$hide=mobile

Young Paster sehemu ya tatu (03)

YOUNG PASTER EP 03 Ilipoishia MCHUNGAJI MCHANGA Aliongea bwana yohana huku bwana Jacob akitabasamu….. Huku kanisani masikini eva n...

YOUNG PASTER EP 03


Ilipoishia

MCHUNGAJI MCHANGA

Aliongea bwana yohana huku bwana Jacob akitabasamu…..

Huku kanisani masikini eva ni mtu wa maombi hataki kushindwa na shetani juu ya watu wanaomuandama kumbe jana mzee wa kanisa alimtonya kuhusu akina janet… Sasa eva wa watu kila kukicha ni yeye na maombi, anamuombea mchumba wake afike salama… Lakini sasa uchumba wao unaingia dosari, bwana yohana nae ana binti yake, nae anataka waowane na mtoto wa Bishop jacob…..

Sasa huku ofisini katika maongezi ya bwana Jacob na bwana yohana, yanayo husu muunganiko wa watoto hao wawili, na ni kweli sheria za kiwa mchungaji shariti uwe na mke… Japo wengi wanafosi tu.. Sasa leo bwana yohana anakuja kuzima ndoto za eva mwenye tegemezi la kuolewa na adam, mtoto wa mr Jacob……

ENDELEA NAYO…….

Katika dunia hii, hakuna kitu unachoweza kukiwekea mia kwa mia kuwa utakipa, na si katika simulizi kama hizi bali wapo watu waliotamani kupata kitu fulani katika maisha lakini hawakukipata kwa vizuizi tofauti tofauti… Sasa tukija katika upande wa mapenzi, unakuta wewe mwanaume kuna mwanamke unatamani sana kumuona, lakini kuna vigezo au vizuiz vitakavyo sababisha usimuoe.. Au wewe mwanamke una mwanaume unatamani akuoe lakini kuna vizuiz vingi sana ambavyo vitasababisha asikuoe..

Sasa kwa mwanadada eva, masikini ya mungu, wao hali ya maisha kwao ni ngumu, yaani ni masikini lakini ni mcha mungu.. Kila kukicha yeye na ibada yeye na kanisani, yeye na Biblia, hio yote ni kuiombea familia yake na yeye mwenyewe apate mume bora katika maisha yake, na katika akili yake tayari keshapata mchumba, tena wanapendana sana, na mchumba mwenyewe ni Adam,.. Na Adam huyo huyo ndio anapigiwa debe na Bishop yohana kuwa amuoe mtoto wake….

Sasa tuje huku ofisini kwa mr Jacob
“kwanza tumsifu yesu Kristo mr yohana”
Aliongea mr Jacob huku akitabasamu kwa mbaali kuonesha kiwa ombi la bwana yohana ni zuri sana ila litakuwa na mashaka…
“milele amina”
“umeleta jambo zuri sana tena katika wakati muafaka… Lakini katika uwepo wangu pale nyumbani, nasikia sikia kuhusu mchumba wa adam, ila sijafuatilia sana kwa ukaribu mana mimi sikutambulishwa lakini mke wangu analifahamu hilo… Sasa huoni katika hali hii tunaweza kuwavurugia”
Aliongea mr Jacob, mana kweli anasikiaga habari za Eva kuwa ni mchumba wa adam… Lakini hakutambulishwa…
“ni kweli bwana Jacob,.. Hata mimi mtoto wangu nilizisikia habari kuwa na mchumba.. Ni mwinjilisti mmoja hivi sasa kwa hadhi ya familia yangu, mtoto wangu hawezi kuolewa na mwinjilisti… Mimi kama baba nilikataa hilo na kakubali… Kwanini usitumie nguzo ya uzazi.. Mana wakijichagulia wenyewe tutaonekana sisi hatuna malezi bora.. Na istoshe mtoto wangu nimemlea katika imani.. Yaani sijui niseme nini… Atukuzwe bwana yesu”
Aliongea mr yohana huku akimsifu yesu Kristo kwa neema zake
“amina”
Aliitikia mr Jacob huku kweli akiingiwa na maneno ya Bishop mwenzie kama yeye…
“mr Yohana… Kweli mwanangu a DC am ananisikiliza sana, lakini kwenye hili swala… Hahahahaha, sina hakika”
“basi inaonekana mtoto wako hujamlea vyema”
“tena hakuna mtoto mwenye heshima kwangu kama adam”
“najua na ndio mana nimekufata rafiki yangu wa zamani sana”
“basi wewe niache hilo.. Nitalifanyia kazi”
“bwana yesu ni mkuu… Hakika hawezi shindwa jambo jema mbele za mungu”
Saa hio hio maombi yalishuka, yaani hapo hapo kanisani.. Wafanyakazi kusikia maombi nao wakafumba macho na kuanza kuyapokea maombi toka kwa watumishi hao wa mungu….

Tukija huku kanisani eva akiwa anatoka kanisani baada ya maombi, alikuwa akipita pita katika paking za magari, ikiwa ndio ngazi ya kupandia juu, hivyo akiwa kushika Biblia yake tayari kurudi nyumbani… Akiwa njiani alikutana na akina Janet…
“shalom”
Alitoa sifa kama salamu kwa akina janet,
“shalom eva”
“yesu asifiwe kwakweli”
Aliongea eva kutoa sifa ya bwana wake mwokozi alie hai,…
“unatoka wapi eva”
Aliongea janet lakini ni kama kumkebehi, mana njia wanayokwenda ndio hio hio anayo toka eva, hivyo hakukuwa na haja ya kumuuliza sana
“natoka kanisani janet… Esta hali yako”
“safi tu”
Aliitikia huku akiangalia pembeni, lakini eva alishaambiwa na mzee wa kanisa kuwa watu hao hawana ahueni nae, hivyo hilo analijua vizuri yu na hana shaka nalo
“sawa safari njema kwako”
Aliongea janet huku wakipishana,.. Wakati huo yapata saa 10 za jioni katika misa ya saa 10 ila akina janest wao walichelewa kidogo hivyo eva na waumini wengine walishamaliza ibada ya maombi ya siku hio…

Sasa ikiwa masaa yamekwenda sana na sasa ni saa mbili za usiku,… Tukiwa katika nyumba ya bwana yohana, nae ana familia kubwa tu kama ya Bwana Jacob,… Ila bwana Yohana yeye ana watoto wanne.. Wakiume wawili na wakike waili.. Ila bwana Jacob yeye ana wakike watatu na wakiume mmoja… Sasa wakiwa wapo mezani wanapata chakula kama vile ilivyo kwa mr Jacob wakati wa kula hakuna kuongea,.. Na watoto walipo maliza kula, kila mmoja alishika kona yake ya kwenda chumbani kwake…. Na hapo baba ana jambo la kuongea na mama na ndio mana watoto wamesambaratika kila mmoja kona zake…
“Mama Catherine…. Unajua tayari nimeshaongea na mtumishi jacob kuhusu watoto wetu”
Aliongea bwana Yohana… Lakini mke wake alionekana kutopendezwa na hili mana kama vile atawauzi watoto
“lakini baba Catherine… Huoni kuwa utamnyima mtoto raha ya maisha… Mana umeuvunja muelekeo wake”
Aliongea Melissa ambae ndio mama wa familia ya mzee Yohana…
“mimi ni mzazi ni lazima nifanye maamuzi kama mzazi…. Catherine ni lazima aolewe na mtoto wa mr Jacob”
“nitafanya nini sasa… Sina cha kufanya juu ya maamuzi yako mtumishi wa mungu”
“hayo ndio majibu sasa sio kupingana”
Mama alikubali lakini ni ile kishingo upande… Sasa pendo ambae ndio mtoto wa pili akitoka Catherine mwenye miaka 21 anakuja huyu pendo mwenye miaka 16 hivi au 17..sasa alisikia yale maongezi ya baba na mama… Saa ngapi hajakimbilia chumbani kwa dada yake….

“dada… Dada… ”
Aliita pendo huku dada akiitikia kwa hasira, mana alikuwa usingizini tayari keshalala…
“nini we pendo, hujalala tu jamani mdogo wangu”
“nimesikia kitu kwa baba”
Aliongea upendo huku Catherine akiamka kwa hofu… Mana baba yake kawa mkali sana kwa sasa…
“kitu gani tena”
“baba kamwambia mama… Utaolewa na yule mkaka hensam”
Sasa upendo kumbe anamjua Adam vizuri sana…
“mkaka hensam??? Mkaka hensam ndio nani”
“dadaaa…. Unakumbuka mwaka uliopita, tulikwenda kwenye harusi ya rafiki yako wanjiku… Sasa yule aliokuwa akifungisha ndoa ya wanjiku,… Mtoto wake sasa ndio anatakiwa kukuo wewe”
“unamaanisha mtoto wa mchungaji jacob”
“haswaaaa”
“anaitwa adam”
“ndio huyo huyo… Japo naskia hayupo”
“ndio hata mimi najua hayupo… Ila baba ndio kasema”
Aliuliza kwa umakini mkubwa sana Catherine huku akionekana kama kuipenda taarifa hio…
“ndio.. Na mama kakubali… Dada yule mkaka ni hensam afu kwao kuna hela”
“Peleka ujinga huko.. Kwani siai hatuna hela”
“sawa ila wao wametuzidi ai tuseme ukweli tu”
“ondoka nenda kalale”
Upendo aliondoka lakini huku nyuma, Catherine alionekana kushika kifua chake na kuanza kutabasamu… Kumbe nae anampenda adam sema alisikia kuwa adam ana mchumba wake, hivyo akakata tamaa ya kumpenda, sasa ile ndoto yake ni kama imerudi tena kivingine…. Catherine alikuwa ni mzuri.. Mweupe, ana umbo la kipekee, yaani tuseme uzuri wa eva na Catherine ni sawa sema tofauti ni rangi… Catherine ni mweupe, na Eva ni maji ya kunde,.. Ila wote wana maumbo ya kuvutia… Ila Catherine yeye, kidogo anapenda mavazi ya kisasa, hapo ndipo atakapomshinda eva..
Catherine aliingia Google na kuanza kumtafuta adam katika mitandao ya kijamii,…. Alipomuona roho ilimpasuka na kujikuta anamuita..
“mume wangu… Mungu kajibu maombi yangu,.. Nilikuwa nikikuota usiku na mchana lakini leo ndoto zinakwenda kuwa kweli”
Aliongea hivyo kwa sauti huku akiiangalia ile picha….

Mara mama yake kaingia hapo chumbani, kumbe mama alikuwa akilia jinsi mtoto wake alivyochaguliwa mume… Lakini mama alipoingia hakujulisha kama alikuwa akilia…
“hujalala tu”
“ndio mama… Hata usingizi hauji”
Aliongea Catherine huku akiificha simu yake ili asionekane kama kakubali sana kuolewa na adam..
“au umesikia wazo la baba ako ndio mana hujalala”
“wazo gani tena hilo mama”
Catherine alijifanya hajui chochote kuhusu wazo la baba yake
“amesema eti uolewe na mtoto wa mchungaji Jacob”
“mmmhhhh mamaaaa… Sasa na mwinjilisti wangu je”
“Catherine, ina maana bado hujaachana na huyo mpumbavu”
“yesu wangu mama… Ina maana keshakuwa mpumbavu tena”
Kumbe mama aliongea vile kwasababu baba alikuwa akipita huko kwa nje, sasa hakutaka kujulikana kuwa yupo tofauti na mumewe,…
“mamaaaaaa jamani”
“ah ah… Sikia sasa… Mimi sipo tayari uolewe na mtoto wa jacob, mana yule ana mchumba wake, afu istoshe yule kijana katembezwa sana na baba yake nchi mbalimbali, anajua starehe za kila aina… Mi sitaki uolewe nae”
Catherine alinuna ghafla, mana hata huyo mwinjilisti sio kuwa alimpenda sana,…
“mama mbona mimi nimekubali”
Mama kusikia hivyo alishtuka na kumwangalia mwanae kwa hasira
“unasemaje wewe”
“mama, nilikuwa nikimpenda sana adam, nilikuja kupoteza mawazo juu yake baada ya kusikia ana mchumba”
“ivi Catherine nikuulize swali”
Mama alibadirika kabisa na kua na hasira…..
“swali gani tena mama”
“ivi usichana wako unao wewe…. Mana ile familia ni ya kitajiri haswa, na haitaki mschana ambae hana bikra…. Sasa kama huyo mwinjilisti wako umeshampa…. Jua adam sio wako mama.. We jishaue tu”

ITAENDELEA..

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,149,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,196,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,110,FIFA.com - Latest News,15,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,11,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,207,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,39,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : Young Paster sehemu ya tatu (03)
Young Paster sehemu ya tatu (03)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-tatu-03.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-tatu-03.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content