DEREVA TAXI SEHEMU YA KWANZA (01)

DEREVA TAXI SEHEMU YA 1

Sauti za Ng'ombe, kuku na kadhalika zilikuwa zikisika kutokea nje kidogo ya jiji la Tanga kwenye mji mdogo wa Pongwe. Wakati kelele za wanyama hao zikiwa zinaendelea. Gari moja ya rangi ya kibuluu ilionekana ikiingia kwenye mgahawa mmoja uliopo maeneo ya barabarani kabisa kisha ikasimama, akashuka kijana mmoja mwenye umbo la wastani, mtanashati lakini akionekana ni mtu wa mazoezi kwani mwili wake ulionekana uko vizuri kidogo na wenye kukubali mazoezi hayo kwa mtazamo tu ukimtazama. Akaingia kwenye mgahawa huo wa hapo barabarani kisha akakaa kwenye kiti kimoja kilichokuwa nyuma ya meza isiyokuwa na kitu chochote kile. Ulikuwa ni mgahawa wa kawaida sana. Wakati akiwa anasubiria kuulizwa ama kumuona muhudumu ili kumueleza hitaji alitakalo, simu yake ya kisasa kabisa aina ya Tecno H6 iliita, akaburuza kidole chake gumba kwenye kioo cha simu hiyo kisha akaitupia sikioni na kutulia kidogo kabla ya kujibu kile alichoulizwa na mtu aliyempigia.
"Ndiyo, niko njiani kwa sasa narudi lakini ni lazima nifike nyumbani kwanza nyumbani maana ni siku ya tatu sasa sijajua nyumbani kuna hali gani na si unajua bado ni Bachela kaka," akatulia tena, baada ya muda kidogo akasema tena.

"Aah! Hapana mimi kazi ni muda wowote, hata sasa nikipata kichwa napiga kama kawaida si unajua mjini hapa na hiyo ndiyo inayonifanya nanyakuwa kodi za nyumba kila baada ya miezi mitatu" akatulia tena lakini hapo akiwa amemzuia muhudumu ambaye alimtaka asubiri kwanza amalize kuongea na simu.
"Kesho asubuhi basi nitakuibukia unipe hilo dili maana nipo mkavu sana nimemaliza pesa yote, majukumu ya kifamilia na mimi kama kijana wa kiume sina budi kuubeba ubaba," akamaliza kisha akasema poa na kuishusha simu. Akamtazama yule muhudumu na kumuuliza kuna nini kwenye mgahawa ule. Akajibiwa kuwa ni wali nyama, maharagwe, ugali samaki lakini pia kuna ugali wa muhogo na makande pia yako tayari kama atahitaji. Kwa majibu hayo akatulia kwa muda kisha akaagiza aletewe ugali samaki kwani kama ni nyama huko kijijini alichinjiwa kuku siku ya kwanza na siku ya pili akaangushwa bata hivyo hana hamu tena na kitu kiitwacho nyama. Akaletewa na kuanza kula kwa haraka kidogo huku akiangalia saa yake, ilionekana ni mtu mwenye haraka sana. Alipomaliza alilipia pesa aliyotakiwa kulipa akachukua kombe la maji akamimina tumboni mwake akatoka humo mgahawani akiwa 'top'.

Tom. Yaa hakuwa mwingine huyo kijana bali ni kijana anaekwenda kwa jina la Tom. Wakati anatoka hapo mgahawani, akafuatwa na kijana mmoja aliyekuwa amevaa suti nyeusi iliyomkaa vizuri huku akiwa na Brifcas mkononi mwake.
"Kaka nilikuwa nakusubiria wewe hapa," alisema kijana huyo akiwa amesimama mbele ya Tom..
Ndiyo kaka nakusikiliza!" aliongea Tom akiwa anamtazama vizuri huyo kijana ambaye hakuwa akitabasamu sana.
"Nimekuona ukiingia hapa na bila shaka wewe ni dereva Taxi?" akaweka ulizo huyo kijana lakini kabla Tom hajajibu lolote, huyo kijana akaendelea.
"Naelekea Mjini maeneo ya Chumbageni sijui ni kiasi gani utanichaji?"
Mh! Akagumia Tom kwa ndani ya moyo akatafakari kwa kina kidogo kabla hajatoa jibu la kukubali au kukataa. Ni kweli alikuwa akielekea mjini hata yeye lakini hilo halikuwa sababu ya kusubiriwa. Kweli ni dereva Taxi lakini pale nje pana Taxi ngapi hadi asubiriwe yeye. Gari yake hakuipaki kwenye foleni ya Taxi, ameipaki kama msafiri tu aliyekwenda kupata huduma na kuendelea na safari yake. Huwenda likawa zali lakini hata hivyo alikuwa na njaa ya hela ukizingatia amekwenda kuzitoa sana huko kijijini. Pamoja na mawazo yote hayo kupita kichwani mwake lakini akakata shauri.
""Nitakufanyia shilingi elfu kumi kaka," alisema Tom.
"Kaka nilikataa hizo bei za Taxi nyingine maana hiyo ni bei ya kawaida kutoka hapa hadi mjini, nimeona wewe unaelekea mjini na ndiyo maana nikaona nikufuate maana itakuwa nafuu kidogo," akaongea yule kijana nadhifu. Tom akamtazama tena huyo mteja akajua hakuna shida sana kwakuwa anakwenda huko huko mjini haitakuwa na shaka sana akataka apewe Elfu nane jamaa akasema kuwa anashilingi elfu saba. Tom hakutaka maneno mengi sana akakubali. Wakaelekea mahali gari ilipo wakapakia na safari ya kuelekea mjini ikaanza.
**************
UPANDE MWINGINE mjini, mambo yalikuwa yanakwenda kama ilivyopangwa. Mji ulikuwa uko na mishemishe na pilikapilika za hapa na pale. Mpishano wa vyombo vya usafiri na waenda kwa miguu ulikuwa ni mkubwa sana. Ndani ya chumba kimoja kwenye jingo la shirika la nyumba la Taifa, (NHC). Hii ilikuwa ni ofisi moja ya siri sana ambayo ilikuwa ikifanya mambo yake kwa siri kubwa mno. Kunaonekana watu wawili wakiwa kwenye mavazi ya kawaida sana lakini ghali. Umri wao ulionekana kupiga hatua kidogo na kutaka kuwaacha. Mmoja wa wale wazee alinyanyua mkono wake uliobeba saa akatazama muda, alipoushusha akasema.

"Tunaweza kukawia ujue na hii inatakiwa iishe leo," aliongea akiwa anaendelea kupanga mafaili fulani kwenye shelfu dogo la vitabu.
"Hatuna sababu ya kukawia, huu muda ndiwo tunaopaswa kuutumia sasa," yule mwenzake akajibu huku akiwa amesimama wima. Yule mzee wa kwanza akalitupia kabatini faili lililobakia mikononi kisha akalifunga kwa kufuli kabisa kisha akasimama na kutoka mule sebuleni akisema.
"Dakika tano nitatumia, tukutane Bandari Holi," baada ya kusema yale, huyu wa pili hakujibu kitu bali alitoka akafika kwenye sehemu ya kazi ya katibu muhtasi akamuachia maagizo ya msingi kisha akatoka nje kabisa ya jingo lile. Aliingia ndani ya gari moja ndogo nyeupe akachukua koti la suti alilokuwa amelitundika nyuma ya kiti cha dereva akalitia mwilini kisha akakaa vema na kukamata usukani barabara. Dakika tano mbele ziliwakutanisha tena ndani ya Bandari holl kama ambavyo walikubaliana mwanzo. Ila hapa yule mzee wa kwanza alikuwa amevaa mavazi tofati kidogo. Alikuwa amepiga suti za rangi ya kijivu tupu na moka safi za bei ya juu mno. Waliingia hadi ndani ambako kulikuwa na ukumbi mkubwa wa mikutano. Ukumbi ulikuwa mtupu sana kulikuwa na viti tu ambavyo havikukaliwa na kiumbe wa aina yeyote. Hawakushtushwa na jambo hilo hata kidogo walichokifanya ni kupitiliza hadi kwenye mlango mmoja uliopo kwenye kona ya ukumbi ule. Yule mzee wa kwanza akafungua mlango na kuingia akifuatiwa na yule wa pili ambaye hakuwa amebadilisha mavazi yake. Ndani ya chumba kile kidogo ambacho kilikuwa kimesheheni vitu vingi vya kiofisi na viti vya gharama vilivyozunguukwa na meza kubwa sana ya umbo la Yai. Kulikuwa na watu wawili tu mule ndani, hawa walikuwa ni watu wa makamo hawakuwa wazee wala vijana. Ofisi hii waliitumia kwa nadra sana na ilikuwepo kwa vikao muhimu na maalumu.

"Hadi sasa hajafika huyu kijana?" aliuliza yule mzee wa kwanza huku akichukua nafasi yake.
"Bado hajafika," alijibu mtu mmoja kati ya wale waliokutwa pale.
"Tulidhani sisi ndiyo tumechelewa," aliongea yule mzee wa pili naye akiwa tayari amekaa kwenye nafasi yake. Kabla jibu lolote halijatoka, mlango wa kile chumba ukafunguka, kijana mrefu kidogo mwenye mwili ulionawiri kimazoezi akiwa amevaa sarawili nyeusi ya kitambaa huku akiwa amevaa shati la rangi ya maziwa lililochomekewa vema huku akiwa amevaa mchongoko wa maana wa rangi ya sarawili yake. Aliurudisha ule mlango lakini kabla hajapiga hatua hata moja, sauti ya kumtaka aufunge kwa komeo kabisa ule mlango ikamkuta palepale. Akaufunga kama alivyoelekezwa na kuja kuchukua nafasi yake.
Shikamoni wazee wangu na wale wakulingana nami habari zenu?" akasalimia namna hiyo.
"Tunapaswa kuitikia wote marahaba hakuna wa kulingana naye hapa," akajibu mtu wa pili kati ya wale waliokutwa mule ndani. Yule kijana akatabasamu huku akiwatazama vema wale watu na kutulia kwa muda na ukimya nao ukachukua nafasi. Mzee yule wa kwanza akatoa mawani yake ya macho na kuiweka machoni kisha akavunja ule ukimya kwa kujikohoza kidogo kisha akasema.
"Tuko nje ya muda na safari ni hatua," akaweka kituo kidogo halafu akaendelea tena baada ya kuyazunguusha macho yake kwa kificho kidogo.
"Roi!" Akaita kisha akasema.
"Umekuja kwetu moja kwa moja na ofisi yako nzima iko hapa. Utashangaa najua kwanini uko hapa lakini huo mshangao usiupe nafasi kabisa kwani umekuja hapa kwa jambo la msingi sana na linatakiwa likamilike kesho na tuwe tumepata majibu ya kujua nini tunapaswa kufanya. Unasafari ambayo mwanzo wake ni leo hii, muda wowote baada ya kikao hiki kuisha. Unatakiwa uende Kauzeni, huu ni mji ambao uko katikati ya Mhinduro na Maramba pia ni njia panda ya kwenda huko milimani Churwa hadi Kuze Kibago," alisema yule mzee kisha akatoa ramani moja iliyopo kwenye karatasi na kuiweka mezani.
"Zamani huu mji ulikuwa maarufu sana kwani hapa palikuwa na Kiwanda cha utengenezaji kamba za mkonge almaarufu kama 'Korona' kwa wakazi wa mji huo. Utapitia muheza halafu ukifika muheza utakamata barabara inayokuja Hospitali ya Mtakatifu Augustino (Hospitali ya Teule). Utanyoosha na hii barabara kama unavyoiona hapa kwenye ramani kisha unaiacha hii inayokwenda amani wewe utaingia kuume. Hii ndiyo itakayokufikisha huko unakotakiwa uende," alipomaliza kusema hayo akaigamia kiti na kuwatazama wajumbe wote waliomo mule ndani. Roi aliyekuwa makini kuitazama ile ramani akanyanyua sura yake na kumtazama yule mzee aliyekuwa anatoa maelekezo. Yule mzee akamtazama yule kijana kisha akashusha mawani yake mezani baada ya kuiangua kutoka surani mwake. Akendelea.
"Kuna bidhaa muhimu sana imehifadhiwa hapa Roi. Bidhaa hiyo inatakiwa ifike hapa ikiwa hai hata kama itapata madhara lakini iwe hai tu. Mtu huyu amebeba siri nzito na muhimu sana hivyo kama akifa basi tutakuwa tumepoteza na hatutajua la kufanya. Ni mzee sana huyo anafahamika kwa jina moja tu la herufi za siri. 'T.D' Hilo ndilo jina lake, ni siri sana," akatulia yule mzee na kujilaza kitini mwake akawa ananesanesa huku akiwa anamtazama Roi usoni. Roi muda wote huo alikuwa kimya tu akifuatilia ule mpango.
"Gari yako utaiacha hapa na ukitoka hapa utaingia kwenye gari tuliyokuandalia sisi, hatuta wasiliana nawe kwa simu wala nini bali tutawasiliana kwa jumbe fupi ya maneno na hutatakiwa ujibu ujumbe wa aina yoyote ile bali sisi ndiyo tutakaokutumia na ni kwa ajili ya muongozo na si kitu kingine," maelezo haya yalitoka kwa yule mzee wa pili. Alipokwisha kusema hayo akafungua mkoba wake uliopo juu ya meza ile ya Yai, akatoa kifaa kidogo sana mfano wa simu ya Nokia ya tochi ile ya kizamani almaarufu kama jeneza halafu akamsogezea Roi na kuiweka juu ya ile ramani.
"Jina langu ni Kichambua," akajitambulisha baada ya kuweka kile kifaa mezani.
"Naitwa Kasa," yule mzee wa kwanza akadakia kisha na wale wengine nao kujitambulisha. yule wa kwanza aliitwa Zubery na mwengine alikuwa ni Ezekiel Charless. Utambulisho wao ulikuwa wa kinamna namna sana lakini haikustaajabisha kwa mtu kama Roi.
Unachotakiwa kukumbuka ni umakini tu, tumeingia makubaliano muhimu sana na kitengo chako cha kuhakikisha tunaipata hiyo bidhaa ikiwa hai na kama itapotea ni wazi unapaswa kuitafuta kwa gharama zozote zile na tunachokihitaji kwa bidhaa hiyo kipatikane," akaongea yule mzee aliyejitambulisha kama Kichambua.
"Unaweza kupoteza maisha maana sina imani na usalama kabisa japo kila kitu kinafanyika kwa siri sana," akadakia Kasa. Roi akageuka kumtazama Kasa lakini Zubery naye akachomekea.
"Dili husakwa na wengi, Roi akagandisha macho usoni kwa huyu Zubery kwani maneno yake ni machache lakini yalikuwa na uzito fulani. Huyu mwingine kama si kujitambulisha jina lake inamaana asingeongea kabisa. Roi huyu hakumshughulisha sana. Akawatazama wote kila mmoja kisha akauliza kama kila kitu kiko sawa.
"Kila kitu kiko sawa unachotakiwa kwa sasa ni kukiwasha hicho kifaa," akasema Kasa ambaye ndiye aliyekuwa ni mzeee kuliko wengine wote pale. Roi akakusanya kila kitu alichotakiwa kukusanya akatia mfukoni akapiga hatua moja na kutaka kuondoka.
"Simu na vitu vyote vya kimawasiliano unatakiwa uviache hapa," akasema Zubery huku akiwa na lile lile tabasamu. Roi akageuka na kumtazama yule jamaa kwa muda kisha akasema kwa kukereka kidogo.
"Sijatoka mtaani na kuja hapa, nina akili na najitambua, vitu vyangu vya msingi vitakuja kuchukuliwa na mtu hapo nje, siwezi kuviacha hapa boy," alisema hivyo kisha akafungua mlango na kutoka mule ndani. Kasa na Kichambua nao wakatoka akifuatiwa na Ezekiel lakini Zebery hakutoka alisimama na kusogea dirishani na kutazama chini ambako kulikuwa na maegesho ya magari. Roi alibonyeza kinobu kidodo sana kwenye ufunguo wa gari aliyopewa, gari moja mpya kabisa ya rangi nyekundu ikalia kengele. Akaisogelea hadi ilipo hiyo gari kisha akatoa kifaa kidogo kwenye mfuko wake wa suruali na kukiweka juu ya paa la ile gari. Kifaa kile kikatoa miale ya mwanga mkali huku kikiwa kinazunguuka taratibu hadi kilipo maliza mzunguuko wake mmoja, kikazima kwa muda wa sekunde tatu kisha kikawaka taa ya kijani tupu. 

ITAENDELEA.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : DEREVA TAXI SEHEMU YA KWANZA (01)
DEREVA TAXI SEHEMU YA KWANZA (01)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/dereva-taxi-sehemu-ya-kwanza.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/dereva-taxi-sehemu-ya-kwanza.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content