I WILL BE BACK SEHEMU YA 04

I WILL BE BACK 4
Ilikua ni majira ya saa sita usiku wakati mawingu mazito yalipoonekana kuufunika mwezi na kufanya nyota zionekane kukosa ushirikiano kiasi cha kufanya giza kubwa liutawale mtaa wa Nanning mahali ilipokuwepo airport maarufu ya jiji la Beijing.
Lakini wakati mawingu mazito yanapoonekana kuufunika mwezi na giza kubwa kuutawala mtaa wa Nanning hali ilionekana kuwa tofauti kidogo katika maeneo ulipokuwepo uwanja wa ndege katika mtaa huo.
kwani taa nyingi kubwa zilionekana kutoa mwanga mkubwa bila uchoyo wowote na kuusaidia umati mkubwa wa watu zaidi ya 250 waliokua wakisubiria kukaguliwa mizigo yao kwa ajili ya kuianza safari yao ndefu ya kutoka katika bara lililokua likiaminika kuwa bara kubwa kuliko bara lolote duniani.
Wakati taa hizo kubwa zikionekana kuutendea mema ule umati wa watu zaidi ya 250 mimi pia nilionekana kuwepo miongoni mwa ule umati wa watu ulioonekana kutendewa wema na zile taa kubwa zilizokua zimelizunguka karibu eneo zima la uwanaja wa ndege wa pale jijini Beijing.

Wakati umati huo ukionena kuusubiri kwa hamu kubwa sana muda wa kukaguliwa mizigo kwa ajili ya kuinza safari ndefu ya kutoka katika bara la Asia mpaka bara la Afrika
Kwangu hali ilionekana kua tofauti kabisa kwa sababu ya matatizo yaliyokua yamenitokea siku moja kabla ya kuianza safari yangu na kufanya niichukie safari hiyo ya kurudi nyumbani
Nchini Tanzania
Kiukweli kitendo cha mke wangu Tressy kuniacha pasipo ya mimi kumtendea kosa lolote kiliniumiza sana kiasi cha cha kufanya niichukie safari yangu hiyo ya kurudi nyumbani huku nikiamini kua kila mtu alikua akiniona mjinga kwa sababu ya kitendo changu cha kumuamini mke wangu Tressy na kumuachia mali zangu zote mikononi mwake zikiwemo akaunti zangu zote za benk, magari nyumba pamoja na kampuni zangu mbili za usafirishaji.

Wakati nikiwa mawazoni huku nikionekana kutousuburia muda huo wa kukaguliwa mizigo kwa hamu kama ilivyokua kwa watu wengine ghaflaa!!! nilihisi kuguswa na mtu katika bega langu la kulia na kufanya nigeuke nyuma na kumtazama mtu yule aliyekua amenigusa bega langu.
Mungu wangu!!! Nilisema mara tu baada ya kugeuka nyuma na kumtazama yule mtu aliyekua amenigusa bega langu la kulia na kufanya nigeuke nyuma kwa uwoga na kumtazama kwa sababu ya kutofahamiana na mtu yoyote pale Nanning.
Alikua ni bwana James Scoutland mvulana wa kizungu aliyeonekana kuwa na umri wa kati ya miaka 22 hadi 24 ambaye alikua ni miongoni mwa wateja wangu wa kwanza wa kampuni yangu ya usafirishaji kabla sijaja masomoni nchini China.

“Hey mr.James I never thought if I will see you here”
(Hey bw.James sikudhani kama ningekuona hapa)
Nilimwambia bwana James huku nikitengeneza tabasamu bandia usoni mwangu kwa ajili ya kuyaficha matatizo yaliyonikuta siku moja kabla ya safari yangu na kumkumbatia kwa furaha.
“Me too mr.Davis but how are you and what about youre family are they safe?”
(mimi pia bw,Davis lakini vipi hali yako na hali ya familia yako vipi ipo salama)
Bwana James aliniuliza huku akiifungua mikoni yake kwa ajili ya kulipokea kumbatio langu.
Nadhani James aliniuliza bila ya kujua kuwa swali lake liliuumiza sana moyo wangu kiukweli alipouliza kuhusu familia yangu nilijikuta nikiumia sana moyo kwani bila shaka alikua anaulizia hali ya mtoto ambae mpaka kwa wakati huo hakuonekana kua damu yangu pamoja na Tressy ambae mpaka wakati huo niliokua nikiongea na bwana James hakua mke wangu tena.
Lakini licha ya swali lake kuumiza sana moyo wangu lakini nilijikaza kiume nikamjibu kuwa wapo salama na muda si mrefu Mungu akipenda nitakwenda kuonana nayo nilimjibu huku bwana James huku nikiyazuia machozi yaliyokua yakitaka yaanze kunitoka na sikua na jinsi zaidi ya kufanya hivyo ili kuyaficha matatizo yaliyokua yamenikuta

Basi mara baada ya kusalimiana na bwana James tuliongea nae mambo mengi sana ya kibihashara huku tukipiga stori mbili tatu za hapa na pale kisha akanitambulisha kwa mdogo wake aitwaye Slyvester ambaye nae alikua akisafiri usiku ule katika ileile ndege ya shirika la Ethiopia na safari yake ilikua ikiishia nchini Kenya.
Basi baada ya kunitambulisha kwa mdogo wake Slyvester maongezi yetu yaliendelea kwa muda wa kama nusu saa zaidi wakati ambapo watu walianza kuingia kwenye chumba cha kukaguliwa mizigo yao kwa ajili ya kuinza safari.
Kitendo cha watu watu kuanz kukaguliwa mizigo kilifanya niagane na bwana James ambaye yeye aliniambia kuwa atakua pale chini China kwa muda wa miezi mitatu zaidi kwa sababu ya shughulu zake za kibiashara.
  
    “Goodbye mr James if God wishes 1 day we will meet again at any time in any country ”
(kwaheri bw.James kama Mungu akipenda siku moja tutaonana tena katika muda wowote na katika nchi yoyote) 
nilimwambia bwana James huku nikijiandaa kubeba mizigo yangu kwa ajili ya kuingia katika chumba cha kukagulia mizigo
    “Goodbye too mr Davis and thank you so much for what youre company did to me some few years ago”
(kwaheri pia bw Davis na nashukuru sana kwa jinsi kampuni yako ilivyonifanyia miaka michache iliyopita)
   “thanks you and goodbye once again mr James”
(nashukuru na kwa heri kwa mara nyinigine bwana James)
Nilimwambia James huku nikimpa mkono wa kwa heri
“thanks mr Davis but I wonder why you were dicided to sell all of youre company”
(asante sana bw Davis lakini nashangaa kwa nini uliamua kuyauza makampuni yako)
Kiukweli kauili ile kutoka katika kinywa cha bw James ilinishtua sana kiasi cha kufanya niutoe mkono wagu uliokua mikononi mwake.
“what do you say mr James?” nilimuuliza kwa mshangao mara baada ya kuoamini ile kauli yake niliyoisikia
“Davis are you serious? Last four months when I was in Tanzania I came to youre company inorder to make a busness but I met all of youre company selled to some one who called Motemapembe a guy from Congo.
(Davis upo siriasi ? miezi minne iliyopita nilipokua Tanzania nilikuja katika makampuni yako kwa ajili ya kufanya biashara lakini nikakuta yote yameuzwa kwa mtu mmoja aitwaye Motemapenbe kutoka Kongo)
Bwana James aliniambia kwa msisitizo huku akionekana kutoamini kama kweli sikua nimeyauza makampuni yangu .
kiukweli sikutaka kabisa kuyaamini maneno ya bwana James nilijikuta nikianza kulia huku nikishangaa kwa nini Tressy aliamua kunifanyia hivi yaani kaamua kuniacha bila ya mimi kuwa na makosa yoyote lakini kama haitoshi kaamua kuuza mali zangu
hali yangunilianza kubadilika ghaflaa na kua kama ya jana usiku pale hotelini Guangzhou

“Sorry mr Davis I don’t think if I will pain you like this very very sorry but whats wrong”
(samahani bw Davis sikudhani kama ningekuumiza kiasi hichi samahani sana laikni ni nini tatizo)
Bwana James aliniuliza huku akionekana kushangaa sana kwa jinsi nilivyokua nikilia 
“my wife has betraying me”
( mke wangu amenisaliti ) nilimjibu bw James huku nikilia safari hii nililia kwa nguvu zaidi mpaka baadhi ya watu waliokua bado hawajaingia kwenye chumba cha kukagulia mizigo walinishangaa .
“So why you lied to me that they safe”
(sasa kwanini ulinidanganya kuwa hawajambo) bw James aliniuliza
Sikumjibu kitu chochote zaidi ya kumuangalia na kuchukua mizigo yangu kisha nikaanza kupiga hatua kuelekea katika chumba cha kukagulia mizigo.
Lakini kabla sijapiga hata hatua mbili mbele bwana James aliniita tena niligeuka nyuma na kumtazama bila ya kumsemesha neno lolote
“Please mr Davis take care of my young brother”
(samahani mr Davis naomba umuangalie mdogo waangu) 
Bw James aliniambia na kufanya nisimame na kumsubiri huyo mdogo wake Slyvester ambaye tulikua tukisafiri nae kwa ndege moja nay eye alikua akiishia nchini Kenya.
“Ok all of you fly well”
(sawa safirini salama) bwana James aliniambia mara tu baada ya mdogo wake kufika pale mahali nilipokua nimesimama hatua chache kutoka kwa mr James
 
Basi baada ya Slyvester kunifikia niliongozana nae mpaka chumba cha kukagulia mizigo huku mabegi yetu pamoja na simu na kifaa chochote cha chuma kikikaguliwa kwa mashine maaulum zilizokua zimeunganishwa na kompyuta kubwa sana za kisasa
Baada ya kukaguliwa na kukuta hatuna matatizo yoyote tulienda moja kwa moja mpaka sehemu ilipokua imesimama ndege hiyo
Ilikua ni mwendo wa kama dakika 5 ndipo tulipoifikia ndege ile ndege ya Ethiopia na baada ya kuifikia tuliingia ndani mimi nilikaa siti za mbele tofauti na Slyvester ambaye alikaa siti za nyuma kidogo 
Nilikaa siti moja pamoja na wazungu wawili mmoja alikua wa kike na mwingine wa kiume ambao niliwakuta wameketi niliwasalimia kisha nikaketi huku tukisubiri abiria wengine waingie na ndipo tuianze safari yetu.

             ………ITAENDELEA………………

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : I WILL BE BACK SEHEMU YA 04
I WILL BE BACK SEHEMU YA 04
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/i-will-be-back-sehemu-ya-04.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/i-will-be-back-sehemu-ya-04.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content