Young paster sehemu ya nne (04)

YOUNG PASTER EP 04:


Ilipoishia..

MCHUNGAJI MCHANGA

uolewe na mtoto wa jacob, mana yule ana mchumba wake, afu istoshe yule kijana katembezwa sana na baba yake nchi mbalimbali, anajua starehe za kila aina… Mi sitaki uolewe nae”
Catherine alinuna ghafla, mana hata huyo mwinjilisti sio kuwa alimpenda sana,…
“mama mbona mimi nimekubali”
Mama kusikia hivyo alishtuka na kumwangalia mwanae kwa hasira
“unasemaje wewe”
“mama, nilikuwa nikimpenda sana adam, nilikuja kupoteza mawazo juu yake baada ya kusikia ana mchumba”
“ivi Catherine nikuulize swali”
Mama alibadirika kabisa na kua na hasira…..
“swali gani tena mama”
“ivi usichana wako unao wewe…. Mana ile familia ni ya kitajiri haswa, na haitaki mschana ambae hana bikra…. Sasa kama huyo mwinjilisti wako umeshampa…. Jua adam sio wako mama.. We jishaue tu”

ENDELEA NAYO……

Katika maisha ya kuoa kuna wanaume hawajali uthamani wa mwanamke, nikimaanisha BIKRA… Na wengi wetu hua tunaoa wanawake wasio na bikra, lakini kuna mahali mwanamke akukosa bikra tu, basi hata kuolewa kwake ni kwa tabu, hususan Zanzibar… Mzanzibari akikosa bikra ataolewa sawa lakini ataishi kwa masimango sana, na hata familia haitompenda sana mana wanahisi kaleta nuksi katika familia yao… Au kama hana bikra pia huenda akaolewa mke wa pili… Kule wanajali sana bikra tofauti tanganyika yetu.. Hua tunaoa tu… Lakini kama na sisi tungelikuwa na mikakati kuwa bila bikra mwanamke haoleki,.. Walahi nakuapia ungekuta kila mschana ana bikra huko mtaani… Lakini sasa hakuna.. Na pia Tanzania wapo ambao bila mwanamke asie na bikra haoi….

Sasa tukiwa katika simulizi hii ya YOUNG PASTOR, kumbe mr Jacob hataki mtoto wake aoe mwanamke asie na bikra,… Sasa hapa Catherine alikuwa akiulizwa na mama yake kuhusu usichana wake upo au keshampa yule mwinjilisti wake…

“ivi usichana wako unao wewe…. Mana ile familia ni ya kitajiri haswa, na haitaki mschana ambae hana bikra…. Sasa kama huyo mwinjilisti wako umeshampa…. Jua adam sio wako mama.. We jishaue tu”
Aliongea mama huyo aitwaye Melissa, ambaye ndio mke wa mr Yohana au Bishop yohana..
“niambie, mbona wantumbulia macho mimi”
Mama alikuwa mkali sana juu ya mtoto wake, mana yeye roho ilikuwa ikimuuma kwa kitendo cha mtoto wake huyo kuchaguliwa mchumba ingali ana mchumba wake,….
“mama, toka nizaliwe… Simjui mwanaume wa aina yeyote ile… Kama huamini nikague uone”
Aliongea Catherine huku akiamka na kuanza kufunua ahumizi lake ili mama amkague
“nitolee ujinga wako apa”
Aliongea mama yake Catherine huku akiondoka na kufunga mlango kwa hasira,… Sasa swali linakuja je? Mbona mama hataki mtoto wake aolewe na adam, kwanini??… Hapo kuna jambo zito hatulijui tu…
Wakati Catherine bado anaendelea kuangalia picha ya Adam katika mitandao ya kijamii, akiwa anahubiri katika moja ya makanisa yao mwaka uliopita, mana mwaka huu wote hakuwepo Tanzania, hivyo hizo ni picha za awali tena katika tovuti ya kanisa lao, mana adam hata mitandao ya kijamii hajawahi kujiunga… Sasa Catherine alichukuwa picha kadhaa katika tovuti moja inayomiliki makanisa yote, yaani makani yote ya Bishop Jacob, habari zake hupatikana katika tovuti moja… Hivyo Catherine alichukuwa picha kadhaa na kuziposti kwenye ukurasa wake wa Instagram, na kuandika maneno kadhaa katika picha hizo.. Na wakati huo ni usiku yapata kama saa 4 hivi

Kesho yake ikiwa ni siku nyingine tena,… Catherine aliamka akiwa na furaha sana kwa swala lile, sasa inashangaza kuwa kwanini Catherine alimpenda huyo mwinjilisti ingali alikuwa akimpenda adam… Hapo napo kuna maswali…. Catherine hata kuoga kwake, alikuwa akimuwaza tu adam, yaani sijui ampe nini baba yake kwa kufikiria jambo kama hilo… Hivyo Catherine yupo tayari Eva amkose adam…. Wakati huo mzee yohana nae alikuwa akijiandaa kwenda katika shughuli zake za kawaida, mana ukishatoa wito ulioagizwa na mungu wako juu ya watu wake basi hakuna shida hata ukienda kutafuta kula…

Wakati huo huku nyumbani kwa akina Eva,… Msichana mpole mtaratibu, akiwa anafanya usafi huku akiimba kwaya za kumsifu bwana yesu…
“yeeeesuuu alinitendea weema, na kila siku nipo naeeee”
Sasa akiwa anaimba mara ghafla mama yake katoka…
“heee eva mwanangu hujaenda kanisani”
Aliongea mama huyo wakati huo anatoka nae kuelekea kanisani,..
“mama, bite hayupo kaenda shule… Sasa nani atafanya usafi”
“sawa.. Hebu hakikisha misa ya pili haikosi sawa mwanangu”
“sawa mama… Tumsifu Yesu Kristo”
“milele amina”
Mama alibeba Biblia yake huku akielekea kanisani…

Sasa huku kanisani, kuna wale wasichana ambao hawapo kwa ajili ya kumwomba Mungu wao, kazi ni kufuatilia maisha ya watu, hususan ya mwanadada Eva,…
“heheheheeeee, Yesu kafanya miujiza kwakweli janet”
Alikuwa ni esta aliomkuta janet akiwa katika bustani ya hapo kanisani anajisomea Biblia,…
“wewe esta.. Hebu tulia kuna ukurasa unanipa ashki ya kuusoma”
Aliongea Janet ambae ndio mbea mkubwa lakini cha ajabu umbea aliokuja nao esta Janet haujui…
“ivi janet, ulijuaje kuwa eva hatoolewa na adam”
Sasa wakati wanaongea hilo, na mama yake eva ndio anatokea na kusikia hilo neno, japo eva wako wengi, lakini aliposema na adam… Huyu mama ikamjia tu huenda ni eva wake,..
“una maana gani esta”
“iv unamjua yule mschana wa mtumiahi yohana”
“yuleeee… Ndio ana wasichana wawili.. Catherine na Pendo”
“sasa huyo Catherine… Ona alichoandika juu ya picha ya adam”
Esta alifungua simu yake na kumwonyesha janet…..


yalikuwa ni maneno yalioandikwa katika picha alioipost Catherine katika akaunti yake ya Instagram,… Sasa janet alivyo hakaushi kaamka kwa furaha na kupiga kelele
“nilisema mimi…. Masikini na tajiri wapi na wapi… Mi najua tajiri kwa tajiri masikini na masikini mwenzie”
Sasa mama eva ndio anasikia hizo habari na kushindwa kuelewa inakuwaje hapa, mana kasikia kila kitu kasolo tu hayo maneno yalio andikwa katika picha ya adam huko Instagram,…
Mama roho ilianza kumuuma, mana mtoto wake atakuwa katika hali gani endapo atasikia taarifa hizi..
“Eehh mungu wangu… Pokea maombi ya mwanangu”
Aliongea mama huyo huku akinyoosha mikono juu katika msalaba uliopo mlango hapo ikiwa na sanamu la Yesu katika msalaba huo…. Mama aliingia ndani lakini akina janet hawakujua kuwa mama eva aliwasikia wakiongea jambo hilo.. Mama alitamani kumwambia mwanae kupitia simu, asije kanisani  lakini sasa alisita mana ni sehemu ya kila mja kumwomba Mungu wake…

Sasa huku nyumbani kwa akina adam, au Bishop Jacob,.. Akiwa anafungiwa tai na mke wake…
“sisi leo hatutofika mana tunakwenda kumpokea mtoto…. Na wewe pia usichelewe huko”
Aliongea mama huyo huku akimkaba mtumishi tai yake…
“nyie kampokeeni tu…. Ila nitamjulisha mr Yohana kuwa, amtaarifu mtoto wake kuwa adam anakuja”
Sasa mama adam yeye bado hajagusiwa kuhusiana na habari za adam kumuoa mtoto wa mr yohana..
“sasa huyo mtoto wa mr yohana na adam wanahusiana vipi”
“heeeeeeee, mama Jessica, ivi sijakwambia”
“umeniambia lini mimi jamani baba Jessica”
“Mr yohana, kasema yupo tayari mtoto wake aolewe na adam… Na sasa adam anatakiwa kuwa mchungaji rasmi, na kama ulivyosema kuwa hawezi kupewa uchungaji bila kuoa… Sasa sio vibaya kumuoa mtoto wa yohana”
Mama kusikia hayo maneno, kwanza alishika kifua chake kuashiria hio habari kwake sio sahihi kabisa… Mana huyu mama anamjua mtoto wa kike mkubwa wa mzee Yohana, ni mschana mzuri sana na ana tabia nzuri lakini… Mama adam anamjua kiwa Catherine havaagi nguo za heshima japo sio mhuni lakini nguo zake ni za kisasa mno, kitu ambacho mama adam sidhani kama atakubaliana nacho…
“sasa hapa tunapoteza muelekeo wa mtoto wetu”
Aliongea mama Jessica huku akiwa hana hata nguvu, mana mume akiamua kitu, basi hata mke kuzuia ni asilimia chache sana….
“kwanini mama Jessica….. Mtoto wa mr Yohana si unamjua wewe…. Sio mbaya akiwa mwali wako… Nipe koti langu niende kanisani”
“baba Jessica…. Adam ana mchumba wake lakini”
“sikutambulishwa, hivyo simjui… Aoe mwanamke ninaemjua mana mr Yohana ana maadili mazuri hivyo najua hata watoto wake watakuwa kama baba yao”
Mzes Jacob alichukuwa koti lake kisha huyo kaelekea katika gari yake.. Na wakati huo mr Jacob anampigia aimu mr Yohana kuwa amwambie mtoto wake Catherine aelekee Airport mana adam anawasili leo katika uwanja wa ndege wa KIA (Kilimanjaro International Airport)
Mama alikuwa akisikia taarifa hio ikotolewa kwa njia ya simu.. Lakini mama akiwa na huzuni juu ya mtoto wake kuozeshwa mwanamke ambae ana tabia ya kisasa, japo kwa namna moja ama nyingine ni mschana mstaarabu, lakini mavazi yake tu ndio shida kwa jamii.. Mana hata kanisani kwao yeye hajali anachokivaa…
“mama, mbona umekuwa mnyonge hivyo, na ulisema leo unapika chakula kizuri kwa ajili ya kaka adam”
Alikuwa ni Jessica mtoto wa kwanza katika familia hio, ana miaka 28 na adam ana miaka 24,… Kisha anafuatiwa na martha 20  na maria 15, yaani mama kawapangilia vyema watoto wake, wasipishane sana….
“Jessica, ivi umelisikia wazo la baba yako”
Aliongea mama huyo kama vile anataka kumpa taarifa hio…
“taarifa gani tena mama”
“kasema, Adam atatakiwa kumuoa mtoto wa mr yohana”
“Whaaaaat???…. Yule mvaa vimini au yupi”
“huyo huyo”
“baba kawaza nini lakini”
“mimi hata sijui”
“ila mama, yule mschana ni mzuri haswa”
“mimi sihitaji uzuri wa sura au umbo… Nataka mwanamke mwenye tabia nzuri”
“sasa mama… Na eva wa watu maskini kama namuona vile”
“mimi hata sijui nitamwambia nini yule mtoto, mana anavyoniheshim… Mana anajua fika tayari mimi ni mama mkwe wake… Na nimeahamkubali eva kwa asilimia zote”
“sio wewe tu…. Hata mimi nampenda sana eva… Ila kwa jinsi adam anavyompenda Eva… Heeee patachimbika hapa mjini”
“kwanza… Mpigie simu eva aje nyumbani… Twende naye Airport”
“sawa”

Sasa huku nyumbani kwa akina Catherine, baada ya kupata taarifa kuwa adam anakuja leo na ndege ya saa kumi jioni… Huezi amini Catherine katoka kanisani mpaka nyumbani, hapo kitandani kwake kumejaa nguo na hajui avae ipi ili aende Airport kumpokea mtarajiwa wake… Na taarifa hio kapewa na baba yake live bila chenga, japo alianza kuisikia toka jana… Sasa hapo hajui avae nguo gani,.. Mama vimini…..

Sasa huku kanisani mzee Jacob akiwa yupo kwenye lifti kuelekea ibadan… Alishika simu yake na kumpigia mtoto wake….
“halooo, shalom”
Huyo ni mzee Jacob, lakini sauti ya adam haisikiki hapo
“habari ya safari mwanangu”
Ni huyo huyo Jacob ama Bishop Jacob
“ok sasa…. Katika watu watakao kupokea hapo Airport, mmoja wapo ni mtoto wa mr Yohana”
Aliongea mzee Jacob huku kama vile adam kamuuliza kitu mzee wake
“najua hujui baba…. Ila ndio atakuwa mkeo, baba yako nakuchagulia mke mwenye heshima bora.. Anaeijua dini na ana wlimu kama ulivyo mwanangu”
Aliongea mzee huyo kwa kumsifia Catherine…
“nimeshasema mimi baba yako.. Na hakuna wa kupinga hilo… Huyo mchumba wako mimi simtambui… Na usipofanya hivyo lile kanisa nitalibinafsisha kwa watu wengine”
Adam alionekana kukataa swala hilo, lakini mzee akachimba mkwara wa hali ya juu kwa mtoto wake
“adam, hata wazee wa kanisa hawawezi kukubalia kuwa mchungaji endapo hutakuwa na mke… Mchumba wako yupo hapo Airport anakusubiri.. sawa”
Aliongea mr Jacob huku akiwa kama anamlazimisha mtoto wake amuoe Catherine…
“hayo sasa ndio maamuzi mwangu… Hongera kwa kunielewa baba yako”
Mzee Jacob alionekana kuwa na furaha juu ya adam kukubali wazo la baba yake…

Baada ya masaa kadhaa kupita, familia ya mr Jacob ikiwa imejaa katika uwanja wa ndege mkoani Kilimanjaro,…. Lakini kati yao mtoto wa mr yohana yupo hapo hapo.. Na pia Eva nae yupo hapo hapo.. Lakini sasa Catherine yeye anajua tu kuwa adam ana mchumba lakini hamjui huyo mchumba mwenyewe, hivyo hapo EVA NA CATHERINE hawajuani kabisa, ila wanajuana tu ile kiumini umini, Eva anamjua Catherine kama mtoto wa Bishop Yohana, lakini hajui kama ni mchumba mwenzie….. Huo ni ubabe alioufanya mama yake adam, na wakati huo masikini eva hajui lolote kuwa kuna taarifa za kitoolewa na Adam…. Eva alikuwa anaruka ruka kwa furaha…. Masikini ya mungu, laiti angelijua kuwa hapo hana chake, basi hata hapo Airport asingetakiwa kuja, sasa mama Jessica au mama adam hakumwambia kitu eva…

Dege kubwa liliokuwa linatua katika uwanja huo, yaani eva alitamani hata kuifuata ile ndege kabla haijasimama, lakini kapoozeshwa na mama mkwe wake, mana ni mwaka sasa umepita hajamuona mchumba wake,.. Walishuka abiria wote,… Na Adam alikuwa ni abiria wa mwisho kushuka
Laaaa haulaaaa…..
SHARBIN RASHIDI KINGAZI ndio mwenye jina la Adam katila simulizi hii, na ndio yeye akiwa kapigilia suti yake saafi… Kweli mwenye mali ni mwenye mali tu… Eva ndio mtu wa kwanza kumuona adam wake,… Yaani hivyo alivyoanza kukimbia, utapenda yani…. Sasa Catherine nae anashangaa huyu anaeanza kukimbia kwa kujiua ua ni nani… Hakuta kujua sana, ila nae alianza kumkimbilia adam… Wakati huo adam kashika kibegi chake.. Mana begi kubwa linabuluzwa na wahudumu wa hapo uwanjani…. Maskini Adam kasimama na asijue amkumbatie yupi kati ya wawili hao
PATAMU APO……

Je? Adam atamkumbatia nani? Mana taarifa ya Catherine anayo yote, hivyo anamjua Catherine vizuri tu. USIKOSE
DONATE VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Your donation helps the Admin to be even more active in sharing quality blog templates. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni