Young Paster sehemu ya ishirini na nne (24)

YOUNG PASTER EP 24
Ilipoishia ………..

MCHUNGAJI MCHANGA

“yes boss”
“maliza kila kitu na kazi iendelee sawa”
“sawa boss”
Adam alikasirika sana, yaani kamuacha mercy kule, anakuja huku, kumbe ni kitu kidogo tu….
“pumbavu sana… Sasa nampataje tena mercy….”
Aliongea adam mana namba yake hana, ila mercy ndio mwenye namba ya adam, hivyo hana budi kumsubiri apige…

Basi adam alirudi zake nyumbani, geti lake hufunguka kwa rimote hivyo hakuna haja ya kuwa na mlinzi wa kufungua geti…. Aliingia mpaka ndani, lakini aliona viatu vya kike pale nje ya mlango wa kuingilia ndani.. Alikuwa ni dada yake… Adam alipaki gari lake kisha akawa anaingia ndani, lakini sasa alipofika hapo sebuleni, macho yake yalitua kwenye meza ndogo ya kioo,… Na dada yake ambaye ni Jessica, kakaa kwa pembeni, sasa adam kuangalia ile meza ya kioo… Aliikumbuka meseji aliotumiwa na wini mchana akiwa anatoka kanisani… Aliifungua ile mesuna kuisoma tena….. Laaaaa haulaaaaaaa, adam kachelewa kuijibu meseji hio

SHUKA NAYO………

Katika maisha huwa majuto ni mjukuu, na hutakiwi kupuuza kitu katika maisha yako yote, usiwe na dharau juu ya jambo fulani linalokuja mbele yako,…

Adam akiwa yupo njiani kuja nyumbani, toka kanisani,… Simu yake iliingia meseji, kuangalia alikuwa ni wini ndie aliemtumia adam meseji kuwa….
“Samahani mtumishi… Natamani kuja leo ila mama kanibana sana… Lakini kule chumbani kwako, nimedondosha chupi yangu ya rangi ya bluu bahari,.. Ilikuwa kwenye mkoba wangu,.. Nilipokuja kwako sikuwa nimeivaa, ila ilikuwa kwenye mkoba… Sasa nadhani vile ulivyourusha mkoba uvunguni, ndipo ilipotoka…. Naomba uwahi kabla dada yako hajakwenda kufanya usafi.. Nakupenda sana mtumishi wangu.. Mmmwaaaahhhh”

Hio ndio meseji iliyotumwa na wini afu adam akaipuuzia… Na kuendelea na mambo yake…
Sasa adam kafika huku nyumbani, kaikuta ile ile chupi aliotumiwa meseji na wini, tena Jessica kaitandika hapo makusudi, bonge la chupi,… Mana umbo la wini sio mchezo. Na hata ukiiangalia haiwezi kumuenea Jessica, ila adam alipoona vile akaanza maneno mengine tena.. Mana tayari yupo kwenye 18 za Jessica ambaye ni dada yake…

“dada? Naona sasa tunavunjia heshima,… Yaani mpaka unaamua kunionyesha nguo yako ya ndani kweli… Una maana gani juu ya hili… Mimi staki tena uje kwangu staki.. Ni tabia gani unanionyesha mimi”
Adam alijifanya kuwa mkali, na hio nguo hata ukiiangalia kwa macho haimuenei Jessica, mana Jessica alikuwa hana umbo kubwa….. Jessica alikasirika sana kwa maneno ya ndugu yake,….
“adam sasa naona unakokwenda siko… Yaani ufanye ujinga wako badala ukubali uchafu ulio ufanya, afu unaniambia mimi nakuonyesha nguo ya ndani, ivi una akili wewe… Umeingiliwa na nini mdogo wangu… Mbona umekuwa wa ajabu hivyo… Hii kitu nimeikuta uvunguni mwa kitanda chako,.. Na hii kitu sio mpya hii… Imetumika hii, nina wasiwasi jana ulikuwa na mwanamke huku ndani”
Adam alidakia juu kwa juu
“weeeeeee ushindwe wewe…. Ishia hapo hapo mana sasa unanitusi… Nadhani unajua mimi sijaoa, nawezaje kuwa na mwanamke ingali najijua”
“kwahio hii imetokea wapi”
“nikuulize wewe… Tusivunjiane heshima dada angu tafadhali sana”
“basi nyumba yako inahitaji maombezi,.. Kuna ushetani unacheza humu ndani..”
“watakuwa majini mahaba hao wamesahau nguo zao”
Aliongea adam na kumfanya Jessica kushangaa sana
“jini mahaba??? Kwani jini mahaba wanaonekana kama binadamu”
“ndio, usiku wa manane…. Toka nje zunguka nyuma ya nyumba… Utawaona”
“kwa huku kwako au”
“hata kule nyumbani pia ukitoka saa nane usiku utawaona, na wanavaa nguo kama sisi tu… Aiseee ata sijui chumbani kwangu wameingia saa ngapi”
Adam alianza kumdanganya dada yake kuhusiana na jini mahaba, mana Jessica yeye hajui ishu za jini mahaba zinakuwaje na hata huyu adam mwenyewe hizo ishu hazijui vizuri, sema kasikia sikia tu…
“eeee mungu wangu…. Sasa kwenye familia yetu jini mahaba wanafuata nini”
Aliongea Jessica huku akiiangalia ile nguo
“tena iweke kwenye mfuko mweusi kisha itupe pale kwenye dastibin, mana ikionekana hivyo watarudi kuichukuwa… Na nimesikia wakikukuta karibu nayo, wanakuua”
Jessica kuskia hivyo, alitafuta mti na kuishika kwa mti, huku akiiweka kwenye m uko mweusi, kisha akatupa kwenye chombo cha takataka…. Wakati huo adam anapumua kwa nguvu mana kazi ya uongo sio ya mchezo mchezo,.. Alikaa katika sofa huku akiweka mkoba wake ambao una Biblia chungu nzima….
“hakula tayari, mi naondoka zangu… Ila mchungaji, fanya maombi hao jina mahaba wasiendelee kuja”
“Usijali… Nataka siku moja niwaite familia nzima… Mje hapa tufanye maombi, mana hatujaifanyia maombi hii nyumba”
“sawa…. Tufanye Jumapili ijayo”
“wala Usijali, ndani ya mwezi huu tu”
“sawa, mi naenda”
Jessica aliondoka huku adam akihakikisha kweli kaondoka,.. Alipoondoka alikimbilia kwenye dastbin na kuichukuwa ile chupi kisha akaihifadhi kwenye gari,…

Kesho yake adam akiwa nje ya kanisa lake katika hali ya kupunga upepo baada ya ibada, na hapo anasubiri kuingia misa ya pili ili kwa wale waumini ambao wanaishi mbalimbali hivyo wamechelewa kufika kanisani, hivyo yupo benet nao, hawaachi…. Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda, kanisa linazidi kupunguza idadi ya watu,… Kwani mpaka sasa ana waumi karibi 200, lakinj mwanzo alikuwa najaza kanisa mpaka wanafikia waumini 450 mpaka 500 mana kanisa ni kubwa, lakini sasa hivi hata 200 kuwakuta ni ngumu na kanisa lale linafanya ibada za kawaida kila siku….
“tumsifu Yesu Kristo”
Alikuwa ni Catherine ndie aliemfata adam mahali alipokuwa kakaa…
“milele amina”
“baba mtumish…. Mi naona ni muda wa kuwa pamoja huu… Tunachelewa kufunga ndoa”
Aliongea Catherine huku akifikicha vidole vyake chini….
“ivi bado unataka kuolewa na mimi…. Huna bikra mama”
“lakini mtumishi… Bikra si uliitoa mwenyewe jamani…”
“ndio, lakini mimi sitasema hilo… Mimi nitaanza kutangaza kuwa wewe huna na bikra na hufai kuwa mke wangu, au mke wa mchungaji”
“Haaaaaaaaaaaaa baba mtumish, lakini sio vizuri, bikra uitoe wewe afu uikatae”
Adam aliona kama wanapigizana kelele tu
“sasa naona unataka nianze kutangaza hapa hapa kanisani si ndio eee”
“ah ah ah ah… Basi baba mtumishi… Yaishe”
“kuanzia leo.. Staki mazoea… Sitaki unifate fate..sikupendi, wewe ni mzuri lakini haupo kwenye moyo wangu”
“basi… Lakini naomba iwe ni siri yako… Sitaki mtu ajue kuwa sina bikra… Ila nitaumia sana adam… Wewe ni mwanaume wa ndoto zangu”
“basi kaendelee kuniota tu”
Adam alianza kuwa na dharau za hapa na pale,.. Na ndio tayari Mabadiriko kwake yaanza hivyo…
“kwa sasa umekuwa mtu wa ajabu sana mtumishi,.. Kwa sasa hufai kuongoza umati wa waumini kama ulionao kwa sasa… Sasa unatakiwa kuwa kama muumini mwingine… Hufai tena kuwa mchungaji…. Nakuchukia sana adam… Nakuchukiaaaaa”
“mke wangu ni eva mama…. Nilikwambia na kukuonyesha kule kwenu, lakini hukutaka kunielewa… Nikaona wacha nifanye kwa vitendo… Sasa naona vitendo vimefaa na vinafanya kazi”
“sawa…. Hata kwenye harusi yako sintosita kuja”
“sawa…. Nami sintosema na pia kwenye harusi yako sintosita kuja”
Adam nae Aliongea hivyohivyo alivyo ongea Catherine,…. Kitendo kilichozidisha kumliza Catherine
“lakini adam wewe ni mbaya sana… Acha na utumishi wa mungu… Mana huendani nao kabisa”
Aliongea Catherine huku akilia sana, mpaka aliondoka zake tena kwa hasira mno,… Lakini ukiangalia ni kweli, Catherine aliambiwa kuwa adam ana mchumba wake, lakini hakusikia maneno ya mama yake akajua adam atabadilisha muelekeo wa kumuoa yeye badala ya eva… Sasa adam kaamua kumtoa bikra ili kiherehere kiishe,… Mana bila bikra adam hatakiwi luoa mana ana nafasi kubwa katika dini, hivyo haitakiwi mke ambae ananyooshewa vidole kuwa katembea na mtu fulani kabla ya kuolewa na mchungaji, hio ndio haitakiwi… Adam aliingia kanisani kufanya ibada kwa mara nyingine tena kwa wale waliochelewa kufika misa ya kwanza,…

Baada ya muda adam alimaliza kazi ya mungu, hivyo alitoka akiwa kama wa kwanza ili wanaobaki kwa ajili ya ibada zao binafsi wafanye…
Lakini adam alipoingia tu kwenye gari, mara rose nae kaingia kama vile mtu anaomba lift,…
“habari yako pasta”
“salama tu…. Vp mbona umeingia haraka haraka hivyo”
Adam alimuuliza rose kwanini kaingia haraka haraka hivyo…
“najua hunikumbuki tena”
Aliongea rose huku akilegeza mjicho wake kama kungu manga,…
“nakukumbuka sana tu, sema sasa aaahhh”
“aaahhh nini… Twende nikapajue kwako,..”
“mchana huu”
“yes,… Ebu endesha basi”
Adam alilembuliwa mpaka akakubali kuondoa gari, lakini hapo watu wanajua rose kaomba lift tu,… Na wakati huo eva yupo ndani ya kanisa akiwa sambamba na waumini wengine, yaani eva ndie aliekuwa mwanamke bora kwa adam na ndio mana akamchagua yeye… Lakini eva hatoamini siku anajua adam ameanza ufuska,…. Sasa adam wakati huo anajisemea moyoni tu kuwa
“mtoto ana balaaa, huyuuu… Yaani anakubali kuingia kwa mtumishi adam… Na mchana huu wa saa nane hii….”
Alijisemea na kuongeza kiwa
“apa akifika apike kwanza tule….afu tunakwenda kupumzika…. Nitamkanyaga huyu leo.. Heeeee”
Lakini sasa akiwa anaongea hivyo katika moyo wake, ghafla alimwona mercy kasimama getini kwa adam, kama vile alikuwa akimsubiri yeye….
“mungu wangu…. Sasa yule nae kafuata nini”
Aliongea kwa sauti ya chini kana kwamba hata rose hajasikia… Mana kulikuwa na nyimbo ya kwaya ikiimba humo kwenye gari,… Mercy alipoliona gari la mtumishi adam, alifurahi mno, lakini furaha yake iliisha pale alipoona ndani ya gari kuna mtu, tena mwanamke,… Adam alibonyeza rimoti geti ikafunguka…
“tumsifu yesu Kristo mercy”
“milele amina mtumishi….”
“haya niambie, leo sjakuona kanisani kabisa yani”
“ndio, leo kichwa kinaniuma sana… Nimekuja tufanye maombi”
“oooohhhh Afadhali hapa uungane na mwezako,… ”
Sasa wakati adam anaongea hivyo, rose alikuwa anamfinya adam kuwa asimruhusu kuingia mana atapoteza pointi yao….
“sawa…”
Mercy alikubali kuingia hapo ndani lakini alikasirika sana baada ya kumuona rose akiwa ndani ya gari…. Sasa walipofika ndani, adam kaanza kutoa Biblia zake,.. Na adam anajua kabisa hakuna aliekuja kwa nia ya maombi ila kwakuwa wamekutana, aliamua kuwe na maombi ya wakati huo,…. Adam alianza kushusha maombi huku wao wakipokea kwa imani zao…. Adam aliangusha maombi mzito mazito mpaka jasho kumtoka…
“haleluyaaaaaaaa”
“aaaameeeen”
Akina rose waliitikia kisha wakafumbua macho kana kwamba ibada yao imefikia tamati…
“nawashukuru sana kwa kufika hapa.. Mana mmenipa imani ya kwamba mpo pamoja nami… Ahsante sana nawatakia safari njema”
Adam aliongea hivyo, ili mmoja wao aondoke,… Lakini sasa wote kila mmoja wao kaja kwa ajili ya raha za mapenzi, yaani kila mmoja kaja spesho kwa ajili ya kulala kwa adam.. Lakini wao hawajuani kuwa mwenzie kaja kufanya nini….
Rose anajua mercy kaja kuombewa aondoke… Lakini sivyo,… Na mercy nae anajua rose kaja kuombewa na aondoke zake… Sasa kila mmoja anamsubiri mwenzie aondoke, mana rose akisema aondoke.. Basi mercy lazima atafunwe na aadam, na mercy akisema aondoke, basi rose lazima atafunwe na adam… Sasa wakawa wanategeana kuamka, mana hawajuani,…..
“sasa we rose si uondoke tayari ushaombewa”
Mercy aliongea kimoyomoyo kumtaka rose aondoke
“we mercy, ushaombewa kichwa chako si kimepona… Ondoka basi”
Rose nae alijisemea kimoyomoyo kumtaka mercy aondoke… Lakini hawajui kuwa nia iliowaleta kwa adam ni moja tu… Hivyo wote wanasubiri kitu kimoja ila hawajui…
“jamani… Ibada imeisha… Tuonane kesho kanisani sawa jamani…nawatakia safari njema”
Adam aliongea kwa sauti huku akiweka Biblia zake katika kibegi…
Mara rose akanyanyuka kabisa,.. Mercy alifurahi kimoyomoyo kwa kumuona rose kunyanyuka aondoke zake…. Lakini ghafla rose akasema
“mtumishi,… Nionyeshe jikoni kwako nikuoshee vyombo ndio niondoke”
Daaaahhhh mercy alichola,….. Huku akijisemea kimoyomoyo kuwa
“we rose, si uondoke, kama ni hivyo vyombo nitaosha tu”
Aliongea mercy lakini ni katika moyo wake,… Na yeye akaona wala sio mjinga… Hapa hakuja kufanya maombi kamfuata adam….
“mtumishi… Nguo zako chafu ziko wapi… Nikusaidie kufua”
Huyo ni mercy nae anataka nguo chafu za kufua….. Adam alioa hii sasa kali ya mwaka…. Atafanyeje… Na nani ataondoka wa kwanza???….

ITAENDELEA…..

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : Young Paster sehemu ya ishirini na nne (24)
Young Paster sehemu ya ishirini na nne (24)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-ishirini-na-nne.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/young-paster-sehemu-ya-ishirini-na-nne.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content