SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA TATU (03)

SAFARI YA KUZIMU
NA ZUBERI MARUMA
03
Whatsupp: 0767433106
"Haaaaaaaaaaaa haaaaaaaaaaaaaaaaaa haaaaaaaaaa"
Ghafla wakashtushwa na kicheko kikali!,muda ule ule mvua ikikata na pakirudi kama mwanzo!
Kama akukunyesha mvua!
Wachawi wale wakiwa katika taharuki kwa hali ile ambayo aikuwahi kutokea kabla katika himaya yao wakatoa heshima pasina kuamini kile wakionacho katika macho yao!....
Lusifa alikuwa mbele yao....
"Kinzungu uvinza nzae" ( hudumu utawala wa kizungu)
Lusifa akaanza kwa kuwasalimia
"Nzaeeeeeee" (hudumuuuuuuuu)
"Kinzungu uvinza nzaeeeeee"
"Nzaeeeeeeeeee"
"Ahsanteni wana kinzungu sasa ningependa kuwajulisha jambo kwanza nashkuru kwa sadaka mnipayo kila mwezi katika familia zenu,na sadaka mnipayo kila siku katika makundi ya watu mbalimbali
Niwapongeze kwa ilo,nadhani mfuasi wangu kuzimu bi Chausiku na msaidizi wake Bi Mwadawa washawaeleza kuwa malkia wa wa wachawi hawamu hii hanatoka kwenu!,
Na nadhani Jana ndo ilikuwa siku ya bi Selina kusema amtakaye kumtoa sadaka akamtaja mwanaye wa kike Irine ghafla hali ikabadilika naomba mtambue wote kuwa yule ndo malkia wenu ivyo bi Selina angetaja mtoto mwingine kwa kuwa si anaye wawili?!
Na cha mwisho kwanzia sasa bi Selina ni kiongozi wenu kwa kuwa ni mama mkwe wangu hivyo atakuwa kiongozi wa wote akifatia na bi Chau na Kidawa!
Baada ya maelezo Yale bi Selina akuamini kwa utukufu ule wa kisheitwani aloupata,ghafla kizungu zungu kikamshika akapoteza fahamu
Lusifa palepale akatoweka
Ngoma zile zika anza kupiga wachawi wakaingia kati kuanza kucheza,wakimzunguka bi Selina na kumpa heshima,kelele zile za ngoma alianza kuzisikia kwa mbali hatimaye akafumbua macho yake!
Bado akuamini kama siku moja mtoto wake angekuja kuwa malkia wa wachawi,hiyo ilikuwa ni heshima ambayo hata akuihisi
***
Chumba kilikuwa kitulivu,ukimya ukitawala mwanga wa mishumaa ilowekwa katika stuli ndani ya chumba kile ilifanya viumbe vile viwili vilivyovaa mashuka meusi na kukaa kitako wakinyoosha miguu kuonekana waziwazi,ghafla wakaanza kusugua matako yao sambamba na kuongea lugha isoeleweka!
Lugha waloitambua wenyewe!,pamoja na kutoa miguno macho yao ya njano waliyageuza na kuleta taswira ya kutisha
"Cheche kuvisa! Cheche kuvisa kuvisa ranga langa chilanga"
Bibi Chau aliongea kwa sauti ndogo huku akizidi kusugua makalio yake katika simenti ya chumba chake kile!
Wote wawili walikuwa na uchungu katika mioyo yao,walitegemea kwa heshima waloiletea himaya yao wangepata nafasi watoto wao au wajukuu kupata nafasi ya umalkia ila bahati ile ilienda kwa mtu mwingine!
"Lazima tufanye kitu bi Selina ana nguvu gani kutuzidi sisi?! Je huyu mtoto wake ana uzuri gani kuwazidi watoto wetu"
Bi Chau akaongea kwa uchungu
"Lakini ighandee tutafanyaje? Na mkubwa ndo kasha amua"
Bi Mwadawa akaongea kwa kukata tamaha,
"Kuna cha kufanya mpz!,ni tumwangamize yeye na mtoto wake huyo Irine"
"Tutawezaje si hatakuwa akilindwa na waruvaa"
Bi Mwadawa akajibu waruvaa akimaanisha Lusifa
"Ni mungu wetu sote hawezi kutukasirikia kwa shirki yoyote"
Bi Chau akaongea kwa kujiamini!
"Basi nakusikiliza!"
"Twende kwanza katika hiyo sadaka yake baada ya kumla nyama mwanaye ndo tuianze vita!
" sawa bibi,"
Wakatoweka
***
Giza lilitawala katikati ya usiku ule katika nyumba ya bi Selina,ghafla alishtuka katikati ya usingizi
Ni baada ya kusikia kelele katika paa la nyumba yake!
Hatua kama za mtu akikanyaga kwa kishindo!
Alijua kashatembelewa na wenzake akajinyanyua na kukaa kitako miguu akainyoosha mbele na mikono yake!
Ghafla sauti za paka wakasikika nje wakilia,na ghafla viumbe vitatu vikaibuka chumbani mule!
Wote wakiwa uchi kama walivyozaliwa Bi Chau,bi Mwadawa,bi Ami ,na BI Selina wakatoweka na kutokea katika chumba cha watoto katika nyumba ile!
Katika kitanda walilala watu wawili Irene na mdogo wake bi Selina akamwangalia mwanaye shoti zikatoka katika macho yake!
Ghafla kijana yule alojulikana kwa jina la Sam akafumbua macho yake,alipopokelewa na maumivu makali ya kichwa!
Akuwaona wachawi wale walosimama wima pembeni ya kitanda chake!
Akamuamsha Dada yake Irene huku akizidi kujigalagaza kwa maumivu makali ya kichwa!
"Dada naumwa nakufa Dada"
Irene alishtuka na kuwasha taa ya chemli mdogo wake alikuwa kaloa jasho mwili mzima cha ajabu bado alitetemeka baridi!
Mpaka meno mdomoni yaligongana,
Irene huku akiwa kama kachanganyikiwa akauendea mlango na kuufungua huku akiita mama,mamaaa
Selina pale aliposimama akatoweka,na kuwa acha watatu wale ambao kwa haraka bi Chau alimsogelea Sam akampaka dawa flan na kumtoa pale ,bi Ami akaweka limgomba kisha bi Chau akamwongoza mtoto yule mpaka nyuma ya mlango ule na kumwambia akaye!
Kama zuzu Sam akaketi!
Selina alikuja kutokea chumbani kwake katika kitanda chake akajifanya amelala,kwa kuwa hakuwa na kawaida ya kufunga chumba Irine alizama moja kwa moja na kuanza kumuamsha
"Mama! Mama! Mamaaaa"
Selina akafumbua macho,
"Nini usiku huu"
"Sam anaumwa mama"
Selina aka amka wakaelekea mpaka chumbani,ambapo Irine aliuwona ule mgomba kama mdogo wake! Akaanza kumwita akiangua kilio
"Sam mdogo Angu amka!,"
Akapeleka kichwa chake kusikiliza mapigo ghafla akaangua kilio baada ya kugundua mdogo wake AMEKUFA!
Selina na mwenzake wakapeana ishara,Selina naye akaanza kulia!...
Majirani usiku ule ule wakaanza kuwasili!....
Bado Sam kule nyuma ya mlango alibaki akishangaa!, Dada yake na mama yake wakilitaja jina lake kwa uchungu kwamba amekufa wakati yu hai...
Akaunyanyua mguu kutaka kutoka eneo lile....
Daaaah sijui nini kiliendelea?!
DONATE VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Your donation helps the Admin to be even more active in sharing quality blog templates. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni