SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA KWANZA (01)

SAFARI YA KUZIMU
NA ZUBERI MARUMA
01
Whatsupp: 0767433106
ISINYE
WILAYA YA GANJA
SAA TISA NA DAKIKA THELATHINI NA TATU USIKU
Ganja ilikuwa ni moja wapo ya kijiji kilichopo ndani ndani kabisa ya mkoa wa Rununu nchini Isinye
Kijiji hiki kilisifika kwa kuwa na uchawi na si ivyo tu Imani potofu zilitawala ndani ya kijiji hiki!
Kuuwana kwa Imani za kishirikina,kutengwa ilikuwa ni moja wapo ya sifa kubwa ya kijiji hiki ambacho hata ivyo hakikuwa na maendelea hata!
Katika nyumba moja ya makuti katikati ya usiku huo nje ya nyumba ile ghafla akazuka bibi mmoja hivi.
Bibi huyo aliyezeeka na ngozi yake kukunjana, bibi Yule baada ya kuzuka katika nyumba ile mkononi akiwa kashika usinga alivaa nguo nyeusi tiii
Na pia usoni alijichora chora macho yake yalikuwa mekunduuu yaka angalia pande zote nne za dunia!
"Cheche kuvisa,....cheche kuvisa.....cheche kuvisa.......cheche kuvisa"
Alisema hayo maneno kwa kila upande alokuwa akiutazama huku akipiga na usinga wake!
Ghafla akaachia mluzi!,na kujigeuza paka!
Akatoweka
Bibi yule alikuja kutokea ndani ya chumba kimoja wapo cha ile nyumba akiwa uchi wa mnyama,alikuwa akicheza pembeni ya kitanda cha kamba alicholala mama mmoja!
Mama yule akafumbua macho
"Bi mwadawa amka muda umefika!"
Bibi yule alokuwa uchi akamnong'oneza mama yule alolala naye akapiga mwayo na kwa uvivu akajiamsha!
Akaiendea kaniki yake ila kabla ajajifunga bibi yule akamwoneshea ishara bi mwadawa akaelewa ishara ile
Waka acha kicheko kikali!
Na ghafla wote wakatoweka
***
KATIKATI YA MSITU PANDE
KATIKA MTI MKUBWA WA MBUYU
Eneo lile la msitu ule lilikuwa kimya si nzige wala aina yoyote ya ndege,mdudu,au mnyama alotoa sauti yake!
Hali ile ya utulivu ilitulia kama dakika tano na ghafla milio ya fisi na paka waka anza kusikika katika mbuyu ule!
Na hata maeneo ya mbali na pale!
Ghafla juu wakaanza kuonekana viumbe vikitua vikiwa vimekalia nyungo,vikiwa uchi wa mnyama! Mikononi vikiwa na usinga
Si hivyo tu viumbe vingine vilikuja vikiwa juu ya wanyama aina ya fisi!,sasa ile hali ya ukimya ikatoweshwa
Makelele yakatawala!,
Makelele ya ajabu sambamba na kuzuka viumbe vya ajabu tena makundi kwa makundi
Sasa walijipanga maduara maduara na kuanza kucheza ngoma ambayo ilisikika ikilia pasina mpigaji!
Ngoma ambayo si wachawi wale waloisikia tu hata mtu wa kawaida uliyoko karibu na msitu ule ungekuwa macho muda ule ungepata kusikia
Ila Mara kibao wana kijiji usiku walisha uvamia mbuyu ule ila hawakubahatika kuwaona walopiga ngoma zile
Jambo ilo likabaki Kama Imani ya kijiji!
Wachawi wale wakaendelea kucheza,ghafla mbele ya mvule ule palipokuwa na viti viwili wakazuka watu wawili
Ni yule bibi pamoja na mama kidawa,kuzuka kwao kukarudisha hali ya utulivu!
Kama mwanzo!,si sauti ya fisi , paka wala ngoma zile!
Ni wazi wale walikuwa ni viongozi wao,wakasimama!
Wachawi wale wakaweka duara moja kubwaaa
"Cheche kuvisaaaaaaaa"
Viumbe vyote vikaitika
"Cheche kuvisa"
"Kuvisa ranga" bibi yule akasema kwa ukali
Navyo vikaitika hivyo hivyo " kuvisa ranga"
"Ranga shiranga"
"Ranga shiranga"
"Ranga shiranga"
"Ranga shiranga"
Ghafla waka anza kuimba wakizunguka kama watoto wachezavyo ukuti ukuti!
Waliporidhika bibi yule akatoa ishara kwa kuwaoneshea usinga wake wachawi wote wakatulia
"Kinzungu uvinza nzae" ( udumu utawala wa kizungu)
"Nzaeeeeeee" ( udumuuuuuuuu)
"Kinzungu uvinza nzaeeeeee"
"Nzaeeeeeeeeee"
"Ahsanteni wana kinzungu kwa kuwa pamoja tena katika usiku huu ila Leo tumechelewa na tuna muda mdogo! Sana wa kufanya yetu,benki yetu hazina damu mungu lusifa analalama atupandikizi magonjwa na Mkumbuke ametuhaidi kutupatia malkia wa wachawi wote kutoka katika himaya yetu ya kinzungu sasa kama tusipo mfuraisha nini kitatokea?!"
Bibi yule aliongea huku kundi lile la wachawi wa kimsikiliza kwa makini!,naye akaendelea....
"Magonywa yanatakiwa yatawale katika kijiji hiki!, siyo ivyo tu tuzidi kutengeneza chuki baina ya watu sawa wana Kinzungu"
Wachawi wote wakapiga mbinja kushangilia,bib
i yule akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akaita akimwangalia mmama mmoja ambaye hakuwa na furaha hata chembe tangu amefika eneo lile!
"Selina john"
Mama yule akiwa ana ruka ruka akasogea mpaka mbele ya mvule ule akasimama mbele ya bibi yule na mama kidawa akainama kidogo kutoa heshima!
"Juma tano hii kafara ipo kwako ivyo na dhani unajua unapaswa umuandaye nani kama sadaka kwa mzimu wa mti huu na shukrani kwa mungu wetu lusifa na chakula chetu kwa nyama yake"
Mama yule akainama kukubali huku machozi yakimtoka,ni mama alojaliwa watoto kumi lakini amekula wote na sasa wamebakia watatu nako jumatano anatakiwa atoe mmoja kwa nini asilie!
Taratibu mama yule akarudi eneo lake huku bado akiendelea kulia
Wenzake wakishangilia ngoma zile zikaanza kulia tena wakaanza kucheza kama kawaida yao

Na baada ya hapo wakatoweka kwa lengo la kwenda sasa kuwanga!....
Je nini kiliendelea?!


ITAENDELEA
DONATE VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Your donation helps the Admin to be even more active in sharing quality blog templates. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni