DEREVA TAXI SEHEMU YA PILI (02)

DEREVA TAXI SEHEMU YA 2

Akaisogelea hadi ilipo hiyo gari kisha akatoa kifaa kidogo kwenye mfuko wake wa suruali na kukiweka juu ya paa la ile gari. Kifaa kile kikatoa miale ya mwanga mkali huku kikiwa kinazunguuka taratibu hadi kilipo maliza mzunguuko wake mmoja, kikazima kwa muda wa sekunde tatu kisha kikawaka taa ya kijani tupu. Akakichukua na kukizima akakirudisha mfukoni mwake. Akafungua mlango na kujiingiza ndani ya ile gari. Alikuwa na uhakika na usalama kwa asilimia kubwa sana kutokana na kuiskani ile gari kwa kifaa chake kile. Baada ya kuwa ndani ya ile gari, alitoa simu na kubonyeza tarakimu kadhaa na kuiweka sikioni.
"Nadhani umeniona.....fanya hima nataka kuondoka sasa," alisema na kukata simu ile. Kulikuwa na mtu ambaye hakuwa mbali na hapo na alimuweka kwa siri na ilikuwa ni makhsusi kabisa. Muda mfupi mbele, alionekana binti mrefu mwenye mavazi ya kisister duu akiwa anaisogelea ile gari kwa mwendo wa kilimbwende. Alikuwa ni mrefu kwenda juu, pua ya upanga, shingo ya Twiga na kifua kichanga, akiwa amevaa kijifulana kidogo juu alichokikunjia mikononi huku chuchu zake mkito zikiwa zinatikisika. Alifika kwenye gari ile kioo cha gari ile kikapandishwa juu.
"Vipi?" akahoji yule binti kwa sauti ya chini baada ya kuinama ili kuwa sawa na lile dirisha.
"Chukua hili begi dogo, sitakiwi kuwa na kitu chochote cha mawasiliano,"
"Usalama wako utakuwaje sasa?"
"Cat kumbuka mimi ni nani na nakutana na mangapi, Kitengo kimeshakubali kutenda kazi hii na pia si kwamba ni kazi ambayo kitengo kimechukua pesa kwa ajili ya kazi hii bali kazi hii ni kwa taifa pia,"
"Kazi gani hiyo Roi?" akauliza huyo binti akiwa katika wasiwasi .kubwa.
"Hakikisha unahifadhi sehemu salama kila kitu nilichokiacha," alisema Roi kisha akafunga kioo cha gari ni kama aliyoyauliza Cat hayakuwa na uzito, binti yuke mrembo akageuka na kuondoka. Wakati yale yakiwa yanafanyika, kule juu kwenye kile chumba alimoachwa Zubery, alikuwa akishuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea pale chini.
"Yeah! Hii ni bomba sana inatakiwa iwe kitaalamu zaidi," alijisemea huku akitabasamu lakini ghafula, aliweka umakini dirishani pale baada ya kumuona Kasa akiwa anagonga kioo cha gari ya Roi aliyekuwa ameanza kuliondoa gari taratibu.
"Kuna kompyuta kwenye dash bodi lakini usiiguse......zima gari kwanza," alisema kwa sauti ndogo sana Kasa akiwa pale dirishani mwa ile gari. Roi akazima gari na kumtazama huyo mzee usoni.
"mambo yakikuwia ugumu tuwasiline kwa hiyo simu na iwe kwa siri sana, kuna laini iko humo ndani utaitumia hiyo na utakapoipata hiyo bidhaa muhimu iliyobeba siri nzito kwa faida ya serikali, hakikisha hiyo simu unaiangamiza na isionekane," alisema Kasa lakini muda huo Zubery alikuwa akipiga picha kwa kutumia simu yake pale dirishani. Baada ya kuchukua zile picha akaondoka zake. Gari ya Roi ikaondoka nayo kwa mwendo wa taratibu kabisa kuingia barabara hii na ile hadi kuikamata barabara kuu iendayo kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani.

'Mauwaji ya kutisha yatokea huko jijini Arusha. Gari ndogo aina ya MARK II. Yenye namba za usajili T. 6171. Iliyokuwa ikitumika kama gari ya biashara almaarufu kama Taxi, yakutwa imetelekezwa kwenye barabara ya kutoka Moshi Arusha. Ndani ya gari hiyo kumekutwa watu wawili wakiwa wamepoteza maisha kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo mbalimbali ya miili yao. Na pia mauwaji kama hayo hayo na yenye kufanana na hayo kwa kila kitu, yatokea huko jijini Tanga maeneo ya barabara ya Pangani. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa matukio yote mawili ambayo yamehusishwa na gari hizo za kibiashara'

Ilikuwa ni taarifa fupi ya habari ya saa nne asubuhi iliyokuwa ikirushwa na chombo kimoja cha habari. Habari hii ilikuwa ya kushangaza sana na ya kutisha kwa ujumla wake, haikujulikana sababu ya ajali hizo wala chanzo chake. Kichwa kilimuuma sana mtu mmoja aliyekuwa akitazama hiyo ajali iliyokuwa ikitangazwa asubuhi hiyo. Kile kitendo cha watu waliokutwa garini humo wakiwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali, ndicho kilichokuwa kikimfikitisha kwa majira hayo. Alitazama kwa makini sana lakini hakuweza kung'amua kitu. Taxi zilizotumika zilikuwa zikifanana tofauti ilikuwa ni mistari iliyochorwa ubavuni na namba za usajili za gari hizo lakini kila kitu kilikuwa sawa. Hofu yake ni kuhusu gari zilizotumika, zilikuwa zikifanana na ya kwake. Nini hii? Akajiuliza lakini hakutaka kuipa nafasi sana hali hiyo ubongoni mwake. Alikuwa tayari ameshajifanyia usafi akatoka na kuingia barabarani na gari yake. Akiwa garini anapokea simu, simu hii ilimtaka afike Makorora kwa ajili ya kumfuata mtu huyo aliyempigia. Simu hiyo ilipokatika akaitazama ile namba vizuri, namba aliifahamu kwasababu aliihifadhi kwa jina la mteja mpya. Jana tu leo anataka nimfuate, nimpeleke wapi tena? akajiuliza. akakaza mwendo ili kuwahi kwani alikuwa na miadi na rafiki yake siku hiyo. Alifika Makorora mahali ambapo alitakiwa kumkuta huyo mteja wake akapaki gari na kusubiri. Muda si mrefu huyo jamaa alifika na kujifungulia mlango na kuingia.
"Tom habari yako ndugu yangu, za tangu jana?" alisalimia huyo kijana mara baada ya kuingia ndani humo. Tom akatulia kidogo kwa kabla ya kujibu kwani akilini mwake hakukumbuka kama alijitambulisha kwa jina lake mbele ya mteja huyo. Lile jina limeitwa kitaalamu sana na muitaji hakuonekana kubahatisha.
"Nzuri tu kaka.....!" akaamua kumpiga teke Chura hakuona haja ya kuumiza kichwa, aliamini ni mteja kama wateja wengine na i anawezekana alijitambulisha lakini kutokana na wingi wa uchovu, akili yake ikawa imekataa kuhifadhi kumbukumbu.
"Aaah! Kumbe sikujitambulisha kwa jina langu kaka?" akakatisha yule kijana kwa kudakia.
"ndiyo, hukuwahi kuniambia kwani ulikuwa na haraka sana jana kaka,"
"Hudah," akasema.
"Hudah?" akahoji Tom.
"Yaa, unatakiwa kuniita kwa jina hilo kaka na si vinginevyo," akajibu huyo kijana wa kuitwa Hudah.
"Wapi leo unataka nikupeleke?" akahoji Tom.
"Hivi hapa na Maramba ni kiasi gani Tom, nadhani kama nikitumia gari yako basi nitafika kwa wakati maana inakimbia sana na mashine yake inaonekana kuwa ni nzima sana,"
Hudah, Maramba ni mbali sana halafu ukizingatia jana nilikuwa safari, nimechoka sana na sitaweza kutoka nje ya hapa mjini kaka nisikudanganye," alijibu Tom.
"Ni kiasi gani kutoka hapa hadi maramba kwani?"
"shilingi Elfu arobaini kaka"
"Ohoo! Kumbe nitakuwa nimekupa na nyongeza kubwa sana rafiki yangu, tafadhali nipeleke maana ni muhimu sana na nitakupa kiasi cha shilingi laki moja na nusu," Kiasi hiki ni kikubwa sana kwa safari hiyo. Tom akashtuka moyoni lakini usoni alionekana wa kawaida, alipotazama kwenye kioo cha pale mbele kilichokuwa kikimuonesha abiria wake, akakutana na tabasamu kutoka kwa Hudah. Hili nalo likampa swali. Mbona kama yuko makini sana na ni kama ananiwekea mtego? Alijiuliza mawazoni Tom. Laki moja na nusu kwa safari ya shilingi Elfu arobaini tu? Akajiuliza tena. Ngoja huwe.....!
"Unajua ukarimu wa mtu na jinsi anavyomchukulia binadamu mwenzake, ndivyo huleta urafiki wa kweli na huongeza marafiki wapya kila kukicha. Kazi yako inaendana kabisa na jinsi ulivyo. Dereva Taxi anatakiwa awe ni mcheshi na mkarimu ili kuweza kumpa amani Abiria wake pindi asafiripo naye," aliongea Hudah huku ile sentensi ya Tom ikiwa inaning'inia hewani baada ya kuikatisha. Tom akapata wazo jipya na kumchukulia huyu jamaa ni wa kawaida sana na huwenda ni kwamba amependa huduma yake tu. Wakati akiwa njia panda asijue ni lipi afanye baina ya kuikubali hiyo safari au aikatae, simu yake ikaita. Akapokea.

"Lazima leo tufike Muheza mapema ili tuwahi kurudi," aliongea mtu huyo aliyepiga simu.
"Nimekuelewa Mudy niko njiani kwa sasa nakuja huko na kwakuwa tuko nje ya muda wewe jiandae nikukute uko fiti," alijibu Tom huku akiishusha simu yake na kumgeukia mteja wake akamwambia.
"Utanisamehe kaka, unajua bado sijaanza kazi rasmi toka nitoke safari na ndiyo maana kuna ratiba nyingi nilijipangia. Nakwenda nawe hadi Kituo bangi nadhani pale utapta gari ya kukupeleka huko, huwezi kukosa nina hakika,"
"Basi hakuna shaka nia na lengo ni kufika mapema tu," alijibu Hudah.
"Usiwe na shaka utafika mapema na utaifurahia safari pia," alijibu Tom huku akiingiza tena gari yake barabarani. Muda mfupi wakawa wamefika kituo Bangi. Tom akashuka na kuwacheki jamaa zake pale wakapeana sabahi na vicheko vya hapa na pale. Akamfuata kijana mmoja hivi na kumpa lile dili lakini wakati Tom anamaliza kutoa lile dili, Hudah akawa tayari ameshaongea biashara na kijana mwengine na kwa wakati huo alikuwa akimuaga Tom. Mh! Hili likamfanya kijana huyo ashtuke na kujiuliza mengi kichwani mwake. Inamaana ni mwenyeji huyu wa maeneo hayo. Yule kijana aliyepewa dili na Tom akapata kichwa kingine cha haraka.
"Mzee wa matukio usihali, nimepata kichwa tayari acha dogo akamate dili," aliongea yule kijana. Tom akalitazama gari linaloondoka na yule jamaa asiyemuelewa, anayetaka kupelekwa Maramba kwa pesa kubwa kiasi kile. Gari ilikuwa nyeupe isiyo na rangi mchanganyiko huku ikiwa na mstari wa blue ubavuni kuzunguka gari zima. Hakutaka kuwaza sana alichoamini labda amependa upya wa gari ile. Alichokifanya yeye ni kuwasha gari yake na kuondoka lile ene. Akampitia jamaa yake anayekwenda kwa jina la Mudy wakaianza safari ya kwenda huko Muheza.

*****
Siku hiyo hiyo Roi alikuwa barabarani akiwa kasi sana, mwendo wake ulikuwa ni mkali kiasi kwamba kila gari anayopitana nayo lazima watu wajiulize hiyo gari imebwa ama, maana ilikuwa kwenye mwendo mkali mno. Muda mfupi tu alikuwa ameshaingia muheza na kuingia kuume akawa kama anayetaka kuingia kituo cha mabasi cha wilaya hiyo, akanyoosha akaja kutokea Amtiko kisha kuchukua njia ya Bombani, Amani. Alipofika mbele baada ya kuuwacha uwanja wa mpira wa miguu wa Jitegemee, akaiacha hiyo barabara ya Amani akakamata ya Kicheba, Bamba hadi Maramba. Hii ilikuwa ni barabara ya changarawe. Haikuwa barabara nzuri sana na viongozi walionekana kama kuisahau barabara hiyo. Mwendo wake haukuwa wa kasi sana wala wa taratibu sana. Muda wote macho yake yalikuwa yametulia kwenye dira moja iliyokuwa ikimuonesha sehemu aendayo huku akiwa na ramani iliyokuwa ikimuongoza vema. Alipita Kicheba, Mabungu, manyoni. Wakati anaingia Misozwe, kunaujumbe ukaingia kwenye kile kifaa chake cha mawasiliano alichopewa. Akakichukua na kuangalia kuwa ni ujumbe gani, akakutana na maneno machache tu.
"Hakikisha hakuna maongezi zaidi ya kujitambulisha kama tulivyokuelekeza," ujumbe huo ukakoma. Roi akakitia kwenye mfuko wa shati kile kifaa kisha akaongeza mwendo maradufu.

**********
*********

SAHARE JUU YA JINGO refu la ghorofa kama sita ama saba, ndani ya chumba kimoja, anaonekana mtu mmoja akiwa karibu na dirisha akiwa amelipa mgongo dirisha hilo. Hakuwa akitazama nje, alikuwa amegeukia ndani lakini mgongo wake ukiwa umeelekea dirishani. Muda huo huo mtu huyo aliyepo hapo dirishani kwa mtindo huo, akapokea simu.
"Yuko misozwe kwa sasa,..... vipi kuhusu watu wetu watawahi?" mtu aliyempigia mtu huyo wa kwenye hicho chumba, aliuliza baada ya utangulizi usio salamu.
"watawahi," alijibu kifupi yule mtu wa mule ndani ya lile jingo ambaye ki umri hakuwa mtu mdogo kwani hata mgongo wake uliweka kiduva/kibiongo kidogo kuashiria mri ulimpiga mkono.
"Nini wanafanya wakifika kwa hiyo hazina?" akauliza mpigaji wa simu.
"Mzigo ni dili lakini pia hatuuhitaji," alijibu mtu yule wa kwenye lile jingo refu akiwa na maana ya kuwa wanaweza kuubeba mzigo kwa sababu ni dili lakini kama ikiwa ngumu kuubeba basi wanatakiwa kuuwa na ndiyo maana akajibu kwa namna ile.
"Ok, nitazidi kukupa taarifa na hatua za huyu mtu hadi mwisho wa safari," aliongea huyo mtu simuni kisha simu hiyo ikakatwa. Yule mtu pale kwenye dirsha, aliishusha simu yake na kuirudisha kwenye mfuko wa shati lake jeupe kisha akapiga hatua ndogondogo akiwa haonekani sura yake zaidi ya mgongo tu. Akafika kwenye meza kama ya kiofisi iliyopo hapo ndani akanyakua koti lake la suti na kulipachika begani kisha akachoropoka mule ndani. Alikuja kutokea nje ya jingo lile lakini hapa akiwa anaonekana miguu tu. Alikuwa amevaa viatu virefu vyeusi na suruali ya rangi ya ugoro ambayo haikurandana hata kidogo na vile viatu wala koti lake la suti ambalo hakulivaa kwa wakati huo bali alilitupia kwenye gari baada ya kufungua mlango kisha akajitumbukiza naye na kujifichwa kwenye gari ile ya vioo vy giza. Ni nani huyu asiyetaka kuionesha sura yake. Mashaka matupu.

Mwendo wao ulikuwa ni wa kawaida sana, walipiga domo hadi wakachoka sasa walikuwa kimya kabisa kilichokuwa kikisikika ni muungurumo wa injini ya gari pekee. 

ITAENDELEA.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : DEREVA TAXI SEHEMU YA PILI (02)
DEREVA TAXI SEHEMU YA PILI (02)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/dereva-taxi-sehemu-ya-pili.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/dereva-taxi-sehemu-ya-pili.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content