YOUNG PASTER SEHEMU YA KUMI NA SABA (17)

YOUNG PASTER EP 17


Ilipoishia…..

MCHUNGAJI MCHANGA

“hallo mr jacob Michael, hali yangu nzuri”
“bwana weee, hapa nipo nje ya kanisa la kijana wangu… Yaani huezi amin makanisa yangu yamepungua waumini, siwezi kuamini kwamba nilikuwa siwezi kuwahesabu waumini wangu, lakini sasa naweza kuwahesabu… Siamini kuwa wanahamia kwa adam taratibu”
“sasa watakaje wewe”
“enheeeeeee, hilo ndio swali zuri kwangu…. Niambie sasa nifanye nini”
“mtu mwenye upako wa kweli, kiukweli sisi hatumuezi…. Ila ipo njia moja tu na ndio itakayomwangusha mtoto wako”
Aliongea jehova huku jacob akishangaa
“njia moja tu… Na ndio ya pekee”
“yes…. Hebu niambie… Mtoto wako kaoa?”
Mr jehova aliuliza kuwa adam kaoa
“hapana, bado hajaoa”
“yeeeeees….. Hio ndio njia pekee iliobaki, na ikishindikana hio, basi mwache amtumikie mungu wake”

ENDELEA NAYO……

Mr Jacob ni kiongozi mkubwa wa dini, tena ana pesa chafu sana, lakini unaweza kujiuliza ni kwanini anamfuatilia mtoto wake, na wala hawalingani kwa lolote ispokuwa uwezo wa kiroho ndio tofauti,..
Mr Jacob anamtumikia shetani,.. Na ikumbukwe kuwa shetani na mungu ni vitu viwili tofauti,.. Na adam anamtumikia mungu, siku zote shetani hana upendo na wana wa mungu, hivyo shetani kila kukicha anabuni mbinu mpya ya kumganya mwanadamu aingie upande wake, mana hapendi wawepo upande wa mungu…

Wakati damu ya Yesu ikizidi kuwatakasa kondoo wa mchungaji adam, kumbe baba yake yupo nje na anataka kuhakikisha hawezi kumzidi kwa lolote, mana alimwagiza kisomo hiki, yeye kaenda kusoma kisomo anachokijua yeye bwana adam… Hivyo siku ya ibada kama leo siku ya Jumapili mr jacob alifika kwa siri katika kanisa la Eden Church… Baada ya kuona watu zaidi ya mianne wakiwa ndani ya kanisa hilo tena wengi wao ni waumini wake wa makanisa mbalimbali,…. Mr Jacob Alimpigia jehova ili kujua nini cha kufanya mana kijana anampanda kichwani,… Yaani ishu za kishetani hazina cha mtoto wa baba… Kikubwa uende sawa na maagizo….

“hapana, bado hajaoa”
“yeeeeees….. Hio ndio njia pekee iliobaki, na ikishindikana hio, basi mwache amtumikie mungu wake”
Aliongea bwana jehova huku mr Jacob akiona mbona kama hio njia ni ngumu sana, mana katumia ubaba wake wote adam aoe lakini hajaoa, sasa leo anakuja kuskia kuwa kuto kuoa kwa adam ndio njia pekee ya kumfanya asionekane tena kuwa kama mchungaji…
“kivipi sasa bwana jehova, mana sijakuelewa hapo”
“fanya mpango awe jirani na mwanamke mzuri… Amshawishi kijana huyo… Yaani akigusa tu, basi.. Ile dhana yote ya haki katika mwili wake itatoka”
“mmmmmhh sio kwa kijana wangu.. Nimelea mwenyewe huyu.. Sidhani kama alishawahi kuwa na mwanamke, kiufupi ni kwamba hajawahi na wala sikuwahi hata kumsikia kuwa ana mwanamke wa ajabu ajabu, zaidi ya kusikia tu kuwa ana mchumba wake na hata yenyewe tu anakaa nae mbali”
“duuuuu, uyo kiboko… Ila sasa mwanaume ambaye hajawahi kufanya tendo la ndoa, ndio mzuri huyo… Changamkia hilo jambo na uwe makini”
Aliongea bwana jehova, lakini swala hilo kwa bwana Jacob ni gumu, kwasababu alisha jaribu mara kadhaa
“nitajaribu bwana kama itafaa”
“nakutakia bahati njema”
Mzee Jacob aliumiza kichwa atatumia njia gani, mana kama ni Catherine alishampa hio nafasi… Mr Jacob alimpigia Catherine, ambaye yupo humo ndani ya kanisa hilo hilo la adam…
“njoo hapa nje”
Aliongea mr jacob, na kweli Catherine hakuchelewa, alikwenda mpaka pale alipo mr Jacob,..
“tumsifu yesu Kristo baba mchungaji”
Alisalimia Catherine huku mchungaji jacob akipanda katika gari pamoja na Catherine,….
“milele amina….. Vp, humo ndani kuna watu wangapi”
Kumbe mzee jacob anapata taarifa zote kupitia kwa Catherine,…
“mmmhhh baba, kule kuna watu zaidi ya 400, kiukweli anafanya vizuri kwa sasa”
Sasa mzee anashangaa na Catherine anaipenda hali ya adam….
“umefikia wapi kwa sasa”
“kwa sasa sihitaji kwenda nae haraka kwasababu, mapenzi hayalazimishwi hivyo nataka niende nae taratibu”
“hapana.. Unakosea… Nenda hata kwake,.. Kaa nae karibu mimi nataka mtoto wangu aoe, kaa nae karibu sana fanya juu chini wewe ni mschana mzuri.. Au nikupe pesa… Kuna dola za kimarekani milioni 10, ukifanikiwa nakupa hizo pesa”
Catherine kusikia dola milioni 10 za kimarekani, ni mabilioni ya kitanzania,
“lakini baba… Mchungaji ambae hajaoa Haruhusiwi kukaa na mwanamke ndani labda iwe ndugu”
Aliongea Catherine, mana kweli Catherine anampenda sana adam, lakini nae anajua sheria na taratibu za dini, mchungaji ambae hajaona Haruhusiwi kuwa na mwanamke ndani, sema wachungaji wa karne hii wanakosea… Na sio lazima kila kitu kiwe kimeandikwa katika maandiko, kwani vingapi vimeandikwa na havitekelezwi, sasa Catherine yeye pia anajua maadili anayotakiwa kuwa nayo mchungaji ambaye hajaoa, lakini mr jacob akaliweka wazi kuwa
“aaaaaa… Hivyo ni visheria tu na wala havizuru”
“mmmnhhhh baba…. Unajua wewe ni kiongozi wa dini tena mkubwa.. Sasa najigunza nini kupitia hili”
“Catherine basi wewe humpendi kijana wangu”
“hapana baba, nampenda, ila sheria za dini ndizo zinazo nibana baba”
“sasa mimi ndio nakwambia, hakuna lolote, ni vijisheria tu vya kumfanya mchungaji asije akawarudia kondoo wake, na ndio maana wakasisitizwa waoe, mana wakioa hata kondoo wa kike ataogopa kumsogelea mchungaji kwa maana ana mke… Hivyo kuoa kwa mchungaji ni ili asiwarudie kondoo wake wa kike… Haina maana kubwa”
“kumbe ni hivyo”
“haswaaaa… Mimi nimeanza injili toka hujazaliwa, kipindi nipo na baba yako”
Aliongea mr Jacob kwa upotoshaji wa dini, mana alichokiongea sio sahihi ila ni njia ya kumfanya Catherine azidi kukaa karibu na adam,
“mmmhh sawa baba, nitajaribu… Mana nampenda sana adam”
“basi hio ni nafasi yako… Jitahidi akuoe… Fanya juu chini mfunge ndoa.. Nitakuzawadia dola milioni 10 za kimarekani”

Maongezi yao yaliisha, wakati huo huku kanisani kulikuwa na upako mzito, yaani adam alikuwa akitoa ibada nzuri ambayo kila muumini ilimuingia katika moyo wake, tofauti na baba yake anapoongoza ibada huwa haiwangii waumini mana ndani yake kuna nguvu za shetani,…

Baada ya maombi,… Sasa ni saa ya kupata elimu ya utiifu dhidi ya binadamu kwa ujumla…
“heshima…. Heshima ni kitu cha bure katika hii dunia yetu.. Usitake kumdharau mtu kwasababu ya imani yake,…

Naomba nitoe elimu kwa waumini wangu wa kweli.. Haleluyaaaaaaaaa”
“aaaaaaameeeeeeeeeen”
“bwana yesu asifiwe sana”
“Ameeeeeeen”

“nataka niweke heshima ya dini zetu ili tuheshimiane, mana kuna majina tunaitana juu ya Waislamu na Wakristo,… Kaka tafadhali sana njoo mbele”
Adam alimwita kaka mmoja muumini wa kanisa lake, ambae ni mwinjilisti
“tumsifu yesu Kristo, bwana alie hai”
“milele amina”
“eti.. Nataka nikuulize wewe mwenye imani kama yangu…. Ivi unapoomba na kusema PEPO TIKAA hua tumanaanisha nini”
Aliongea adam huku waumini wakiwa makini sana, mana hapo adam anafundisha imani jinsi inavyotakiwa kuwa mana ukiwa na imani afu humpendi binadamu mwenzio basi imani yako ni bure
“aaahhhh hua tunaposema pepo toka, wengine wanamaanisha Waislamu, kitu ambacho wachungaji hukosea”
“ww unajua kwanini wanakosea”
“kwasababu hawana elimu juu ya uongozi walio nao..”
Aliongea kijana huyo kisha adam akawageukia waumini na kusema
“angalikuwa yupo muislamu hapa tungemuuliza nae… Ila kwa ninavyojua mimi hua Waislamu nao hutuita sisi makafiri kama tunavyowaita pepo katika maombi yetu… Ila ni kwa wale wachungaji ambao wameivamia fani ya uchungaji, hawana kipawa wala wito.. Lakini hali hii sii sawa,… Huezi kumwita binadamu mwenzio pepo au kafiri,.. Ninyi wote mungu wenu ni mmoja, wote mnamwabudu mungu mmoja, kwanini shetani awavuruge… Hii yote ni njia ya shetani, ili nanyi mgombane…. Haya wewe bwana Joseph, tufanye wewe ni mwislam nami ni Mkristo,… Hebu niambie mimi ni kafiri”
Adam alianza kutoa mifano mingi sana, ili waumini wa imani tofauti wasichukiane wala kuitana majina ya ajabu
“mchu… Mchu..”
“usiogope we niambie mimi ni kafiri… Usifanye mwislam sasa”
“mchungaji adam wewe ni kafiri”
“enheeee safi kabisa… Sasa nami nakuuliza… Ukafiri wangu ni upi”
“wanavyodai wao ku”
“ah ah.. Upo kama mwislam, hivyo jisemee wewe”

tunavyodai sisi, ukafiri wenu ninyi hamsali kwa kusujudu, kama sisi… Na wengine tunasema kuwa kuna mnyama Haruhusiwi kuliwa nanyi mnakula”

“safi sanaaaaaaaa…. Tumsifu Yesu Kristoooooo”
“milele aminaaaaaaa”

“ni kweli, hivyo ndivyo Waislamu wanavyotuona sisi ni makafiri…. Je nikuulize na wewe ukiwa kama mwislam…”
“niulize”
“mbona karibia waganga wooote wa kienyeji ni Waislamu, kwanini?… Na tunasema kuwa hata uchawi mwingi hutokea kwao na ndio mana tunawaita mapepo”

“ni kweli, mchungaji na hio ni mbinu ya shetani kwa wale wasiojua…. Kwasababu huezi kumnyooshea mwenzio kidole ingali nafsi yako yenyewe inalia…”

“safi kabisa…. Bwan yesu asifiweeee”
“ameeeen”

“alichoongea bwana Joseph ni sahihi kabisa… Kafiri ni mtu ambe hamwabudu mungu na anakwenda tofauti na maagizo ya Mungu, na ni shetani peke yake….. Na pepo ni huyo huyo shetani, ila sio binadamu mwenzio,.. Wewe unamnyooshea mwenzio kwa hili… Mbona wewe unafanya lile? Je pepo au kafiri ni nani… Usimhuku mwenzio ingali wewe mwenyewe hujui hukumu yako ni ipi.. Sisi sote dunia ni watoto wa baba mmoja, hivyo ukimwita mwenzio KAFIRI AU PEPO basi hata wewe ni hivyo hivyo, mana baba yetu ni mmoja, tuacheni kudharauliana.. Someni dini iwaingie vizuri ndipo muongeee……… Kwa mfano baadhi ya waislamu huweka mikutano kule mitaani, wenyewe wanaita mihadhara… Hua wakiweka mikutano mule,… Wakristo huenda pale ili wakabishane nani anajua dini na nani hupo sahihi katika dini yake, matokeo yake sisi wakristo tunashindwa kwasababu, hatufuatilii misingi ya imani ya pili… Kwa mfano yule muislamu anaetisha mhadhara pale,.. Yule anajua Biblia kuliko hata wewe muumini wangu… Sasa angalia, muislamu kama yule kaijuaje Biblia ambayo wewe unalala nayo kila siku lakini kwenye mabishano yao unashindwa… Ni kwamba ulishamdharau katika akili yako… Waswahili walisema.. Huezi mwangusha adui yako kama hujui akifanyacho… Mchunguze adui yako jua kila kitu chake kisha mdondoshe.. Lakini sisi tunapuuza hilo.. Afu unaitwa mchungaji wa makanisa zaidi ya 50, lakini ukienda kwenye mihadhara unashindwa.. Pata elimu ya Biblia kwanza… ”

“tumsifu Yesu Kristo”
“ameeeeen”

“juzi juzi hapa… Nilimsalimia mfanyakazi wangu kule mjini… Nina mfanyakazi mmoja ni mwislam… Nilimsalimia Asalam Aleykh…. Haaaa nakumbuka nilikuwa na waumini wangu wawili wapo hapa lakini siwataji… Walinishangaa sana kusikia nimetaamka salamu ya Kiislamu.. Na hio sio salamu ya Kiislamu, kama tulivyo izoea… Sasa wacha nijaribu tafsiri ya salamu hii iko hivi”

“ASALAM ALEYKH (Amani iwe juu yako)….. Hapo hakuna neno muislamu hapo, hivyo hata Mkristo anaweza kuitumia….. Sasa tatizo liko kwa yule anaetikia salamu hio… Kama ni Mkristo ndio umesalimiwa hivyo na mwislam, basi itika hivi… WALEYKH (amani iwe juu yako na wewe) hapo hakuna neno muislamu, hivyo hata Mkristo anaweza kuitumia….. Lakini hio ni salam kwa wale wenye imani au dini tofauti,… Sasa tuangalie kuna tofauti gani wakisalimiana Waislamu wenyewe kwa wenyewe… Inakuwa hivi….. ASALAM ALEYKH (amani iwe juu yako)…. Hapo hakuna neno muislamu, sasa angalia huyu mwislamu mwenzie anaeitikia… WALEYKH MSALAM (amani iwe juu yako muislamu mwenzangu)…. Umeona tofauti ni kidogo ya hio MSALAM yaani (muislam)… Kwahio mkisalimiana watu wa dini tofauti kwa salamu hio.. Muitikiaji asiimalize yote, yaani asifike kwenye MSALAM… Hata kama ni muislamu asiitikie WALEYKH MSALAM,… Kwasababu aliomsalimia sio muislamu mwenzi.. Anatakiwa aishie WALEYKH… Na hata wewe Mkristo, itikia WALEYKH.. Hata zamani kabla yetu ndivyo walivyokuwa wakisalimiana, lakini Karne yetu tumekuja kujazwa imani iliochanganyikana na shetani, mpaka tunachukiana kiroho Waislamu kwa wakristo… Ila kiwazi wazi tupo pamoja, lakini kiroho tu ndio tupo tofauti…. Tupendane, sote tumetokana na baba mmoja… Ni matabaka tu haya, na mungu hapendi umnyooshe mwenzio kidole cha ubaya……. Mi naona leo niishie hapa… Wiki ijayo nitakuja na mada nyingine…. Naomba wale wa chain player tukutane saa 10 jioni…. Haleluyaaaaaaaaa”
“aaaameeeeen”

