DEREVA TAXI SEHEMU YA KUMI NA TANO (15)

TAXI DRIVER SEHEMU YA 15
Saa 8:00 usiku

Mh! Akagumia kasha akavuta hatua na kutoka eneo hilo. Alichokiona ndicho alichokikusudia kukiona sasa kazi ilikuwa ni moja tu ya kujua Hudah ni nani na kwanini anamhusisha na mauaji yanayoibuka kila mawio na machweo.

Usiku wa saa tano kama na nusu hivi, ulimkuta Hudah na wale jamaa kwenye gari ndogo wakielekea maeneo ya bandarini. Jamaa hao walikuwa ni wale waliomuibukia mkurugenzi wa ofisi ya upakuzi na upakiaji mizigo siku ile na kuacha bahasha na maagizo baada ya kumkosa muhusika. Leo wapo pamoja na hudah na safari ikiwa ni moja. Walipofika kwenye jingo la bandari, waliteremka kutokea garini humo na kupiga hatua ndogondogo kuingia bandarini. Punde gari nyingine nyeusi yenye vioo vya kutoruhusu wa nje kuona ndani iliingia mahala hapo na kuegesha mahala pa kuegeshea magari na ilikuwa ni pembeni kidogo mwa gari waliofika nayo akina Hudah. Waliteremka wazee watatu, mmoja akiwa amevaa kofia kubwa ya pama na mawani ya macho huku akiwa amevaa suti ya rangi nyeusi na hao wengine wakiwa wamevaa suti za rangi tofauti kila mmoja na rangi yake. Mmoja alivaa ya rangi ya kijivu na mwingine akiwa na ya rangi ya ugoro. Wakaelekea kule ambako akina Hudah wameelekea. Walipofika ndani kabisa ya Bandari, wakawa wameongezeka yaani si sita kama walivyoonekana bali kuliongezeka mtu mmoja naye ni Gambe. Waliongozana pamoja kwa siri kubwa huku wakipita upenuni mwa makontena mbalimbali wakijitahidi kukwepa mwangaza wa taa zilizokuwa zikipiga eneo hilo. Safari yao ikaishia kwenye Kontena moja lililochorwa mistari ya kibuluu ubavuni. Gambe akalisogelea na kulifungua mahali na mlango mdogo wa kufojiwa ukafunguka. Giza lilikuwa zito ndani ya Kontena lile, Hudah pamoja na Gambe wakatoa kurunzi ndogo zenye mwanga mwembamba wakaingia ndani ya lile Kontena nyuma wakifuatiwa na wale wazee huku wale watu wawili wa kukata mwili wakisubiri nje ya Kontena lile kwa lengo la kusimamia usalama.

"Mali ipo vizuri na bado ina ng'ara," aliongea Hudah mara baada ya kumulika mahali na kuona boksi la wazi lililokuwa limesheheni silaha za aina mbalimbali lakini kukiwa na maboksi mengine ya kufanana na hilo yakiwa yamefungwa. "Natumai kwa hili ni kusubiri tu tusikie nini wataamua kwani tayari zana za kutosha zipo na kwa hili hatuna wasiwasi," Aliongea Mzee Hasheem huku akitoka ndani ya lile Kontena na Hudah akilifunga lile boksi. "Utaendelea kulitunza hapa kwako siku zote na sisi tutaendelea kukulipa hadi misheni yetu itakapokwenda kukamilika," Aliongea Hasheem akimtazama Gambe usoni. "Ni kwa muda gani sasa mzee maana uvamizi haukawii kutokea hapa wa viongozi na kutaka kufanya ukaguzi wa Kontena zote, huoni kama yaweza kuwa hatari?" Akaonesha wasiwasi wake Gambe. "Hawataweza kulitilia shaka Kontena chakavu kama hili," alijibu lakini pamoja na kujibu mzee Hasheem akamsogelea zaidi bwana huyo na kumwambia kuwa asiwe na shaka na kikubwa kinachotakiwa ni yeye kuwa makini kama ambavyo alikubali kuwa hivyo, hakuna jambo ambalo linaweza kuzungumzwa halafu wao wasijue. Bado Gambe alikuwa na wasiwasi mkubwa sana juu ya uhifadhi wa silaha hizo na hili hata yeye binafsi lilimkosesha raha kiasi muda wote anakuwa makini na matamshi yake hasa awapo sehemu za ulabu. "Kikubwa ni pesa ambazo zitakuwa zikiingia kwenye mifuko yako kila wiki kwa ajili ya ulinzi huu, tambua tu gharama tunazozitumia ni kwa ajili ya kulinda mali zetu, sasa endapo kama kutatokea uzembe wowote ule, kifo kitaishi nawe," Alisema Hasheem kasha akaondoka hapo kwa mwendo wa haraka huku wale wengine wakimfuata kwa nyuma. "Amesemaje huyu? Ebo! Yaani mimi nitakufa! Asinitishe bwana huyu mzee. Akafanya kofia lile kama kaahidiwa wokovu wa milele!" Aliongea kwa kupayuka Gambe mara baada ya kuambiwa maneno yale. Ni kweli atakufa akileta uzembe na wala si uwongo, watu hao walikuwa hawana mzaha hata kidogo kwenye kazi yao. "Lakini kweli hebu ngoja niwe makini zaidi bado napenda kuishi na pesa zao pia ninazihitaji kwa kiasi kikubwa sana. Lakini yule mzee sijui kama atakuwa ni timamu, maongezi yake ni kama mgeni aliyekaribishwa Pepeta za Pemba na ikiwa hajui kuzila," Akasema kasha akapiga kite cha huzuni na kutikisa kichwa na kuufanya mdomo wake alioulegeza utikisike kama Tanga la Mashua. Akaondoka hapo kwa mwendo wa kujisukuma na kupotelea gizani.

Unaweza usijue unachokifanya lakini unayoyafanya yakawa na maintiki makubwa sana kwa jamii yako na kuleta mambo yenye kufurahisha. Maisha aishio mwanadamu wa leo ni maisha magumu sana yaliyotawaliwa na mambo mengi yenye kukatisha tamaa, mabaya yanatokea na kuwaumiza wengi na wengi huishi na mabaya hayo bila kujua wanatakiwa kufanya nini ili kuondokana na mabaya hayo. Kila mmoja na kilio chake na kila anayelia au kukutwa na kilio hicho huona chake kina nafuu kuliko kilichompata mwenzake. Watu wanaishi kwa mazoea na mazoea hayo yanapobadilika huwa ni fimbo mbaya yenye kuadhibu maisha yake kwa ujumla. Wengine wanaamua kutoka kwenye maisha yao ya awali na kuingia kwenye maisha mengine kutokana na kuona kule walikokuwako mwanzo hakukuwa kuzuri kwao lakini inapofikia wakati akayazoea maisha haya mapya aliyoamua kuishi, huja jambo moja pekee ambalo ni kusahau mapito. Haijalishi mtu huyu atayasahau kwa namna gani mapito yake aliyoyapitia lakini nd'o tayari yameshakuwa mapito na hatokaa na kukumbuka tena. Maisha hayo mapya yanampa faraja ya kuona kumbe ni bora aishi hivyo kuliko vile alivyokuwa akiishi mwanzo. Hata kama hayuko huru wakati mwingine lakini ilhali maisha hayo yameridhiwa na nafsi yake basi huwa ni yenye kuwa bora kwake...

Unapatwa na jambo baya ambalo linaweza kukupa uchungu mkubwa pengine likapelekea kubadilisha mfumo mzima wa maisha yako kwa mara nyingine. Hii huwa mbaya zaidi. Nani anaweza kuwa mshauri wako tena kama unapoishi tu kulikuwa hakuna hata jirani uliyekuwa ukimtegemea au mkitegemeana kwa kupeana mahitaji madogo madogo. Unaona jinsi ambavyo maisha yako yatakavyokuwa magumu, unaona jinsi utakavyorudi nyuma kwa kasi na ukiwa hukutaka tena kurudi huko.

Moniela Jaffar alimaarufu Moni. Binti huyu alikuwa ni mtu mwenye roho ya kutenda unyama kipindi hicho cha nyuma na alikuwa akiishi maisha ya kutegemea kupewa kazi za hatari au hata kumwaga damu ya mtu ilimradi mkono wake uende kinywani. Maisha yake yalikuwa yakitegemea kulipwa ujira mkubwa na matajiri wenye kuutumia utajiri wao vibaya. Akawa anaishi hivyo, akawa analisukuma gurudumu la maisha yake kwa namna hiyo. Balaa likaibuka baada ya kujua kuwa aliko si sahihi na hiyo ikiwa ni baada ya kuona alikuwa akiwakumbatia wahalifu huku akienda kinyume na serikali yake. Akamwaga manyanga chini na kuchoma mikoba kasha akanawa mikono na kuwa kinyume na wale aliokuwa akiwatumikia na kuhamia upande wa pili wa sarafu. Hili likawa ni jambo baya kwake, akakutana na shambulio kubwa lililotaka kuondoka na maisha yake, shambulio la bomu akiwa ndani ya nyumba yake na alipojaribu kutoroka pia shambulio hilo likamfuata hukohuko barabarani na kujikuta akiwa kwenye wakati mgumu sana ndani ya gari aliyokuwa akiitumia kutorokea mara baada ya kuishinda mitihani ya awali ya kifo baada ya kuokolewa na babu asiye mjua. Na hiyo ni baada ya kukutana uso kwa uso na Roli la mizigo. Hapo akashindwa kuelewa alitokaje garini na asijue nini kiliendelea hadi pale alipokuja kujikuta mikononi mwa babu huyo tena ambaye alikuja kujitambulisha kwake kama Master Dao. 

