SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA TANO (05) | BongoLife

$hide=mobile

SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA TANO (05)

SAFARI YA KUZIMU
NA ZUBERI MARUMA
05
Whatsupp: 076743310
"Watu walikuwa wanasema wewe umeua ndugu zetu kumbe ni kweli mama na Leo una niua na Mimi mwanao!"
Maneno Yale yakamchoma moyo wake Selina!, ghafla akakiachia kile kisu kwa uoga na kuanza kurudi nyuma mikono akielekeza mbele akikataa
"Hapana! Hapana! Hapana!..."
"Nimekukosea nini mama yangu mpaka unataka kuniua?!"
Sam akazidi kulalamika kwa uchungu huku sasa akilia
"hapanaaaaaaaaaaaaaa!!!!"
Selina aka achia sauti Kali,ilochanganyikana na mwangwi!....
Sasa alibadilika ,macho yalikuwa makali tena yenye unjano kama wa macho ya paka!,alihema kwa hasira na sauti ilitoka ya kutisha!
Macho yake Yale makali yakatua katika nguo ya mtoto wake!,akuliona lile fundo lililochomwa na sindano na Uzi ndani yake!
Machale yakamcheza Selina!,akauhisi mchezo japo akujua ni yupi aliyemchezea,akajua kaingia katika vita Kali na wenzake wasopenda mwanaye kuwa malkia wa wachawi!
Hao ma hadui zake ndiyo walotoa lile fundo wakitegemea Selina angesitisha ile kafara!,
Na kitendo chake cha kusitisha kingemuuzi waruvaa wao na hapo angesitisha wazo lake la kumfanya Irene malkia
Ndiyo! Huo mchezo ulifanywa na viongozi wa muda mrefu wa himaya ile bi Chau na bi Kidawa wakitaka watoto wao ndo wapate nafasi ile!
Selina akuwa tayari akamtumia pepo mwanaye, pepo mchafu Sam akadondoka na kuanza kutapa tapa pale pale akamuwahi na kumchoma kisu cha kifuani damu zikaruka katika nguo yake ile nyeusi mpaka usoni
Akausambaza ulimi wake kulamba ile damu iloruka karibu na mdomo wake!
Wachawi wote wakaanza kushangilia na ghafla ngoma zikaanza kulia ishara ya kukubalika kwa sadaka ile,wakacheza kwa dakika chache na hatimaye Seli akachukua kisu na kuchuna ngozi ya kichwa akaukuta ubongo akaupasua na kuchukua kipande na kula. Damu ilokuwa maeneo Yale ya ubongo akaimimina katika kikombe na kuusogelea mbuyu ule
"Cheche kuvisa,cheche kuvisa ,kuvisa ranga, langa chiranga, mizimu ya wantu na gantu,mizimu ya mababu na mababu mlonikabidhi mkoba pokeeni chakula hichi cha mwili wa lembwekeze wenu kama sadaka kwa waruvaa mlungu wavai"
Selina akaongea huku akimimina damu ile katika mvule ule,na wakati akiimimina damu ile ilitoweka!....
Ikimaanisha sadaka imepokelewa
"Shirki ni mbaya sana ndugu zanguni tuepukeni nayo aina faida hapa duniani na kesho ahera zaidi ya hasara hapa duniani na pia kesho ahera"
Basi: baada ya kumaliza wachawi kadhaa wakasogea kumsaidia kuupasua mwili wa Sam na baadhi ya miili waloenda kuifukua makaburini wakakata manyama kila mmoja akashika pande lake ikiwa mbichi vile vile na kuanza kuila
Ilikuwa ni hali ya kutisha kula nyama ya binadamu mwenzako na kunyonya damu yake!
MUNGU ATUEPUSHE
****
SURA YA PILI
Alikuwa ni msichana Mrembo mwenye uzuri wa asili, macho yake madogo kama ya mdoli mashavuni alijaliwa dimpoz au vishimo vilivyomwongezea uzuri,alikuwa na shingo ndefu midomo mizuri japo akupenda kuipaka liplistick
Kifuani alijaliwa mchomozo wa vimatiti vidogo vilivyochomoza watu wasasa upenda kuihita saa sita!
Pia alikuwa na hips zilizojichora na kujipinda kukamilisha umbo no 8 nyuma hakuwa na wowowo kubwa ila pia akunyimwa kiungo icho
Alijaliwa mapaja makubwa na mguu wa bia,kwa uzuri huo na rangi yake ya chokulate ilisababisha apate usumbufu kwa wanaume
Ni mwanaume gani angemwangalia pasina Kumpenda Irene?! Mtoto wa Selina mama alosifika kwa uchawi kijijini pale
Pamoja na sifa zile mbaya Irene alimtetea kwa nguvu zake zote mama yake!,Mara nyingi alipenda kusoma biblia yake na icho kilimsaidia aishi kwa amani kwani umtegemeapo yeye MUNGU ukutoa katika wasiwasi na shaka
'Mama yangu anashika biblia mchawi awezi shika kitabu hicho'
Kila Mara alijifariji kwa maneno hayo pasina kujua ule ulikuwa ni kiini macho ile aikuwa biblia Bali kitabu cha kawaida!
'Mama yangu anaingia kanisani!,mchawi awezi ingia kanisani'
Akazidi kujipa moyo pasina kujua hata mule walipoingia alikuwa kanisa la haki zaidi ya watumishi wale kutumia nguvu za shetani katika ibada zao
Na makanisa kama Yale yalijaa waumini,kutokana na mvuto wa kiushirikina walokuwa nao kiongozi wa makanisa yale
Irine akiwa shuleni wakati wa 'break' alipenda kukaa na kijana mmoja alokuwa ndo mpz wake Christopher au Chris kwa kifupi ndo jina la kijana huyo,alokuwa na sura nzuri (hb) na mwenye akili pia darasani!
Siku hii ya Leo Irine akuwa na raha kabisa!,hiyo yote ni kutokana na maneno kuendelea kuenea juu ya mama yake kuwa mchawi na ndo kamuua Sam mtoto wake wa mwisho
Ghafla mpz wake akatokea na kumfata kwa bashasha....
:"CHRISS mambo?" (huku akimpa mkono)
"poa tu beby nambie!" alijibu chriss huku akiupokea ule mkono!
"ni mawazo tu mpz wangu!" ghafla chris akamkatisha
"Unamwazia mama yako yule mchawi?"
"Nini?"
IRINE akuamini masikio yake,ghafla akabadilika,hasira zikampanda,sura ya upendo yote ikatoweka uso wake ukauvaa chuki!,akuamini kama Chriss kijana alompenda na kumfanya chaguo lake naye angekuwa upande wa kumtuhuma mama yake vibaya
"yani hata wewe CHRISS nikupendaye?,mfariji wa moyo wangu,una amini mama yangu ni mchawi?"
sasa hasira ziligeuka na kuwa majonz,aliuliza irine huku akiwa analia akageuka ili aondoke lakini CHRIS akamdaka mkono
"IRINE my love si unajua NAKUPENDA? siwezi kukudanganya mpz wangu,amini mama yako SELINA ni mchawi wa kutupwa na anayetakiwa kurithi ni wewe mtoto wake,ukubali ukatae uwo ndo ukweli!"
"CHRIS nilikupenda sana!,ila kwa ilo tusi ulilo nitukana leo its ovar,inatosha chris siwez kuwa na wewe tena!"
"IRINE usiwe mkali usipaniki mpz wangu NITAKUDHIBITISHIA kuwa mama yako ni mchawi! nilijiandaa kukwambia ukweli leo mimi babu yangu ni mganga"
akaweka mkono mfukoni na kutoka na kaupande cha mzizi akampa irine mtoto yule wa kike akasita kukipokea ila baada ya kujishauri kidogo akapokea
"chukua hiki si unaitaji kugundua ukweli juu ya mama yako? usiku kabla ujalala kitafune kisha ulale kesho utanifata mwenyewe na utanambia na utakacho ona plzzz usipige kelele kwani kufanya ivyo watajua umewagundua kitakachofuata ni wewe uwe mchawi au ugeuzwe msukule"
IRENE bila kusema kitu akakiweka katika begi lake na kuondokaa akipania kuujua ukweli!....
UNAJUA NINI KITAENDELEA?!.
IRENE ATAUJUA UKWELI?! NA ITAKUWAJE
ITAENDELEA. 

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA TANO (05)
SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA TANO (05)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/07/safari-ya-kuzimu-sehemu-ya-tano-05.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/07/safari-ya-kuzimu-sehemu-ya-tano-05.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy