Featured Post

HOUSE GIRL WA DADA SEHEMU YA 06

HOUSE GIRL WA DADA
SEHEMU YA 6
WHATSAPP 0623132416
ZANZIBAR
Alice alivyoanguka chini alianza kupiga fujo San kila mtu alishangaa sana na Bibi yule alizidiwa na kuondoka zake alimuacha alice akiwa ameshikiliwa huku akipiga fujo sana baada ya saa moja kupita huku yule mzee meshaki akizidi kuomba.
Alice alizidi kulege na kuanza kuongea kwa kuomba msamaha hapo aliongea vyote alivyokuwa akifanya tangu utotoni na kwa nini alifikia hatua ya kuwa vile!
Na kusema nani aliyesababisha yeye kuwa vile na kupandikizwa jini mwilini mwake!
Alice aliliegea sana na nguvu kumuishia baada ya kuombewa na mzee meshaki ambapo alianza kumuuliza kwa nini unaisumbua familia hii nan alikutuma uje kuisumbua familia hii
Alice alianza kuelezea mkasa wote kwa nini huwa anakuwa katika hali ile na kwa nini huw hali chakula kingi
Alianza kutoa historian ya baba yake kumbe aliweza kumkabidh maswala ya uchawi kipindi ndio yuko darasa la tano tu na alikuwa anauwa vijana wa kiume umri kuanzia kiaka 15 hadi 25
Na pia alisema huwa anauwa watoto wadogo wa kike ambao ndio wamezaliwa hivyo alikuwa ameplan kumuuwa mtoto wa dada yangu na mimi pia
Ila alikuwa akisita kimiuwa kwa sababa familia yake ilipenda niwe mme wake na walitaka nikabidhiwe kila kitu maswala ya utajili maana alisema baada ya kukabidhiwa uchawi alizidi kuwa maarufu kwa kazi yake
hivyo kila sehemu alikuwa anaenda kiasi kwamba ilifika hatua akawa na uwezo wa kuzama chini ya bahari kwenda kuongea na mawakala zake
Na yule Bibi ndio aliyempeleka na yeye chini ya bahari kwa ajili ya kuwa na nguvu kubwa sana na kuitawala dunia kiuchawi na awe na asili ya jini
hivyo alizidi kuelezea jinsi chakula alivyokuwa akikipika na kukileta mezani nakusema alikuwa hapiki, yeye
wakati mwingine aliwatumia ndugu zake kuweza kumsaidia kupika lakin walikuwa wanapika wakiwa uchi na kupanga chakula walipanga wakiwa uchi pia
juice wakat mwingine alikuwa anatengeneza juice ya dam iliyochanganywa na mikojo hakika alielezea vitu Ving sana siku hio!
Mzee meshaki alimuuliza unataka mini ndani ya nyumba hii alice alisema namtaka huyu mtoto na huyu kaka maana ndio ilikuwa target yangu niwapate ila huyu mtoto namtaka akiwa amekufa na huyu kaka namtaka awe mme wangu
Mzee meshaki alikemea Mara moja alice alizimia na kupoteza faham ziku hio walimnenyua na kumpeleka chumbani kwa ajili ya kumpumzisha mzee meshaki hakutaka kumuacha alimfuata hukohuko na kuzudi kumuombea
Wakati akimuombea dada yangu alianza kulia maana tulikuwa tunalishwa uchafu na chakula cha ajabu sana kiasi kwamba alisema akipata fahamu tu kesho nampeleka kwao hakuna cha kumsamehe?!
Alice kule chumbani alizidi kuombewa na yule mzee bila kukara tamaa baada ya nusu saa alice alistuka nakushangaa sehemu alipolazwa alitaka kuongea lakin alikuwa bubu kwa muda ule hakuweza kuongea wala kusikia chochote
Mzee meshaki alimuamru alale alizidi kumuombea tena na tena baada kama masaa sita anamuombea tu miale ilianza kutoka machoni na vidoleni kwa alice na sauti na miungulumo ya ajabu ilianza kusikika!!
Sauti za kukili makosa zilisikika mle ndani kila mmoja alishangaa na alice alianza kuinuka na kutaka kukimbia lakin mlango ulikuwa umefungwa
Alimtishia mzee meshaki kuwa atamuuwa lakini hakuogopa alizidi kuomba na sauti zile zilizidi kusikika kama mwangwi chumbani mle aiseee nilishangaa sana maana nilikuwa nimezoea kuona kwenye movies tu!
Baada ya ukimya ule ndani ya chumb kile mzee meshak alitoka kule chumbani na kuja sebuleni huku jasho likiwa linamtoka sana mimi na Dada pamoja na shemeji yangu tulibaki kushangaa tusijue cha kufanya hapo ndipo mzee meshak alituruhus kwenda kumuona Alice!
Nilikuwa wa kwanza kuingia chumbani na nilimkuta amelala kitandani huku hawez kuongea chochote alikuwa bubu kusema ukweli hata kusikia alikuwa hasikiii nilimtikisa alinitazama na kunionesha ishara ya kutaka maji ya kunywa nilimuelewa nilienda kumchotea na kumletea alikunywa maji sana muda muda huo na
hapo alionesha ishara ya kuhisi njaa na alitaka chakula nilitoka na kwenda kumletea ubwabwa alikula kiasi kwamba kila mmoja alimshangaa ulikuwa haijawahi kutoke tangu alipokuja pale kwa dada yangu alibaki kulia kila alipokuwa akinitazama machoni
alitamani kuongea kitu lakin sauti yake ilikuwa haitoki alilia sana baada ya kuombewa na kutulia aliomba nafasi ya kupumzika tulitoka wote chumbani na kumuacha huko mwenyew mzee meshaki alisema tumuache muda wa kuongea ukifika ataongea kila kitu maana amesharudi kwenye hali ya kawaida ya ubinadamu msimuogope!
Siku hio ilinibid mimi kushika usukani pale nyumbani nilifanya shuguli zote za pale nyumbani niliweza kuandaa chakula cha mchana nilimpakulia Alice chakula chake na kumpeleka chumbani kwake nilimuamsha aliamka na kukaa kitandani nilimnawisha lakin kila alipokuwa akiniangalia alikuwa analia sana hadi nikaanza kuogopa tena!
Nilionesha woga lakin alitikisa kichwa kuonesha kwamba nisimuogope nilitoka chumbani kwake nilienda kukaa sebuleni na kuanza kula chakula changu
wakati naendelea kula Alice alitoa sauti na kuanza kuniita clifforddddd niliitika na kukumbia kufungua mlango wake niliingia nilivyomuangalia kitu cha kwanza aliniambia nisimuogope yeye ni binadam kama mim na mimi nilimjibu ata sikuogopi Alice ndio maana nilkuwana wew muda wote kwa nini nikuogope Leo?
Aliniomba nikamletee mmaji ya kunywa tena niliendea na kumletea pale chumbani kwake aliniangalia wakati nimesimama na kuniuliza unafanya nini huko sebuleni?
Nikamjibu Niko nakula
Sawa wrngine wako wapi?
Nnikamjibu wako chumbani kwao
Mmmmmmmh! Wanadili kunifukuza au
Nikamjibu hapana wanamambo yao tu ata usijali huwezi kufukuzwa wew ni mwanafamilia .
Aliinama nakuanza kujutia hali ile aliyokuwa nayo alianza kuongea baadhi ya maneno ya kumlaumu baba yake mzazi nilimnyamanzisha sana hadi chakula changu kilipoa siku hio
baada ya muda kidogo Dada yangu aliniita na kuniuliza Alice ameanza kuongea niakamjibu ndio ok .
Sasa mwambie akipumzika na usingizi ukiiisha aje sebuleni baadae nitakuwa na maongezi nae itabidi wote muwepo!
Nikasema swa Dada!
Hapo sister aliondoka zake na kutuacha wawili nyumbani lakini Alice alilia sana na kujutia hali ile aliyokuwa nayo
nilikaa nae karibu sana maana nilihisi atajiua na nilimuomba azidi kumuomba mungu.
Nilitaka kutoka nje lakin alinishika mkono na kusema anataka kukaa na mimi nikasema hapana ngoja nikafanye kazi huko nje au twende wote alikataa niliamua kuondoka nje na kufanya shuguli zangu baada ya kumaliza nilikaa sebuleni mwenyewe
Alice alikuja na kukaa karibu yangu na kuanza kuniongelesha
Clifford naomba usiniogope tena mimi ni binadam kama wew ile hali imeshanitoka maana kipind kile nilikuwa nawaza kuua tu muda wote na kufanya vitu vya ajabu sasa najiona Niko sawa!
Oooooh Usijali Alice mimi ni binadam siwez kukuogopa usilie tutazidi kukupenda sana ila nilianza kumuuliza maswali kadhaa na alinijibu vizuri sana
Hivi Alice hio hali ilianzaje hadi kufikia hatua ya kuwa hivyo maana ulikuwa unatisha ulikuwa unanichukua na kunipeleka sehem mbaya Mara baharini na tulikuwa tunapaa kwanini lakini ulikuwa unatufanyia vile..
Alianza kunijibu na kusema Clifford ni story ndefu sana .mimi nilianza kufanya hiz kazi nikiwa na miaka mitano maana tulikabidhiwa na baba yangu mimi na Mdogo wangu aitwaye Salehe ila yeye alikataa
mimi nilivyoanza kukataa baba alinilazimisha sana na nilianz kupatwa na ugojwa wa kifafa ulinitesa sana na nilikuwa naanguka Mara kwa mara na kila usiku ukifika baba alikuwa anakuja na watu wake kuja kunichapa kila siku nilikuwa naamka na alama za fimbo na nilihisi maimivu sana
hivyo nilizidi kuteswa sana kipindi hicho kwa upande wa kaka yangu salehe yeye alikuwa mkubwa aliondoka nyumbani kuanzia kipindi hicho hadi Leo sijui yuko wapi.
ITAENDELEA Kesho Usikose Hapa Hapa
By Ahmad Mdowe
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni