UCHAFU WA MUME AIBU YA MKE

Bibi usafi bibi,usafi si kudeki na kufagia pekee laa!! Usafi wako wa mwili na usafi wa mumeo pia.

Kina dada mmejisahau kabisa usafi wa mume kwa kitu kimoja! Kina dada mmejisahau kwenye kitu kimoja kwenye usafi wa waume zenu!! Somo tahadhari na kocho somo narudia tena kocho bibi kocho!! Aibu kocho ya mume mpaka yambadilikia rangi mwilini na habibity wake habari huna!! Kocho ya bluu imevaliwa mpaka rangi ya kocho yafanana na ngozi ya kiuno mmmmhhh!!! Aibu somo yangu na aibu hii si mume pekee bali ni aibu kubwa sana kwa mke. Somo yangu kioo cha mume ni mkewe,mume mkague kabla hajatoka ndani sio kutazama tu kodi ya meza imeachwa basi! Huo ni mwiko somo yangu.

Mwanamke upo makini kuitazama chupi ya mtoto kutwa wambadili na kuzifua lkn mke mwezi nzima hata hujui mume kavaa kocho kwa siku ngapi!! Usione mume ni mtu mzima bibi lkn kwenye hili la kocho mume hua sawa na kitoto kidogo tu!! Mume kama hukumzonga bibi nakwambia kocho anaweza kuvaa mpaka mwezi,somo yangu hakuna kitu kazi kwa mume kama kubadili kocho kila siku! Mume yuradhi kubadili nguo kutwa mara mbili lkn si kocho na maadamu kocho haivaliwi kichwani ndo kabisaaaaaa.

Wanaume wanahadhirika kwenye dala dala hasa daladala ikijaa na lile joto ndo mtihani maana mwengine kama kakukaribia nawewe umekaa kwenye siti pua zako zipo karibu na vikalio ndo utaomba gari ifike uendako huepukane na balaa hilo!! Kocho mpaka yajenga ukungu kiunoni mke uko wapi? Hata kama waume ni wabishi lkn na mke akiwa mbishi hapo ndo balaa.somo yangu mumeo akipita kuwapa watu kero kwa uvundo wa kocho yake aibu waipata wewe unayekumbuka kumfulia suruali na shati kisha wapuuza kumkagua kocho lake.somo kocho mume asivae zaidi ya siku mbili!! Na kama anaiplenda sana na kuivua hataki basi fua usiku asubuhi avae, lkn si kumsusa loooo!!

Nakukumbusha tena somo kioo cha mume ni mke usikubali kupata aibu kwa mambo madogo kama hayo. Chupi mtoto wambadili kutwa mara 4

Comments

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment