$hide=mobile

NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI SEHEMU YA 02

NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI SEHEMU YA 2 WHATSAPP 0655585220 ZANZIBAR Matangazo bado yalikuwa yakiendelea kufanyika, makanisani watu walitangaz...

NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI
SEHEMU YA 2
WHATSAPP 0655585220
ZANZIBAR
Matangazo bado yalikuwa yakiendelea kufanyika, makanisani watu walitangaziwa kuhusu mkutano huo mkubwa wa injili. Kila mtu alichanganyikiwa, Wakristo wengi wakatamani kuhudhuria mkutano wa mhubiri huyo aliyekuwa akivuma duniani.
Viwanja vya Jangwani vikaonekana kuwa vidogo kwani Wakristo wengi jijini Dar es Salaam walipanga kwenda huku hata wale waliokuwa mikoani nao wakisafiri kuelekea jijini humo kwa lengo la kusikiliza mahubiri kutoka kwa mhubiri huyo.
Baada ya siku kukatika, hatimaye mkutano mkubwa wa Injili ukaanza katika viwanja hivyo. Siku ya kwanza, alihakikisha anamuimbia Mungu kwa uwezo mkubwa ambao hakuwahi kuimba maishani mwake mwote.
Sauti yake ilipoanza kusikika, watu walichanganyikiwa, kila mtu akaangalia vizuri jukwaani, alitaka kumuona msichana aliyeimba kwa sauti nzuri na kali kiasi kile. Macho yao yalitua kwa msichana Nandy ambaye alinyanyua mkono mmoja juu huku mwingine akiwa ameshikilia kinasa sauti.
Aliimba kwa nguvu, jasho lilimtoka, hakujali, katika kumuimbia Mungu hakujali kitu chochote kile. Mawazo yake na akili yake ilikuwa kwa Mungu wake, alicheza na kurukaruka kiasi kwamba wakati mwingine alionekana kama kuchanganyikiwa.
Mkutano ulipomalizika, kila mtu alimfuata na kumsifia kwani siku hiyo ya kwanza alionekana kuwa moto wa kuotea mbali kwa jinsi alivyomsifu Mungu. Kila alipopongezwa, hakuchukua utukufu, aliwaambia watu kwamba utukufu ulikuwa kwa Mungu aliyekuwa juu.
“Ila umeimba bwana!”
“Nashukuru mama! Utukufu kwa Mungu,” alisema kila alipofuatwa na kusifiwa.
Akaanza kujiandaa, baba yake, mzee Gwamaka alikuwa akimsubiri kwa kuongea na watu mbalimbali. Hakutakiwa kuondoka mapema kwa kuwa kanisa lao ndilo lililoandaa mkutano, alitakiwa kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa kabla ya kesho kuja na kuendelea na mkutano.
Wakati akiendelea na marafiki zake kuweka vitu vizuri akasikia akiitwa kwa nyuma, alipogeuka, macho yake yakatua kwa kijana mmoja ambaye alipiga hatua kumsogelea pale alipokuwa.
Kwa kumwangalia kijana huyo, isingekupa kazi kugundua kwamba alitoka katika familia ya maisha mazuri. Alivalia shati jeupe, tai nyeusi na suruali nyeusi huku akiwa na miwani ya macho.
“Bwana Yesu asifiwe Nandy,” alisalimia kijana huyo kwa sauti ya upole kabisa.
“Amen kaka!” alijibu na kuendelea na kazi yake.
“Mungu amekubariki sana, amekupa kitu adimu mno. Umeimba kupita kawaida, hiyo sauti yako, hakika mshukuru sana Mungu!” alisema kijana huyo huku akiachia tabasamu, japokuwa palikuwa na kigiza fulani lakini Nandy aliliona vizuri tabasamu lile.
“Nashukuru! Utukufu kwa Mungu!”
“Naitwa Dickson Kambili!” alijitambulisha kijana huyo na kumpa mkono lakini Nandy hakunyoosha mkono wake kumsalimia.
“Nashukuru kukufahamu!”
“Basi sawa. Ulinzi wa Mungu uwe nawe. Usiku mwema, Mungu akutangulie kama alivyomtangulia baba yetu, Ibrahim,” alisema Dickson maneno mengi ili naye aonekane aliijua sana Biblia.
“Amen!” aliitikia Nandy huku akiendelea kupanga vitu. Dickson hakutaka kujali, huyo akaondoka zake huku akionekana kuwa na furaha kuzungumza na msichana huyo kwa siku ya kwanza.
Dickson alikuwa akisubiria kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa lengo la kwenda kusomea utabibu chuoni hapo. Moyo wake ulikuwa na furaha tele, hakuamini kwamba mara baada ya kupambana kwa kipindi kirefu hatimaye alikuwa akitimiza ndoto yake ya kuwa daktari katika maisha yake.
Tangu alipokuwa kidato cha kwanza, alikuwa akimwambia baba yake mara kwa mara kwamba alitamani sana kuwa daktari, alipokuwa akienda hospitalini, aliumia kila alipokuwa akiwaona wagonjwa wakiugua vibaya na wengine kushindwa kabisa kusimama kama zamani.
Moyo wake uliuma na kujiona kuwa na uhitaji mkubwa wa kuwasaidia wagonjwa hao na hivyo kupanga kusomea utabibu kitu ambacho alikuwa njiani kwenda kukamilisha ndoto yake. Matokeo yake ya kidato cha sita yalikuwa vizuri na alipata alama za juu na hivyo kutakiwa kujiunga katika chuo hicho.
Alikuwa akisubiri siku ya kwanza kwenda kujiunga chuoni huko. Kwa kuwa baba yake alikuwa na pesa nyingi, alichokifanya ili kumfanya mwanaye kuwa na furaha, aone kile alichokuwa amekifanya kilikuwa na thamani sana, akamchukua na kwenda naye nchini Ufaransa.
Hiyo haikuwa mara ya kwanza, tangu alipokuwa kidato cha kwanza, alipokuwa akifanya vizuri alichukuliwa na kupelekwa nchi mbalimbali kutembea. Alikuwa na maisha mazuri, alipata alichokitaka na kila siku aliishi maisha matamu kana kwamba alikuwa peponi.
Wakati akiwa nchini Ufaransa, akapewa taarifa kwamba mhubiri wa kimataifa, Benny Hinn angekuwa nchini Tanzania katika mkutano mkubwa wa siku saba.
Hakutaka kubaki nchini Ufaransa, kwa kipindi kirefu alikuwa akisikiliza mahubiri kutoka kwa mchungaji huyo, aliyapenda, alipenda namna alivyokuwa akihubiri na hata kuwaombea watu hivyo kumwambia baba yake kwamba ni lazima wakatishe ziara yao ya kutembelea sehemu mbalimbali jijini Paris na hivyo kurudi Tanzania.
Hilo halikuwa tatizo, baada ya siku mbili wakarudi nchini Tanzania na hivyo kushiriki katika mkutano huo. Hakuwa na maisha ya wokovu lakini alipenda sana kusikiliza mahubiri. Kila alipokuwa akipata nafasi ilikuwa ni lazima kusikiliza mahubiri mbalimbali huku naye akimuomba Mungu kwamba siku moja baadaye aje kuwa mhubiri mkubwa kama alivyokuwa Benny Hinn.
Japokuwa alipenda sana dini na mahubiri lakini pia Dickson alipenda sana wanawake. Kwake, wanawake walikuwa kila kitu, aliwapenda, alipokuwa akiwaona moyo wake ulifarijika mno.
Mpaka kumaliza kidato cha sita, alikuwa amekwishatembea na wanawake wengi. Alipendwa kwa kuwa alitoka katika familia ya kitajiri lakini mbali na utajiri huo, Dickson alikuwa na sura nzuri mno.
Wanawake walimbabaikia na wengi kumuita Trey Songz kwa kuwa tu alifanana na mwanamuziki huyo kutoka nchini Marekani. Kila msichana aliyekuwa akimuona, hakutaka kumpita Dickson pasipo kumsalimia, kwao, kijana huyo aliitetemesha mioyo yao na hivyo kujikuta akilala na wanawake wengi hata wale ambao hakuwa akiwafikiria kabisa.
Siku ya kwanza ya mkutano huo mkubwa wa injili alikwenda katika Viwanja vya Jangwani huku akiendesha gari la thamani aina ya BMW X6 ya bluu. Alipofika sehemu ya kuegesha magari, akalisimamisha na kuteremka.
Watu waliokuwa pembeni wakabaki wakiliangalia gari hilo. Lilikuwa zuri mno, wengi wakatamani kumuona mtu ambaye angeteremka humo kwani wengi walihisi kwamba angeteremka mtu mzima, mwenye kitambi huku mkononi akiwa na saa ya thamani ya Rolex.
Mlango ukafunguliwa na Dickson kuteremka. Alivalia suruali nyeusi, tai nyeusi na shati jeupe huku akiwa na miwani ya macho. Kila mtu aliyemwangalia kijana huyo, alichanganyikiwa, hawakuamini kumuona kijana aliyekuwa na sura nzuri kama alivyokuwa Dickson.
Hakutaka kujali, aliwaona wanawake wengi wakimwangalia lakini akapiga hatua na kuingia katikatika ya umati wa watu na kutulia. Mkononi mwake alikuwa na Biblia yake, hakutaka kuzungumza na mtu yeyote, mahali hapo, alikuja kwa lengo moja la kumuabudu Mungu, hakufikiria kumfuata msichana yeyote yule japokuwa wakati mwingine moyo wake ulikuwa ukipambana vikali kumkumbusha kwamba alikuwa mkutanoni wakati macho yake yalipotua kwa wanawake warembo.
Baada ya dakika kadhaa, mkutano ukaanza rasmi. Aliyatafakari maisha yake, alijua jinsi alivyokuwa akimchukiza Mungu. Maisha yake yaliteswa na dhambi moja tu ya uzinzi ambayo ilimng’ang’ania kupita kawaida.
Alipambana na dhambi nyingine nyingi, alizishinda lakini dhambi hiyo ya uzinzi haikumuacha hata kidogo. Ilimtesa, kila alipotaka kuyabadilisha maisha yake, alianguka mara baada ya kumuona msichana mrembo.
Siku hiyo alifikiria mambo mengi, alimuomba Mungu msamaha, alihitaji kuwa msafi, hakupenda kuishi katika maisha aliyokuwa akiishi kwa sababu tu alihitaji mabadiliko kwa nguvu zote.
Aliyafumba macho yake, alikiinamisha kichwa chake chini huku akiendelea kumtafakari Mungu na maisha aliyokuwa amepitia mpaka kufikia siku hiyo. Wakati akiwa amekiinamisha kichwa chake, akasikia sauti nzuri kutoka jukwaani.
Sauti ile iliposikika tu, moyo wake ukamlipuka, akakaza moyo wake, hakutaka kuuinua uso wake kuangalia kule jukwaani ili kuona ni msichana gani aliyeitoa sauti hiyo na kuanza kuimba nyimbo za kuabudu.
Moyo wake ukashindana na akili yake. Akili ilimwambia auinue uso wake na kuyafumbua macho yake kumwangalia msichana huyo ila moyo wake ilimwambia kwamba hakutakiwa kufanya hivyo, huo ulikuwa ni muda wa kumfikiria Mungu na hivyo alitakiwa kutulia.

By Ahmad Mdowe 

ITAENDELEA……………………………….

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,149,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,196,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,110,FIFA.com - Latest News,15,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,11,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,207,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,39,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI SEHEMU YA 02
NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI SEHEMU YA 02
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/07/namtaka-mpenz-wangu-arudi-sehemu-ya-02.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/07/namtaka-mpenz-wangu-arudi-sehemu-ya-02.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content