Featured Post

HOUSE GIRL WA DADA SEHEMU YA 04

HOUSE GIRL WA DADA
SEHEMU YA 4
WHATSAPP 0623132416
ZANZIBAR
Niliingia chumbani kwa alice usiku maana nilimuahidi amsadie dada yangu asimuuwe nitaenda kulala naye kama alivyonipa shert lake lakin kitandani kwake nilikuta nyoka ndio amejikunja .
Nilipiga kelele usiku ule nyingi sana na kuanguka chini nilipoteza faham nilipata fahamu baada ya siku tatu nikiwa hospital na dada yangu alikuwa amesharuhusiwa yupo nyumbani!
Baada ya kupata fahamu sikuweza kutulia nilikuwa kama nimechanganyikiwa maana sikutaka kumuuamini binadam yeyeto nilihisi wote wako kama alice lakin kwa muda huo nilikuwa siwezi kuongea badala yake nilikuwa bubu tu!
Dada yangu alilia sana maan walishindwa kujua naumwa nini walikuwa wakipima ugonjwa wanaona Niko sawa sina ugonjwa mwilini mwangu
Hapo ndipo walizidi kuchanganyikiwa kwa muda ule alice alikuwa anakuja hospital akiwa na mtoto wake mkononi pamoja na yule bibi cha ajabu alianza kulia na kumuomba bibi yule aweze kunitoa kwenye hali ya ububu
Bibi alimsikiliza na kunitoa ububu hapohapo niliongea na alice alikaa kitandani kwangu nakusema anajutia kuwa vile maana alikuwa hataki kuishi maisha Yale alilazimishwa na baba yake mzazi hapo
sikuweza kumjibu kwa muda japo pale walikuwa hawamuoni nilimuangalia tu na alianza kuniomba msamaha kuwa nimsamehe lakin sikutaka
Bibi alimpiga alice kibao cha shavuni alidondoka chini sikuweza kumuinua na Bibi alisepa baada ya dakika kadhaa alice aliinuka na kuondoka myumbani
Na mim nilinuomba daktari aniruhusu na kwenda nyumban wakati niko njiani mama yangu alinipigia simu na kuniambia mwanangu matokeo ya kidato cha sita yametoka na umefaulu hivyo inakupasa urudi nyumbani kwa ajili ya kujiandaa na chuo
Nilishangilia na nilikuwa nafuraha kubwa siku hio nilifika nyumbani kwa Dada na kuwapa habari hiyo wote walifurahi na alice alikuja kunikumbatia bila ya kumuogopa dada na aalininong’ oneza sikioni nakupenda napenda sana tuoane Clifford alivyosema hivyo nilistukia nimesema tu ushindweeeeeeee!! .
Duuuu alice alianguka chini na kuanza kujigalagaza dada na shemeji walikuwa hawaelewi kinachoendelea mimi nilikaa pembeni tu baada ya dakika kadhaa aliinuka na kwenda chumbani kwake
Alilia sana ! dada yangu alienda chumbani kwake na kumuuliza kulikoni imetokea vile alice hakujibu chochote alibaki kuduwaaa!
Usiku uliingia na chakula kiliandaliwa wakati tumekaa tunataka kula alice alikaa karibu yangu na aliniomba nimpakulie chakula wakati napakua Dada alisema mmmmmh! ,siku hizi mnapakuliana chakula angalieni ohoooo
Shemji nae alimdakia na kusem kwani tatizo liko wapi wakipendana poa ndoa itafungwa ahahahahahaha kilikuwa ni kicheko cha watu wote pale mezani
Tulianza kula kwa muda huo sikuweza kuhisi chochote kwenye chakula lakin kadri nilivyoendelea kula nilikuwa nahisi radha tofauti ya chakula mdomoni nilishindwa kula lakin watu wote waliiendelea kula chakula kasoro mimi
Niliwaza kulikoni wakati nawaza alice alinikanyaga mguuni na kusema Clifford kula au hujapenda chakula changu leo?
Nilisema nimekipenda lakin nimewahi kushiba nilijiinamia na kutaka kuondoka lakin alice alinikanyanga tena hapo niliona sahani mbili tofauti yenye vyakula moja ilikuwa na nyamba mbichi na glass yangu ilikuwa imejaa damu
Nikajua moja kwa moja nilikuwa nakula vyakula vile niliinuka na kuondoka kulala nilifika mle chumbani na kwenda kuoga nilivyorudi chumbani kwangu nilikutana na mtu amevalia ngui nyeupeeee zinang’aa lakin alikuwa haonekani machoni
Sikuweza kumjua ni nani alichokisema ni neno moja tu alisema tunakuhitaji kuzimu tunataka tukukabidh Mali zako!
Hapo aliondoka nilibaki nashangaa nisijue cha kufanya baada ya muda kidogo alice alingia chumbani kwangu na kunishika bega
Sikuweza kumsemesha ila yeye alisema clifirod umependwa sana kwetu hivyo unahitajika ukakabidhiwe utajili na safari itaanza leo kwenda kuzimu na alisema mimi so binadam wa kawaida nimekupanda napenda tuishi wote .
Alisema aliyekuja kukwambia amevalia nguo nyeupe ni baba yangu na palepale alice alitoweka sikuweza kushituka maana nilikuwa mimeshatishwa vya kutosha
Nilijiandaa kulala na nikajitupia kitandani pale nilikaa kwa muda ule nikiwa nawaza maneno ya alice na yule mtu mweupe kabla usingizi haujanipitia alice aliingia chumbani kwangu kwa kupitia kwenye kona ya chumba changu
Alikuja kukaa kitandani na kunishika mkono alianza kusema twende kwa wazaz wangu na ukabidhiwe Mali zako pale alice alisema nifumbe macho na baada ya kufumba macho gafla ulivuma upepo chumbani kwangu na akaniambia hatupitii mlangoni tunapitia ukutani
Ukuta ulijigawa Mara mbili tulipita na kuanza safari nyingine baada ya muda kidogo tulifika baharini hapo aliniambia nifumbue macho nilifumbua na kujikuta tuko baharini
Nilishangaa sana wakati nazubaa alitoke msichana mwingine wa kiarabu alianza kunivuta mkono na kunipeleka chini ya maji!.
Tulivyofika baharin mimi na alice alikuja mwamke wa kiarabu na kunishika mkono na kuingia ndaji ya maji kwa muda ule niliona mlango unafunguliwa ilikuwa ni barabara nzuri sana
Tulizama ndani ya maji kulikuwepo na nyumba nzuri sana inakila kitu ndani tuliingia na nilikalishwa kwenye kiti na kusubiria nilichoitiwa
Wakati nimekaa pale alikatiza msichan mmoja sebulen na kunisalimia nilimuangalia lakin sikuweza kujua anaelekea wapi.
Nilijiona niko pekee yangu mle ndani nilisimama na kuchungulia dirishani na niliona maji tu ndio yameizunguka nyumba aisee nilishanga sana!
Alikuja yule Bibi akiwa ameshika fimbo ya kung’aa sana inatoa miale ya kuumiza macho alikaa kwenye kiti chake na kuanza kunielezea!
Wakati nimekaa alice alikuja na yeye lakin utofauti niliouna kwa alice siku hio nikwamba miguu yake ilikuwa kama kwato sikuweza kushituka nilitulia na alikuja kukaa karibu yangu!
Bibi alianza kusema sasa ni muda wa wew Clifford kuhama ulimwenguni na kuja kuishi na sisi huku chini ya bahari mkeo ndio huyo na duniani unamali nyingi sana ukikubali zitakuwa zako
Kuanzia sasa na kuendelea hivyo utaishi na mkeo na pia utakuwa unakuja kututembelea kila usiku ukiwa na mkeo alice.
Bibi yule aliniinua pale na kunipeleka chumba kimoja alikifungua na niliambiwa nikae alimuita binti yule aliyekatiza sebuleni nilipofika na alikuja na kusema nimekuita hapa umtambue huyu nisipokuwepo yeye ndiye atakuwa anaruhusiwa kuingia chumba hiki cha siri.
Kwa muda ule sikuona kitu chochote ndani ya kile chumba zaid ya viti tulivyokuwa tumekalia mim na yule bibi kizee alinyoosha fimbo yake na nilikua naona kinachoendelea nyumbani ni kipi kwa usiku ule
Nyumba nzima na kona za nyumba niliziona kama Niko duniani hapo tilimaliza alinyoosha tena upande mwingine niliona pesa nyingi sana nadhan ilikuw kila pesa ya nchi ilikuwepo pale ..
Na alinyoosha upande mwingine na zilitokea nyumba za kifahari nzuri mno zinakilakitu ndani kila samani unayoijua wew ilikuwemo ndani ya nyumba hii na kusema clifford utakuwa mmiliki wa Mali hizi zote na kuishi na mtoto wangu!.
Duuuu niliwaza sana maana nilikuwa siongei chochote zaidi ya kuelekezwa vitu mle ndani bibi yule alimaliza kunionesha Mali zile alianza kunizungusha sehemu za starehe mle ndani duuuu kumbi zilikuwa zimepabwa zina kila aina ya kinywaji wanawake vyote vilikuwepo kiasi kwamba kwa duniani ni sehemu chache sana
Tulikaa pale na watu walianza kutumbuiza cha ajabu waliimba nyimbo za matusi na nilikuwa sioni sura zao wale wanaoimba pale jukwaani na walikuwa uchi wa mnyama kabisa
Baada ya kumaliza kuimba chakula kililetwa na kuwekwa mbele yetu!
Duuuu chakula kile nilkuwa sijui ni chakula cha aina gani nilikiangalia na nilkataa kula alice alikuja kunilisha lakin nilikataa na alianza kuchukia maan ilikuwa mbele ya watu wake wengi sana
ITAENDELEA
by Ahmad Mdowe
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni