Young Paster sehemu ya tisa (09)

Young Paster 09


Ilipoishia …

MCHUNGAJI MCHANGA

Sasa ile anafika tu ndani ya kanisa, alikutana na viongozi mbalimbali wa makanisa hapa jijini Arusha,.. Lakini alipoangalia vizuri alimwona Catherine na baba yake, ghafla akamwona hata baba yake mr jacob, lakini mr Jacob alikuwa katika moja ya jasira mno,… Adam alijua sasa hapa kumekucha, akiangalia vizuri mpaka wale wanaohusika na mambo ya ndoa wapo, hapo tumbo la adam likaanza kuwaka moto,… Mana hakuutegemea huu wito utakuja kuwa hivyo,
“asifiwe bwana mwokozi wetu alie hai”
Alitoa salam huku akivuta kiti akae,
“milele amina baba mchungaji”
Adam alikuwa na hofu, mana hapo hakukuwa na muumini mdogo mdogo hata mmoja, yaani wote hapo ni viongozi wakubwa wa makanisa mbalimbali hapa jijini, yaani muumini mdogo mdogo ni Catherine peke yake, sasa haijulikani pana kikao gani

ENDELEA NAYO……..

Adam alikuwa haamini kama leo anafungishwa ndoa ya lazima lazima, mana kama ni kanisa lake tayari limeshakamilika kila kitu, ni yeye kuchaguliwa kuwa mtoa huduma katika kanisa hilo, mana kama ni wito anao na tayari keshapokea wito kuwatumikia kondoo wa bwana,.. Adam alianza kukusanya hasira, na hapo ni mbele ya viongozi mbalimbali wa makanisa yote hapa jijini Arusha… Mabishop wote wamejaa hapo, na haijulikani kuna nini… Lakini wakati adam akiendelea kuwaza kuhusu kikao hicho, ghafla lililetwa joho la rangi nyeusi mchanganyiko na nyeupe,.. Tena joho jipyaaaaa…. Hajakaa vizuri mara yliletwa maji ya baraka,.. Mpaka hapo adam aifurahi sana, na hapo hapo Mabishop wakaanza kufurahi na kupiga makafiri,…
“haleluyaaaaaaa”
“ameeeeeeen”
“nasema haleluya”
Alisifu Bishop mmoja mkubwa hapo jijini, huku viongozi wengine wakipokea sifa hio,…
“aaaameeeen”
“bwana asifiwe sanac
“ameeen”
Maji ya baraka yaliletwa kisha akamwagiwa adam,… Yaani hapa sasa ndio anaupokea wito wa kuwa mchungaji rasmi, mana mchungaji wa kanisa ni lazima uchaguliwe na wakuu wa makanisa, sio lazima Mabishop wawepo, hata pasta wa kawaida anaweza kukuchagua kuwa pasta.. Ila sema mr Jacob yeye anajulikana sana na hakupenda mtoto wake apokee wito kwa kusua sua,..
“mpaka sasa umeshapokea wito, sasa unaweza kuliendesha kanisa lako… Bwana yesu asifiweeeeeeee”
“aaaaaaaaaaaaaaameeeeeeeen”
Zilikuwa ni shangwe japo hapakuwa na waumini wengi zaidi ya hao hao viongozi,.. Yaani muumini anatakiwa kusikia tu kuwa tayari mambo yamekuwa mambo,… Mwanamke wa kwanza kumrukia adam alikuwa ni Catherine,… Adam alitamani sana kumkwepa lakini ilishindikana kwasababu kuna baba yake binti, kuna baba yake huyo adam… Afu watu wakubwa walikuepo, na hapo ndio kwa mara y kwanza Catherine analipata kumbatio la adam.. Kumbe Viongozi wote wameshajuzwa kuhusu adam na Catherine, saaa ngapi hawajaanza kusema
“inapendeza sana… Watoto wa viongozi kuoana, inapendeza sana”
Aliongea Bishop mmoja ambae nae ni mualikwa, adam hakutaka kuonyesha nidhamu mbaya mbele ya viongozi wakubwa wa makanisa,..

“kuanzia leo… Sasa una kanisa lako.. Sasa hata ukianza na waumini 10.. Utajua mwenyewe, ni wewe na juhudi zako”
Ilikuwa ni kauliza ya baba yake adam, ikiongea nae…
“ni kweli… Hata sisi usione sasa tuna wito wa Bishop, sisi tumeanza na muumini mmoja, mpaka sasa tuna makanisa meeengi sana.. Tena huyu mtoto ana bahati nzuri sana… Sisi enzi zetu tulikuwa na makanisa… Yaani hata halijapauliwa… Lipo wazi kabisa… Lakini wewe unakwenda kuanza uchungaji ukiwa na kanisa la kifahari”
Yalikuwa ni maneno ya pasta mmoja aliohusika katika swala zima la kumbariki katika kulitoa au kulitangaza neno la Mungu,… Na uzuri adam amekwenda chuo cha Biblia na kuyasoma yote yaliostahiki.. Mana kusoma Biblia kila mmoja anajua,.. Tatizo ni kuifafanua maana zake…
“bwana Yesu asifiwe”
Aliongea adam huku akinyoosha mikono,..
“milele amina”
“kwanza niwashukuru wote kwa ujioni wenu, naamini yoye hayo ni kwa neema za mungu…. Bwana yesu awatangulie viongozi wangu”
“ubarikiwe kijana…. Umri wako ni mdogo, ila wito unapoupata huna budi kuufanyia kazi”
“ni kweli mchungaji… Nashukuru sana kwa kunidhihirishia wito huu… Yesu awabariki saaaana”
Aliongea adam kwa furaha ya hali ya juu mno, huku akiketi katika kiti,…
“unajua sisi tunapomchagua mtu kuwa kiongozi wa kanisa fulani,.. Kwanza hata wakati wa kumwita haambiwi, na pia anapokuja hatutakiwi kuonyesha sura za furaha, ispokuwa huzuni mwanzo mwisho”
Aliongea Bishop mmoja mwenye asili ya kizungu, huku Mabishop wengine wakipokea maneno hayo, kana kwamba ndio torati yao ya kila wanapomteuwa kiongozi mpya wa kanisa fulani,…. Adam alifurahi sana mana alijua kutokana na kukataa kuoa huenda asipate nafasi ya kupata wito wa kuchunga kondoo wa bwana… Lakini pia hakuwa na wasiwasi sana kwasababu siku ile anawekwa kikao na baba, mama na dada, kuna mtu alimpigia simu akiwa yupo nje tena ndani ya gari,… Kama unakumbuka kuna sehemu aliongea na mtu fulani ila sisi hatukujua aliongea na nani… Sasa adam alipokuwa akitoka nje alikutana na mzee wa kanisa lao hilo alipokuepo muda sio mrefu,…
“ukawachunge vyema kondoo wa bwana…. Hakikisha unakwenda na junsi hali inavyotakiwa. Sawa bwana mchungaji”
Aliongea mzee wa kanisa na wakati huo Catherine keshapata nafasi ya kumganda adam, yaani siku moja yu kupata nafasi ya kumbatio la adam basi kamganda moja kwa moja…
“mzee ndio mana juzi nilikupigia simu, kuwa ivi ukikataa kuoa unaweza kweli kukabidhiwa kanisa.. Uliposema ndio… Kiukweli nilifurahi sana mana napenda kuwa mchungaji katika roho, yaani nimejikuta tu napenda, sasa sikutaka ndoto zangu kuishia njiani, au wito wangu kuishia njiani”
“basi baba mchungaji.. Kilichobaki sasa ni kiteuwa wasaidizi wako katika kanisa lako… Wazee wa kanisa, waalimu, nabiii, na wengine wengi wenye vipawa vyao”
Aliongea mzee wa kanisa huku Adam akitoa mkono wa Catherine kwenye bega lake,…
“kama ungelikuwa ni mwanamke mwenye adam, basi huu uzungu wako ulitakiwa uwe mkiwa wawili na mumeo, sio huku kwenye nyumba za ibada”
Adam alimwambia Catherine, mana Catherine ile nafasi ya kumbatio ndio kapata dezo, kaganda kabisaa… Yaani adam anamchukia sema ni mtumishi wa mungu, hivyo hatakiwi kumchukia mtu kiasi hicho….
“mtumishi adam… Lakini kwanini unanifanya kuwa mdhaifu kwako.. Eti baba”
Adam hakutaka kumjibu chochote kile zaidi ya kuagana na mzee wa kanisa…  Kisha akawa analielekea gari lake,… Na Catherine nae yupo nyuma yake
“huna pakwenda”
Adam alimuuliza Catherine…
“baba mtumishi… Hata yesu alikuwa na wafuasi wengi sana mpaka wanawake,.. Lakini hakuambiwa awaoe, sasa siwezi kulazimisha kitu ambacho hakitakiwi,… Mimi ni kondoo wako, nipe nafasi kwenye kanisa lako… Hata ukiniweka kwa waimba kwaya, nitashukuru sana baba mtumishi”
Catherine aliongea mengi, yaani kama unamuona ungelimuonea huruma, lakini kweli hapo anafunika riziki ya mwenzie ambaye ndio mwenye nafasi ya kuolewa na adam,
“siwezi kuteuwa mwimbaji wa kwaya anaevaa nguo fupi”
“nipo tayari kubadirika kwa njia yeyote ile, na pia nitamheshim mama mchungaji mtarajiwa”
Hapo adam kidogo akapata timaini juu ya maneno ya Catherine
“apo sasa kidogo umeongea pointi… Nipe muda nitakuchagulia nafasi kanisani kwangu”
Aliongea adam wakati huo Catherine alitamani hata kupiga magoti kwa kukubaliwa nafasi yeyote ya kanisani kwa pasta adam… Na hivyo ndivyo alivyotaka,.. Sasa mambo yanaiva taratibu, maskini eva wa watu sijui atakaza buti kwa staili gani, mana ndio taratibu anaanza kunyang’anywa mume… Basi adam alipanda gari yake na hata Catherine nae alipanda gari yake kisha kila mtu akapita njia yake… Ukumbuke adam aliwaacha mama yake na dada yake kule nyumbani kwake wakiendelea kufanya usafi mana adam ndio alikuwa anahama siku hio….. Moja kwa moja mpaka nyumbani kwake, lakini kwa bahati mbaya hakuwakuta walikuwa wameshaondoka muda tu, lakini mezani alishaandaliwa kila kitu, sasa maisha ya ubachela ndio anayaanza…. Hapo anawaza kanisa lake litakuwa na vipawa vya aina gani, yaani alikuwa akipanga mengi sana juu ya kanisa lake,…. Lakini ghafla simu yake inaita, kuangalia alikuwa ni mama yake.. Alipo pokea tu akakutana na sauti ya mama yake
“haleluyaaaaaaaaaa….. Bwana Yesu Kristo atukuzwe kwa kupambana juu yako mwanangu.. Hongera, nimepata taarifa sasa hivi tayari umeshaupokea wito ulioitwa na baba muumba”
Aliongea mama adam huku akionyesha kuwa na furaha ya hali ya juu, na aliamini mpaka hapo adam hawezi muoa Catherine, mana ilikuwa bila kuoa hapewi wito huo, sasa keshapewa….
“tumsifu yesu Kristo, baba alie hai”
“milele amina mwanangu”
“mama… Kesho nahitaji kwenda kulifungua kanisa na nyimbo za kuabudu,… Siku nzima waumini wajue tayari kanisa limeshafunguliwa.. Mama.. Kanisa langu litakuwa kanisa la kipekee katika huu ulimwengu.. Litakuwa kanisa la uokovu kwa kila muumini”
“baba nakuunga mkono… Dada yako huyu hapa nae anaruka ruka”
“mpe simu dada Jessica”
Adam alitaka kuongea na dada yake, mana alipo waacha, hakusema anakwenda wapi,
“YOUNG PASTOR in the church… Thanks Jesus, for your power to my brother”
Alikuwa ni Jessica akiyaongea hayo maneno kwa furaha ya hali ya juu
“sasa ndio nini hivyo… YOUNG PASTOR ndio maneno gani dada”
“mtumishi adam… Haijawahi tokea kwa kijana mdogo kumiliki kanisa, tena kwa kishindo… Hata wewe unajua ni kanisa gani linamilikiwa na kijana? Hakuna, yaani wewe ndio wa kwanza”
“basi sawa lakini hilo jina si sahihi, nitakushtakia kwa mungu”
“basi baba mtumishi… Ila nina furaha sana juu ya jambo hili, kesho nakuja kushinda kanisani kwa ajili yako kaka yangu”
Yalikuwa ni maneno ya Jessica, yaani familia nzima ipo nyuma ya adam, yaani inapendeza zaidi kwa hali kama hio…..
Baada ya masaa kadhaa ikiwa ni usiku, Adam alifanya maombi kabla ya kulala kisha akalala zake ikiwa ndio siku ya kwanza kulala katika jumba hilo kubwa sana…..

************
Ghafla alishtuliwa na ngurumo za ajabu, akiangalia saa ni saa nane za usiku, na ngurumo hizo zinatokea humo humo ndani, adam alisali kabla hajafuatilia ngurumo hizo, ilikuwa ni usiku tena tena umeme ulikuwa umekatika,.. Hakuna kitu kibaya kama umeme ukatike afu jumba kubwa tena yupo pekee,…. Alichukuwa simu yake na kuwasha tochi kisha akaanza kuzunguka ndani ya jumba hilo… Alipita vyumba vyote lakini muumgurumo bado ipo kama vile kuna watu wanasali kwa imani ya kishetani,… Lakini kuna chumba kimoja hicho hajawahi kukifungua toka kuzaliwa kwake, yeye hukiona tu.. Hakutaka kukiacha, na kweli katika hicho chumba kulisikika sauti za wati kadhaa wakifanya ibada,.. Wakati huo adam nywele zake zinamchemka.
Kiukweli ni sauti zilizokuwa zikitisha sana…. Lakini adam ni mtumishi wa Mungu, yupo tayari kufa kwa ajili ya kondoo wake, kama alivyokufa Yesu Kristo kwa niaba ya wakristo wote,.. Adam alikibonyeza kitasa cha mlango na kwa bahati nzuri hawakufunga mlango, hivyo adam akasukuma mlango ule kisha akaingiza kichwa…. Ilisikika tu sauti ikisema
“haaaaaaaaaaa”

Je? Kuna nini katika maisha ya adam, na kwanini wafanyie ibada katika jumba hilo?? USIKOSE

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : Young Paster sehemu ya tisa (09)
Young Paster sehemu ya tisa (09)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-tisa-09.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-tisa-09.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content