input license here

Young Paster sehemu ya pili (02)

YOUNG PASTER EP 02

Ilipoishia

MCHUNGAJI MCHANGA

“mamaaaaaa….. Usiseme hivyo”
“sikuombei umkose mwanangu… Ila wanaume wa siku hizi…. Siwawekei mia kwa mia… Hawakawiii kubadirika”
“ni kweli mama… Lakini sio kwa mtu mwenye imani kama adam”
“eva mwanangu, mimi ni mama yako… Nimekuficha mengi sana kuhusu adam…. Na nikisema nikuambie nitakupoteza mwanangu… We mpende tu”
Eva alitoa jicho kuskia mama yake anasema maneno hayo…..
“unasemaje mama”
“una kifua cha kubebea jambo mwanangu, tusije kuanza kupepeana na kanga hapa”
Aliongea mama yake eva huku wakikaa vizuri kitandani
“mama… Nipo tayari kumwacha adam kama ana tabia chafu”
“heeeeee wewe ndio wa kusema hivyo”
“mamaaaaa Niambie basi nijue”

ENDELEA NAYO……

Eva alikuwa na wasiwasi mno kuhusu mchumba wake ambaye mama anasema ana siri nzito sana juu ya adam.. Sasa eva kakaa kwa umakini ili kuweza kujua ni siri gani hio ambayo mama anaijua… Eva alitamani hata kutoa chozi, lakini ghafla mama anacheka kweli mpaka machozi yanamtoka kwa kucheka,..
“kumbe mwanangu unampenda sana adam… Mimi nikajua utakuwa umemsahau kabisa kutokana na muda aliokaa masomoni sana… Kumbe bado unampenda… Kiukweli hakuna lolote mwanangu, nilikuwa nakutisha tuuu”
Hapo eva akashusha pumzi nzito kisha akachukuwa Biblia na kuanza kusoma kama vile kamkasirikia mama yake…
“mwanangu usinune basi jamani… Yesu hajafundisha umnunie mama yako eva”
Eva kweli anajua sheria na mafundisho alio yaacha bwana yesu
“mama, sijakununia mama angu”
Aliongea eva huku akimkumbatia mama yake,…
“najua nimekuuzi mwanangu”
Mara bite kaja mpaka chumbani,.. Yaani watoto wa huyu mama ni wazuri, mpaka basi sema hali ya maisha kwao ni ngumu mno, na wanaishi hivyo hivyo kwa nguvu za mungu….

Tukiachana na familia ya akina eva sasa turudi huku kaisani, walikuwepo waumini waliosikia fununu za kuwa mtoto wa bishop jacob yukaribuni kuja Tanzania kutoka masomo, hivyo hizo ndio atori zilizo zagaa katika kanisa hilo… Inaonekana ni jinsi gani adam anapendwa na waumi sasa hatujui adam ana lika gani na ana rangi gani, na yupoje yupoje.. Bali sifa zake ndio huongelewa zaidi….
“ester, iv umesikia za chini chini kuwa adam yukaribuni kuja”
Aliongea dada mmoja ambaye ni muumini wa kanisa hilo la mr Jacob
“adam gani tena…. Au adam yule wa karne ya 5”
“aaahhh we ester huelewi kwanini”
“sasa Janet, mi namjuaje huyo adam”
“si adam wa Bishop Jacob”
Ester kusikia ni adam wa bishop Jacob nae alitahmaki, walikuwa wasichana wengi na wao pia walitahamaki….
“we janet muongo… Adam si yupo Nigeria kimasomo wewe”
“sasa anakuja.. Nimeskia za chini ya kapeti… Wiki hii ndani ya Arusha”
“eeeeh bwana weee…”
“alafu sasa…. Umeona kanisa lake”
Alizidi kuongea janet huku wengi wakiwa hawajui…
“weeee, ina mana mchungaji Jacob ana kanisa lingine”
Aliuliza mmoja wa marafiki wa janet
“sio la mchungaji Jacob ni la adam”
Aliongea janet tena kwa kujiamini haswa….
“we janet wewe, unajua bwana yesu hajafundisha uongo”
“sasa huu ni uongo au ukweli”
“skia adam, hana mke, adam bado anaishi kwa baba yake… Adam bado ni mdogo, hawezi kabidhiwa kanisa… Kwanza huo upako wa mpaka apewe kanisa kautoa wapi”
“heeeeeee Cecilia,… Ivi hujui kuwa uchungaji ni wito toka kwa mungu.. Uchungaji aio lazima awe…… ”
Ghafla janet alinyamaza baada ya kumuona mzee wa kanisa akipita maeneo hayo, mana wanacho kiongea ni siri, bado hakikuwekwa wazi kuwa kijulikane, ni nyepesi nyepesi tuuuu…. Baada ya mzee wa kanisa kupita janet aliiacha ile mada mana ni hatari sana kwa midomo yao
“ester, unajua mimi nawadokezeeni tu.. Sasa tuachane na hii mada”
“ok, afu… Leo nimemwona eva karuka ruka pale alivokutana na mama mchungaji”
Aliuliza ester mana jenet kwa fununu hajambo
“hapo ndio hata mimi nikajua kuwa adam anakuja wiki hii… Mana baada ya pale nikamfuata bite mdogo wake eva ndio nikamuuliza mbona dada yako amekuwa na furaha sana.. Ndio akaniambia kuwa mchumba wake anakuja”
Aliongea hivyo janet huku akina Esta na wengine wakacheka….
“ivi janet, eva anajidanganya kabisa kuwa ataolewa na adam…. Aache kutafuta mtoto wa Bishop kama yeye, aje aoe maskini kuliko hata mimi”
“we ester wewe, chunga mdomo wako huo… Ukisikiwa unaongea huo ujinga, mi simo”
Aliongea janet huku akishika mkoba wake na kuanza hatua kana kwamba hawahitaji maongezi yanayo muhusu eva…

Baada ya masaa kadhaa kupita sasa tukiwa huku nyumbani kwa Bishop Jacob, wakiwa mezani wanapata chakula cha usiku…. Na hapo walikuwa wakiomba kabla ya kula,… Kama kawaida wa wakristo lazima waombe maombi marefu tena wengine huchukua hata dakika 10 kwa maombi tu… Familia yenye watu watano, baba na mama na wasichana watatu… Baada ya kuomba walianza kula huku vikisikika vijiko tu vikigongana katika sagani, yaani hawaruhusiwi kuongea wakati wa kula… Ukweli walikuwa ni matajiri sana, yaani haikuwa mboga saba kama tunavyojua… Hata mimi mwandishi, naona kuna vibakuli zaidi ya kumi… Yaani, yaani walizidisha hata sio ile mboga saba… Walimaliza kula hatimae mfanyakazi anapata kazi ya kuwaandalia maji kila mmoja wao, japo wasichana hao wana malezi bora hivyo hawahitaji kuletewa maji.. Wanayafuata wenyewe,…. Baada ya hapo watoto wote waliondoka na kuingia kwenye vyumba vyao, mana kila mschana ana chumba chake… Jumba lenyewe kubwa kama kanisa…
“haya baba mtoto…. Mwanao ndio huyo anakuja….umemuandalia nini mana sasa akija ni kazi moja hapa mtashindana weeeee”
“ahahahahahaha…. Mama Jessica,.. Mimi nina tabu gani… Kanisa lake limeshafaa, akija nitawaita wazee wa makanisa yangu yote… Kama anafaaa kuwa mchungaji aendelee”
“kama anafaa?.. Kivipi.. Kwani huko shule kaenda kufanya nini kama sio kujiongeza… We si unamjua mwanao, yaani kabla hajaenda huko, akishika tu mtu kichwa anadondoka chini na hapo hajaenda Nigeria, je akirudi itakuwaje”
“na ndio mana nikampeleka kwa rafiki yangu, yaani najua makanisa yote ni ya mwanangu.. Sina pingamizi juu ya hilo”
“mmmmhhh angalia msije mkaanza ushindani, mana kazi ya mumgu yahitaji uvumilivu toka kwa bwana yesu… Tumuombee mtoto wetu huko aliko”
“milele amina”
Walikuwa wakiongea huku wakipata juis kwa mbali,…

Baada ya siku hio kupita na leo ni siku ya jumatatu, mr Jacob amiwa katika shughuli zake, mana unaambiwa tii wito wa mungu kisha katafute kula… Hivyo siku za juma bishop Jacob yeye huwa bize na kazi zake, na katika makanisa yake kuna wale mapasta wadogo wadogo ambao watakuwepo wiki yote kwa ajili ya maombezi, na Jacob ana ofisi yake inayohusu kanisa… Hivyo ya kanisani ni kanisani na kazini ni kazini… Bishop jacob ni mtu wa kumuomba mungu kila wakati, yeye na Biblia, kwani hata kazini kwake ana Biblia aina zote,.. Wafanyakazi waliopo hapo ni wakristo wote, yaani kila mfanyakazi ana rozali yake mezani, bwana Jacob akiingia ofisini kwake ni yeye na neno la mungu, hataki kupitwa na lolote….
Akiwa hapo ofisini mara ghafla simu yake inaita, alikuwa ni Bishop james, yaani huyo ni kipawa mwenzie mwenye kipawa cha Bishop,…
“tumsifu Yesu Kristo james”
Alisalimia jacob huku akitabasamu kwa mbaali
“milele amina… Naona kwenye kikao sikuoni huku njiro”
“aahhh nimetingwa kidogo… Si unajua kijana wangu hayupo sasa hivi nahangaika mwenyewe, mana angalau alikuwa anafuatilia miradi ya baba yake lakini sasa hayupo”
“aaahhh lakini nadhani ni wito wa mungu juu ya kulitangaza neno la bwana yesu alie hai”
“ndio, na hana muda atarudi”
“yesu asifiwe bwana jacob”
“milele amina… ”
“basi nilikuwa nakujulia hali tu.. Mana sijakuona katika kikao cha leo”
“hakuna shida mtumishi wa Mungu”
“haya siku njema na yesu akutangulie”
“milele amina… nawe pia”
Simu ilikatika na mzee akaendelea kupata neno la mungu,… Na uzuri wa wakubwa kama hawa hua wana vitabu vya mungu vya pande zote mana hata hapa kwa Bishop jacob, ana kitabu cha Kiislamu, ni kawaida ya viongozi wakubwa hua lazima ujue neno la upande wa pili ili kujua kama kuna utofauti na upande wao,.. Hata papa mwenyewe ana kitabu cha Kiislamu,… Na ndivyo inavyotakiwa kujua upande wa pili wa dini ya mwenzio… Na sio kuwa hawakiwezi kukisoma, wanakiweza haswa… Na sio hao tu hata wale viongozi wa dini ya kiislamu kuna basdhi yao wanaijua Biblia kuliko hata wewe Mkristo ambae ni kitabu chako kotakatifu..

Tukija huku kanisani alionekana eva akiwa anaomba sana… Na siku hio kulikuwa na maombi ya kawaida tu, na hakui na watu wengi kama ilivyo Jumapili,… Eva ni mschana aliopendelewa kila aina ya mwili wake, yaani kiukweli ana haki ya kuitwa mrembo wa kanisa, japo haitowahi kutokea lakini hio nafasi inamfaa….
“eti yule, aje kuitwa mama mchungaji.. Inawezekana kweli”
Aliongea Janet wakiwa katika mlango wa kuingilia, mana eva alikuwa bize na maombi huku akiwa kafumba macho yake….
“nashangaa hata mimi…. Ww ulizani adam ni wa mchezo mchezo”
“lakini janet? mbona familia zao zinajuana”
“hata kama esta, ila sio rahisi adam kumuoa eva”
“hebu kaone kanajifanya kanajua dini sanaaaaa”
“weeee janet sio vizuri, huko tunapokwenda sasa ni unafiki jamani janet… Hebu tuyaache hayo”
Lakini sasa kumbe walipokuwa wakiongea walikuwa wakisikiwa na mzee wa kanisa… Kitu ambacho hajakipenda mzee huyo….  Lakini hakuwaambia kitu chochote…
“huyu mzee katokea wapi”
Aliongea janet huku wakimshangaa

Baada ya siku hio kuisha,… Bwana Jacob akiwa kazini ikiwa ni siku ya Jumanne,.. Alikuwa na rafiki yake aliokuja kumtembelea ofisini kwake,..
“yusi ni mkuu, madam tumekutana leo basi yesu katenda miujiza”
“ni kweli bwana Jacob, yesu amefanya makubwa na nadhani anakwenda kufanya makubwa”
“yesu asifiwe bwana yohana”
“amina”
“haya nipe taarifa za jimbo lako”
Aliuliza kumaanisha ampe taarifa ya makanisa yake yanaendeleaje… Mana hata huyu bwana yohana ni Bishop kama alivyo bwana Jacob.. Hivyo vipawa vyao ni sawa..
“bwana weee, nataka Yesu afanye miujiza juu ya vijana wetu”
Aliongea bwana yohana…. Huku bwana Jacob asielewe maana ya maneno ya yohana…
“ni kweli ila sijakuelewa”
“aaahhhh, juzi uliniambia kijana wako yupo karibuni kuja… Na ulisema ana kanisa lake lipo tayari, nami najua kabisa kijana wako baado hawezi kukabidhiwa kanisa bila kuoa… Nina binti yangu, kwanini yesu asifanye miujiza juu yao”
Aliongea bwana yohana huku bwana Jacob akitabasamu…..

Huku kanisani masikini eva ni mtu wa maombi hataki kushindwa na shetani juu ya watu wanaomuandama kumbe jana mzee wa kanisa alimtonya kuhusu akina janet… Sasa eva wa watu kila kukicha ni yeye na maombi, anamuombea mchumba wake afike salama… Lakini sasa uchumba wao unaingia dosari, bwana yohana nae ana binti yake, nae anataka waowane na mtoto wa Bishop jacob…..

Sasa huku ofisini katika maongezi ya bwana Jacob na bwana yohana, yanayo husu muunganiko wa watoto hao wawili, na ni kweli sheria za kiwa mchungaji shariti uwe na mke… Japo wengi wanafosi tu.. Sasa leo bwana yohana anakuja kuzima ndoto za eva mwenye tegemezi la kuolewa na adam, mtoto wa mr Jacob……

Je? Nini kitaendelea???
Related Posts

Related Posts

Chapisha Maoni