Young paster sehemu ya sita (06) | BongoLife

$hide=mobile

Young paster sehemu ya sita (06)

Young Pastor 06Ilipoishia

MCHUNGAJI MCHANGA

“ati nini…. We ulifikiri napenda uolewe nae, sipendi hata kidogo.. Umuache mkaka wa watu mpole kiasi kile,.. Mwanangu… Kwani John kakufanya nini lakini”
“mama tuachane na mambo ya John”
Catherine aliongea hivyo huku akitoka nje na kile kibegi,…
Wakati huo adam anashuka katika gari kwa hasira sana,.. Tena kwa dharau anakwenda kumfungulia eva mlango, na wakati huo Catherine anaona live bila chenga…
“unamuona mchumba wake,… Kwanza ona nguo alizovaa… Pili muangalie juu mpaka chini, kama kuna kitu cha kisasa alichokitia mwilini, hebu jiangalie na wewe mwanangu, kila kitu mwilini mwako ni kitu cha kisasa… Haya Adam huyo hapo, mwambie kuwa unampenda”
Melissa alimchana mtoto wake live bila chenga,… Kweli Catherine akijiangalia, uzuri anao, shepu anayo. Labda na tabia anayo… Lakini sasa mwili wake umejaa udigitali mwingi mnoo….
“baba, karibu”
Alimkaribisha mama kwa shangwe
“Ahsante mama… Tumsifu yesu Kristo”
“milele amina mtumishi”
Adam alimgeukia Catherine kisha…

ENDELEA NAYO……..

Wanasema huezi lazimisha maji kupanda mlima hata siku moja, mzazi wa adam ambae anataka mtoto wake huyo kuoa mtoto wa rafiki yake mr yohana,… Lakini kwa upande wa mtoto wa mr jacob hakuridhika na matakwa ya baba yake,…

Wakiwa uwanja wa ndege baada ya Catherine kukosa kumbatio toka kwa Adam, alifanikiwa kuondoka na begi dogo la Adam, na aliondoka nalo makusudi ya kwamba ni lazima angelikuja kule nyumbati ili alipate kumbatio kwa uzuri akiwa kwao,.. Kweli akili yake ilizaa matunda kwa kitendo cha adam kufika kwao, ila kupata kumbatio kama alilopata eva pale Airport, hakuweza kulipata…

“baba, karibu”
Alimkaribisha mama kwa shangwe
“Ahsante mama… Tumsifu yesu Kristo”
“milele amina mtumishi”
Adam alimgeukia Catherine kisha akamsalimia kwa kumpa mkono
“shalom dada”
Aliongea adam huku akimpa mkono Catherine….
“shalom”
Catherine aliupokea mkono kiunyonge sana tena ni kwakuwa anamuheshim sana, mana kitendo cha adam kumwita Catherine DADA, alijiskia vibaya sana….
“Samahani mtumishi… Iv huna taarifa zangu zozote”
Catherine aliona bora kuongea tu, mana kama mtu mwenyewe hata haonyeshi kuwa na upendo juu yake
“nimekuja kuchukuwa vitu vyangu, hio ndio taarifa niliokuja nayo”
Aliongea adam huku akinyoosha mkono wake kuashiria anataka begi lake,….
“Catherine, unamchelewesha mtumishi”
Aliongea mama yake Catherine huku Catherine akilitoa begi hilo aliokuwa kalikumbatia,… Mtumishi adam alilipokea begi hilo na kumgeukia mama take
“mama, asifiwe bwana yesu”
“milele amina baba”
“basi mimi naona niwaache”
“mungu akutangulie mtumishi wangu”
Aliongea mama yake Catherine huku adam akimpa eva lile begi,… Adam alimfungulia eva mlango, Catherine anaona live bila chenga…. Baada ya kumaliza akaja katika upande wake wa dereva, lakini kabla hajaingia aliita
“Catherine…. Taarifa zako ninazo, lakini umechelewa… Nina mchumba na nakwenda kumuoa hivi karibu, ndio huyu hapa Eva… Bwana yesu akutangulie Catherine… Ahsante”
Adam aliingia katika gari kisha huyooo,… Lakini alipokuwa anatoka getini akakutana na baba yake Catherine akiwa katika gari yake, Adam alishusha vioo na kumsalimia
“Shalom baba mchungaji”
“shalom mtumishi, habari ya uzima”
“aahhh Tunamshukuru mungu.. Anatenda miujiza”
“basi tumsifu yesu Kristo”
“milele amina”
Mzee anajua fika labda adam kamleta Catherine mara baada ya kutoka airport, kumbe kilichofatwa huku ni begi tu… Mzee Yohana anaingia nyumbani kwake, anamkuta Catherine kuvimba haswa…
“raha gani hii mwanangu, unaolewa na kijana mwenye heshima zake,.. Umeletwa mpaka nyumbani upewe nini mwanangu”
Aliongea Bishop yohana bila kujua lolote, wakati huo mama yake Catherine yupo ndani anakaukia kucheka tu… Ile kimoyo moyo, mana kweli hapendi mtoto wake aolewe na mtumishi adam
“baba,… Adam kaja na mchumba wake hapa”
Aliongea Catherine huku machozi yakimlenga lenga,
“Unasemaje?”
“ndio, tena kaniambia kuwa huyo ndio mchumba wake na anatarajia kumuoa wiki hizi… Hivyo hahitaji usumbufu na mtu”
Aliongea Catherine, wakati huo maongezi yakiendelea, tayari simu ilishawekwa maskioni siku nyingi sana,..
“hello mr Jacob… Tumsifu yesu Kristo”
“milele amina”
“habari ya siku mbili tatu”
“aaahh bwana yesu ashukuliwe sana”
“Samahani mr Jacob, kijana wako hujampa taarifa juu ya kinachoendelea”
Mr Yohana alimuuliza bwana Jacob
“kwanini Unauliza hivyo ingali anajua kila kitu,.. Namuamini kijana wangu hana shida”
Aliongea bwana jacob bila kujua kilichoendelea huku
“numepishana nae getini kwangu hapa sasa hivi tu”
“si unaona sasa, umbe kaja? Hawa ni watoto wetu bwana”
“lakini nadhani hayupo tayari kwa hilo mana nimemkuta binti yangu kanuna na istoshe kaja na huyo anaesemekana ni mchumba wake”
“unasemaje?.. Amekuja na huyo binti mwingine”
“inavyosemekana”
“hebu nipe hii siku ya leo… Tutayamaliza, wewe ni rafiki yangu toka utotoni, mpaka sasa tupo pamoja.. Nataka tuwe ndugu sasa, hahahahaha.. Bwana yohana kiwa huru bwana”
Aliongea mr Jacob huku akiwa na furaha sana juu ya kutaka kumpa mtoto wake mke ambae ni mtoto wa rafiki yake
“sawa mr jacob, staki binti yangu aolewe na vijana wa ajabu ajabu… Mimi ni mtu na heshima zangu”
Aliongea mr yohana wakati huo Catherine ndio anazidi kujiskia raha na kupata nguvu zaidi mana swala hilo limeshikiliwa na wazazi,…
“usijali kabisa ndugu yangu… Bwana yesu atuongoze”
Aliongea bwana Jacob kisha simu ikakata,

Huku nyumbani kwa akina adam akiwa ndio anaingia nyumbani kwao, Jessica aliwahi kumpokea mdogo wake, na anamheshimu sana mdogo wake,.. Jessica ndio mtoto wa kwanza katika hii familia,..
“imekuwaje huko wifi”
Aliongea Jessica huku akiingiza kibegi ndani,
“wala hakuna lolote, alimwambia tu kuwa ana mchumba wake”
Wakati huo wakiulizana hivyo adam hakuwepo hapo, kumbe alishatoka kitambo tu, na Wakati huo ni mida ya saa 11 za jione kwenda saa 12,… Adam alifikia kwenye nyumba moja mpyaaaa, ila imeshaisha ujenzi, kumbe adam ana nyumba kabisa yaani akirudi huko sio mtu wa kukaa tena kwa baba yake,… Ilikuwa ni nyumba kubwa mno na haistahili aishi pekee bali mke.. Katika nyumba hio kila kitu kilisha wekwa, yaani hapo ni kuhamia tu,…

“ondoa hofu, lazima uilewe na kaka yangu”
Ni huku kwa akina Adam, Jessica akiwa anamhakikishia eva kuwa ni lazima aolewe na adam,…
“sawa wifi yangu, ila kama hili jambo wamelishika wazazi, huoni itakuwa ni hatari kwangu”
“ondoa shaka, mimi namjua vizuri adam… Nimemkuza mwenyewe.. Namjua haoi mtu pale”
Aliongea Jessica, lakini wakati huo eva anataka kirudi nyumbani,… Haraka haraka Jessica anampigia adam simu..
“we subiri upelekwe mpaka nyumbani unaogopa nini”
Aliongea Jessica huku simu ikiwa sikioni
“sawa”

“haloo mtumishi… Njoo basi umpeleke mwenzio nyumbani”
Aliongea Jessica kwa kumuita mtumishi,.. Ni jina ambalo wamelizoea kwa watu wengi na pia kutokana na kipawa chake..
“sawa nafika hapo sasa hivi”
Kweli haikuchukuwa muda adam alifika nyumbani kwao na kumchukuwa eva,….

Sasa huku kazini baba yake Adam anatoka kazini, anawaza cha kumwambia mtoto wake, kwanini kaenda kuleta fujo katika nyumba ya watu,

Wakati huo mama yake eva alikuwa hana raha mana toka mchana hajamwona mtoto wake,… Bite ambae ndio mdogo wake na eva pia alikuwa ni mtu wa wasiwasi, tena mama ndio kabisa kwasababu asubuhi kuna maneno aliyasikia toka kwa akina janet,.. Mama na mtoto wake bitw wakiwa wamekaa hapo nje kila mmoja kashika tama, na tayari kagiza kameshaanza kutanda,.. Waliona taa za gari zikiwaelekea huku waliko…, taa iliwakera mno mana walikuwa katika dimbwi la mawazo,…. Ghafla gari inasimama karibu yao na adam anashuka na kumsalimia mama mkwe
“mama, shikamoo mama”
“marahaba baba, ooooohhh mtumishi? Tumsifu yesu Kristo”
“milele amina”
“karibu ndani”
Wakati huo eva nae ndio anatoka ndani, bite akamkimbilia dada yake baada ya kusalimiana na shemeji yake,… Mama haamini kama leo mwanae kaletwa na gari japo aio mara moja kuletwa na gari, ila kwa sasa kuna changamoto kidogo hivyo lazima kuwepo na mshangao kiasi,…
“karibu baba mtumishi”
“Ahsante sana….”
“biteeee, we bite… Hebu kalete maandazi haraka mtumishi apate chai”
Aliongea mama kwa kumtuma bite, lakini adam alikataa kupata chai kwa maana ya kuwahi nyumbani,… Kweli kwa akina eva maisha si mazuri, yaani ni watu wanaomtegemea mungu vibiashara vidogovidogo ambavyo mama huyo huweka nje ya kanisa ili apate kuuza angalau hata juisi,… Na ukiwaona huezi jua kama ni watu wa dhiki, mana wahenga walisema kuwa, UMARIDADI HUFICHA UMASIKINI,… Ghafla simu ya adam iliita, kuangalia jina, alikuwa ni baba yake
“haloo mchungaji”
Aliita adam huku simu ikiwa sikioni
“sijakukuta nyumbani upo wapi usiku unaingia huu”
“aahh nakuja sasa hivi baba”
“hebu wahi nina maongezi na wewe”
“sawa”
Adam hakutaka kuchelewa, alimuaga mama yake eva kisha akatoka zake nje… Aliingia katika gari lakini ghafla eva kaja nae kaingia katika gari,
“nimeona sms yako, kuwa ukitoka nikufuate”
Aliongea eva, kumbe hakutaka kumuita mbele ya mama yake…
“ndio, kwani ni vibaya kumuita mama mchungaji wangu”
“hahahahaha hapana si vibaya”
“ok… Shika hiki kiasi, kitawasaidia”
“lakini baba mtumishi”
“lakini haitakiwi,… Ashukuliwe baba muumba kwa riziki kupatika…. Kwaheri, tuonane kesho kanisani.. Afu, naomba hio pesa ikiisha unipe taarifa,… Staki mama mkwe akakae juani tena, kuleni vizuri muombeni mungu sana.. Mwezi huu huu naweza kuoa”
Aliongea adam huku akiwasha gari
“Catherine au”
Aliongea eva huku akiwa kashika tama
“sina uwezo huo, naoa nilichokipenda.. Hata vitabu vya mungu viliandika, Mpende anaekupenda”
Adam aliongea mengi sana,… Kumbe hata kabla ya adam kuondoka, yeye ndio alikuwa akitegemewa na familia ya eva,.. Mana baba yake eva alikuwa ni mzee wa kanisa moja wapo kati ya makanisa ya mr Jacob, hivyo baada ya kifo cha baba yake eva,… Adam aliamua kubeba jukumu zima la familia hio, mana mzee yule alikuwa akiishi kwa sadaka za waumini, sasa hayupo, nani achukue sadaka.. Hakuna…. Hivyo adam kachukuwa jukumu hilo peke yake…. Na anajua waliteseka sana kipindi yupo masomoni,.. Japo aliwaachia kiasi kikubwa cha fedha,..
“mtumishi jacob kaniita, hivyo wacha nimuwahi”
Aliongea adam kumaanisha baba yake kamuita….
“sawa,… Naomba bwana yesu aingilie kati mahusiano yetu, mana tuna nia njema na huu ulimwengu”
Aliongea eva,.. Na wakati huo ibada ikadondoshwa hapo hapo kwenye gari,… Mama na mtoto wake bite kusikia ibada inadondoshwa, nao wakaungana nao kwa kupiga magoti kisha kuomba sambamba na wao,..

Baada ya maombi, adam aliondoka zake…. Sasa eva anakwenda kukagua kapewa kiasi gan,…
“yesu wangu, kakupa pesa zote hizi”
Aliongea mama yake eva huku wakizimwaga mezani,…
“mama, unajua kweli mtumishi adam anaona mbali sana… Hivi kajuaje kuwa humu ndani tunaishi kwa uwezo wa mungu pekee… Kajuaje kuwa hatuna kitu.. Mama?? Ashukuliwe baba Muumba mbingu na ardhi”
Kiukweli pesa walizopewa zilikuwa ni nyingi, kwa haraka haraka, labda ni kitu kama laki tano hivi, ila inazidi zaidi ya hapo…… Walifurahi sana na kuzidi kumuombea mtumishi adam

Huku kwa mzee jacob akiwa kaketi Katika sofa la uvivu, yaani lile la kulala,… Ghafla alisikia honi ya gari,.. Alijua tu ni mtoto wake adam ndio anakuja… Kweli alikuwa ni adam, au mtumishi adam

Je? Kwenye maongezi wataongelea nini?? Na kama ni swala la adam kumuoa Catherine, je Adam atakubali au atapinga….

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : Young paster sehemu ya sita (06)
Young paster sehemu ya sita (06)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-sita-06.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-sita-06.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy