Young Paster sehemu ya thelathini na moja (31)

YOUNG PASTER EP 31

Ilipoishia ………..

MCHUNGAJI MCHANGA

“heeeeeee nani tena”
Adam aliuliza huku kichwa kikianza kumuuma, mana mercy yupo ndani,..
“huyu dada anakujaje kufanya usafi saa hizi jamani”
Aliongea adam huku akizunguka vyumba vyote,…Adam alikwenda kufungua mlango huku akisema
“namfungulia afu namfokea hata kama ni dada angu,.. Najua nikimfokea kwanini anakuja saaa hizi, najua hatoingia ndani”
Aliongea adam huku akifungua mlango mdogo ili amtokee huko huko nje ampe makavu live…. Sasa alishangaa ni familia nzima mpaka mama, mbaya zaidi hata eva yupo..
“heeeee mama.. Kulikoni tena”
Adam aliongea kwa mshangao mkubwa, huku akiwa kama haamini, sasa adam saa hio hio baada ya kufungua mlango aligeuka na kutaka kurudi ndani kabisa….
“wewe fungua mlango… Afu si ulisema unaumwa wewe…. Hebu fungua mlango tumekuja na daktari”
Adam haamini kwa ujio huo, ilimbidi tu afungue geti kubwa, waingie ndani

SONGA NAYO…….

Sasa hapa tuanzie nyuma kabla ya ujio wa akina Jessica na mama yake pamoja na eva,….

Njia alionekana Catherine akiwa na gari yake kuja kwa akina adam, yaani nyumbani kwao,.. Lakini hatujui ujio huo ulikuwa ni wa nini, na nyumbani kwa akina Jessica, eva yupo kajaa tele,.. Catherine alishika simu yake na kumpigia adam,…
“halo mtumishi, tumsifu yesu Kristo”
Huyo ni Catherine aliomsalimia adam kwa kumsifu yesu Kristo, wakati huo adam kakamatia kiuno cha mercy,…
“milele amina…. Haya kunani saa 12 hii jioni”
Aliuliza adam na hapo alikuwa mchangamfu mana alikuwa katika kiuno cha Mercedes..
“Samahani, hapa naelekea kwenu, nakwenda kuwaomba msamaha kwa yote yaliotokea,.. Na kukuacha huru na mchumba wako”
Aliongea Catherine tena kwa huzuni sana
“aaahhhh, katika siku umenifurahisha ni leo, yaani upo tayari mpaka kwenda kwa wazazi”
“sio nipo tayari, ndio naenda nipo njiani hivi sasa”
“sawa, safari njema mama angu,.. Nakupenda sana kama rafiki yangu”
“sawa mtumishi… Ila tafadhali sana, asijui mtu kuwa umenitoa bikra yangu”
“mpaka sasa anaejua ni mmoja tu”
“nani tena jamani adam”
“mimi tu”
“aaaahh we akili yako haiko sawa wewe”
“mimi mchungaji mzima akili yangu haipo sawa”
“Nisamehe baba mchungaji”
“ebu nenda na safari zako, tusije kuharibiana siku jioni hii”
Catherine alikata simu ili asije kumvuruga adam mana hakawii kuvurugika,… Catherine aliendelea na safari yake ya kwenda kwa akina Jessica kuwataka radhi kwa mvurugo wa kifamilia aliouleta, mana adam mpaka sasa hajaona kwasababu ya huyu huyu Catherine,

Sasa baada ya muda ndio mama yake adam anampigia mtoto wake adam kumuuliza ishu ya eva kubakwa yeye anaijua,… Wakati huo adam keshamaliza hemu lake kwa mercy, sasa kachoka kweli… Mara simu inaita, alipocheki ni mama yake,.. Alimpokea na kuongea nae, lakini wakati wanaendelea kuongea, mercy alikuwa anakuja huku akiwa anaimba kwaya, na hapo hapo adam alisema hajiskii vizuri,… Sasa adam akakata simu ili mama yake asisikie sauti ya mwanamke hapo ndani, mana Haruhusiwi kuwa na mwanamke ndani,.. Sasa vile alivyokata simu iliwafanya wana familia kupatwa na wasiwasi afu ukizingatia adam anaishi peke yake,… Ikabidi wafunge safari familia nzima kasoro baba na mfanyakazi.. Mana baba alikuwa hayupo,…

Sasa walipokuwa wanatoka getini, ndio wakakutana na Catherine nae anapiga honi ili afunguliwe aingie,… Sasa wakakutana mlangoni, lakini familia ilikuwa na haraka sana ya kutoka mpaka Catherine akashangaa wanakwenda wapi wote afu kwa haraka hivi… Ikabidi apige honi kama kiwauliza… Ndipo mama akafungua kioo na kumwambia Catherine kuwa
“Samahani mwanangu… Uje kesho.. Sasa hivi tunakwenda kumchukuwa daktari twende kwa adam anaumwa sana”
“mungu wangu… Anaumwa saa ngapi na muda huu…. Uuuww basi nami nakuja huko”
Catherine anamalizia kuongea tu, mama katoa gari kumchukuwa daktari,

Sasa Catherine anajiuliza kuwa, huyo adam kaongea nae sasa hivi tu na alikuwa kachangamka… Sasa iweje awe hoi mara hii… Sasa Catherine Ikabidi tena apige simu kwa adam
“Catherine una nini we mtoto wa kike, mbona msumbufu hivyo”
Aliongea adam baada ya kupokea simu ya Catherine
“yaani unadiliki kuisumbua familia yako eti unaumwa… Wewe unaumwa wewe”
“nani kakwambia mi naumwa”
“mbona nimepishana na mama yako dada yako akiwa na yule mchumba wako wanakuja kwako eti unaumwa”
Aliongea Catherine huku adam akishangaa,
“ati unasemaje wewe?.. Wanakuja huku kwangu”
“ndio”
“lakini mimi sijasema naumwa”
“ndio wanakuja hivyo… Tena nilitaka kuja sasa siji… Acha izo kusumbua watu”
Mara simu ikakata,… Kumbe adam kaikata makusudi kwasababu Catherine hamalizi kuongea maneno yake

“Mercedes, we mercy… ”
“abee”
“chukuwa kila kilicho chako na uende”
“kuna nini? Si ulisema tunalala wote”
Aliongea mercy huku akiwa mvivu kutoka
“mercy jamani… Mama na Jessica wanakuja huku eti mi naumwa”
“sasa kwanini useme unaumwa jamani”
Mercedes alikuwa hataki kutoka kabisa,…
” nakuomba mercy,.. Wanakuja na gari ya nyumbani watakukuta mama angu ondoka”
Mercedes aliona bora atoke asije kumharibia mpenzi wake,.. Mercedes haraka haraka hata kuoga hajaoga, kakusanya kila kilicho chake na janaba lake, kisha kaitiwa bodaboda kisha hiyooo kaondoka zake….

Adam akarudi ndani haraka akatandika kitanda kisha akaenda kuoga,.. Aliporudi alianza kumwaga marashi nyumba nzima, mana wanawake hua wanajuana harufu zao, alimwaga marashi mengi mpaka vinakera sasa…. Sasa akakaa kwenye sofa.. Ndio ghafla anaskia honi inapigwa huko nje… Adam alikwenda na kujifanya kama hataki kufungua hivi lakini hapo yupo free kabisa…

“wewe fungua mlango… Afu si ulisema unaumwa wewe…. Hebu fungua mlango tumekuja na daktari”
Adam haamini kwa ujio huo, ilimbidi tu afungue geti kubwa, waingie ndani

SASA HAPA TUENDELEENI TULIPOISHIA..

Adam alifungua mlango gari ikaingia mpaka ndani kwenye paking, kisha wakashuka kwa kumkimbilia adam..
“we si ulisema unaumwa wewe”
Aliongea mama yake adam baada ya kushuka kwenye gari,
“ingieni ndani kwanza mbona mpo nje kama wezi…”
Aliongea adam, hata mama haamini adam siku hizi kabadilika sana,… Basi wote na daktari waliingia ndani
“daktari, hebu mpime huyu mtoto, anaweza kujifanya anajikaza tu hapa… Mana namjua huyu ni muoga wa sindano na dawa… Mpime”
Mama Jessica aliongea huku dokta akifungua mikoba yake aliowekea zana zake,..
“lakini mama, mimi mbona siumwi, nilikwambia tu mimi ni mchovu, sijiskii vizuri… Ndio simu ikakata mana mtandao ulikuwa unasumbua”
“sasa kwanini usipige tena jamani…. Afu mbona huku ndani kuna marashi sana, unaishije na marashi mengi hivi… Utaumia wewe”
Aliongea mama, baada ya kunusa marashi yaliokithili kiwango cha kupigwa,…

Dokta alimpima lakini kweli hakuwa na ugonjwa wowote ule, ila ni uchovu tu ndio uliomsumbua…
“basi baba,… Utarudi na mwanangu marha, akupeleke kisha atatukuta hapa”
Aliongea mama huyo, kuwa dokta huyo apelekwe na martha, kisha atarudi hapa….
Basi martha alitoka na dokta huyo kama vile kumpeleka mana walikuja nae na gari yao, hivyo wasimwache arudi kwa tax au bodaboda,..

Sasa baada ya martha kuondoka na dokta, mama alianza kukumbushia ishu ya eva kubakwa ni ya kweli au inakuwaje,
“mwanangu, kuna picha zimeanza kuzagaa mitandaoni, picha zinazoonyesha nguo za eva… Tumeziona, lakini eva anasema hilo swala unalifahamu, ndio mana nikakupigia muda ule ili nijue”
Aliongea Rebecca au Joyce… Huyu mama yake adam ndio anaitwa Joyce au ukipenda mwite Rebecca..

“ni kweli mama…. Alinipigia simu usiku ule, nikatoka lakini kabla sijafika nikakuta kelele, nikaona nitoe msaada kwanza kisha nifuate pale kanisani… Lakini kumbe huyo huyo ninaemfuata ndio aliokuwa anapiga kelele kichakani… Lakini kwa bahati nzuri, hawajafanikiwa kumgusa jpo nilimkuta kazimia… Sasa kutokana na ile hofu na haraka ya kumwahisha hospitali, nikasahau kukusanya zile nguo… Hivyo ndivyo ilivyotokea, lakini eva ni mzima na hajaguswa licha ya kusaminisha mimi mwenyewe, pia tulipofika hospitali alipimwa na daktari wa kike, na pia akamthaminisha na kugundua, bado hajaguswa… Kwahio kama kuna taarifa tofauti mlizo zipata ni uongo”

Adam alimaliza kuongea, na mama hakuwa na la kusema tena,… Alimkumbatia eva kwa mara nyingine tena,…
“pole mwanangu… Usiwe Unakwenda misa za usiku”
Jessica nae hakuwa mbali kumwomba msamaha eva kwa kuwahi kumsemea mabaya bila kuchunguza,… Na adam Hujaogopa kusema ukweli wote mbele ya mama yake, mana akianza kuongopa, eva atachukiwa na familia ya adam…
“Nisamehe wifi yangu… Unajua katika familia yetu, hatutaki mwanamke ambaye atanyooshewa vidole na watu… Nisamehe sana mana kwa dakika chache tu nimetokea kukuchukia ghafla tu kwa hilo… Nisamehe”
Aliongea Jessica huku eva akimsamehe kila mmoja… Na sasa eva na adam wanasubiri siku waamue kuoana, mana ruksa imeshatoka kwa baba yake aliekuwa kizuizi cha ndoa hio.. Shida ya baba alitaka adam awe mhuni mana ana nguvu za upako wa kweli kuliko baba yake, hivyo akiwa mzinifu, mana yake keshatekwa na shetani, hivyo upako tena atakuwa hana… Na ni kweli adam sasa hata akihubiri sasa mahubiri hayana uzito wowote ni kama anapiga kelele tu,… Mwanzo akihubiri yaani mtu mwenye mapepo hata akiwa njia ya kanisa, anatetemeka, lakini sasa hivi hata awe nae karibu hatetemeki.. Ni kama ule usemi usemao, eti mwenye ndoa hawezi kushauriwa na mtu asie na ndoa… Sasa wewe ni shetani utawezaje kunishauri niache ushetani ingali wewe mwenyewe ni shetani…

Siku zilikwenda na leo ni siku ya Jumapili adam akiwa anajiandaa kwenda kanisani,… Mana ni muda wa kwenda kutoa ibada kwa waumini wake,… Mtumishi alitinga suti yake saafi kisha akatoka, wakati huo ni mtu mwenye furaha sana,.. Mana mahusiano yao yeye na eva ndio yanazidi kupamba moto… Wambea Wambea wote walikaa kimya mana wazazi wakikubali sijui wewe mbea una nafasi gani,….

Adam anafika kanisani kwa mbwembwe nyingi, na sasa kaacha mambo ya kuwa na wasichana mara kwa mara, sasa kupunguza kabisa… Na wapo baadhi ya wasichana keshagombana nao tayari, mana aliusikia umbea kuhusu mpenzi wake, adam anajua walikuwepo wasichana wengi waliotaka kuolewa nae,….

Sasa adam anaingia kanisani, anashangaa anakuta waumini nane tu akiwa ni mama yake, dada zake watatu, Eva na mdogo wake pamoja na mama yake, na mwingine wa nane ni vero, yule mschana aliosema ana bikra na ataolewa na adam… Huezi amini adam alivua miwani na kuangali kanisa lenye uwezo wa kubeba watu 400 (mia nne)  na zaidi, leo limebeba watu nane,.. Wakati huo watu hao nane walikuwa wanajifariji kwa kuimba kwaya, yaani hata wale wasichana ambao keshatembea nao kimapenzi pia hawapo,… Hapa ndio tujue kuwa mungi hachezewi, unakuwa kiongozi wa dini afu unafanya ufuska,.. Adam hakutaka kuingia kanisani, mana kanisa lilikuwa likipunguza watu kila siku, sasa leo limefikia watu nane tena familia yake yote ndio iliokuja kumsapoti adam…

“mbona anaondoka”
Aliongea Veronica, baada ya kumuona adam anaondoka kwa hasira,… Mtumishi wa Mungu hutakiwi kuwa na hasira za aina hio, kama wenyewe wanavyosema kuwa MCHEZO HUU HAUHITAJI HASIRA

Mama alitoka kuja kumwangalia mtoto wake kwanini haingii ndani, na katoka kwa hasira hivyo… Mama anatoka nje anakuta gari ndio inaondoka,…. Mungu hachezewi na maneno yake,.. Mnasema eti Yesu Kristo kaondoka na dhambi zetu, nani kasema…. Yaani ufanye dhambi zako afu umtegemee yesu, wewe na dhambi zako utachomwa peke yako, fanya yanayompendaza mungu wako kwa imani yako… Sasa familia kuona adam katoka na gari, na wao wakaingia kwenye gari kisha haoo,.. Vero na yeye hakukaa, akaondoka zake, mtu wa mwisho kutoka ni eva peke yake na mama yake na mdogo wake,… Wao walifanya maombi yao kisha eva akahakikisha kafunga kanisa kila mahali na ufunguo akawa nao,.. Alitoka zake taratibu mpaka nyumbani na hapo alikuwa na familia yake,…

Mama wa adam na familia yake walikwenda moja kwa moja nyumbani kwa adam, mana walimfukuzia hawakumwona, sasa sijui kaamkwa na kichaa au vipi..
Walifika nyumbani wakapaki gari nje mana rimoti hawana, ila funguo ya mlango mdogo anayo Jessica mana yeye ndie anaekuja kufanyaga usafi huku, hivyo ufungua anao,..
Waliingia mpaka ndani lakini hawakukuta mtu,… Mama alichoka, nanni lazima achanganyikiwe mama huyu,…
“hebu wewe baki hapa, ngoja mimi niende nyumbani huenda kaenda nyumbani”
Aliongea Joyce kuwa Jessica abaki yeye aende nyumbani,… Aliondoka na watoto wake wawili akamwacha Jessica peke yake,.. Kisha mama akaondoka…

Sasa huku mjini,… Mjini kumechafukwa,… Walikuwepo waumini waliomfahamu adam hata gari yake wanaifahamu
“Angel, we angel”
“nini bwana miriam”
“sio nini… Ona hii si gari ya mchungaji adam hii”
“mmmmhhh kama yake kweli”
“sio kama yake kweli… Ni yake, mi najua mpaka namba ya gari”
Aliongea miriam kuwa yeye anaifahamu gari ya adam,..
“pasta adam hawezi kuja kupaki gari mazingira haya… We unamjua pasta vizuri kweli wewe miriam… Mtu aliosomea dini aje hapa”
Sasa Angela akiwa anabisha, miriam alimuona adam mwenyewe,…
“haya sasa ona anachokifanya adam pale…. Bisha sasa na yule sie”
Aliongea miriam huku Angel akibaki domo wazi
“haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa…. Adam ndio kawa vile… Maskini ya mungu, adam kakutwa na nini tena”

Je? Adam anafanya nini?? USIKOSE

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : Young Paster sehemu ya thelathini na moja (31)
Young Paster sehemu ya thelathini na moja (31)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-thelathini-na.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-thelathini-na.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content