Hili ndilo lilikuwa tegemezi lake lakini angalia. Tegemezi lake la pekee lililokuwa likimpa matumaini ya kuishi kwa amani siku moja limeondoka tena kwa kifo cha kupigwa risasi. Nani ni taa yake tena kwenye maisha yake haya. Hili anaona kwa macho yake mawili likimrudisha kule ambako hakupenda kurudi. Apizo lake moyoni kuwa atarudi kwa ajili ya Master Dao, likawa linaishi na sasa yuko katika harakati hizo. Mbali ya yote hayo bado alikuwa akipingana na akili yake juu ya mtu mmoja tu ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake na huyu ndiye aliyemfanya kuwageuka watu waliokuwa wakimtumia vibaya na hatimaye kukutwa na masaibu hayo. Hakuwahi kumuona wala kuipata historia yake, mbaya zaidi hakuupata muda wa kumuuliza mtu aliyekuwa akiishi naye kuhusiana na mtu huyo. Akaamini pengine alikumbwa na makubwa kuliko yaliyomkumba yeye na kupoteza maisha. Picha ya mtu aliyekuja na kuondoka na mwili wa Dao siku ile ya tukio wakati yeye akikimbia mikono ya watu aliohisi wamemzidi nguvu, ikawa inajirudia kichwani mwake na muda mwingine kujiuliza mwenyewe ni nani mtu yule? Swali hili likawa linazidi kuutesa moyo wake. Kwa mbali alimuona japo alivaa maski usoni mwake lakini alimfananisha na Roi kwa asilimia kubwa sana japo ilipita miaka mingi tangu kuachana kwao na mabadiliko ni makubwa pia lakini aliamini fika alikuwa ni yeye hadi kupelekea kujiahidi kuwa siku moja atakutana naye. macho yake aliyakumbuka hata kama sura ile ilijificha kwenye maski nyeusi. Akili yake ilikuwa ikimwambia kuwa yule alikuwa ni Roi japo hakujipa imani moja kwa moja.

Huyu ndiye alikuwa Moni wa CHAGUO SAHIHI. Mbele yake kulikuwa na bunduki fupi ya 'Short gun' na kasha kubwa lililosheheni risasi pia pembeni mwa hiyo Short gun kulikuwa na bastola ndogo ambayo ilikuwa imemezeshwa risasi tayari. Muda nd'o huu na yule kijana ndiye atakayenipa mwanga. Akawaza kasha akatoa kibebea rasasi kwenye bunduki ya Short gun na kushindilia risasi, iliposhiba akakirudisha na kuvunja kwa nguvu na kuinyanyua juu kasha akafumba jicho moja na kuwa kama anayelenga mahali. 

"Ulinikomaza wewe kwenye tasnia hii ya silaha ambayo sikuwa mweledi nayo. ukanifunza mapigano kama binti yako au mjukuu wako ukiamini kipo kipindi kama hiki nitakachotakiwa kujua ni kwanini walikuficha kule na kwanini hawakuwa wamekupa ulinzi wa kutosha kama kweli ulikuwa una kitu muhimu kwa serikali na mwisho ni kuwatafuta waliokutenda mabaya. Dao! Asante sana mzee wangu," Alijisemea kwa sauti ndogo huku akiizungusha ile silaha ndani mule akiwa bado amebana jicho lake moja. Akanyanyuka na kuacha kila kitu pale mezani na kujiingiza chumbani aliporudi, alikuwa na begi la kubeba mgongoni mikononi mwake. Akapaki kila kitu kwenye begi lile kasha bastola ile akaifutika kiunoni mwake na kujiweka sawa, akatazama muda kwenye saa ya ukutani, ilikuwa ni saa 09:06. Akatoka moja kwa moja hadi barabarani akiwa makini kuangalia pikipiki yoyote inayopita. Muda mfupi mbele alikuwa makorola akiwa anaelekea mjini kupitia barabara ya Mabanda ya papa. Alipotupa jicho lake pembeni, akamuona Tom akiwa anaingia garini mwake akiwa mwenyewe. "Tafadhali simama pembeni kidogo mwa barabara hadi hiyo Taxi ipite," Alimwambia dereva wa bodaboda Moni, dereva huyo akatii. Muda mfupi gari ya Tom ikapita akaruhusu na gari moja ipite ndipo akaamuru gari hiyo ifuatiliwe hadi inapokwenda. Tom alipofika kwenye mzunguuko wa barabra ya Mabanda ya papa, akaingia kwenye barabara ya kuja Komesho kasha akakunja kuume mara baada ya mwendo mfupi kasha akaiingiza gari yake ndani ya Soko la Mgandini. Alipofika mahali akasimama na kushuka, Moni naye akasimamisha ile pikipiki na kumtaka kijana huyo wa bodaboda kutulia.

"Dada vipi unataka kufumania nini?" Aliuliza swali dereva huyo wa bodaboda. "Aah! Wanaume nyinyi baba yenu mmoja," Akajibu Moni huku akiwa makini kufuatilia nyendo zote za dereva Taxi huyo. Tom akaingia ndani ya soko, Moni akamfuata na kumkaribia kabisa akafanikiwa kunasa maongezi ya kijana huyo. "Ni shilingi Elfu arobaini tu kwa wewe mwenyewe na mzigo huo," Aliongea Tom. "Aah! Tom umekuwa kama hunijui bwana, mimi nitakupa shilingi elfu thelathini bwana, wewe ni ndugu yangu na si kama sikuona gari nyingine bali sikutaka mzigo huu kuupakiza kwenye daladala kwa sababu ya uangalizi wa hali ya juu na ndiyo maana nikatafuta gari ya namna hii, sasa wewe unataka faida yote kuimalizia kwako," Akalalama mtu huyo. "Sasa sikia Mufti, wewe ni mtu mkubwa bwana na unaheshimika, toa elfu thelathini na tano tuondoe mzizi wa fitina, shilingi elfu kumi yote naenda kuinunulia mafuta, mimi acha nife njaa na familia yangu pata wewe uzidi kuinawirisha midevu yako hiyo,"
"Ahah hah hah haaa! Sasa hiyo kufuru Tom Wallah! Hapo mnamkosea Mungu yaani elfu ishirini na tano inayobaki pia wafa njaa, acha kamba bwana. chukua thelathini hii hapa, hii tano wacha nikanywe chai," Alisema huyo mtu mwenye midevu mingi myeusi. "Lete bwana Mufti mbona mgumu wewe kama ngozi ya Nyegere, hebu cheki hiyo midevu ilivyo nawiri waweza sema mahujaji wa huko Makka lakini bado tu wasema huna hela? Aaah!" Akasema Tom huku akiichukua na hiyo elfu tano kasha akamsaidia furushi lake kuliingiza ndani ya gari na yeye mwenyewe kuingia na safari ikaanza. "Muheza si ndiyo umesema?" Akauliza Tom akiwa anafunga kioo cha gari yake lakini maneno yake yalishamkuta Moni mapema sana. Moni alielekea hadi kwa yule dereva wa bodaboda na kumlipa ujira wake na kumshukuru kasha akajichomeka kwa watu na kutokea kwenye Taxi nyingine akaingia ndani. "Nataka uifuatilie hiyo Taxi hadi inapokwenda," Alisema Moni akiwa anaisontea kidole gari iliyopita mbele yake. "Kwani inakwenda wapi hiyo dada yangu?" Akauliza kijana wa gari hiyo huku akiwa ameifungia tela. "Muheza," akajibu kifupi Moni na kutulia, walipofika barabarani akamtaka kijana huyo awe ametanguliwa na gari mbili kabla ya anayo ifuatilia. "Thelathini unayo dada?" Akauliza kijana huyo. "Ungetaka atobaini ingenishinda lakini hiyo hakuna shaka," akajibu Moni. Saa moja na dakika thelathini na tano mbele wakawa maeneo ya Mvuleni, gari aliyokuwa akiendesha Tom ikapunguza kasi kidogo na kusogea mbele kasha ikakunja kulia kuingia kituo kikubwa cha mabasi wilayani hapo lakini hakuingia kituoni hapo bali alinyoosha kuingia ndani ya mji huo. Dereva wa Moni alizidi kufuata bila kusema kitu yeye kazi yake kuu ilikuwa ni kufuata kile anachoamriwa na mteja wake. "Fuata hukohuko naona amepunguza kasi bila shaka anakaribia kufika," alisema Moni baada ya gari ya Tom kuingia Amtico na kuchukua barabara iliyokuwa ikielekea Amani lakini baada ya mwendo mfupi mbele, ikaiacha barabara ya Amani na kuchukua ile inayokwenda kwenye Hospitali ya wilaya hiyo, 

ITAENDELEA

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : DEREVA TAXI SEHEMU YA KUMI NA TANO (15)
DEREVA TAXI SEHEMU YA KUMI NA TANO (15)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/dereva-taxi-sehemu-ya-kumi-na-tano-15.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/dereva-taxi-sehemu-ya-kumi-na-tano-15.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content