HIVI UNAJUA MTOTO WAKO ANAFANYAGA NINI?

Hivi unajua mtoto wako anaendaga wapi? Mara ya mwisho wewe kutoka na mtoto wako kwenda sehemu mkakaa tu na mkaongea, labda mkala icecream kama rafiki ilikua ni nini? Unakumbuka siku ambayo ulimuambia mtoto wako amsalimie mtu flani? Akakataa au akaonyesha uoga, labda ukamchapa kwanini hamsalimii ila hakusema? Unakumbuka siku ambayo mtoto wako ulimuambia alale na flania akaanza kulia?

Unakumbuka siku ambayo mtoto wako ulimuambia aende sehemu flani akakataa. Labda ni shule, alikua anapenda shule lakini ghafla likija suala la shule analia kabisa na hata kukuambia kuwa ni bora umhamishe? Lakini inawezekana kuwa ni kwa ndugu yako, ukamuambia kuwa aende kukaa au kucheza kwa mru flani, lakini akakataa, ila kataa yake unaona ya kimajonzi kabisa kama vile mtu anataka kulia?

Unakumbuka lakini, alinyong’onyea mpaa ukawaza hivi huyu mtoto ana nini? Lakini unakumbuka namna alivyobadilika ghafla na kuwa msiri, yaani unakuta mtoto anakua muogamuoga mpaka huelewi, kila kitu anahisi kugombezwa. Nikuambie kitu huyo mtoto si wa kuchapwa, acha kumpiga, narudia acha kumpiga kuna kiyu, mchukue hata kama ni kila siku jioni toka naye mbali na nyumbani, kaeni kuleni ICecream.

Fanya naye kitu ambcho anakipenda, sio kwa siku moja, hapana, kwa siku moja hutajua. Tumia muda mrefu kuongea naye, mope stori za maisha yako na mdadisia takuambia kitu. Acha kuwa mkali kwa wanao, acha hii mambo ya kuchapachapa na kusema mtoto wangu mimi mtundu! Hapana, ongea ina matokeo mazuri kuliko chapa. Mfanye mwanao kuwa rafiki atakuambia kila kitu ukimfanya adui basi utakuja kuambiwa kila kitu na majirani na hakitakufurahisha.

Nishamaliza sasa kama wewe unaona uko bize sana hata kumsikiliza mwanao huwezi endelea kutafuta pesa!

#SHARE Iddi Makengo
DONATE VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Your donation helps the Admin to be even more active in sharing quality blog templates. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni