CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA TANO (05) | BongoLife

$hide=mobile

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA TANO (05)

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu)
 
MTUNZI: Minnah De Embaccas

Whatsapp :0656282898

SEHEMU YA TANO (05)

ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE: wakwanza ni kaka yao.alipita akamsalimia baba yake, na kupitiliza chumbani. Hakika alijikuta anawaza sana matukio, yaliyomtokea shule. " mmh!! Au vicent amepata msichana mwengine?". Alijiuliza."kama ni kweli sitakubalii kwanza sina imani hiyo, labda atakuwa na jambo lingine, ila shule ile nzima, hakuna anaenikamata kwa uzuri".alijiwazia mwenyewe,akijiuliza na kujipa majibu mwenyewe. Ila gafla aka...... ENDELEA.
Ila gafla akakumbuka kitu. "mmh si alisema kuwa, tunawasiliana kama kawaida ngoja tuone kama itakuwa hivyo kweli". Alijisemea peke yake, vanessa huku akijiuliza, na kujipa majibu mwenyewe.kiufupi mapenzi yalisha mchanganya, hakujua afanye nini, kumueka vicent kwenye mstari. Aliwaza sana, mpka akapitiwa na usingizi,akasahau hadi kwenda kula chakula..
******
Niram akiwa bado yupo chumbani, alikuwa ana mfikiria sana vicent, mpka akawa anajiuliza,ni kwa nini amfikirie kama vile. " mmh mbona sasa nawaza upuuzi, kipi ambacho kinanifanya nikumbuke lile tukio la asubuhi".ila gafla kuma kitu akakumbuka, kikamfanya aangue kicheko siyo cha nchi hii. "hahhhhhhahhh!! hhhah!! uwiiii mama weeeeh hhh!!". Alicheka niram kama kichaa. " hivi sasa kilichokuwa kimemgandisha mpka asiondoe gari ni nini?".alijiuliza kisha akaendelea. "maana mtu aliduwaa kama kaona ela alafu yupo pekee yake anavizia jinsi ya kuikwapua hahhhah!!".alijisemesha mwenyewe kisha akacheka tena kwanguvu. Mala mlango ukafunguliwa, Akaingia mama yake ,inaelekea ndo kwanza alikuwa anafika,maana kipochi kilikuwa kwapani. " Eeeeh!! Mwenzetu vipi unaumwa ukichaa, mbona unacheka peke yakoo?".aliuliza mama yake,huku akiwa amesimama mlangoni, kwenye chumba cha binti yake.Niram alishtuka, maana hakutegemea uwepo wa mama yake eneo lile. Ila aliuficha mshtuko wake. "Eeeeeh!! Mama bwana kuna mwalimu wetu alianguka, wakati anaingia darasani, basi nikikumbuka nachekaaa".alivunga niram huku akijifanya kuwa makini na anachokingea. "wewe mtoto shetani si bure mwalimu kaanguka ndo unacheka hivyoo haaahhhhah hatarii, haya vua hizo nguo ukale, maana nakujua wewe hapo ulipo ujala ". Aliongea mama niramu, huku anapiga hatua kwenda nje. "sawa mama naja". Alijibu niram, mara ukasikika mlango paaaaah!, alikuwa mama niramu anafunga mlango . "uhhhhhhhhuh!!"alishusha punzi ndefu niramu, maana akutegemea kama angeweza kudanganya, haraka hivyo. Alibadili nguo nakutoka kwenda kuchukua chakula..
*******
Vicent alikuwa chumbani kwake, akichezea laptop yake.huku ana kula lakini mawazo mengi, yalikuwa kwa niramu. Alijiuliza kwanini ametumbukia juu ya mapenzi ya msichana, wakihindi hakika chakula hakikulika ,alikuwa na mawazo ya hatari yaliyo mfanya, chakula aone kichungu. " ntajitahidi kumtafuta naimani ntampata tu".alijiwazia kimoyomoyo, asijue aanzie wapi, amalizie wapi.ila gafla akiwa kwenye dimbwi la mawazo, alisikia simu yake inaitaaa. Ngrrrrrrrri ngrirrrrrrr!! "nani tena huyoo?". Alijiuliza huku akijiinua kuifata ,kwenye kochi maana yeye alikuwa kitandani. " daaaah!! Anataka nini tena huyuuu aaah!!".alilalamika vicent huku anaipokea simu. "hellow vanessa". Aliongea " yes bby nimekumic nikaona nikupigie". Ilisikika simu upande wa pili alikuwa vaness. " Oooh!! Kumbe niambie". "vicent nilikuwa na kukumbusha lile ombi langu nililokuomba". " lipi hilo?".alihoji vicent huku akimsikiliza kwa makini. "ni lini utanipa penzi lako?, nashindwa kujizuia vicent". Alilalama vanessa huku akisubiria, jibu upande wa pili. "Vanessa hivi kumbe jini wako apendi amani eeh!!?".aliuliza vicent, na kabla ajajibiwa akaongeza neno. " hivi leo nilitoka kukuambia nini hivi upo serious kweli wewe?, naomba usinitibue kama unawaza ngono badala ya kusoma ni wewe mimi naomba unikaushie kabisa".aliongea kwa jazba vicent, huku mikunjo kwenye paji la uso,likionyesha ni jinsi gani amechukia. "ooh nisamehe bby, mi nilikueleza tu hisia zangu wala sitaki tugombane".alijitetea vannesa maana alijua ashaharibu. " oky nikutakie jioni njema kesho mungu akipenda" aliongea vicent, na bila kusubiri jibu simu ikakatwa. Kiukweli vanessa, alijilaumu kwanini aliongea vile, aliilaani ile siku kwani aliiona siku mbaya kuliko zote. Baada ya kukata simu, vicent alikirudia kitanda na kujibwaga bado kidogo angemwaga chakula, kwenye kitanda. " Oooohsh!! Yote sababu ya huyu mwanamkee aaah!!". Alilalama vicent, huku lawama zote akimtupia vanessa. Eti wadau ukipenda sana unaonekana msumbufuu eeeh?.. Tuendeleee.. Basi vicent akachukua kile chakula na kukiweka chini akaendelea na ratiba zake .
********
Ilikuwa muda wa saa mbili kamili usiku(02.00) vanessa alikuwa yupo selbeni na mdogo wake wa mwisho wa kike, aliitwa juliana.kifupi unaweza mwita juli, walikuwa wanaangalia tv.wengine wakiwa na mishemishe zao, huku wazazi wao wakiwa wameshaingia chumbani,maana hata muda wa kuangalia taharifa ya habari aukuwepo, kutwa watoto wanaangalia movie zao. Ndio maana mzee wao anaamua ajununulie gazeti.. Muda wote wapo sebleni ila vanessa alikuwa kimya, kama anawaza jambo. Ila juli aliiona hali tofauti aliyokuwa nayo dada yake .. "vipi dada unaumwa mbona ueleweki leo?". Swali la juli lilimshtua vanessa ,kwenye dimbwi la mawazo akawa hana jibu sahihi la kumpa akabaki, kumbabaisha tu " hamna juli mdogo wangu nawaza mitihani sijui itakuwa migumu?".alivunga vanessa na kujifanya kuuliza ili kupoteza mada. " mmmh!! Dada usiwaze mbona nakuaminia itakuwa ya kawaida muhimu usome ". Alimjibu juli, vanessa akatingisha kichwa kukubali. Ila hakukaa sana akamuaga nduguye akaingia ndani kwake.
*********
Siku ya pili, vicent alitoka mapema nyumbani, aliwahi shule kabla hata ya rafiki zake. Hii yote ni kutokana hata usingizi haukupatikana,kutokana na mawazo aliyo nayo. Alikuta baadhi ya wanafunzi wapo darasani, Alifika akakaa kwenye kiti na kufungua begi,kuchukua kitabu na kuanza kusoma. Ila hata sijui nini kilimtuma kutazama mbele maaana alijikuta anatoa macho......itaendelea

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA TANO (05)
CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA TANO (05)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/07/choice-of-my-heart-chaguo-la-moyo-wangu_98.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/07/choice-of-my-heart-chaguo-la-moyo-wangu_98.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy