CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SITA (06) | BongoLife

$hide=mobile

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SITA (06)

CHOICE  OF MY HEART (chaguo la moyo wangu)

 

MTUNZI: Minnah De Embaccas


 Whatsapp :0656282898


 SEHEMU YA SITA (06)


ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO: Siku ya pili, vicent alitoka mapema nyumbani, aliwahi shule kabla hata ya rafiki zake. Hii yote ni kutokana hata usingizi haukupatikana,kutokana na mawazo aliyo nayo. Alikuta baadhi ya wanafunzi wapo darasani, Alifika akakaa kwenye kiti na kufungua begi,kuchukua kitabu na kuanza kusoma. Ila hata sijui nini kilimtuma kutazama mbele maaana alijikuta anatoa macho. ENDELEA.......

Alijikuta Anatoa macho, baada ya kuona,marafiki zake nao wamewahi shule. Aiseeee vicent alichekaaaa sana, mpka akajishika tumbo. "hadi nyinyi mmewahi leo aaah kweli mtihani siyo poa".aliongea vicent huku anawatazama kwa zamu. "mimi mwenyewe sijaamini nilivyo kuona ndo maana nikasimama mlangoni nihakikishe ni wewe au hahhhhhah".aliongea Richard huku anaelekea kule alipo vicent.ila cha kushangaza suma akuchangia neno zaidi ya kuachia tabasamu na kutembea kwenda walipokuwa wenzake. "aiseeee kama tuliambizana yani"aliongea tena vicent. Hapo suma ndo na yeye akanyanyua,mdomo wake na kuongea. " hivi unajua kwanini nimeshindwa kuongea chochote?,nikwasababu naona uchuro hapo nje nimekutana na rich, hapa nakuona wewe, nikawa najiuliza hivi hawa waliambizana nini mimi wamenichunia ila nimewabamba".aliongea suma,huvu anavuta kiti anakaa. "hii ili iweje sasa imetokea tu"alijibu richard. "sisi hatuwezi kukufanyia hivyo kwasababu sote ni wamoja". Alisema vicent, suma hakuwa na neno. " oyaa tusomeni basi kabla muda wa kwenda mstalini aujafika"aliongea tena vicent. "poa mwanangu umeongea point" alijibu suma.basi kikapita kimyaa,kila mtu alifanya yakeee kwa muda huo. 

*******

Mwezi ulipita,hatimae miezi, na si vicent, wala niram aliye kumbuka kama walishawahi kuonana. Basi ilikuwa weekend, moja walionekana marafiki, watatu wakiwa wamesimama stendi ya mabasi,si wengine bali ni vicent, richard na suma wakiwa wamevalia nguo za nyumbani.ilibaki kama wiki mbili wafanye mtihani. Ilionyesha kuwa walikuwa wamelewa kwenye maongezi sasa sijui vicent, walikuwa wanasubiri usafiri maana vicent hakuwa na gari siku hiyo. 

Mara gaflaa walishtushwa na sauti, nyororo iliotokea,barabarani.

"vicentiiiiiiiiiiiii" ilikuwa sauti ya niramu, aliekuwa ndani ya range nyekundu, huku akiwa amependa,kupindukia wanasemaga kadamshi, ile mbayaaaa. Wote macho yalikuwa mbele,ila hakuna mtu alieshtuka kama vicent, maana akutegemea kuonana na binti yule ana muwaza siku zote. Na ilikuwa muda


Awajaonana. Kiukweli vicent, moyo ulikuwa unampenda mbio vibaya.ila alijikaza, huku nyuma suma pamoja na richard, aisee!! Macho yaliwatoka maana walishindwa kuelewa, wanae muona machoni mwao, ni jini au malaika. Vicent alijikongoja mpaka kwenye dirisha la gari, na kumsababishia niram. " mambo niram siamini kama ni wewe, kumbe unani nakumbuka? ".alijikuta anaongea mfululizo vicent huku akiuliza, swali humohumo. "poa vicent, nakukumbuka sana vp leo huna usafiri? Maana naona kama mpo wenyewe mnasubiri usafiri? ".aliuliza niram,huku macho akiwaelekezea wakina rich. "aaah ndiyo tunamsubiri dereva tax mmoja hivi,katuambia hayupo mbali".alijibu vicent huko akiangalia huku na kule kama anaetafuta kitu. "haah kwani mnaelekea wapili niwape lifti?maana mimi naelekea mbezi"aliuliza niram. Vicent akapiga mahesabu ya haraka,alafu akaongea. "aaah! Wale wanarudi nyuma ila mimi naenda kunduchi" alijibu vicent. Ila wadau ngoja niwaambie kitu, vicent ameongopa, kwasababu wenzie wanaenda kawe sawa yeye anaenda kunduchi, ila njia ni ileile wameachwa wakina suma, yeye angeendelea mbele, ila aliamua kusema vile ili aweze, kutupa ndoano Kiulaini. Tuendelee, basi niram akamwambia "basi twende nikupe lifti waage wenzio".vicent akachomoka na kuwafata, wenzie alimkuta suma anashauku si mchezo. " vipi yule ndo yule demu uliesema? Na anaelekea wapi ili atupe lift basi kama vipi" alijikuta anaongea maneno,mfululizo na swali juu. "hamna aendi huko kaniambia nimsindikize kariakoo".aliongea vicent huku anageuka nyuma, akagongana macho na niram,wote wakatabasamu. "duuuh mwana kwahiyo umetuacha? ".aliongea richard huku anakazia macho kwenye gari. "aaah aina jinsi ila chukueni hii mpande tax".alisema vicent huku anazamisha mkono mfukoni na kutoa noti tatu za elfu kumi akamkabidhi suma. Suma alizichukua na kuzitia mfukoni. "oyaaa Usikose kutupigia ukifika home"alisema rich. Na suma akadakia. "ndiyo utupe data zote maana duuuh! Mpaka nakuonea wivu".vicent hakutia neno aliishia kutabasamu huku Anaendelea kutembea, basi aliingia ndani ya gari, huku ukimya mwingi ulitawala.vicent akaona avunje ukimya, "basi nilijua utanisahau kabisa".aliongea Vicent Huku ametoa tabasamu hafifu usoni mwake, Huku macho yanatazama mbele. "Ooooh!!Hapana siwezi kukusahau,mtu muhimu Kama wewe Kwa ule Msaada wako ".aliongea Niram,huku anamwangalia Vicent, macho yakakutana, wote wakatabasamu, Niram akageuka mbele na kuendelea, kuushika usukani akizidi kukanyaga mafuta. "hahhhhah!! Ni kweli niram lakini Siyo wote wanao kumbuka fadhila".aliongea Vicent ,Huku kimoyomoyo akiomba wasifike haraka. "haaahhh sawa bwana Wala ujaongopa, ".aliongea niram,huku akizidi kuuchapa mwendo, na bahati nzuri hakukuwa na foleni. "niram nikuombe kitu Kama hutojali? ".aliuliza Vicent Huku amemgeukia kabisa, aliongea Kwa sauti nzito, tens yakubembeleza. "usijali Kama kipo Ndani ya uwezo wangu ntakupa".alijibu niram. Vicent hakaona asizubae Sana, akasema alilokusudia."nilikuwa naomba unisaidie namba yako ya simu ili niwe nawasiliana nawe hata kukujulia Hali,maana tushakuwa marafiki".aliongea Vicent,kwa umakini wa hali ya juu ili asije kukosea step,akamkwaza Niram. " Ooooh!! Wala usijali Kwa hilo".alisema niram, huku anamtajia namba zake. Vicent aliziandika kwenye simu yake. " asante sana".alishukuru vicent. "asante nawe kwa kushukuru".alijibu niram, mara ikawa kama vituo viwili vicent ashuke. "sasa niram mie nashuka hapo kituo kinachofuata utaniacha hapo" aliongea vicent, lakini kama ungemuona moyoni mwake, alichukia kupita kiasi, alitamani wazunguke mpaka alfajiri. Duuuuh kweli mapenzi siyo poa wadau. "haaah ni hapo oky sawa"alijibu niram, na alipofika, akakanyaga break, na kusimamamisha gari. "oooh!!asante sana umenifaa mungu akufikishe salama".aliongea vicent huku anafungua mlango wa gari na kushuka. "haya asante ufike salama pia".alijibu niram, akawasha gari na kuishia, vicent alibaki anampungia mkono, mpaka alipo ishia. Kiukweli ile siku aliiona ya bahati sana kwake, hakika alikuwa na furaha mno. Alifika kwao. Akagonga geti likafunguliwa, alikuta mlinzi akamsalimu, na kuingia ndani hakumkuta yeyote ndani zaidi ya house girl. Alimsalimia akajitupa kitandaniii , pwaaaaaaah!! Aliangalia sana juu vicent, hakika kuwa na namba ya niram,kwake ilikuwa ni furaha tupu. 

*********

Vanessa alikuwa mezani wakipata chakula cha usiku, maana leo ilikuwa weekend kwahiyooo alikuwa mwenyewe jikoni, ila leo mawazo yalipungua kwani mawasiliano yalikuwa kama zamani na hadi asubuhi ya siku hiyo, vicent alimuaga kuwa atatoka na wakina richard. Mara ghafla alishtukia, akizibwa macho. "mmmh juliana nini bwana,ebu acha mzaha njoo ule"aliongea vanessa. " mmmh dada kwahiyo wewe mtu wako wa karibu ni Vanessa tu? ".aliuliza kwa manung'uniko Clara. Mdogo wake wa nne akitoka huyo ndo juliana, kumbuka wakiume ni wawili kwenye familia yao na ndio wakwanza na wapili. "hamna mamy wote nawapenda ila nilijua yeye, kaa chini ule mdogo wangu".aliongea Vanessa kwa sauti ya kubembeleza,huku akimvuta akae. Basi mambo yakaisha,walikula kwa furaha, wazazi na kaka zao hawakuwepo, walibaki wenyewe. 


*********

Niram alikuwa chumbani kwake akijisomea, wakati huo alikuwa ameshakula, alikuwa kitandani miguu kuegemeza ukutani, muda wote alikuwa mtu mwenye tabasamu usoni, kilicho mfurahisha akijulikani

Mara ghafla simu ikaanza kuita...... Itaendelea

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SITA (06)
CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SITA (06)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/07/choice-of-my-heart-chaguo-la-moyo-wangu_75.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/07/choice-of-my-heart-chaguo-la-moyo-wangu_75.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy