Young Paster sehemu ya kumi (10) | BongoLife

$hide=mobile

Young Paster sehemu ya kumi (10)

YOUNG PASTER EP 10Ilipoishia ,,,,
MCHUNGAJI MCHANGA

Hakuna kitu kibaya kama umeme ukatike afu jumba kubwa tena yupo pekee,…. Alichukuwa simu yake na kuwasha tochi kisha akaanza kuzunguka ndani ya jumba hilo… Alipita vyumba vyote lakini muumgurumo bado ipo kama vile kuna watu wanasali kwa imani ya kishetani,… Lakini kuna chumba kimoja hicho hajawahi kukifungua toka kuzaliwa kwake, yeye hukiona tu.. Hakutaka kukiacha, na kweli katika hicho chumba kulisikika sauti za wati kadhaa wakifanya ibada,.. Wakati huo adam nywele zake zinamchemka.
Kiukweli ni sauti zilizokuwa zikitisha sana…. Lakini adam ni mtumishi wa Mungu, yupo tayari kufa kwa ajili ya kondoo wake, kama alivyokufa Yesu Kristo kwa niaba ya wakristo wote,.. Adam alikibonyeza kitasa cha mlango na kwa bahati nzuri hawakufunga mlango, hivyo adam akasukuma mlango ule kisha akaingiza kichwa…. Ilisikika tu sauti ikisema
“haaaaaaaaaaa”

ENDELEA NAYO……….

Ilikuwa ni siku nzuri kwa mchungaji adam kukabidhiwa fimbo zidi ya kondoo atakao wachunga, lakini siku hii hii ya leo, ilikuwa na balaa katika upande wake, kwani siku ambayo anahamia katika nyumba yake hio, na ndio siku anapewa wito dhidi ya kipawa chake,.. Na siku hio hio mishale ya usiku alianza kusikia ngurumo za ajabu katika nyumba hio, sauti hizo zilimfanya ashtuke na kuanza kutoka taratibu ili kubaini ni sauti gani na ni akina nani… Adam alizunguka ndani ya jengo hilo kubwa ambalo kwa wakati huo umeme ulishakatika hivyo alikuwa akitumia simu kama tochi,… Bila uoga aliweza kuzunguka jengo lote,… Sauti zili zilinyamaza wakati akiwa anazunguka.. Lakini sasa katika pita pita, alikipita chumba kimoja, hicho chumba hua anakionaga tu na hajawahi kuingia katika chumba hicho toka kuzaliwa kwake,… Adam alisali pale pale kisha akashika kitasa cha mlango, tayari kwa kufungua… Ndani yake zilisikika sauti za kusali kwa njia ya shetani…. Adam bila kuogopa alifanikiwa kufungua huo mlango na kuingiza kichwa chake,.. Sauti iliyosikika ni ya adam akiwa katahamaki

*************
“haaaaaaaaaaaaaa”
Alikurupuka kitandani huku akifikicha macho yake, kana kwamba alikuwa usingizini, na hio ilikuwa ni ndoto na haikuwa kweli,… Mana umeme ulikuwepo, na pia nyumba alio iota sio hio ya kwake, bali ni nyumba ya familia yao kule alipotoka, yaani alipokuwa akiishi na wazazi wake.. Na ndio mana kuna mahari paliandikwa kuwa, chumba hicho hajawahi kuingia toka kuzaliwa kwake, maana yake ni kule kwa wazazi wake na sip hapo kwake…
“shindwa kwa jina la Yesu…. Pepo mchafu tooookaaaa”

Kesho yake adam aliamka asubuhi sana akaingia jikoni kutengeneza chai, mana ikumbukwe kuwa adam ana kampuni ambayo ni mali aliopewa na baba yake ili aendelee maisha yake, na hapo bado hajakabidhiwa mali vizuri, hio aliopewa ni moja ya kampuni za mr Jacob, na mtoto wa kiume ni yeye pekee,.. Adam si mvivu wa kupika, na haruhusiwi kuishi na mwanamke wa aina yeyote yule, hata mchumba haruhusiwi kuishi nae ispokuwa kusalimiwa tu… Au kama anataka kufanyiwa usafi wa nyumba na mmoja kati ya waumini, basi yeye hatakiwi kuwepo pale usafi unapofanyika, anaeruhusiwa kufanya usafi humu au hata kulala, ni dada zake na mama yake tu basi… Ndio wana ruhusa ya kuja kuishi hapa, ila mwanamke yeyote yule haruhusiwi kuishi hapa ispokuwa mkewe tu, hivyo kama pasta hujaona… Basi haruhusiwi kuishi na mwanamke ambaye hujamuoa,… Hata mchumba hairuhusiwi… Wakati akiwa jikoni alikuwa akiikumbuka sana ile ndoto, haijawahi kutokea katika maisha yake

Sasa huku kanisani kwa adam,… Kumbe taarifa za ufunguzi wa kanisa hilo zilishasambaa kila kona, hivyo palikuwa pakipambwa vizuri kwa ajili ya kuabudu siku nzima kwa furaha,.. Waumini walikuwa wengi sana ingali kanisa ni jipya, hata adam atashangaa sana kuona siku ya kwanza tu ana waumini wengi sana,.. Lakini sasa mwanamke wa mbele sana alikuwa ni Catherine, na inaonekana waumini wengi alikuja nao yeye,… Mapambo ya kila aina yalipambwa katika kanisa hilo lililojengeka kwa vioo vitupu,… Wengine walikuwa wakifanya usafi, wengine walikuwa wakifunga majukwaa, vinywaji mbalimbali kasoro vilevi pekee ndivyo vilivyo kosa nafasi ya kuletwa hapo…

Huku kwa adam akiwa anakunywa chai baada ya kumaliza kupika, simu yake ilikuwa katika sikio
“haloo…. Tumsifu yesu Kristo”
“milele amina baba mtumishi… Hali ya kuamka waionaje”
Alikuwa ni Eva ndie aliepigiwa simu
“bwana Yesu ndie kila kitu katika usingizi wangu… Ashukuriwe na bwana muumba mbingu na ardhi”
“amen, vp baba mtumishi…. Kiukweli sijalala kwa furaha… Nimepata habari kuwa, tayari umeupokea wito toka kwa Bwana wetu”
“ndivyo ilovyo”
“Ashukuriwe bwana yesu”
“amen…. Uko wapi sasa eva”
“nipo nyumbani najiandaa kwenda kanisani”
Eva alikua hana taarifa yeyote kuhusu ufunguzi wa kanisa la mchumba wake,
“mama mchungaji”
“ndio, baba mchungaji”
“ina mana huna taarifa juu ya kanisa lako”
Adam alimuuliza eva, lakini eva kweli hakuwa na taarifa
“sina taarifa… Na kwanini usingeniambia”
“Samahani, huenda furaha ilinizidi mpaka kusahau jambo jema kama hili”
“enhee, nipe taarifa”
“kuna maombi ya kufungua kanisa, na sasa kila mmoja mbona anajua”
Aliongea bwana adam huku eva akifurahi sana na kuairisha kwenda kanisani kwa baba yake adam, ili aende kwenye kanisa la mchumba wake,
“upo wapi sasa baba mchungaji”
“nipo nyumbani, namalizia kunywa chai”
“utatoka na familia yako”
“hapana, nadhani wao wameshatangulia, na hata hivyo mimi sipo kule tena, nimeshahama”
“weeee baba mtumishi, unasema kweli”
“ndio, mbona nimehama jana na hapa nakunywa chai”
“nani kapika hio chai”
“nimepika mwenyewe, si unajua sheria na taratibu za mchungaji mbae hajaoa”
“nazifahamu na ndio mana sijatamani nije nikupikie… Ila utateseka sana baba mchungaji,… Nipo tayari kwa hali yeyote baba mchungaji sitaki uteseke”
“hebu ngoja tutaongea vizuri…  We jiandaa nakupitia hapo nyumbani”
“sawa baba mchungaji”
Adam alimaliza kunywa chai haraka iwezekanavyo, kisha akatafuta suti nzuri na kuanza kuinyoosha nyoosha na pasi mara moja… Kisha huyoo kapanda gari yake.. Uzuri wa geti yake inafunguka kwa rimoti, hivyo hakuwa na shida ya mfungua geti,..

Sasa huku kwa akina eva,.. Alikuwa kujiandaa kawaida sasa alipo pata taarifa kuwa, kanisa la mchumba wake linafunguliwa,.. Alivua mavazi aliokuwa kavaa, kisha akavaa mengine, tena vazi safi na la heshima, hilo lilitakiwa kuvaliwa kwa siku maalum, si unajua familia ambazo hazijiwezi vizuri, hua wana mavazi ya kutokea na ya kawaida, tofauti na tajiri, yeye akitaka kutoka anakwenda dukani
“we vipi hilo gauni kuna nini”
Mama aliuliza kuhusu gauni hilo ambalo lilikuwa na kitambaa chake cha kichwa, kitambaa chenyewe kimetengenezwa kama kofia, unavaa tu, magauni ya kinaigeria hayo…
“mama, hili ni speho kwa ajili ya EDEN CHURCH”
mama alishangaa kusikia Eden Church, mana hilo kanisa anajua bado halijatengemaa….
“Eden Church, si hili kanisa la mtumishi adam”
“ndio mama…. Leo ndio linafunguliwa rasmi”
Mama nae kuskia hivyo, anaachajwe sasa kwa mfano, kwenye kanisa la baba mkwe, japo mama anajua kuna fununu kazisikia lakini hakutaka kumwambia mtoto wake, mana anahisi atamvunja moyo…
“nitakwenda ndio, lakini nitachelewa kidogo si unajua mambo ya nyumbani, ila mwambia mchungaji, nitakuja na hongera sana”
“sawa mama”
Eva siku hio alikuwa katupia mapak basi, yaani hapo ndio kavunja kabati, saa ngapi hata adam hajampita, mana kabadirika eva, anavaaga nguo za heshima lakini siku hio, kavaa nguo ya heshima mpaka imepitiliza,..
Lakini uzuri ni kwamba eva analijua gari ya mchumba wake,.. Sasa lilivyompita eva hakutaka kumkimbilia au kupiga makelele… Eva alikaa usawa wa saiti mira kisha akapunga mkono, kwahio adam atamuona kupitia saiti mira.. Na ni kweli adam aliona kuna mwanamke anampungia mkono lakini hajamjua ni nani,… Adam alijua huyo mwanamke anaomba tu lifti, sasa adam akampa ishara kiwa anarudi amsubiri hapo… Eva akashika simu yake,.. Kumbe sababu ni vocha hana, na ndio mana alishindwa kumpigia..
Eva alituma tafadhali nipigie, ili hata adam ajue kuwa aliompita ni eva,… Adam kuangalia kweli alikuwa ni eva, alicheka sana huku akisema
“mama mchungaji ana haraka huyo,.. Nakuja mama subiri”
Adam aliongea hivyo kumaanisha kuwa, eva yupo nyumbani,.. Hivyo hajampigia kwakuwa anakwenda huko kwao…

“heeee eva, ivi ni wewe kweli”
Alikuwa ni rafiki yake eva, aitwaye wini..
“ina maana hujawahi kuniona na hili gauni au”
“heeeee…. Eva? Shalom”
“shalom.. Vipi, unakwenda wapi”
“ndio nilikuwa nakwenda kanisani, tena nilikuwa nakuwaza sasa hivi kuwa tayari umetoka au bado”
“ok Tuachane na hayo… Ebu nipe simu yako mara moja”
“ya nini tena”
“we nipe si ina dakika”
“ndio”

Je? Nini kitaendelea???…

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : Young Paster sehemu ya kumi (10)
Young Paster sehemu ya kumi (10)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-kumi-10.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-kumi-10.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy