SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA NANE (08) | BongoLife

$hide=mobile

SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA NANE (08)

SAFARI YA KUZIMU
NA ZUBERI MARUMA
08
Whatsupp: 0767433106
"Ha haaaa haaaaaa haaaaaaaaa na itakuwa hivyo lazima tutoe sadaka!".
Kicheko kikasikika na bi Seli akazidi kusisitiza!....
Wote wakakaa mkao wa kula kumsikiliza ni sadaka ipi ingetajwa....
"Basi bi Seli akaendelea.......
" na sadaka yenyewe ni ya huyo alomfumbua Irine na kumueleza siri zetu!....
Wachawi wale wa kahema kwa kupata uhafueni!,lazima usiku wa Leo tumle nyama!....
"Kinzungu nzinga nzaeeeeee!"
"Nzaeeeeee!"
"kinzungu nzinga nzaeeeeee"
"Nzaeeeeee"
"Ok asanten wana kinzungu na Leo usiku Mimi pamoja na wenzangu bi Chau na bi Mwadawa tutaenda katika nyumba yake tuivute roho yake tukisaidiwa na " bakas"
Bakas ni jini mbaya atawalaye siku ya jumamosi Mchawi kabla ya kumchukua mtu Msukule hufanya Mkataba Maalum na Jini huyo “BAKAS” ili amsaidie katika kazi hiyo, na kuna Sadaka maalum ambayo hutoa kumlipa Jini huyo kama malipo ya kazi yake.
" kinzungu uvinza nzaeeeeee
"Asanten sana ni wakati wa kwenda kuanza kazi na saivi ni saa saba na dakika tano saa tisa tuonaneni tena hapa hapa huyo kiumbe tayari atakuwa katika mikono yetu!....
Viumbe vyote vikatoweka
***
Ilikuwa ni mida ya saa nane usiku, katika nyumba alokuwa akiishi Chriss ghafla nje nyumba ile wakatokea wale wachawi watatu!
Walirudi kinyume nyuma mpaka katika mlango wa kuingilia ndani ya nyumba ile!
Ghafla wakatoweka na kutokea ndani ya nyumba ile nje ya chumba cha Chris,
Bi Seli akaweka mdomo wake katika tundu la mlango na kuwa kama anavuta kitu!,pale kitandani Chris akawa akiangaika!
Ghafla akatoa mdomo wake katika kitundu kile na kupuliza chupa aloishika na kuifunga! Tayari alisha iteka roho ya kijana yule wote waka achia kicheko na kutoweka
Kwa kuwa muda ulikuwa umeshaenda wakarudi eneo lao la mbuyuni ambapo waliwakuta wenzao tayari washawasili!
Kila mmoja akiwa na kifurushi chake mwingine alikuwa na mtoto mchanga, mwingine mkono wa maiti mguu kalio moja ili mradi kila mmoja alibeba kitu
" kinzungu uvinza nzaeeeeee "
"nzaeeeeee"
Wanachama wale wakaitika kwa furaha bi Selina akaendelea...
"Tu namshukuru Waruvaa tumefanikiwa kuichukua nafsi ya yule mpumbavu pasina mtihani wowote japo wengi tulitegemea kwa kuwa baba yake yu mganga ingetuwia vigumu ila haikuwa ivyo sijui ndo mganga ajigangi au vipi lakini kwanza nyumba aina zindiko ivyo tumeingia kirahisi na kufanya yetu ivyo kesho kutwa jumamos ndo siku ya kumfanya kitoweo kinzungu uvinza nzaeeeeee"
"Nzaeeeeee......"
Baada ya maneno yale wakaendelea na shughuli zao za kawaida ikiwemo kila mmoja kula kile kifurushi alichokuja nacho
***
Alifumbua macho yake na kupokelewa na maumivu makali ya kichwa...
Kulikuwa tayari kumepambazuka akajiinua taratibu toka pale kitandani.
Aliuhisi mwili wake ni mzito,akachukua maji katika ndoo lengo akaoshe kichwa kupunguza maumivu ,kwa maumivu Yale hata shule siku hiyo akupanga kwenda!
Chris akiwa na ile ndoo ya maji kabla ajafika bafuni ghafla kizunguzungu kikali kikamshika akadondoka vibaya chini na kutulia pale pale!
Ulikuwa ni mshtuko kwa wazazi wake!,lakini hakukuwa na jinsi kwani waliamini alipangalo Mungu binadamu huwa awezi kulipangua!
Kwa kuwa kijana yule hakuwa na ndugu wa mbali sana mipango ya mazishi haraka sana ilianza, na siku ilofatia jumamosi akazikwa katika eneo la pale nyumbani!
***
Ilikuwa ni usiku wa manane wa siku ya kuamkia jumamosi eneo lile la makaburi wakazuka viumbe wawili!
Mmoja alikuwa ni bi Selina alokuwa kavaa shuka jekundu na usoni kajichora mkononi alikuwa kashika usinga,
Pembeni yake alikwepo mbabu alokuwa na wastani wa miaka 50 mpaka 55 alojaliwa ndevu nyeupee nyingi pia mvi zilikipendezesha kichwa chake!
Mzee huyu alijulikana kama "Bakas" jini lililotumika kufufua wafu na misukule ilochukuliwa kishirikina
Lengo la kuwa pale ni kuuchukua ule mwili msukule kabla awajaugeuza sadaka ya kualalisha vita na malkia wao mtarajiwa Irene
Balkis alikaa upande wa kichwani kwa maiti alipoelekezwa na bi Selina akakaa upande wa miguuni kila mmoja wao aka anza kufanya uchawi wake!
Selina alisugua matako katika ardhi pale alipokalia,huku akisema kwa sauti ndogo akinuizia kwa kurudia rudia...
"Mortoo tombo mivi" maana yake ni "aliye ndani ya kaburi ni wangu"
balkas alinuizia vitu visivyoeleweka huku akinyunyuzia majani mkakasia (acacia) ghafla shoti zikatoka katika macho yake na kuliendea kaburi lile!
Ghafla mwili wa Chriss ukaja juu ya kaburi!,ukiwa umelala vile vile!...
Balkis akamwangalia Seli kwa tabasamu ,Seli akalirudisha tabasamu lile ghafla wote wakageuka Seli na Balkis na kugusanisha makalio yao
Wakatoweka
Walikuja kutokea nyumbani ambapo bi Seli alimrudishia kijana yule roho yake aliyoiweka ndani ya chupa akamnywesha dawa Kali ya kumzuzua,baada ya hapo akamfunga kamba akisubiria mida ya kafara ifike ili amtoe!
Chris alikuwa ni Kama mbuzi aliyosubiria muda wake achinjwe!....
Na masaa yakazidi kukatika hatimaye muda ule wa kutoa sadaka ukawadia!.....
Je nini kitaendelea?!
itaendelea kesho panapo ma

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA NANE (08)
SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA NANE (08)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/07/safari-ya-kuzimu-sehemu-ya-nane-08.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/07/safari-ya-kuzimu-sehemu-ya-nane-08.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy