Featured Post

ALINIKUTA MZIMA, AKANIHARIBU NA KUNIACHA KWA KUNIDHALILISHA!

WANAUME HAWA JAMAN CHAAA MI NIMESOMA NIKAONA NIILETE NA HUKU 

YAMENIKUTA; ALINIKUTA MZIMA, AKANIHARIBU NA KUNIACHA KWA KUNIDHALILISHA!

Sikuwahi kufikiria kuwa naweza kufanya kitu kama hicho, mume wangu aliponiambia kwa mara ya kwanza kufanya mapenzi kinyume na maumbile nilijua kama ananitania. Nilihisi kama ananichora na alikua ananipima kama ninafanya hayo mambo na wanaume wengine au la. Niling’aka na kumuambia hapana, mimi siwezi kufanya kitu kama hicho. “Lakini mke wangu mimi nimeshazoea, nimeteseka kwa muda mrefu, nimekua nikichepuka na Malaya lakini naona nitakuja kukuletea magonjwa, mimi siwezi kabisa kuvumilia, nakupenda mke wangu na sitaki kuendelea tena kukusaliti.”

Aliongea huku akitoa machozi, mimi nilimkataiakatalaka, alikasirika na kugeukia upande mwingine, hatukugusana mpaka asubuhi. Tangu siku hiyo tulianza kuwa kama maadui, alianza kuwa mtu wa kuchelewa nyumbani, kisirani kila siku na tukawa tunagombana sana. Niliumia sana na ile hali nikitamani hali ya zamani kujirudia, nilitamani awe mwanaume niliyekutana naye kipindi hicho tunapenda sana hana hayo mambo lakini haikua hivyo. Sikua tayari kumpa mapenzi kinyume na maumbile, nikifikiria madhara yake nilishindwa kabisa kukubaliana na hilo.

Alikaa kama mwezi hivi bila kuniambia chochote, siku moja wakati tunafanya mapenzi aliniandaa vizuri, aliniandaa kuliko kawaida yake, nililegea mwili mzima na alifanya mapenzi na mimi kwa ufundi kuliko maelezo. Lakini hakuweza kufika, alikaa kifuani kwangu kama dakika 30 hivi bila yeye kukojoa, nilipata raha lakini nilianza kuchoka, ghafla nikiwa sina hili wala lile mume wangu alinibania chini, alinishika vizuri kisha akabadilisha njia na kuniingilia kinyume na maumbile, nilijaribu kujitoa kwake lakini haikuwezekana, alikua na nguvu sana, alinizidi nguvu na alifanya mpaka akamaliza.

Niliumia sana siku hiyo, mwili ulikua unawake moto, michubuko ya kutosha na nafsi iliumia. Asubuhi aliniomba msamaha akilia, alinimbia kuwa kashindwa kuvumilia na hajui nini chakufanya. Alilia sana lakini nilishindwa kabisa kumsamehe. Niliondoka na kwenda nyumbani, nilienda kumuona dada yangu ambaye alikua likizi kwa Mama, yeye alikua ni kama rafiki yangu, nilimuambia kila kitu, lakini tofauti na mategemeo yangu alinipa jibu ambalo lilizidi kunichanganya.

“Mdogo wangu shukuru mume wako anakuambia, ukiona hivyo basi jua kuwa anataka kuacha lakini hawezi. Wewe kama mke ndiyo unatakiwa kusaidia mume wako kuacha, wanaume hawa hata usipo wapa wewe wanaenda kwingine huko an atakuletea maradhi. Minajili yeye anapenda na amekuambia basi fanyeni kwa kipimo, si kila siku mimi mwenyewe na shemeji yako tunafanya kwa hamu, hakuna mwanamke ambaye hafanyi siku hizi, changamka mdogo wangu ukiona watu wanapendeza kwenye ndoa jua kuna mambo huko!”

Dada aliniambia, nilijikuta naishiwa pozi, nilirudi nyumbani kwa mume wangu kutulia, sikumuambia kuwa nimekubali kufanya, ingawa maneno ya dada yangi yalishaniingia lakini nilinyamaza kimya nikajifanya bado nimekasirika. Mume wangu alizidisha mapenzi, akaacha pombe na kuwa mtu wa kuwahi kurudi nyumbani. Tulianza kuw ana furaha, usiku mmoja wiki moja baadaye wakati tunafanya mapenzi aliniambia. “Mke wangu sitaki nikulazimishie, mimi nakupenda naomba tujaribu tena kama hutapenda basi nitaacha sitakusumbua tena.”

Nilikubali kishingo upande nikitaka kujifunza na kujua ladha yake, nilishaanza kuwaza kwanini anapenda kuna tofauti gani. Tofauti na siku ya kwanza ambayo ilikua ni kilazima laizma sasa alifanya na mimi kwa mahaba, aliniandaa vizuri, alinifanyia kila kitu kwa ustadi na kweli nilipenda. Mpaka tunamaliza niliifurahi na tangu siku hiyo ndiyo ukawa mchezo wetu, wakati mwanzo nilisema nitafanya mara moja moja lakini nilijikuta naoze na napenda, ikawa tunafanya karibu kila siku, nilizoea kiasi kwamba njia ya kawaida niliona kama napoteza muda tu.

Maisha yaliendelea na nilikua nafurahia ndoa, nilipata mtoto wa pili kwa njia ya upasuaji kwani nilihofia kuumbuka. Nakumbuka siku ambayo siwezi kuisahau kulikua na sherehe nyumbani kwa mume wangu, ilikua ni ubatizo wa mtoto wa shemeji yangu, kipindi hicho nilikua na kama miaka mitatu tangu kuanza kufanya mapenzi kinyume na maumbile, nilishazoea na tayari nilishaanza kuona madhara yake ingawa yalikua madogo.

Kupata fangasi sehemu za haja kubwa na wakati mwingine kujichafua ilikua jambo la kawaida ingawa ilikua kidogo sana, hakikua kitu cha kuonyesha hata mume wangu hakujua, niliona aibu kumuambia kwani nilihisi anaweza kunichukia na kutafuta wanawake wengine. Nakumbuka nilikua nimevaa gaini langu la rangi kama ya pinki flani, fupi mpaka magotini la kubana, nilikua nimesimama ninacheza, upepo ulikuja na kama watu wengine niliutoa bila kujua kua umetoka na nini.

Wakati nacheza nilihisi kitu kama majimaji kinatoka sehemu ya nyuma, kunashuka mpaka chini, kumbe tayari nilishachafuka huku nyuma, nakumbuka kuna katoto ka kaka yake na mume wangu kakaniambia “Shangazi umekalia maji.” Kabla sijajiangalia vizuri kale katoto kaliruka na kukimbia huku kameshika pua, “Shangazi kajinyea!” kaliongea kwa sauti, kila mtu aligeuka na kuniangalia mimi. Nilijishika nyuma na kweli nilikua nimeshajinyea, kinyesi kilitoka bila mimi kujua.

Mama mmoja aliyekua jirani yangu alichukua kitenge chake alichokua kajitanda na kunipa nijifunge, nilikiimbia na kutoka nnje huku kila mtu akiniangalia, mume wangu alikuepo na mwanangu mkubwa wa miaka saba naye alikuepo. Aliponiona nimeadhirika alianza kulia, kule nnje mume wangu alikuja, tukaingia kwenye gari sisi wawili na kuondoka, hata watpto tuliwaacha. Aliniuliza nini kimetokea kama naumwa sikua na jibu, nilimuambia kuwa nislishaona dalili kwa kutokwa tokwa na maji maji mara kwa mara lakini yalikua yakiloanisha tu nguo za ndani na nilikua sijui kama nimejisaidia.

Alinipeleka mpaka nyumbani kisha kurudi kuwachukua watoto, aliwaambia watoto nilikua naumwa na si kujinyea ila ilishasambaa mtaani. Kila mtu alikua anajua na wote walijua ni sababu gani. Kama wiki mbili baadaye mume wangu alikuja na kuniambia “Itabidi urudi kwenu.” Nilimuuliza sababu lakini hakunipa jibu, alisema hawezi tena kuendelea kuishi na mimi kwani nimemtia aibu. Nilijua utani lakini alilazimisha, alinirudisha nyumbani kwetu akabakia na watoto akawapeleka kwa dada yake.

Kuja kushituka mwanaume ameanza kutangaza kuwa nimemdhalilisha na nimekua nikiichepuka nafanya mapenzi kinyuma na maumbile na wanaume wengine. Ndugu zake walikua wanamuonea huruma na kumuona kama mhanga, kweli niliumia kwani yeye ndiyo kanifundisha na sijawahi kukutana na mwanaume mwingine zaidi yake. Nilimtafuta na kumuuliza kwanini ananiacha wakati yeye ndiyo alinifundisha akasema kuwa suala la mimi kujiharishia mbele za watu limemuaibisha sana hivyo hawezi kukaa na mimi kwani ataonekana na yeye anafanya huo ushenzi.

Aliniambia “Mimi ni mtu na heshima zangu, ni bora watu wajue kuwa ulinisaliti na wanaume wengine kuliko kujua kama mimi nafanya mapenzi kinyume na maumbile. Isitoshe siwezi kufanya tena na wewe kwani huna ladha kama zamani, sifurahii tena.” Aliniambia na kweli aliniacha, ni mwaka wa pili sasa nimejitahidi sana sijafanya mapenzi kinyume na maumbile lakini mpaka leo bado sijiamini kutoka nnje hivi hivi, kila wakati najikagua na siwezi kutoka bila kuvaa nguo za ndani tatu tatu naamini nitapona na kuwa sawa ila sitamani tena wanaume kwani mimi mwenyewe najionea kinyaa.

***MWISHO. 
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni