UKIMPENDA SANA MTU USIYE MUAMINI, JIANDAE KUJIUA/ KUWA KICHAA !

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
NI mwaka mpya na mambo mapya lakini kiukweli kwenye suala la mapenzi hakuwezi kuwa na mambo mapya.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
Mambo ni yaleyale na ndiyo maana hata nitakayokuwa nayaandika hapa kwa mwaka huu hayawezi kuwa tofauti sana na yale ambayo tumekuwa tukielezana kila siku.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
 Leo nitazungumzia jinsi ambavyo unaweza kujiweka katika mazingira ya kujiua au kuwa kichaa endapo utatokea kuwa kwenye mapenzi na mtu ambaye unampenda sana lakini humuamini.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
Ukijaribu kufuatilia utabaini kwamba, huko mtaani kilio cha wengi walio kwenye uhusiano ni kutowaamini wapenzi wao na kila wakati kuhisi wanasalitiwa. Wapo ambao si tu kwamba wanahisi bali wanawafumania kila kukicha.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
Kwa kifupi kasi ya wapenzi kusalitiana imekuwa ikishika kasi kila siku kiasi cha baadhi kuhisi bila kusaliti hawasikii raha.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
Yaani wanapatilizwa kila kitu na wenza wao lakini bado wanatoka nje. Unakuta mwanaume ana mke mzuri anayejua mapenzi na kila kitu lakini bado mwanaume huyo haridhiki na anachepuka.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
Pia wapo wanawake ambao wamebahatika kuwapata wanaume ‘handsome’, wanaojua mapenzi na kujali pia lakini bado tamaa za usaliti wanakuwa nazo. Ukiuliza kipi kigeni wanachofuata huko nje, huwezi kupata jibu la maana.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
Nilishawahi kufanya uchunguzi huko nyuma kwa kuzungumza na baadhi ya wapenzi kuhusu hili suala la kusalitiwa.
🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞

Wengi walikiri kujua kwamba kuna uwezekano mkubwa wapenzi wao wanawasaliti lakini wenyewe wanadai ni mambo ambayo wakiyafuatilia sana wanaweza kujikuta wanaachana wakati huenda bado wanapendana.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
“Hivi unadhani ni wakati wa kuamini asilimia zote kwamba husalitiwi? Binafsi kwa ninavyomjua mume wangu na huu utitiri wa wanawake ‘cheap’ huko mtaani, nahisi kwake itakuwa ngumu sana kuvumilia, ila kinachonifanya niwe na amani ni kwamba, ananiheshimu na sijawahi kumfumania.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
“Hilo ndilo linalonifanya niwe mpole ila najua hakosi mchepuko na nikimfuatilia najua wazi nitamfuma, tutagombana na hata kufikia hatua ya kuachana, sasa ya nini hayo?
🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞

 “Maana ninachojua ni kwamba, ukimfuatilia sana mpenzi wako unatafuta sababu ili muachane, sasa kama hauko tayari muachane ni vyema ukamuamini na kama huko pembeni ana vichenchede, ni yeye na Mungu wake,” alisema Sharifa wa Sinza jijini Dar ambaye ndoa yake sasa ina miaka 10.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
Mwingine ambaye nilibahatika kuzungumza naye alijitambulisha kwa jina la Juma wa Nguvumali, Tanga. Huyu anaeleza kuwa, amekuwa akishuhudia wanawake wengi anaowaheshimu akiamini kwamba wametulia na wapenzi wao wakiwasaliti wapenzi wao. Hili linamfanya hata mpenzi wake asimuamini kwa asilimia zote.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
“Huwa nawaona wanawake ambao sikuwahi kufikiria kuwa wanaweza kuwasaliti wake zao lakini wanafanya hivyo. Mfano kuna shemeji yangu, mke wa rafiki yangu, ni mpole sana, mtaratibu na anaonekana asiye na ‘time’ na wanaume.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
“Huwezi kuamini siku moja nilimfuma akiingia gesti na mwanaume. Nilipigwa na butwaa na hapo ndipo nilipoamini kwamba hakuna asiyesalitiwa na kama yupo basi ana bahati sana.”

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
Hao ni watu wachache tu ambao niliongea nao lakini wengi walikiri usaliti upo tena wanaoongoza kusaliti ni wale ambao wapenzi wao wanawaamini sana. Kuna ambao walifikia hatua ya kukiri kwamba eti wakibaini wapenzi wao wanawasaliti na wao wanachepuka.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
Hii yote inaonesha ni kwa jinsi gani mapenzi ya sasa usaliti unachukuliwa kama fasheni. Yaani mama fulani akimuona shoga yake ana ‘kibenten’ basi naye anatafuta ili waende sawa. Huu ni ulimbukeni uliopitiliza.
🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞

KIPI KIFANYIKE?

Kutokana na utafiti huu niliofanya ambao naamini hata wewe unakubaliana nao, kuna kila sababu kila aliye kwenye uhusiano kumuamini mwenza wake kwa kiwango kinachostahili. Sisemi umuamini tu hata kama unaona anakuchezea rafu, lahasha! Muamini pale ambapo una sababu ya kufanya hivyo.

🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞
Ukiona dalili za wazi kwamba anakusaliti, ukafuatilia na kugundua ni kweli ana mtu au watu wengine unaochangia nao penzi, hutakiwi kuvumilia. Mtu huyo atakuwa hana nafasi kwenye maisha yako hivyo haraka muweke kando maana ukiendelea kuwa naye unatafuta kujiua au kudata.
🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞🦞

TAFAKARI CHUKUA HATUA

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : UKIMPENDA SANA MTU USIYE MUAMINI, JIANDAE KUJIUA/ KUWA KICHAA !
UKIMPENDA SANA MTU USIYE MUAMINI, JIANDAE KUJIUA/ KUWA KICHAA !
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/ukimpenda-sana-mtu-usiye-muamini.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/ukimpenda-sana-mtu-usiye-muamini.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content