Mtumishi adam alimaliza ibada muda mrefu sana ila aliamua kutoa neno la hekima kwa waumini ili kujenga upendo dhini ya dini zetu… Mana kuna usemi wa ndani ndani kuitana majina ya ajabu… Sasa leo adam akaamua kuwapa elimu juu ya imani zetu……. Wakati hui ni saa sita za mchana adam akiwa anapanda gari yake kuelekea nyumbani kwake kupumzika kwa muda kisha arejee tena kanisani,… Ghafla eva na rafiki yake wini wamefika… Lakini wakati huo huo Catherine nae anataka kuingia katika gari, ikumbukwe kuwa Catherine kapewa kazi upyaaaaa,.. Lakini catherine alipoona gari ina watu, akasita kwenda mana yeye sio wa kugombania kama wale.. Yeye ni spesho, basi Catherine yeye alipanda gari yake, kisha na adam akaondoka zake… Aliwapeleka akina Eva kisha akarudi nyumbani kwake… Alikoga vyema kisha akaingia jikoni, mana leo Jessica dada yake hakufika japo bado ni mapema mno… Lakini akiwa anakata kata vitunguu, ghafla mlango uligongwa… Hakuwa na wasiwasi alikwenda kufungua mana ilikuwa ni mchana wa saa saba hivi,
“waoooo sasa kwanini usiniite mtumishi”
Adam alishangaa kumwona Catherine yupo hapo…
“we Catherine, ina maana hujui sheria na taratibu za dini kwa mchungaji ambae hajaoa”
Aliongea adam huku akiwa mkali sana juu ya Catherine kuja hapa…
“hivyo ni visheria vyetu tu.. Wala havina madhara”
“sitaki.. Naomba utoke nje Catherine”
“sawa, lakini jua nakupenda baba mchungaji, nipe nafasi”
“nimesema toka….”
Lakini sasa cha ajabu, Catherine alianza kupandisha aketi yake taratibu, ili tu kumsumbua akili yake..
“Catherine naomba utoke haraka sana”
“sawa,.. Ila nina joto sana… Nipe nafasi ya kuoaga japo kidogo tu”
“kaogee kwenu bwana”
Adam alikuwa mkavu haswa, yaani Catherine ni msichana mzuri na aliobarikiwa maungo, lakini huezi amini adam hakumuona kabisa..
“nioge hata tone la maji”
Sasa mbaya zaidi ni kwamba adam hatakiwi kumsogelea kwa kumsukuma, yaani mchungaji ambaye hajaoa mwisho wa kumshika mwanamke ni kule kanisani tu, mbele za watu na ni wakati wa maombezi, ila tofauti na pale Haruhusiwi kumsogelea mwanamke…
Sasa Catherine alikumbuka maneno ya mwisho ya mr jacob akisema kuwa

“najua adam anaijua sana sheria na taratibu za mchungaji ambaye hajaoa… Na anazifuatilia sana… Ukiwa ndani kwake hawezi kukugusa, hata ukiingia chumbani kwake hatokugusa mana Haruhusiwi… Kuongea ataongea sana.. Lakini kukugusa hakugusi”
“unasema kweli mchungaji”
“haswaaaa…. Yaani utaamua hata kwenda popote ndani ya nyumba hio lakini hatokaa kukugusa,.. Ila kwa kuongea ataongea sana… Lakini kukugusa hawezi”

Sasa Catherine alipokumbuka hivyo, alinyanyuka na kuelekea chumbani kwa adam… Na kweli adam alikuwa ni wa kuongea tu,
“Catherine unanivunjia miko ya utumishi wangu, tafadhali sana naomba uende Catherine”
Catherine hakutaka kusikia badala yake akaingia, adam hataki hata kuingia huko chumbani…

Sasa adam akakaa katika sofa na kuwaza sana…. Sasa akakumbuka kuna siku alimkuta baba yake anaongea na simu kule nyumbani kwao, na ile simu alikuwa akiongea na baba yake Catherine ambaye ni mr yohana…. Sasa mr jacob kuna swali alimuuliza baba yake Catherine.. Sasa adam ndio anakumbuka siku ile baba yake akamuuliza mr Yohana kuwa….

Je? Lilikua ni swali gani…. Na je adam atalifanyia kazi hilo swali??

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : YOUNG PASTER SEHEMU YA KUMI NA SABA (17)
YOUNG PASTER SEHEMU YA KUMI NA SABA (17)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-kumi-na-saba-17.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-kumi-na-saba-17.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content