USIMLAUMU KWA KUCHEPUKA, YAWEZEKANA WEWE NDIYO CHANZO | BongoLife

$hide=mobile

USIMLAUMU KWA KUCHEPUKA, YAWEZEKANA WEWE NDIYO CHANZO

Ni jumaine nyingine nzuri tunapokutana katika elimu ya mapenzi na ushauri  kujuzana na kujadiliana kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano wa kimapenzi.  Leo nataka tujadiliane kitu tofauti kidogo ambacho huenda kikawaudhi baadhi ya watu na kuwafurahisha wengine. Lakini, kwa kuwa lengo letu ni kuwekana sawa, ni lazima tulizungumzie. Napenda kuzungumza zaidi na wanawake. Kama wewe ni mwanamke, umewahi kujiuliza mumeo anahitaji nini zaidi kutoka kwako?
Yawezekana likawa ni swali ambalo unaweza kulitafsiri kwamba halina maana, lakini majibu yake ni mapana zaidi. Wengi huwa wanafikiri hitaji kubwa la mwanaume kwa mwanamke, ni kufanya mapenzi tu na huenda hata wewe ungenijibu hivyo.
Lakini je, hilo ndiyo jibu sahihi? Ipo wazi kwamba tendo la ndoa ndiyo linalo-ikamilisha ndoa yoyote, iwe imefungwa Kikristo, Kiislam, Kimila au Kiserikali. Hakuna ndoa ambayo inaweza kukamilika bila wanandoa kukutana kimwili, hakuna ubishi katika hili. Lakini je, hilo ndiyo hitaji pekee linaloweza kumfanya mumeo akaridhika na wewe?
Wanawake wengi, hasa wasichana wanaoanza kuingia kwenye ulimwengu wa mapenzi, huhisi kwa sababu wao ni warembo, wana mvuto machoni mwa wanaume au wana maumbo mazuri, basi hiyo ndiyo tiketi ya moja kwa moja ya wao kuolewa na wanaume wazuri na kudumu kwenye ndoa zao.
Hata hivyo, wanapoingia kwenye ndoa wanakutana na hali tofauti kabisa kiasi cha wengine kujuta kwa nini wameolewa. Kinachowafanya wajute ni kwamba, wameingia kwenye ndoa wakiwa hawaelewi wanaume wanahitaji nini zaidi kutoka kwao.
Kwa kutokufahamu huko, huelekeza nguvu zao nyingi kwenye tendo la ndoa, lakini mwisho hugundua kwamba kumbe tendo la ndoa siyo kitu pekee kinachoweza kuwafanya waume zao wakawapenda na kuwathamini.
Hali ni tofauti kwa wanaume wasiooa ambao kwao, ipo wazi kwamba hitaji lao la kwanza kwa wanawake, huwa ni ngono na wakishakidhi haja zao, huwa hawana tena mpango. Kwa hiyo, tukubaliane kwamba mwanaume akishakuoa na kukuweka ndani, hitaji lake kubwa siyo tendo la ndoa pekee.
Sasa kama ni hivyo, kumbe wanaume huwa wanahitaji nini kutoka kwa wake zao? Winston Parker, ni mshauri na mtaalamu wa mapenzi na uhusiano kutoka nchini Marekani, katika kitabu chake cha What a Man Needs From a Woman, anaeleza kuwa jambo kubwa ambalo wanaume wanahitaji, ni utiifu kutoka kwa wake zao.Anaeleza kwamba udhaifu mkubwa wa wanaume, ni kuona wanasikilizwa na kupewa utii kutoka kwa wake zao na kudekezwa kama watoto. Hata kama mwanaume akiwa ‘mtata’ kiasi gani, anapokutana na mwanamke anayemheshimu, kumsikiliza, kumtii na kumdekeza, ni lazima atazama kwenye penzi lake hata kama si mzuri wa sura wala umbo kiasi cha watu wengine kuanza kuulizana ‘anampendea nini yule’?
Ipo kasumba ya wanawake wengi siku hizi, kudai usawa hata katika mambo ambayo hayahitaji usawa. Mwanamke anakuwa jeuri, mkaidi na hamuheshimu kabisa mumewe. Akikatazwa kufanya jambo fulani anaona kama anatawaliwa, anafanya hata kama anajua mumewe hapendi, kisa ‘haki sawa’.
Matokeo yake, mwanaume wa aina hii akikutana na mwanamke anayemsikiliza na kumheshimu, hata kama ni hausigeli wake, yupo tayari kumkabidhi moyo wake na kumuonesha mapenzi ya dhati. Huenda hii ni miongoni mwa sababu zinazowafanya mahausigeli wengi kupindua ndoa za mabosi wao.
Sihalalishi kwamba kama mwanamke ana udhaifu huu basi aadhibiwe kwa usaliti, hapana. Wengine wanakuwa na tabia hizi kwa sababu ya malezi waliyolelewa, lakini kama wakieleweshwa kwa upole, huweza kubadilika.
Ni matumaini yangu kwamba wanawake watakaopata nafasi ya kusoma ukurasa huu, watabadilika kwa lengo la kuzilinda ndoa zao na kujenga uhusiano imara zaidi. Lakini kwa wasiotaka kubadilika, niwaambie wazi kwamba, wao ndiyo sababu kubwa ya waume zao kuwa na michepuko.
Tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : USIMLAUMU KWA KUCHEPUKA, YAWEZEKANA WEWE NDIYO CHANZO
USIMLAUMU KWA KUCHEPUKA, YAWEZEKANA WEWE NDIYO CHANZO
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/usimlaumu-kwa-kuchepuka-yawezekana-wewe.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/usimlaumu-kwa-kuchepuka-yawezekana-wewe.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy