Young Paster sehemu ya thelathini (30)

YOUNG PASTER EP 30


Ilipoishia

MCHUNGAJI MCHANGA

“mamaaaaa”
“Abeee, kuna nini”
Mama aliitikia huku akija kama kumfuata Jessica…
“kuna nini”
“angalia”
Jessica alimpa simu mama yake na kuanza kuangalia picha…
“hii sketi si ile ambayo, tulishoneshaga kwa ajili ya kwaya”
“ndio hio hio”
“sasa nani kaitupa huku….. Khaaaa hii si nguo ya ndani hiii”
“ndio”
“sasa mbona husemi unaitikia tu”
“mwali wako huyo.. Kabakwa jana”
“whattttttttt?? Una maanisha eva au nani”
“kwani kuna nani mwingine…. Na inasemekana kuwa, alibakwa kwa hiari yake ili amkomoe kaka adam kwasababu anataka kumuoa Catherine”
“Whaaaaaat,… Ina maana huyu mtoto ni mchafu kiasi hiki…. Ngoja kesho kanisani tutaonana tu”
Mama hakujua kama eva keshafika hapo nyumbani…
“kanisani gani sasa na wakati eva mwenyewe yupo hapo sebuleni kaja sasa hivi”
“kaletwa na nini nyumbani kwangu”

SONGA NAYO…….


Kuna ule usemi uliosema kuwa, mazuri mia (100) baya moja (1) lakini unafukuzwa kama mbwa… Umefanya mazuri mengi sana lakini ukifanya moja baya, unafukuzwa iwe ni kazini au sehemu yeyote ile, hua wanasahau mazuri yake yote…

Sasa katika simulizi hii mwanadada eva anakutana na misuko suko ya umbea ingali si kweli kwa kitendo anachosingiziwa na marafiki zake, na ni kweli eva hajabakwa wala nini sema kwakua wini anataka kuolewa na adam, hivyo anamharibia ili aachwe, na licha ya kwamba anamharibia,.. Wini anajua ni kweli eva kabakwa,… Hivyo anahisi anayo yaongea ni kweli, lakini kumbe sio kweli

Eva leo kaitwa kwa wakwe aje apige stori na familia ya mume wake mtarajiwa lakini alipofika tu kakutana na hali ya tofauti kabisa….

“kanisani gani sasa na wakati eva mwenyewe yupo hapo sebuleni kaja sasa hivi”
“kaletwa na nini nyumbani kwangu”
Aliongea mama yake adam huku akienda mbio huko sebuleni ambako eva kakaa tena hana hata wasiwasi, yaani mwanamke ukichumbiwa mpaka kuolewa bila matatizo yoyote, basi mshukuru mungu wako,…
“shalom mama…. Shalom wifi”
Eva alinyanyuka kwa heshima na kuwasalimu wote mama na mtoto wake,…
Lakini Jessica alikuwa kakunja tu mikono huku akitikisa kichwa,… Mama sasa sema ni mtu mzima kiasi afu anajua busara za dini…
“kwanini toka jana hujatuambia”
Aliongea mama yake adam kwa kumfokea eva… Sasa eva anashangaa anaulizwa kwanini toka jana hajawaambia,… Haelewi atawaambia nini,
“ningewaambia nini mama”
Mama hakujibu, alimtupia eva ile simu kisha eva akawa anaangalia lakini eva hakushtuka sana, kushtuka kwake ni kuona kwamba kumbe hio ishu imezagaa hivyo, tena na picha zimepigwa,…
“ni kweli mama…. Lakini hawakufanikiwa kunibaka, kwani kabla ya kuondoka nilimpigia simu adam kuwa naogopa kuja nyumbani mana pale kwenye muembe kulikuwa na watu…. Lakini mtumishi akaniambia kuwa wale ni walinzi tu… Hivyo ikabidi nipite na usiku ule, na kila siku napita na wini lakini siku hio wini alikuwa keshatangulia…. Kweli walinichania nguo na ilifika hatua nikazimia, lakini nilizimia nikiwa tayari nimeshalisikia gari ya mtumishi ikiwa barabarani imesimama baada ya kuskia kelele zangu za msaada… Kiukweli namshukuru mungu, sikubakwa mama… Nipo tayari mkanipime kokote kule… Mnikague mnavyojua… Lakini sijabakwa”

Aliongea eva, hapo mama kidogo akapumua kwa nguvu…
“tutaamini vipi”
Mpaka mama kuuliza hivyo kidogo hasira zaka zimepungua…
“mama… Wewe ni mkubwa wangu na unajua mengi… Fanya chochote utakachojua kuwa mimi bado ni bikra, bado ni mali ya mwanao… Na hata mtumishi analijua hilo, mana siku ananisaidia.. Usiku ule nililala kwake, yaani jana”
Mama kuskia jana eva alilala kwa adam alishangaa
“wewe, hujamvunjia mwanangu masharti wewe”
“mama… Hata mimi nalitambua hilo.. Na pia sikulala nae chumba kimoja… Alilala chumba kingine…. Na adam alinipeleka mpaka hospitalini na pia alinikagua yeye mwenyewe”
“hebu ngoja nimpigie adam atuhakikishie”
Mama alinyanyua simu kisha akampigia mtoto wake….

Wakati huo adam kalala kajichokea mpaka basi,… Mercedes alikuwa jikoni anapika mana wamejikuta wanaumwa na njaa ghafla,… Mana wamepiga mechi,… Mercedes alikuwa anapika huku anashika sehemu za siri lakini ni juu juu ya nguo, yaani kama mtu anaejitomasa tomasa hivi, mana haamini kama adam aliingiza yote ile nanihiii yake,..
Mara simu ikaita kule chumbani kwa adam,… Adam alijivuta kwa kuchoka, na wakati huo inakwenda saa kumi na mbili na nusu za jioni..
“halo mamy, shalom”
“shalom…. Adam nakuhitaji uje nyumbani mara moja”
Aliongea mama huyo huku adam akijifanya mgooonjwa sana
“mamaaa…. Sijiskii vizuri ujue”
Aliongea adam huku mama akishangaa, mana adam katoka hapo nyumbani muda sio mrefu…
“wewe si umetoka hapa mchana ni mzima”
“aahh mama si unajua mahoma homa haya madogo madogo hayakawii kuja”
“heeeeee… Mungu wangu jamani pole”
Sasa ghafla Mercedes anakuja huku anaongea mana hajui kama adam alikuwa anaongea na simu,… Na adam Haruhusiwi kuwa na mwanamke ndani sasa mama akisikia sauti ya kike itakuwaje,… Adam akakata simu ili mama asisikie sauti ya mercy akiwa anaimba kwaya

“heeee… Simu imekata ghafla… Kuna Nini”
Aliongea mama yake adam huku eva akiwa na wasiwasi juu ya hilo,…
“mama twendeni tukamwangalie”
Sasa wazo la eva kubakwa likasahaulika tena, sasa ni swala la kuumwa kwa adam… Saa ngapi Jessica, Eva na mama wanajiandaa waondoke kwenda kwa adam… Maskini adam hajui kama kuna watu wanakuja, afu ndani ana mwanamke

Kule kanisani sasa kwa wale washakunaku,…
“nimeshalichoma huko,.. Simpatii picha eva atafanyaje”
Aliongea Miriam baada ya kutoka kumtumia Jessica picha kwa njia ya wasap,..
“umeshalichoma eeew… Ndio mana nakuaminia miriam”
Aliongea wini mana yeye ndio mwenye tamaa haswa ya kuolewa na adam,… Wakati huo sasa kuna mschana anaitwa vero, yeye baada ya kuzipa hizo taarifa binafsi alifurahi sana, mana anajua adam haoi mwanamke ambae hana bikra, sasa kama eva keshabakwa,.. Basi hana chake…
“sasa nianze kujipa nafasi na kibikra changu”
Aliongea vero huku akiwa peke yake, na vero yeye sio mpenda umbea sana sema kundi la umbea ni marafiki zake… Sasa kumbe vero nae kajitunza tunza ana kauzito kake kanamsumbua sasa kuskia hizo taarifa kwake ni njema… Kwahio inaonekana ni namna gani eva kawabania wasichana wengi kutokuwa na adam, sasa hivi ndio maana mchungaji anatakiwa aoe mapema, ili wasichana wanaomtamani mchungaji waaogope kwakuwa ana mke,… Sasa adam alikuwa anaogopwa kwakuwa ana mchumba na anajulikana kwenye familia, sasa mchumba ndio huyo, sasa mgodi wake hauna madini tena,….
“sasa nianze kuwa karibu yao.. Tena nimshawishi mama akaw karibu na mama adam”
Aliongea Veronica huku akitabasamu kwa furaha… Mara wini alikuja pale alipokaa vero,
“heeee best, vipi peke yako huku, kulikoni”
“wala tu kawaida mbona”
“wala sio kawaida yako wewe”
“wala Usijali”
“sasa.. Miriam tayari keshachoma kwa familia ya adam”
Aliongea wini huku akiwa na furaha kwelikweli
“una maana gani”
“yaani taarifa imeshawadikia walengwa”
“aaaaaaaahhhh unasema kweli wini”
“ooohoooo,… Najua huko kimeshanuka kwa eva”
Aliongea wini kwa mbwembwe zote..
“aaah Afadhali ata taarifa imewafikia mapema”
Aliongea vero kitendo kilichomshtua wini
“kwanini useme Afadhali”
“ndio.. Mana najua adam atatafuta bikra mwengine”
“atapa wapi… Karne hiii aliokuwa bikra ni eva peke yake…. Na wasichana wengi walikuwa wakimwonea wivu kwasababu.. Mahari itakayotolewa ni kubwa.. Afu pili anaolewa na tajiri mkubwa.. Tena mtoto wa kiongozi wa dini… Kila msichana anamwonea wivu na kutamani hata bikra zao zirudi waolewe na adam”
Aliongea wini na kusema kwa miaka hii hakuna mschana kuanzia miaka 20 kwenda mbele awe na bikra, wa mwisho katika dunia hii ni eva pekeee
“wewe wini tengua kauli yako kuwa hakuna mabikra tena…”
“hakuna mama,… Na adam kasema kama eva hana bikra, ataoa mschana yeyote yule”
“akaoe kopo wakati mabikra tupo”
“ati unasemaje wini”
“ndio tayari nimeshamtumia mama yangu meseji aanze kukaa karibu na mama adam…”
Wini alikasirika, yaani kumbe anaishi na vero lakini hajui kama mwenzie ni bikra, sasa leo ndio anajua…
“nyooooo eti mimi ni bikra… Kwa taarifa yako kuolewa na adam hio ni ndoto tu mama… Wewe hata mkono tu hajakushika”
“heeeee sasa kama mimi hajanishika wewe je…. Tena bora hata mimi kuliko wewe”
“heheheheheeeeee haaaloooo… Kwa taarifa yako, adam tayari anaujua utamu wangu,.. Nami naujua utamu wake,… Bikra yako kaitoe na baisikeli huko,… Kwanza sura huna”
Sasa vero anashangaa, ina maana adam keshakuwa mchafu kiasi hicho mpaka kutembea na wini… Malaya wa kanisa anaependa wavulana wa kanisa,…
“utembee na adam ulinge, unajishaua tu hapa”
“eti nini… Kataa sasa, afu nafasi ya kuolewa… Ninayo mimi”
Aliongea wini huku akiondoka zake, mana leo hata ibada hajafanya, kwa umbea ulio wakithiri,… Sasa vero bado haamini kama kweli adam kesha kuwa mchafu kiasi cha kutembea kimapenzi na wini, wenyewe wanamuita malaya wa kanisa…

“jamani eeee, mnamsikia vero kule”
Aliongea wini kama vile alikuwa anamtangazia vero
“kasemaje nae huyo”
“eti ana bikra spesho kwa adam”
“uuuiii hjhhahahhahahah… Jamani vero ana mambo.. Sasa hio bikra kaitolea wapi, au ndio bikra ya malimao hio”
“namshanga yule mwana kichefuchefu”
“uuuuu… Vero ana mambo jamani…”
“afu Miriam, yule vero si ana mpenzi yule”
Aliuliza mschana aitwaye Angel
“ndio tena sio mmoja shost.. Sema ana wapenzi”
“sasa hao wapenzi walikuwa wanaingizia wapi… Puani au skioni… Au usikute mwenzetu alikuwa anatoa 0714”
“inashangaza nae, anatuletea mpya huyu.. Haoni kuachika kwa mtu tu basi wanaona nafasi ni yao”
“tukamsuteni jamani heeee”
“hapana… Kumbukeni hapa ni kanisani jamani sasa tunaongelea mambo gani”
Aliongea rose ambae yeye mwenyewe katembea na adam lakini hasemi kitu katulia kimyaaa….

Sasa huku kwa adam,… Akiwa chumbani kwake kajichokea kweli,… Ghafla alisikia honi ya gari nje ya nyumba yake,…
“heeeeeee nani tena”
Adam aliuliza huku kichwa kikianza kumuuma, mana mercy yupo ndani,..
“huyu dada anakujaje kufanya usafi saa hizi jamani”
Aliongea adam huku akizunguka vyumba vyote,…Adam alikwenda kufungua mlango huku akisema
“namfungulia afu namfokea hata kama ni dada angu,.. Najua nikimfokea kwanini anakuja saaa hizi, najua hatoingia ndani”
Aliongea adam huku akifungua mlango mdogo ili amtokee huko huko nje ampe makavu live…. Sasa alishangaa ni familia nzima mpaka mama, mbaya zaidi hata eva yupo..
“heeeee mama.. Kulikoni tena”
Adam aliongea kwa mshangao mkubwa, huku akiwa kama haamini, sasa adam saa hio hio baada ya kufungua mlango aligeuka na kutaka kurudi ndani kabisa….
“wewe fungua mlango… Afu si ulisema unaumwa wewe…. Hebu fungua mlango tumekuja na daktari”
Adam haamini kwa ujio huo, ilimbidi tu afungue geti kubwa, waingie ndani

ITAENDELEA…..

Comments

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment