Young paster sehemu ya kumi na mbili (12)

Young paster EP 12


Ilipoishia ……

MCHUNGAJI MCHANGA

“kwaheri eva…. Umama mchungaji wako ni huko huko ulikotoka…”
Catherine Aliongea hivyo huku chuma linazidi kuteremka… Sasa Catherine alikuwa anafumba macho, ili akifungua macho akutane na maiti, sasa pale alipo adam, kumbe alikuwa akiongea na yule pasta na kumtambulisha mchumba wake, sasa kile kitendo cha kumtambulisha,.. Adam akamshika eva na kumsogeza kwa mbele ili pasta amuone mke mtarajiwa wa mchungaji adam,… Sasa lile chuma halimuelekei eva tena, bali ni adam… Sasa Catherine ndio alikuwa anamalizia kufunga jicho… Ghafla anashangaa alipokuwa kasimama eva, sasa hivi kasimama adam, kwahio kifo ni cha adam… Alafu mbaya zaidi sasa, kamba ya kuzuia hilo chuma ipo mbali, mana Catherine alisha iachia muda mrefu sana,..
“pasta adam angalia juuuuuuuuuuuu”
Catherine alipaza sauti kubwa, lakini haikufika mbali, mana kelele za hapa na pale kwa shamra shamra za ufunguzi wa kanisa la Eden Church, Catherine haamini kama adam hajasikia sauti yake…. Alijaribu kuita na kuita lakini wapi, na hapo kila mmoja na mambo yake yaliomleta hapo…. Maskini ya mungu mtumishi adam

ENDELEA NAYO……..

Wakati huo adam bado anaendelea kumtambulisha eva kama mke wake mtarajiwa, yaani huyo ndio mama mchungaji ambae anatarajia kumuoa, sasa wakati huo Catherine kashika kichwa huku akiwa kasumba macho ili hata asione kinachokwenda kufanyika katika mwili wa adam,….

Lakini sasa kwa bahati nzuri, ukumbuke Catherine kuna mdada alimtuma kamba, ile ilikua ni njia ya kumtoa yule dada, sasa na dada huyo hakujua kama alitolewa kiujanja ili Catherine afanye mambo yake,.. Sasa alishanga kuona kamba aliokuwa akiifunga imefunga na ilikuwa ikiburuzika chini kama vile kuna mtu anaivuta… Sasa yule dada kuangalia… Laaaaa haulaaaa… Yaani chuma linakwenda moja kwa moja katika kichwa cha adam… Huyu dada hakujali kuwa ataumia kiasi gani, aliirukia ile kamba na alifanikiwa kuishika,.. Lakini sasa lile chuma lilikuwa ni lizito na istoshe lilishaongeza spidi ya kushuka chini sasa hapo ndio kila mtu anaona ila bado adam hajui kitu,.. Dada huyo alikuwa akiburuzwa na chuma hilo ilimradi tu lisifanikiwe kumkuta adam, sasa kwa bahati nzuri zaidi palikuwa na kibao cha zege, chenye jina la kanisa hilo… Hivyo yule dada alipofika pale akakumbatia nguzo moja ya kile kibao,… Lakini sasa kwakuwa lile chuma lilikuwa spidi,.. Lilikata kamba na kushuka sasa lenyewe lenyewe,… Lakini uzuri ni kwamba lilishapoteza muelekeo na halikuwa likimuelekea adam…  Sasa adam anakuja kushtuka chuma limeshafika jirani yake…iliskika sauti
“paaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa”
Walio ona toka mwanzo walishikwa na kigugumizi juu ya kutoa sauti za kumwokoa adam,…
“Catherine anakuja kufungua macho,.. Kwanza anakutana na irene akiwa kakumbatia nguzo huku kamba ikiwa mkononi,… Na hapo irene kachoka kaumia.. Catherine kuamsha macho kwa adam,… Gari ya adam ilikuwa haifai, lile chuma lilidondokea kwenye gari,.. Adam na Eva wapo salama salimini,… Kila mmoja anaangalia kiungo cha hilo chuma lilikuwa wapi,.. Wanagundua ni kule alipokuwepo Catherine,.. Wakati huo Catherine alikuwa akimuamsha irene pale chini,…
“irene, irene… Rafiki yangu jamani amka”
Catherine alikuwa akilia, mana bila irene, leo adam asingelikuwepo katika dunia hii
Sasa adam alipoona kuna mtu kalala chini, gari yake haikuwa na thamani tena, adam alimkimbilia Catherine aliokuwa na irene pale chini… Sasa watu ndio wanaiona kamba ilioshika chuma kumbe irene ndiye aliekuwa akihangaika nayo, watu walianza kumuamsha irene,… Irene aliamka lakini alichubuka tumboni sana tu,..
“hebu tumuwahisheni hospitali”
Aliongea adam huku akimbeba kumpeleka katika gari ya Catherine,.. Adam hakusubiri mpaka Catherine aje kuendesha, aliingia mwenyewe na kuondoka kuwahi hospitalini,… Sherehe zote zikiishia hapo hakuna sherehe tena, mana kila mmoja ana wasiwasi muumini mwenzao kuumia, lakini mbali na hapo pia kuna watu walianza kutafsiri jambo lingine tofauti na ndio mana sherehe ikaahirishwa,…

Adam huku hospitali, maskini irene yupo hoi, hajitambui kabisa, damu zilikuwa zikimtoka kwa wingi, ngozi ya tumbo ilikuwa ikining’inia… Yaani kama huna mayo mgumu huezi angalia mara mbili mbili… Irene alipewa huduma nzuri sana na gharama zote analipa adam…
“dokta, tafadhali sana noamba mtu huyu apone… Yesu aishike roho yake, Israel akose nafasi”
“amen…. Usijali ndugu, hapa ni sehemu salama kabisa”
“nashukuru sana, naomba unipe dakika mbili”
Adam aliomba dakika mbili, ili atoke hapo na kwenda kanisani kuangalia kinachoendelalea,… Lakini akiwa njiani nywele zake zilimcheza ghafla, kana kwamba kuna kitu kapishana nacho lakini hakionekani,.. Alisimamisha gari na kuangalia nyuma lakini hajafanikiwa kuona kibaya chochote kile,.. Aliendelea na safari ya kuelekea kanisani kwake

Wakati huo adam ana wasiwasi sana juu ya irene, mana kaumia vibaya sana, japo uwezekano wa kupona upo, lakini kaumia vibaya sana katika tumbo lale,…

Sasa ile adam kufika kanisani kwake, alitahamaki ghafla kwa kile alichokiona…..
“heeeee, ni nini kimetokea hapa jamani, mbona hali imekuwa hivi”
Adam aliongea hivyo baada ya kukuta uwanja mweupeeee, hakuna hata doa la watu, zaidi ya Catherine, Eva, Mama yake adam, Jessica, na Martha, pamoja na mdogo wake adam wa mwisho aitwaye maria… Yaani watu sita tu ndio ambao anawaona katika macho yake,.. Na hao ndio walikuwa wakikusanya vitu ili kuviingiza ndani na vingine kuvipeleka kwa wenyewe mana vilikuwa ni vya kukodisha…. Mama Adam alimkimbilia mtoto wake na kumkumbatia
“mama, mbona sielewi mimi”
“baba… Hata sisi hatuelewi, yaani tumeshangaa watu wanaondoka taratibu mpaka wakaisha… Yaani siamini mwanangu,…”
Aliongea mama huku akilia, eva nae akafuatia kutokwa na machozi,… Watu zaidi ya 500 waliokuwepo hapo leo wamebaki watu 6 tu… Adam haamini macho yake,.. Basi nae ilibidi asaidie ili sasa kila mmoja akapumzike na hapo hakutokuwa na sherehe tena,.. Lakini sasa hata Catherine alikuwa kama vile haelewi nini chanzo cha ajali hio, wakati yeye ndio chanzo kikubwa sana….
Adam na familia yake walimaliza ile kazi ya kutoa vile vitu,… Mafundi gereji walikuja kulichukuwa gari ya adam ambayo imeharibika sana,… Lakini papo hapo adam anapokea simu,..
“haloo”
Aliongea adam huku akiwa makini kwa kitega sikio
“habari yako ndugu… ”
“salama, nani mwenzangu”
“unaongea na daktari aliokuwa akimtibu mgonjwa wako aitwaye irene ndese,… Kiukweli tumejitahidi sana lakini hatukuweza kuyasaidia maisha yake…. Mgonjwa wako amefariki dunia”
“Yesu wangu Uuuuuuuuuwiiiiiiii… Dokta unasema kweli au”
Familia kuskia adam anapiga kelele na kutaja jina la dokta… Wakajua tu irene hatupo nae
“halo dokta, halo.. Halo…. Yesu wangu weeee… Jamani binti wa watu mama”
“nini tena adam”
“yule binti amefariki dunia”
Catherine kuskia vile alizimia pale pale mana ni rafiki yake kipenzi,… Hakuna ambaye hajatoa machozi kwakweli,…. Mana ilikuwa ni siku muafaka na yenye furaha kubwa duniani, lakini furaha yao imegeuka kuwa huzuni katika nyuso zao,… Basi walimbeba Catherine tena na kumueka katika gari,… Hakukuwa na muda wa kupepeana kwa wakati huo, ukizingua tu ni hospitalini…. Basi waliondoka wote katika eneo hilo walioachwa ni walinzi pekee,…

