Young paster sehemu ya nane (08)

Young paster 08


Ilipoishia ,

MCHUNGAJI MCHANG

Sasa waumini walikuwa wakisikia tu mtoto wa Bishop Jacob karudi, lakini hawakuwahi kumwona kwasababu alikuwa hasalii kanisa hilo,…
Sasa ile adam anaingia tu,… Hata baba yake alishangaa, waumini walinyanyuka wote na kusema
“tumsifu yesu Kristo mtumishi adam”
Hata adam alishangaa, yaani waumini wanampenda kupita maelezo,… Hata Catherine haamini kuwa kanisa zima limenyanyuka kwa ajili ya adam… Mzee jacob haamini, yaani mtoto wake anakubalika kuliko yeye,
“asifiwe bwana mwokozi wetu”
Aliongea adam huku akipunga mkono,.. Lakini sasa vile alivyokuwa akipunga mkono, waumini wengi walikuwa wakitetemeka,.. Adam anashangaa mbona baadhi ya wingi wa waumini hutetemeka… Akajaribu kupungia tena… Sasa kumbe adam hajajua kuwa sio waumini peke yao,.. Mana ndio alikuwa akiwapungia mkono,.. Ghafla ilisikika sauti ikisema
“adam acha, inatosha, hebu chukua kiti na ukae”

ENDELEA NAYO……..

Kawaida ya kanisani au msikitini hapatakiwi kuwa na mapendo, mana pamejaa maombi na dua za kila aina kila siku,…. Hivyo hata pepo au shetani hana nafasi katika nyumba hizi mbili,… Lakini inashangaza ya kwamba katika kanisa kubwa la ROHO MTAKATIFU liliotakaswa kwa damu ya yesu, leo ninaonekana kuwa na mapepo,… Kivipi na wakati linaongozwa na Bishop Jacob, yaani ni wito ulio mkubwa kwa mungu baba

Adam aliingia na waumini wote kunyanyuka katika viti vyao kisha wakamsalimia adam kwa furaha, mana ni mtu aliojaa upako, aliotakaswa kwa damu ya Yesu na akatakasika, na ni kweli sio uongo, adam hakutaka kukaa kimya kwa salamu ya waumini hao, ilibidi nae kwa furaha kuamsha mkono wake juu na kupungua huku akisema
“asifiwe bwana mwokozi wetu”
Lakini sasa cha ajabu na cha kushangaza, aliona watu wakitetema kila anapopunga mkono wake,.. Hio iliashiria kwamba waumini wote hawakuwa sawa,.. Lakini sasa kumbe sio waumini pekee, hata mr Jacob pia ilikuwa ikimtetemesha ile hali ya mkono ukipungwa, huku akitaja jina la mungu… Sasa kwakuwa adam yeye alikuwa haoni nyuma kuwa baba yake nae alikuwa akitetema, ndipo mama yake adam akapaza sauti kwa nguvu na kumfikia adam..

“adam acha, inatosha, hebu chukua kiti na ukae”
Aliongea mama yake adam huku akivutwa na mama yake,… Adam alishangaa hili kanisa limevamiwa na nini? Mbona limejaa mapepo kiasi hicho na baba yake akiwa mhudumu mkuu wa kanisa hilo….. Sasa adam alimsikiliza mama yake na kuketi katika kiti, lakini bado kulikuwa na waumini waliokuwa wakipiga kelele, mana wengine walikuwa wakitokwa na mapepo pale adam alipokuwa akipunga mkono,… Na adam mpaka hapo hajui kuwa hata baba yake alikuwa akitetemeka,…. Baada ya muda waumini walitulizwa na huduma ya kutoa neno la bwana ikaanza rasmi, mana palitokea mvurugano kidogo baada ya adam kuingia,…

“tumsifu yesu Kristo”
Aliongea mr Jacob lakini mpaka hapo ana wasiwasi sana mana kakutana na mtoto wake ni moto wa kuotea mbali, yaani hafai katika swala la kutoa huduma kwa waumini wake,…. Ibada ilifanyika vizuri na hatmae ilikwisha,.. Vipindi mbalimbali vilifanyika, misa misa zote ziliisha na kuna wale wa maombi ya chain player, waliingia na kuanza maombi yasiokatika…

Sasa leo ni siku adam anahamia nyumbani kwake,.. Ni nyumba ya kifahari mno,.. Ukizingatia ni kuwa jana mdogo, ndio anaendea miaka 24 sasa,…
“lakini adam mwanangu,… Wewe bado hujaoa, unahamia huko utaishi vipi,.. Utapikiwa na nani, nani atafua nguo zako, nani atafanya usafi wa nyumba yako mwanangu”
Alikuwa ni mama yake adam, wakati huo adam alikuwa akipaki nguo zake katika begi, mana kila kitu kule kipo ni yeye kubeba nguo zake na vitu vyake vya thamani,…
“mama, wacha nihamie kwangu,… Bwana yesu yupo nami,.. Kama mkate mmoja uliwatosha kundi la watu wa bwana Yesu, sembuse mkate mmoja usinitoshe mimi, kwanini”
Aliongea adam huku akimalizia kupaki nguo zake
“Kwahio unataka kusema kuwa utakwenda kushindia mkate si ndio”
Aliongea mama Jessica, mana hataki mtoto wake ahame hapo nyumbani, ingali anatakiwa kuhama..
Lakini wakiwa bado wanazozana na mama yake mara dada  yake kaingia
“Jessica,.. Mdogo wako ndio anakwenda hivyo”
Aliongea mama huku akimuonyeshea Jessica kwa kidole
“anakwenda wapi? Zimbabwe au”
Jessica alileta utani mbele ya jambo la usiriasi
“staki utani wako Jessica… ”
Mama aliongea huku akiwa hataki kweli utani
“mama, mi naona kweli akae peke yake, mana akizidi kukaa huku, baba atazidi kumbana na kushindwa kufanya mambo yake”
“kumbuka kuna usafi kule, kumbuka atatakiwa kupika huyu”
Aliongea mama Jessica
“mama, mimi nitajitolea kumfanyia usafi kila baada ya siku tatu”
Jessica alivunja ukimya na kusema kuwa yupo tayari kufanya usafi kila baada ya siku tatu,…
“iv Jessica kwanini unataka twende tofauti na mimi lakini”
“mama,… Adam keshakuwa mtu mzima, wacha akae mbali na baba ili kidogo heshima ije”
Walikuwa wakibishana lakini ilikuwa ni kazi bure,… Adam alimaliza kukusanya nguo zake kisha akazitupia katila gari yake… Mana kama ni mali keshapewa nusu ya mali na baba yake… Hivyo hamtegemei baba yake kwa lolote lile, hata kanisa na hio nyumba pia hakujenga kwa pesa za baba yake, ispokuwa zakwake… Baba alishiriki tu kusimamia ujenzi wa kanisa lakini hana asilimia yeyote katika kanisa hilo

“labda niwatakie siku njema, mana ndio nakwenda hivi ili niwahi kuandaa vitu vingine”
Aliongea adam huku akitoka zake
“adam mwanangu… Usije ukaajiri msichana wa kazi, utakosa sifa za kuchaguliwa na wazee wa kanisa”
Aliongea mama yake kwa msistizo mkubwa sana
“mama, najua kila kitu kuhusu hilo.. We ondoa shaka… Baba yangu ananionea sana… Lakini bwana Yesu yupamoja nami”
“milele amina baba”
Waliongea ongea kwa kiasi fulani kisha adam huyoo, lakini alisindikizwa na dada zake na mama pia,… Walifika katika nyumba hio mama akamtangulia mtoto wake kuingia katika nyumba hiyo,… Maombi yalianza mara moja ili kama lipo baya basi liweze kutakaswa kwa damu ya Yesu, maombi yalichukuwa muda kiasi fulani, kisha wakaingia ndani,… Basi dada zake na mama wao walianza kufanya usafi, mana si unajua nyumba mpya, lazima kidogo kuwe na usafi japo ilishafanyiwa Usafi muda mrefu, sema hapo ni kama kufuta futa yu… Adam yeye alikuwa akizunguka zunguka huko nyuma ya nyumba kama vile anakagua baadhi ya mambo, wakati huo anaimba nyimbo za kumsifu bwana Yesu Kristo,…. Lakini ghafla simu yake inaita, kuangalia jina alikuwa ni mzee wa kanisa
“haloo mzee shalom baba”
“shalom… Tumsifu yesu Kristo”
“milele amina baba”
“unahitajika huku kanisa nitajitolea haraka sana”
Simu ilikata ghafla na kushindwa kuelewa kwanini kaambiwa anahitajika haraka sana,.. Adam hakutaka kujiuliza mara mbili,
“bwana yesu kuwa nami kila hatua”
Alinuia baadhi ya maneno kisha akapanda gari
“baba mtumishi, unakwenda wapi tena”
Aliuliza mama yake mzazi
“nimehitajika kanisani mara moja”
“sawa, uwahi kurudi basi mana hatutochukuwa muda”
“sawa mama”
Adam aliondoka kwa usafiri wake, yote hio ni kuwahi alipoitwa na mzee wa kanisa….. Sasa huku ndani sasa mama alimuuliza mtoto wake ambaye ni Jessica kiwa
“hiv Jessica, umeona kilichotokea asubuhi wakati adam anaingia”
Aliongea mama huku Jessica nae pia akishangaa
“mimi pia nilishangaa,.. Kwasababu hata baba nilimwona akitetema kwa maneno machache tu ya adam”
“sasa lile kanisa linaongozwa na nini, kwasababu sio waumini pekee mpaka mchungaji nae ana hali mbaya”
“mama, hapa kuna kitu, lakini bwana Yesu Kristo atajafa miujiza na atatakasa kila pembe ya njia yetu”
“amen”

Huku kanisani sasa adam akiwa katila lift kuelekea kanisani, na hio ni siku ya Jumapili ambapo asubuhi ndio alifanya kile kituko,… Sasa ile anafika tu ndani ya kanisa, alikutana na viongozi mbalimbali wa makanisa hapa jijini Arusha,.. Lakini alipoangalia vizuri alimwona Catherine na baba yake, ghafla akamwona hata baba yake mr jacob, lakini mr Jacob alikuwa katika moja ya jasira mno,… Adam alijua sasa hapa kumekucha, akiangalia vizuri mpaka wale wanaohusika na mambo ya ndoa wapo, hapo tumbo la adam likaanza kuwaka moto,… Mana hakuutegemea huu wito utakuja kuwa hivyo,
“asifiwe bwana mwokozi wetu alie hai”
Alitoa salam huku akivuta kiti akae,
“milele amina baba mchungaji”
Adam alikuwa na hofu, mana hapo hakukuwa na muumini mdogo mdogo hata mmoja, yaani wote hapo ni viongozi wakubwa wa makanisa mbalimbali hapa jijini, yaani muumini mdogo mdogo ni Catherine peke yake, sasa haijulikani pana kikao gani

Je? Nini kitaendelea??

Comments

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment