umri wa kati ya miaka 18 hadi 20 ambaye kwa mara ya kwanza ndiyo alikua anaenda kuikanyaga ardhi ya bara la Afrika hali ilionekana kuwa tofauti kidogo kwani mara tu baada ya kuingia ndani ya ndege tulitengana na Slyvester ambaye yeye alikwenda kukaa katika siti yake iliyokua upande wa nyuma kabisa ya ndege na mimi nikaenda kukaa katika siti yangu iliyokua upande wa mbele kabisa ya ndege karibu na ulipokuwepo mlango wa kuingilia katika chumba cha marubani na hivyo kufanya jukumu hilo la kumtazama Slyvester ilishindikane na kuonekana kua gumu. 

Nilikaa siti ya mbele pamoja na wazungu wawili walioonekana kuwa wapenzi huku mzungu wa kiume akionekana kuwa mkubwa na mrefu kidogo kuliko yule mzungu wa kike.
basi mara baada ya kukaa niliyakatisha maongezi yao kwa kuwasalimia kiukweli walionekana kuwa watu wakarimu sana kwani waliijibu salamu yangu kwa uchangamfu mkubwa sana huku wakiniuliza sehemu niliyokua ninakwenda, niliwajibu kua ninarudi nyumbani nchini Tanzania
mara baada ya kuwepo nchini China kimasomo kwa takribani miaka minne.
walifurahi sana kusikia ninaaenda nchini Tanzania kwani nao walikua wakija hukohuko Tanzania kwa lengo la kwenda kutalii katika mbuga mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenda kuupanda mlima kirimanjaro ambao habari zake zilionekana kuwavutia sana wazungu hao wawili walioonekana kua mtu na mpenzi wake. 
wakati maongezi yangu na wazungu hao yakiendelea msururu wa watu waliokua wakiingia ndani ya ndege ulikua umekwisha malizika na kufanya viti vyote vijae watu pasipo hata kiti kimoja kuonekana kubaki wazi.
baada ya msururu ule kumalizika mlango wa ndege ulifungwana wakati yote hayo yakiendelea mimi pamoja na wale wazungu walioonekana kuwa na hamu kubwa ya kuifahamu Tanzania hatukua tukijua lolote linaloendelea kwa sababu ya utamu wa maongezi yetu yalyofanya nisahau hata matatizo yangu yaliyokua yamenitokea siku chache zilizopita.

Ghalfa!! Nikiwa katikati ya maongezi na wale wazungu wawili sauti laini ya kike yenye lafudhi ya kizungu ilisikika kutoka katika spika nzuri za plastiki zilizokua zimefungwa usawa wa katikati ya kila siti upande wa juu ya paa la ndege hiyo iliyoonekana kupendeza sana kuanzia muonekano mpaka mpangilio wake ambao haukuonekana kutofautiana sana na lile treni nililopanda wakati nikitoka katika mji wa Chang chun kuja jijini Beijing.
“Attention!! We are going to fly very soon, every one make sure you wear the crib well take it down of the seat”
(Angalizo tunakwenda kupaa muda si mrefu kila mtu ahakikishe amefunga mkanda vizuri upo chini siti) sauti ile ilirudia mara kusikika mara tatu kisha ikanyamaza
Ilikua ni sauti ya mhudumu wa ndege ikiwatahadgarisha abiria wote kufunga nikanda kwa ajili ya kuepusha migongano wakati wa ndege kupaa
Sauti ile ya muhudumu ilionekana kutiliwa mkazo kwani mara tu ya kuacha kusikika sauti nyingine za vibanio vya kufungia mikanda ilianza kusikika kwa mbali huku kila mtuu akionekana kuinama na kufunga mkanda kwa ajili ya usalama wake binafsi.
Ilichukua kama dakika 5 ambapo mikanda yote ya mule ndani ya ndege ilionekana kupita katika bega la kila abiria kutoka kwenye ungio la kwanza hadi kwenye kibanio cha pili cha mkanda huo kilichokua upande wa pili wa siti.
Baada ya zoezi hili kuonekana kukamilika sauti ile laini kutoka kwa muhudumu wa kike ambaye hakua akionekana kwa wakati huo ilisikika tena kutoka katika zilezile spika za mwanzo
    “Its our hopes that every one have already wear the crib properly”
(ni matumaini yetu kwamba kila mtu amekwisha funga mkanda ipasavyo)
Sauti hile ya mhudumu wa kike ilisikika huku ikizidi kuongea tena
“we are going to fly now and for those who have health problems there are plastic pocket behind of each seat its special for vomiting”
(tunakwenda kuruka sasa hivi na kwa wale wenye matatizo ya afya kuna mifuko ya plastic nyuma ya kila siti maalumu kwa ajili ya kutapikia) sauti ilizidi kusikika huku ikionekana kusababisha ukimya mkubwa mule ndani ya ndege.
     “we wish you all nice journey and enoj our service”
   (tunawatakia wote safari njema na furahieni huduma zetu)
Sauti ile ilimalizia kusikika kisha ikatulia na ghafla mara tu baada ya ile sauti ya muhudumu kutulia ukimya ulionekana kutawala mule ndani ya ndege ulianza kupotea polepole kwa sababu ya sauti za kukoroma kutoka kwa baadhi ya abiria waliokua wameanza kusinzia.

Ilikua ni saa 8 kamili usiku kwa saa za nchini China wakati ambapo injini zote mbili za ile ndege zilionekana kuwashwa na kuanza kuunguruma huku sauti ya miungurumo hio mikubwa ikianza kusikika mpaka ndani ya ndege na kuonekana kuziunga mkono zile sauti za kukoroma na kufanya ukimya wote uliokua umetawala ndani ya ile ndege upotee.
Injini zilionekana kuunguruma kwa karibu dakika 5 nzima kisha ndege ikaanza kukimbia kutoka mwendo mdogo mpaka kufikia mwendo mkali kiasi cha kufanya zile taa kubwa zilizotutendea wema zionekane kupitia madirishani zikikimbia kurudi nyuma harakaharaka sana.
na wakati taa zile kubwa zikionekana kurudi nyuma kwa kasi sana sauti ya matairi ya ndege hiyo zilianza kusikika kwa mbali kuashiria kua zilikua zimeanza kuicha ardhi ya Beijing China kiasi cha ndege kuinuka mbele kuashiria kuwa tayari tulikua tumeanza kupaa.
kwa heri China hakika hatutakusahau hivyo ndivyo nafsi za watu wengi zilionekana kuongea kwani kitendo cha watu kuchungulia madirishani na kuona jinsi ndege ile ilivyokua ikiiacha ardhi ya China kilionekana kueleza wazi kabisa hisia zilizokuwepo moyoni mwa watu wengi.

Basi kadri ndege ilivyozidi kulifaidi anga la nchi ya China muda nao ulionekana kutokua nyuma katika kuisogelea afrajili ya usiku huo wakati yote haya yakiendelea ukimya nao ulionekana kutawala tena kwani ilikua nni karibu saa 9 na robo usiku wakati zaidi ya nusu ya abiria wote walionekana kusinzia wakati sauti za kukoroma zikionekana kusikika kwa mbali sana huku sauti pamoja na zile ngurumo za injini zikionekana kumezwa na mawingu mazito yalionekana kutoshiba wala kushiba mara baada ya kuumeza mwezi pamoja na nyota hapo awali na kulisababhisha zlile giza zito lilionekana kuzielemea taa za mtaa wa Nanning masaa machache yaliyopita.
Wakati asilimia kubwa ya abiria wakionekana kulala huku wengine wakoinekana kujilazimisha na kuutafuta usingizi kwa lazima mimi bado nilikua nikiongea na yule mzungu wa kiume ambae tulionekana kuzoeana ghafla mara baada ya kujua kuwa safari yetu ilkua ni moja.
Tuliongea mambo mengi sana huku nikimuelezea kuhusu wasifu wa watanzania mila pamoja na tamaduni zao bila kuisahau amani ya nchi yao iliyoonekana kuchukua nafasi kubwa katika mioyo ya watanzania wengi.
wakati maongezi yetu kati yangu mimi na yule mzungu wa kiume yakiendelea yule mzungu wa kike aliyeonekana kuwa mpenzi wake alionekana kulala huku akiwa amekiegemeza kichwa chake katika kiti cha ndege io kilichotengenezwa kwa ustadi mkubwa na kushindiliwa na pamba laini kwa ndani zilizofanya kiti icho kiwe laini na kisiumize pindi mtu aegamiapo.

Kile kitendo cha yule mzungu wa kike kulala kilionekana kumfurahisha sana yule mzungu wa kiume ambaye tangu tuzoeane sikua nimemfahamua hata jina lake.
Sikujua kwa nini alifurahia sana kitendo cha mpenzi wake kulala lakini ghafla nikiwa katika hali ya kumshangaa aliuchukua mkono wake wa kushoto na kuupepesa juu ya uso wa mpenzi wake na aliporidhika kuwa mpenzi wake huyo amelala alinisogelea tena mpaka pale nilipokua nimekaa akamnishika bega 
huku akianza kuongea kwa uoga sana na hofu ya kusikiwa na yule mpenzi wake aleyekua amelala.
Alianza kuniambia mambo ambayo yalionekana kuniogopesha na kunitisha sana kiasi cha kufanya niyakumbuke matatizo yangu yaliyonitokea siku chache zilizopita
Alikua akiongea kwa hofu sana huku akitazama nyuma mara mbilimbili ili kuhakikisha kama yule mpenzi wake bado alikua amelala.

I’m Joe Posmerk” yule mzungu wa kiume alizidi kuniambia huku safari hii akionekana kunong’ona sana kwa ajili ya kuogopa kusikiwa na mtu mwingine yoyote tofauti na mimi.
“I think I trust you and that why I want to tell you my secret which I kept for a long time and I hope you will help me”
(Nadhani ninakuamini na ndio maana ninataka nikueleze siri yangu ambayo nimeitunza kwa muda mrefu sana na ninatumaini utanisaidia)
Kiukweli yale maneno ya yule mzungu niliyekua nimekaa nae na kuongea nae tangu mwanzo wa safari na kujitambulisha kwangu kwa jina la Joe yalionekana kuzidi kunitisha sana huku yakionena kufungua mlango na kuyaruhusu maswali yasiyo na majibu yapokezane kuingia na kutoka kichwani mwangu nilijikuta nikianza kuogopa zaidi 
Kwasababu nilijiuliza ni siri gani anayotaka kuniambia halafu nimsaidie na nitawezaje kumsaidia wakati mimi mwenyewe nilikua na matatizo yangu binafsi yaliyoonekana kuuzidi uzito ufahamu wangu.

                             ………..ITAENDELEA………..

TAARIFA

Kutokana na harakati za maisha hapa na pale tunashindwa ku post kwa wakati, hivyo tunaomba radhi, simulizi hii itakua ikitoka kila jumatatu na alhamisi, tuvumiliane kwa hilo.

TAARIFA YA MUHANDISHI

Simulizi hii ni yake ya kwanza kuiandika, aliiandika mwaka 2014 hivyo anaomba mapungufu yote muyavumilie, bado alikua anajifunza, ushauri , like and share kutoa support.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : I WILL BE BACK SEHEMU YA 05
I WILL BE BACK SEHEMU YA 05
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/i-will-be-back-sehemu-ya-05.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/i-will-be-back-sehemu-ya-05.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content