Baada ya siku kadhaa kupita, wakiwa tayari walishamzika irene… adam akiwa kanisani kwake,.. Tena alikuwa kaketi mazabahuni akiliangalia kanisa lake,… Ghafla alianza kuteremsha maombi yalioambatana na machozi… Adam aliomba takribani masaa matatu tena akiwa peke yake katila kanisa hilo… Na ilikuwa ni siku ya Jumapili,… Sasa mama na watoto wake baada ya kuona mbona adam hayupo kule kanisani kwa baba yake, ndio wakakongojana sasa mpaka huku Eden Church na kukutana na sauti iliokuwa ikishusha maombi ya hali ya juu… Adam kweli alichagulia na mungu kulitangaza neno la Mungu,… Wakati huo eva nae yupo katika msafara wa familia ya akina adam.. Mama na watoto wake walinza kushika vifua vyao kwa maombi matamu yaliokuwa yakishushwa na mtumishi adam,… Ulishawahi kukuta pasta anaomba mpaka analia,.. Na sio kuwa analia bila sababu bali anawasikitikia waumini ambao wapo katika dini kama kebehi, wale wanaofanya madhambi ingali wakijua kila wanachokifanya si halali mbele za bwana…
Maombi yalinza kuwaingia walioko nje,…. Ghafla Catherine nae huyu hapa, ikumbukwe kuwa Catherine ana kazi yake maalum wala hana kinyongo na mtu, shida yake aolewe na adam, anampenda sana kupita kiasi,.. Sasa Saa ngapi Hawajaanza kugala gala hapo chuni kwa ukali wa maombi, adam hajui kama nje kuna watu, maombi anayo yafanya ni makubwa, yale maombi ya ndani ya roho,… Familia nzima ilikuwa ikitakaswa kwa neno,… Inashangaza sana kuwa waumini wa mr Jacob wana mapepo ingali ni mtumishi wa Mungu, na anafanya kazi chini ya mungu lakini ilishangaza sana.. Adam anaomba mpaka analia…. Sauti yake ilikuwa ikitoka mpaka nje ya kanisa….. Sasa kelele zilipozidi ndipo akagundua kuwa nje palikuwa na watu,… Alitoka na kuendelea kushusha maombi juu yao thidi ya kile kilicho watembelea katika mili yao,….
“huna mamlaka ya kuishi katika miili hii, achia na upoteee… Pepo tokaaa, mana hatupo kwa ajili yako, tupo kwa niaba ya mungu…. Damu ya yesu ihusike kuwatakasa watu hawa… Eee mungu pokea watu wako wakiwa wapyaaa… Na uwape upeo wa kutorudi walipotoka… Tokaaaaa…. Aaaamen”
Adam alimaliza kufanya maombi yake huku wale waliokuwa wakigala gala, waliamka na kuanza kujipangusa,…
“mungu wangu… Mbona nimekuwa mwepesi kiasi hiki”
Aliongea mama yake adam…. Mara na wengine walifuata hivyo hivyo
“yesu wangu…. Mama sio wewe tu, nimekuwa mwepesi na sio wepesi tu hata moyo wangu sasa mweupeee”
Adam alifurahi sana baada ya kuskia maneno mazuri kama hayo,…
“Ahsante sana baba mchungaji”
Aliongea eva huku akilia machozi kabisa…. Maombi yaliwafanya kuwa wepesi katika nyoyo zao… Hakika adam ndio chaguo la mungu… Licha ya watu wengi kusema adam ni mdogo sana hakustahili kupewa wito mzito kiasi hicho… Baada ya maombi na ibada kuisha waliondoka zao nyumbani… Na hapo adam anatumia gari ya pale nyumbani kwao mana yakwake bado ipo gereji, hivyo kuna gari anatumia kwa muda japo uwani kwao kuna magari mengi lakini hatamani kuyatumia.. Lakini akiwa anaendelea na safari, ghafla simu yake iliita
“yesu asifiwe fundi”
“milele amina bwana mchungaji… Ah samahani gari yako ipo tayari huku gereji”
“ooohhh unasema kweli fundi”
“ndio.. Unaruhusiwa kuja kuichukuwa kwa wakati wowote mana hudaiwi bwana mchungaji”
“Ahsante sana na yesu akubariki sana… Basi nitafika hapo wakati wa saa kumi ya jioni”
“sawa bwana mtumishi… Mungu akutangulie katika ujio wako”
“amen”
Adam alikata simu na hapo alikuwa peke yake, mana gari anayotumia ni Vitz mayai new model… Hicho ni kigari cha maria, sema adam kaamua kutembea acho wakati gari yake ikiwa gereji… Sasa kwakuwa gari yake ipo tayari hivyo akanyoosha moja kwa moja nyumbani kwao,… Yaani anaongozana na familia yake mpaka kwao.. Ili kuirudisha gari na akachukue gari yake ilio tayari… Catherine kwa wakati huu mgumu aliacha kumsumbua adam, mana yupo katika mawazo toka ile ajali ilipotokea, mpaka leo adam hana raha, ni ile basi tu… Hivyo Catherine alipitiliza kwenda kwao,… Kisha adam na familia yake waliingia njia yao ya kwenda nyumbani….

Mr Jacob alikuwa yupo ndani,.. Aliskia honi ya Vitz ikiwa nje, na anajua gari hio anatumia adam… Na kweli alikuwa ni adam akiingia katika nyumba hio,.. Adam alipofika kwenye parking ya magari aliona gari ya baba yake, hivyo akagundua kuwa mchungaji jacob yupo ndani… Adam aliingia ndani na kumsalimu baba yake
“asifiwe bwana Yesu Kristo”
“milele amina…… Mbona leo sijakuona kanisani”
Aliuliza bwana Jacob huku adam akijibu
“mchungaji… Kwa sasa nina kanisa langu, na linahitaji waumini… Hivyo sipaswi kuwa nalo mbali, kwa sasa nitakuwa nasalia kanisani kwangu”
“oooohhh basi ni vyema… Ila kaa hapo nina maongezi na wewe”
Adam alishtuka kuskia kaa hapo nina maongezi na wewe, mana siku zote maongezi ya mr Jacob na mwanae hua ni ya kukomandi kitu kifanyike…
“kwanini ulikiuka agizo langu”
Aliongea bwana Jacob huku adam akishangaa, kakiuka agizo gani
“agizo gani hilo baba”
“nilikwambia ukasome wapi na umekwenda kusoma wapi”
Adam alishtuka kuskia hivyo, kana kwamba hapo ni kweli alikwenda tofuati na baba yake, na ndio maana hata sasa hivi huduma zao za kiroho ni tofauti kabisa… Kumbe shule aliokwenda kusomea adam huko Nigeria sio alioambiwa akasome.. Adam alichukuwa jukumu la kusoma shule nyingine tofauti na alioelekezwa na baba yake….
“kweli baba, hapo naomba unisamehe, na sikujua kama utalijua hilo… Nisamehe sana baba”
Mr adam alikasairika sana, hata kukubali msamaha wa mtoto wake kakataa kabisa….
“we mtoto ni mjinga kabisa wewe… Kwanini unashindwa kuheshimu maagizo ya wazazi wako”
“babaaa… Nimekuomba msamaha mzazi wangu, Nisamehe bure”
“sitaki kusikia ujinga wako… Na ili nikusamehe ni lazima uoe mtoto wa mr Yohana”
Bishop Jacob aliongea kisha akachukuwa koti la suti yake na kuondoka, hivyo msamaha kwa baba yake upo nje nje kama atamuoa Catherine,… Sasa baba katumia njia nyingine kama mzaz…. Mana radhi za wazazi ndio kila kitu hapa duniani.. Adam alikuwa na mengi ya kuongea lakini alikosa nafasi kwasababu baba yake aliondoka bila hata kumsikiliza mtoto wake.. Adam alinyanyuka pale sebuleni kisha akawa anakwenda upande wa nyuma ya hio nyumba ambapo huko nyuma ndipo jiko lilipo na ndipo mama yake alipo huko baada ya kurudi kanisani yupo huko kwa kazi za nyumbani.. Lakini sasa alipopita kwenye hio korido kuelekea nje,.. Ghafla nywele zake zilimsimama ghafla.. Lakini sasa kila kizidi kutafakari juu ya hilo.. Alikumbuka kuwa hii hii korido hii alishawahi kuiota,.. Hapo hapo kwenye hio korido kuna chumba ambacho toka kuzaliwa kwake hajawahi kukifungua wala kujua kuna nini… Kama vile ile ndoto ilikuwa ni ya kweli, ila hatujui… Adam kugeuza shingo, kweli alikiona kile chumba.. Alisita kwenda na kukirudia kile chumba,.. Alishika kitasa kama vile kwenye ile ndoto,.. Lakini kabla hajafanya hivyo aliangalia huku na kule na kugundua hakukuwa na mtu aliokuwa akimuona… Adam alirudi katika mlango na kuanza kuomba kabla ya kufungua mlango huo…… Alipomaliza alikishika kile kitasa, tayari kukishusha chini ili afungue… Sasa huku nje mama nae anaingia ndani, lakini ghafla akamuona mtoto wake kasimama katika mlango ambae hata yeye hajui….. Sasa kumbe hata mama mwenyewe pia hajui pale ndani kuna nini… Sasa mama hakutaka kwenda,. Hivyo nae akabana mahali ili mlango ukifunguliwa tu, aone humo ndani kuna nini… Mana hata mama mwenye nyumba hajui kuna nini humo ndani…. Adam bila kujua kuwa mama yake anamuona,.. Bila woga mtumishi adam Alishika kile kitasa na kukiminya chini, kisha akasukuma mlango mbele……

itaendelea…..

Comments

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment