Young paster sehemu ya tano (05) | BongoLife

$hide=mobile

Young paster sehemu ya tano (05)

YOUNG PASTER EP 05


Ilipoishia

MCHUNGAJI MCHANGA

Dege kubwa liliokuwa linatua katika uwanja huo, yaani eva alitamani hata kuifuata ile ndege kabla haijasimama, lakini kapoozeshwa na mama mkwe wake, mana ni mwaka sasa umepita hajamuona mchumba wake,.. Walishuka abiria wote,… Na Adam alikuwa ni abiria wa mwisho kushuka
Laaaa haulaaaa…..
SHARBIN RASHIDI KINGAZI ndio mwenye jina la Adam katila simulizi hii, na ndio yeye akiwa kapigilia suti yake saafi… Kweli mwenye mali ni mwenye mali tu… Eva ndio mtu wa kwanza kumuona adam wake,… Yaani hivyo alivyoanza kukimbia, utapenda yani…. Sasa Catherine nae anashangaa huyu anaeanza kukimbia kwa kujiua ua ni nani… Hakuta kujua sana, ila nae alianza kumkimbilia adam… Wakati huo adam kashika kibegi chake.. Mana begi kubwa linabuluzwa na wahudumu wa hapo uwanjani…. Maskini Adam kasimama na asijue amkumbatie yupi kati ya wawili hao

ENDELEA NAYO…….

Katika maisha ya sasa tunasema mwanaume kama mwanamume lazima uwe na maamuzi ya kiume,.. Adam ni kijana mpole sana na kalelewa katika mazingira ya dini.. Na katika kukua kwake kote hajui undani wa mwanamke hata mmoja, yaani haijui siri ya mwanamke ikoje, mana yake ni kwamba hajawahi kutembea na mwanamke, na mwanamke alioapa kumuoa ni eva pekee ambaye nae ni vivyo hivyo hamjui mwanaume,.. Adam kabla hajaamua maamuzi yake alikumbuka siku anapanga safari ya kwenda Nigeria kimasomo zaidi..

KABLA YA KWENDA NIGERIA

“eva… Mimi kesho nasafiri.. Naomba uwe makini na mapepo wachafu juu yako”
kitendo cha Eva kusikia kuwa Adam anasafiri, moyo ulimpasuka huku akishika kifua chake,…
“baba mtumishi, unakwenda wapi.. Na unarudi lini… Hivi kuna usalama kweli huko”
Aliongea eva huku akimshika adam bega lake,..
“nakwenda kimasomo,… Si unaona kanisa langu linajengwa… Hivyo wacha nikajiongeze angalau”
“lakini baba mtumishi, upasta siokusoma, upasta ni wito toka kwa mungu… Sasa kwanini lakini”
“ni kweli,.. Wito numeshaupata na nimeupokea… Na hata sasa naweza kukabidhiwa kipawa hicho, lakini kuna njia ambazo natakiwa kupitia.. Kwa mfano mwanamke anaetaka kuolewa,.. Kabla hajaolewa wanasema lazima awekwe ndani, sasa ule wakati yupo ndani, kuna mambo mengi anafundishwa jinsi ya kuishi ndani ya ndoa yake… Hivyo mimi nakwenda kupewa makatazo yasiofaa nikiwa ndani ya kipawa changu,.. Au yanayo faa, hivyo sina shaka na kipawa changu eva.. Nipo makini sana”
Adam aliongea adam mtoto wa mr Jacob,…
“sawa, ila utarudi lini… Siamini kama nitabaki mwenyewe”
“eva, niruhusu kwa moyo mmoja,.. Itanichukuwa mwaka mmoja”
“yesu wangu na maria, Uuuuuuuuuwiiiiiiii, baba mtumishi, mbona unakaa sana”
“ndio wakati unaotakiwa”
“sawa, sina jinsi juu ya hilo… Naomba uape kwa jina la yesu na mungu wake.. Kuwa utanioa mimi”
Aliongea Eva kana kwamba haamini kama kweli atamuoa, mana anajua Nigeria kumejaa wasichana warembo na wanaojua dini yao kuliko hata eva, na Adam anapenda msichana anaeijua dini na kuitumikia dini yake vilivyo, sasa huko Nigeria ndio wamejaa wasichana wa aina hio
“naapa kwa jina la na la yesu na mungu wangu alie hai… Sintokaa kukuwcha eva,… Na endapo umeshindwa kujitunza eva, naomba siku narudi usinisogelee”
Adam aliapa kisha hapo hapo akamwambia kabisa,… Mana uhusiano wao una miaka lakini hajawahi kumuomba mpaka waoane
“baba mtumishi wangu… Kama sijajitunza, basi hata kanisani kwenu siji.. Mimi ni mali yako, mshukuru mungu, nakuoenda sana baba mtumishi wangu.. Nitajitunza kama alivyonitunza mama yangu… Nenda urudi baba nakusubiri wewe tu”
“hata mimi nakuapia, sintokaa kujigusa ispokuwa kwako tu”
“tumsifu Yesu Kristo alie hai”
“milele amina”
“baba mtumishi, unaondoka lini na saa ngapi”
Eva alimuuliza adam…
“naondoka kesho, ila itakuwa asubuhi baada ya misa ya kwanza kuisha.. Ila nitapelekwa na baba”
“lazima nikuone mpaka unavyopanda ndege.. Nikusindikize mpaka mwisho”
“lakini nitakuwa na baba”
“nitapanda gari tofauti na yakwenu, lakini nikuone tu”

Kwaho yake sasa adam na baba yake wakiwa ndio wanafika uwanjani, lakini kumbe eva alishafika kabla yao, shida ya eva amuone baba mtumishi wake anaondoka salama, alitamani kwenda kumuaga lakini iloshindikana, kwasababu mwanamke anaejieshim hatakiwi kujionyesha kwa baba mkwe mpaka utambulishwe, sasa anaejua utambulisho huo ni mama yake adam peke yake, ila baba bado haja tambulishwa,… Adam alimwona eva akampungia mkono kwa mbali… Lakini huezi amini eva aliona liwalo na liwe, hawezi kumpungia kwa mbalimbali kisa hajatambulishwa.. Huezi amini eva alitoka pale alipo na kumkimbilia adam au baba mtumishi wake.. Adam nae hakutaka kujua yupo jirani na baba yake…. Alinyanyua mikono yake kuashiria kumkumbatia eva,… Baba yake rajabu, alishangaa, japo huyo msichana si mgeni katika macho yake, mana pia ni muumini wa kanisa lake… Hakumuwazia sana mtoto wake,… Wakati huo mzee anasonga mbele huku nyuma adama na eva wanaendelea kuagana… Mpaka wanaachana eva anageuka nyuma na adam anaguka mbele kuuelekea mlango wa ndege husika…..

MWISHO WA KUMBUKUMBU YA ADAM, KABLA YA SAFARI…..

Sasa adam alipokumbuka hilo,… Lakini pia alikumbuka muda mchache uliopita alipigiwa simu na baba yake kuhusu Catherine,… Adam alitabasam kidogo kisha akaweka brifkesi yake chini na kuamsha mikono kuashiria mapokezi mazuri kwa anaekuja…. Adam alimkumbatia huku akiskia sauti ikisema
“Ahsante sana mungu baba…. Umenirudishia baba mtumishi wangu”
Alikuwa ni eva baada ya kukumbatiana na adam wake…. Sasa Catherine anashangaa mbona huyu mschana kakumbatiwa badala yake,.. Catherine hakuwaza mengi sana alijua labda ni muumini wa kanisa lao, hivyo Catherine yeye nguvu zake zote ziliishia kubeba kile kibegi kilichokuwa chini na pia alijiskia vibaya sana, mana kakimbia bure bila mafanikio yeyote… Haikupita muda na familia yote ikamzunguka adam
“mwanangu, umenenepa wewe, haaa.. Yaani unataka kusema mimi mama yako nilikuwa sikupendi mwanangu”
Aliongea mama yake adam huku akiwa na furaha ya kumwona mtoto wake tena,.. Dada yake adam nae hakuwa nyuma
“shalom kaka D”
“shalom…. Asa d ndio nini, umeanza uhuni dada eti ee”
“amna bwana,… D nimehisi ni kifupi cha adam”
“najua dada yangu una maneno mengi kweli wewe”
Aliongea adam huku wadogo zake wakimsalimia kaka yao, ilikuwa ni furaha kuanzia kwa eva mpaka kwa familia yote, kasoro Catherine pekee,

Gari ya familia iliandaliwa kisha wakapanda gari lao… Kisha haooo wakaondoka, ndani ya gari furaha iliyokithiri, eva ndio kabisa usiseme, ana furaha ya ajabu kuliko mtu yeyote hapo ndani,…

Walifika nyumbani, maandalizi ya kupika yalianza,…
“mama, naomba nimpikie adam”
Eva aliomba nafasi ya kumpikia adam na wakati huo adam kakaa katika meza, sasa kuna kakitabu chake anapenda kukasoma pale anapokuwa mwenyewe,…
“martha…. Martha?”
Adam alimuita mdogo wake ambae ni martha,
“Abee kaka”
Aliitika Martha huku akimjia kaka yake
“ebu niletee kibegi changu kipo katika gari”
Aliongea adam huku martha akiharakisha agizo la kaka yake, wakati huo eva yupo jikoni, yaani eva keshakubalika na familia yote, swma ubabe wa mr Jacob kutaka mtoto wa rafiki yake aolewe na mtoto wake,.. Mama alikuwa karibu na mtoto wake akimuuliza habari ya masomo mana ni mwaka sasa toka aende Nigeria… Lakini sasa adam alisahau na sio adam tu bali wote walisahau kuwa pale uwanja wa ndege walikuwa wa9 na Catherine,… Hivyo Catherine ndio alibeba kibegi au briefcase ya adam ambayo ina vitabu vya mungu karibia kibegi kizima…
“kaka sioni mbona”
“aahhh we nawe akuizi huna macho”
Wakati huo eva ndio analeta chakula, tayari keshapika, mama alimtabasamia eva kwa chakula alichopika… Na leo ndio mara ya kwanza eva kuingia kwenye hii nyumba, lakini kazoeleka ghafla tu na hapo yeye hajui kama kipo kinachoendelea juu yake..
“unatafuta nini wifi nikakusaidie”
“kaka kantuma kibegi chake”
Sasa eva yeye ndie alipata kumbukumbu ya pale uwanjani…
“kuna yule dada nilimwona pale uwanjani na ndie aliekibeba, kwani sio ndugu yenu yule”
Aliongea eva,… Sasa mama ndio anafungukwa na akili,..
“afu kweli, ivi Catherine alipita njia gani saa ile”
Aliuliza mama yake adam, kisha adam akamuuliza mama yake kuwa
“kwani si mlikuja nae”
“hapana, alikuja kivyake na gari yake”
“aahhhh… Afu mama, kuna taarifa nimepewa na baba kuhusu yule msichana, mi sielewi mama”
Mama sasa roho ikamshuka, hayo maneno yalimkuna sana eva, na kutaka kujua kinaga ubaga cha huyo Catherine,..
“mwanangu, hata mimi sielewi, ni asubuhi tu hapa baba yako ananiambia kuwa eti ndio mwanamke unaetakiwa kumuoa”
Heeeeee Eva alikuwa nyuma ya mlango, anasikia, yaani ilibaki kidogo tu adondoke,.. Akajikaza kisabuni ila wakati huo alikuwa yupo na Martha, mana hata watoto sio wote wanajua hilo,.. Martha alimshika wifi yake mana anamjua kuwa anampenda sana kaka yake… Martha ni mschana mkubwa ana miaka 20,…
“lakini mama, ina maana umeshindwa kumwambia baba nina mchumba… Au hajui hilo”
“nimemwambia lakini akasema mimi sijatambulishwa”
“sasa ngoja aje… Na eva asiondoke hapa amkute”
“sasa unaenda wapi mwanangu”
“nakwenda kuchukuwa kibegi changu”
Sasa wakati adam anatoka, Martha akamwambia wifi yake kuwa
“ambatana nae, mana najua huyo Catherine katumia akili kwasababu anajua ni lazima kaka adam atakwenda kule, hivyo nenda nae”
Aliongea martha, mana anampenda eva kuliko Catherine,..
“njoo kula kwanza baba”
Mama Jessica alikuwa akimlazimisha adam ale kwanza, lakini hakutaka kufanya hivyo… Mana hasira zilishamjaa…..
Wakati huo eva anatetemeka, ivi atamwambia nini mama yake, familia yake yote inajua ataolewa na adam, baadhi ya makanisa yao yanajua uhusiano wa adam na eva,..
“baba mtumishi, naomba niongozane nawe”
Aliongea eva huku akihisi kukataliwa na adam
“yes, ni sawa twende, tena familia yao yote ikakujue”
Eva hakuamini kumbe adam hakubaliani na swala la baba yake,… Eva aliingia kwenye gari na adam.. Kisha haoo wakaondoka,.. Kweli familia ya mr jacob ni tajiri mno..

Sasa huku kwa mr yohana, Catherine akiwa kakumbatia begi la adam, yaani kusema kweli hata yeye anampenda sana adam..
Mama aliingia chumbani kwa mtoto wake, alimkuta kashikilia begi dogo
“wewe una nini… Mana ulitoka kwa furaha sasa mbona umekiwa hivyo mwanangu”
Aliongea mama huyo, au mama mchungaji kwa mzee Yohana
“mama, nimekwenda uwanja wa ndege, nimeambulia kubeba hiki kibegi tu”
“aaahhhh ina mana adam hajakuona”
“kaniona sana tu, ila kuna msichana ndio kamkumbatia badala yangu”
“lakini Catherine mwanangu, nilikuambia adam ana mchumba lakini husikii”
Aliongea mama huyo na hata yeye huyu mama hataki mtoto wake Catherine aolewe na adam, sasa hatujui ni kwanini
“mama mimi nampenda hivyo hivyo tu, na nilikuwa sina nguvu kwasababu ni moyo wangu tu, lakini sasa hata baba kaingilia kati hivyo nina nguvu na lazima niolewe na Adam”
Catherine hakutaka kukata tamaa, na kweli jambo likiingiliwa na wazazi, sidhani kama mtoto atapinga, tena haswa wazazi wa kiume… Hatari sana.. Lakini wakiwa wanazidi kuongea ghafla honi ilisikika nje ya geti lao, mlinzi alifungua geti kisha gari inaingia ndani… Alikuwa ni adam
“haya si ndio huyo anaingia”
Aliongea mama yake Catherine huku akifunua pazia…
“nilijua tu lazima aje…. Mama twende ukanisaidie kuongea nae”
“ati nini…. We ulifikiri napenda uolewe nae, sipendi hata kidogo.. Umuache mkaka wa watu mpole kiasi kile,.. Mwanangu… Kwani John kakufanya nini lakini”
“mama tuachane na mambo ya John”
Catherine aliongea hivyo huku akitoka nje na kile kibegi,…
Wakati huo adam anashuka katika gari kwa hasira sana,.. Tena kwa dharau anakwenda kumfungulia eva mlango, na wakati huo Catherine anaona live bila chenga…
“unamuona mchumba wake,… Kwanza ona nguo alizovaa… Pili muangalie juu mpaka chini, kama kuna kitu cha kisasa alichokitia mwilini, hebu jiangalie na wewe mwanangu, kila kitu mwilini mwako ni kitu cha kisasa… Haya Adam huyo hapo, mwambie kuwa unampenda”
Melissa alimchana mtoto wake live bila chenga,… Kweli Catherine akijiangalia, uzuri anao, shepu anayo. Labda na tabia anayo… Lakini sasa mwili wake umejaa udigitali mwingi mnoo….
“baba, karibu”
Alimkaribisha mama kwa shangwe
“Ahsante mama… Tumsifu yesu Kristo”
“milele amina mtumishi”
Adam alimgeukia Catherine kisha…

itaendelea…

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : Young paster sehemu ya tano (05)
Young paster sehemu ya tano (05)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-tano-05.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-tano-05.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy