$hide=mobile

Young paster sehemu ya kwanza (01)

Young paster ep 01 Katika kanisa moja kubwa ikiwa ni wakati wa saa nne hivi asubuhi… Kanisa kubwa lenye urefu wa rosheni mbili kwenda ju...

Young paster ep 01


Katika kanisa moja kubwa ikiwa ni wakati wa saa nne hivi asubuhi… Kanisa kubwa lenye urefu wa rosheni mbili kwenda juu.. Na rosheni zote zimesheheni waumini wa lika mbalimbali kuanzia watoto wazee na vijana.. Wakati huo wapo mapasta ambao walikuwa wakitoa sifa kwa Bwana Yesu kwa kutumia nyimbo za injili,… Floo ya chini ya kanisa hilo ni sehemu ya kupaki magari, na floo ya katikati ni ukumbi mkubwa yaani kama kuna ndoa basi hapo ndipo mahali pake, ila pia hio floo ya katika imejaa waumini, mana sio siku zote watu wanaoa, na pia ina skrini kubwa karibia ukuta mzima ule wa mbele, hio ni skrini ya kumuonyesha pasta akiwa floo ya juu, yaani ni kama sinema vile,,.. Sasa hio floo ya juu na ya mwisho, ndio kanisa lenyewe,.. Ukiangalia mazabauni yaani imeng’aa kwa maru maru maalum, yaani pale ni sehemu ya pasta pekee. Na wakati huo pasta bado hajaja, hivyo waumi waikuwa wakitoa sifa za bwana Yesu kwa kupitia nyimbo zilizoimbwa na wasanii mahiri nchini,

Sasa huku chini ilionekana gari moja ya bei mbaya… Ikiwa inapaki, tena ina sehemu yake maalum ya kupaki sio kila mahali,… Ilikuwa ni familia moja iliokuwa ikija kanisani, na ilionekana kuheshimika sana kanisani hapo,… Walikuwa ni wasichana watatu waliotofautiana umri, akiwemo baba yao na mama yao,… Hatua za kuelekea kanisani zilianza taratibu, na kila muumini aliiheshim familia hio,…
“tumsifu yesu Kristo”
Ni waumini waliokuwa wakitoa salamu kwa bwana huyo, huku akiwaitikia
“milele amina”
Yaani waumini wanapanda kwa ngazi, lakini yeye ana lift yake maalum, yaani yeye na familia yake hutumia wao tu,… Alipofika ndani ya kanisa waumini wote wa floo ya katikati na floo ya mwisho walinyanyuka na kutoa salamu kwa pamoja…
“tumsifu Yesu Kristo alie hai mbele za mungu”
Walisema waumini hao huku familia ikiwa ina viti vyao pale mbele, yaani ule ule upande wa waumini, sasa viti vya mbele ni spesho kwa ajili ya familia hio… Lakini pia katika viti hivyo kuna kiti kimoja hakikuwa na mtu, na ni kiti cha mmoja wa familia hio na hakiruhusiwi kukaliwa…. Sasa hatujui huyo aliosalia kukaa pale ni nani,…. Pale pale mr huyo alipanda mazabauni,….

Kumbe huyo bwana ana kipawa cha UBISHOP yaani ni Bishop Jacob… Ni kiongozi wa makanisa yake yapatayo 50 kwa idadi kamili…. Yaani mzee huyu ana makanisa 50 makubwa kama hili na ni yakwake peke yake… Anayasimamia mwenyewe, licha ya kuwa Bishop, bado pia ni tajiri mkubwa… Mana ana makampuni mengi sana, ana viwanda… Huezi amini ni Bishop anaemiliki ndege binafsi, ana magari ya kutembelea kama utitiri,…..
“tumsifu Yesu Kristo kwa jina la baba”
Aliongea Bishop Jacob huku waumini wakipaza sauti zao kwa hali na mali
“milele aminaaaaaa”
Raha sana ukiwa na imani ya dini yako….
Wadada, wamama, wakaka, watoto, wazee…. Yaani malika yote yalijaa hapo, na unambiwa akitoka hapo anakwenda katika makanisa mengine kutoa neno la bwana… Yaani amekuwa mtu wa kutoa neno siku nzima….

BISHOP ni kipawa au cheo kikubwa ambacho ni ukitoka pasta sasa anaefatia kwenda juu,… Anakuwa ni Bishop, lakini pia Bishop ana mkubwa wake ambaye ni ATBISHOP huyu ATBISHOP huyu sio mtu wa kawaida, huyu anaweza kuwa ATBISHOP wa kidunia au wa kitanzania nzima…. Yaani anasimamia au kuongoza makanisa yote Tanzania. Na sio kuwa ni yake lahasha bali anayasimamia tu, na pia sio kuwa anasimamia yote, lahasha bali kuna matawi mengi sana juu ya haya makanisa… Hivyo atasimamia makanisa ambayo ni tawi fulani pekee, hivyo atakuwepo ATBISHOP mwingine wa kusimamia makanisa ya tawi lake husika… Hivyo ATBISHOP ni mkubwa, tuchukulie mfano wa rais…. Afu huyu Bishop yeye tufanye ni kama mbunge… Hivyo katika mkoa mmoja kunaweza kuwa na ma Bishop hata mia moja.. Kutokana na kila mtu kumiliki jimbo lake yaani makanisa yake…. Nakupa tu kwa ufupi ujue vipawa vilivyo….

Sasa Bishop Jacob alianza kuhubiri kama ilivyo kawaida yake, ni mchungaji aliojaaliwa kipawa na upako wa hali ya juu katika kutoa neno la Bwana,…. Waumini walikuwa wakilia kutokana uzito mahubiri aliokuwa akihubiri Jacob,… Machozi kila muuni, wengine kama kawaida yao kudondoka chini wakati wa pepo kutoka,… Na yote hayo ni kwasababu ya mchungaji Jacob au Bishop Jacob

Mahubiri yaliisha na hatimaye ibada ya siku ya Jumapili inakwenda ukingoni,… Lift yake ni ile ile, hachanganyikani na waumini hata siku moja,…. Akiwa na familia yake wanaingia katika gari,…. Lakini wakati wanaingia alitokea mschana mmoja ambae nae ni muumini wa kanisa hilo,..
“tumsifu yesu Kristo mama”
Alisalimia mschana huyo huku akimpa mkono mke wa Jacob,….
“milele amina….. Eva mbona siku hizi huji nyumbani, au kwasababu mwenzio hayupo”
Aliongea mama huyo aliokwenda kwa jina la Rebecca,.. Sasa hatukujua huyo mwenzie ni nani haswa, lakini eva alipokua akisalimiana na mwanamke huyo, ghawna wale wasichana nao wakaanza kumsalimia eva….
“heee wifi hali yako”
Aliongea mtoto mkubwa wa huyo mama aliokwenda kwa jina la Jessica mwenye umri wa miaka 28, ndio mtoto wa kwanza kwenye hio familia, lakini sasa Jessica kamuita eva wifi kitu ambacho hatujui kaolewa na ndugu yake nani, au ndio ile utani tu,… Mara mschana mwingine kasalimia
“shkamo wifi eva”
Alisalimia mschana mwingine aliokwenda kwa jina la martha, mwenye umri wa miaka 20…. Kuna mwingine hakutaka kuachwa nyuma kwa salamu
“wifi eva shkamo”
Alisalimia mschana mwingine wa mwisho, aliokwenda kwa jina la maria ana miaka 15…
“amarahaba mawifi zangu hamjambo”
“hatujambo… Hatukuoni nyumbani”
“aahhh nitakuja Maria usijali”
Eva alikuwa ni mschana mzuri sana na mwenye heshima kwa rika zote,
“mwanangu, kabla mwenzio hajakwenda masomoni, ulikuwa unakuja, lakini sasa hivi huuuji jamani”
Aliongea Rebecca au mama Jessica, au mama mchungaji,…
“mama, hata mimi hua nakuwa na ubize sana… Sasa hivi nadili sana maombi, sitaki mwenzangu anikute nipo nyuma, hivyo nami nakua bize na mungu”
“yesu atakubariki eva,… Na naomba nikutaarifu, mwenzio anarudi wiki ijayo”
Eva kusikia mwenzie anarudi wiki ijayo, alifurahi na kuruka ruka, alimkumbtia mama mkwe wake karibu kudondoshana, mpaka baadhi ya waumini walishangaa kwa furaha hio alionayo eva…
“eva utaniangusha jamani”
“mama, nina furaha kiasi gani juu ya taarifa hio”
Eva ana mdogo wake wa kike aitwaye HAPPINESS, mwenye miaka 15 alikuja pale baada ya kuona dada yake ana furaha…
“tumsifu yesu Kristo mama”
Alisalimia happy huku akiinama chini kuashiria ni heshima ya hali ya juu mno,…
“milele amina,… Heew happy, umependeza Jumapili ya leo”
“ahsante mama… Sifa kwa Yesu”
“amina mwanangu”
Basi waliongea mengi sana na hatimae kila mmoja kuondoka baada ya ibada kuisha,…

Kuanzia hapo Eva alikuwa ni mtu wa furaha siku zote, mana sasa usingizi wake karibu kuja… Eva ni mschana aliolelewa katika mazingira ya kidini na anaijua dini haswa, yaani humwambii kitu kuhusu Bibilia,… Eva alipofika nyumbani alimkuta mama yake kesharudi, nyumbani… Ni familia ya kawaida sana…
“mamaaaa….. Yesu kajibu maombi yangu mama”
Aliongea eva huku akimkumbatia mama yake,…
“ni nini eva… Afu leo sijakuona kanisani ulikaa wapi”
“mama… Leo niliamua kukaa nyuma sana”
“enheee, yesu kajibu maombi yako kivipi… Mana una furaha kweli yani”
Aliongea mama huyo huku mama akiwa anaandaa ratiba zake za jumuiya,..
“mama njoo ndani nikwambie”
Mama eva aliingia ndani ili kumsikiliza mtoto wake…

“haya Niambie”
“mama…. Wiki hii mkwe wako anakuja”
Mama alishangaa kusikia mkwe wako anakuja….
“ina maana umeachana na adam unataka uniletee mwanaume mwingine, eva mwanangu ni mawazo gani unayo”
Mama alikuwa hajamuelewa mtoto wake ana maana gani…
“mama sio kuwa naleta mwanaume mwingine,…. Namaanisha huyo huyo Adam, anarudi toka masomoni”
“weeeee…. Unasema kweli”
“ndio,.. Nilikuwa na mama mkwe pale kanisani ndio kaniambia”
“jamani eva mwanangu”
“nini mama…. ”
Familia hio ni familia fukara sana ila wengi wao wanaona wivu kwa mtoto Bishop Jacob, kuoa katika familia hio, na ni kila muumini anajua uhusiano wa Adam na Eva,… Lakini kwakuwa Eva anaishi katika maisha ya kimasikini hivyo kwao ni kama bahati kuolewa na mtoto wa kitajiri, tena mtoto wa Bishop, yaani sio pasta ni Bishop… Kwa wale waikristo nikisema Bishop nadhani mnanielewa..
“mara paaap adam anashuka kwenye ndege na mke wa kinaigeria… Utafanyeje sasa”
Mama alimwambia mwanae hivyo mana adam yupo Lagos nchini Nigeria, katika vyuo vya dini ya kikristo, japo adam ana nguvu na miujiza kuliko hata baba yake, lakini akaamua kwenda kujiongeza, sasa akirudi huko ni moto wa kuotea mbali,  Sasa baada ya mama eva kusema hivyo, eva alianza kulia huku akisema kuwa….
“mamaaaaaa….. Usiseme hivyo”
“sikuombei umkose mwanangu… Ila wanaume wa siku hizi…. Siwawekei mia kwa mia… Hawakawiii kubadirika”
“ni kweli mama… Lakini sio kwa mtu mwenye imani kama adam”
“eva mwanangu, mimi ni mama yako… Nimekuficha mengi sana kuhusu adam…. Na nikisema nikuambie nitakupoteza mwanangu… We mpende tu”
Eva alitoa jicho kuskia mama yake anasema maneno hayo…..
“unasemaje mama”
“una kifua cha kubebea jambo mwanangu, tusije kuanza kupepeana na kanga hapa”
Aliongea mama yake eva huku wakikaa vizuri kitandani
“mama… Nipo tayari kumwacha adam kama ana tabia chafu”
“heeeeee wewe ndio wa kusema hivyo”
“mamaaaaa Niambie basi nijue”

ITAENDELEA…

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,149,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,196,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,110,FIFA.com - Latest News,15,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,11,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,207,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,39,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : Young paster sehemu ya kwanza (01)
Young paster sehemu ya kwanza (01)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-kwanza-01.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-kwanza-01.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content