SINTOISAHAU SIKU YA WAPENDANAO.

SIMULIZI IITWAYO SINTOISAHAU SIKU YA WAPENDANAO.

Acha niseme ile ndio ilikuwa siku ya wapendanao ambayo sitokuja kuisahau katika maisha yangu yote, ilikuwa ni siku ya wapendanao ambayo ilikuwa imeniumiza kupita kawaida. Nakuhadithia wewe rafiki yangu, nakuhadithia huku nikiwa na maumivu makubwa moyoni mwangu.
Siku hiyo ambayo wapendao mnatakiwa kukaa pamoja na kuzungumza mambo mbalimbali, kutembea sehemu mbalimbali na hata kupeana zawadi, kwangu mimi ilikuwa tofauti kabisa, ilikuwa ni siku ambayo ilinisababishia maumivu makubwa sana, ila maumivu yote haya yalitokana na mpenzi wangu, Prisca Godson, msichana ambaye nilikuwa nikimpenda kupita kawaida.
Naikumbuka sana siku hiyo ya alhamisi, siku ambayo niliwasiliana na Prisca kabla ya wiki mbili na kisha kumwambia kwamba siku hiyo ingependeza sana kama tungekuwa pamoja. Nilitamani sana kuwa na Prisca wangu ila siku hiyo muitikio wake wala haukuwa mzuri.
Sikukasirika kabisa, nilikuwa nimekwishazoea hali hiyo kutokana na mambo mengi ambayo alikuwa akinifanyia Prisca. Alijua fika kwamba mimi, Juma nilikuwa nikimpenda sana, mimi Juma nilikuwa nikimthamini sana ila kwa vyote ambavyo nilikuwa nikivifanya kwa ajili yake, havikuonekana kuwa na thamani.
Kiukweli nilimpenda sana Prisca na ninadiriki kusema kwamba yeye ndiye alikuwa msichana ambaye nilimpenda kuliko wasichana wote. Sijui kwa nini nilikuwa nikimpenda hivi, sijui kwa nini nilikuwa nikimthamini hivi, ila sababu kubwa nadhani kutokana na yeye kunifundiaha mchezo ule mchafu, mchezo ambao nilikuwa nikipenda sana kucheza naye.
Nilimzoea Prisca kama dada yangu, mapenzi yetu yalikuwa makubwa sana ila baada ya muda mrefu mambo yakaanza kubadilika. Kitu cha kwanza akaanza kuwa adimu machoni mwangu, jambo lile lilinisononesha sana, sikuwa nimezoea kukaa siku moja bila kumuona Prisca ambaye alipokuwa akiishi hapakuwa mbali kutoka na nilipokuwa nikiishi.
Mara kwa mara nilikuwa nikielekea nyumbani kwao lakini wala sikufanikiwa kumuona. Namba yake ya simu nilikuwa nayo, nilikuwa nikijaribu kumpigia sana lakini wala hakuwa akipatikana na kama alikuwa akipatikana, hakuwa akipokea simu yangu.
Akili yangu ilichanganyikiwa sana, sikuwa nimegombana na Prisca kabisa, nilikuwa nikiishia naye kwa amani. Sasa kwa nini leo hii alikuwa
hapokei simu zangu? Kwa nini leo hii alikuwa hataki kuonana nami?
Kila nilichokuwa nikijiuliza nilikosa jibu kabisa. Sikutaka kukata tamaa, kitu ambacho niliamini ni kwamba Prisca alikuwa akinipenda sana, tena alikuwa akinipenda zaidi ya mvulana yeyote yule.
Siku zikaendelea kukatika, simu yake ikaanza kuwa bize usiku. Jambo lile liliniuma sana kwa sababu katika maisha yangu, kuikuta simu ya mpenzi wangu kuwa bize usiku, lilikuwa jambo baya sana katika maisha yangu ya mahusiano.
Hapo ndipo ambapo nikaanza kufanya upelelezi wangu wa chini chini, upelelezi ambao wala sikutaka kumshirikisha mtu yeyote yule. Nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kujua kilichokuwa kikiendelea, mpenzi wangu wangu ambaye nilikuwa nikimhusudu kuliko msichana yeyote,
mpenzi wangu ambaye nilimwimbia nyimbo nyingi nzuri za mapenzi, eti leo hii aliamua kunisaliti na kisha kuanza mahusiano na rafiki yangu, Ahmed, rafiki ambaye nilikuwa nimekutana naye Facebook.
Moyoni iliniuma sana, tena iliniuma zaidi ya nilivyokuwa nikifikiria kabla. Sikuwa na jinsi, niliendelea kumpenda kwa mapenzi yale yale ambayo nilikuwa nikiyatumia kumpenda. Moyo wangu ulikuwa ukiumia zaidi na zaidi, Prisca wangu ambaye niliishi naye katika mahusiano kwa miaka nane, leo hii aliamua kwa moyo mmoja kunisaliti na kisha kutembea na rafiki yangu.
Sikuwahi kulia kwa ajili ya msichana ila siku hizo zilionekana kuwa ngumu sana katika maisha yangu, nililia kama mtoto mdogo, Maumivu ambayo nilikuwa nikiyasikia yakizungumzwa midomoni mwa watu yakaanza kusikika moyoni mwangu.
Prisca alikuwa ameamua kuumiza moyo wangu, aliamua kunitesa na kunikumbumbusha kwamba hata mapenzi nayo yalikuwa sumu, tena sumu kali ambayo inaua kwa haraka hata zaidi ya nyongo ya mamba.
Sikutaka kumuacha Prisca, bado nilikuwa nikimuonyeshea thamani japokuwa alikuwa amebadilika sana. Wazazi wake hawakufurahia, nao
walikuwa wakiumia kwani walijua ni kwa kiasi gani nilikuwa nikimpenda binti yao.
Mara kwa mara walikuwa wakinisaidia kukaa naye chini na kisha kuanza kuongea naye lakini Prisca hakuwa akiwaelewa, alikuwa akiwaambia kwamba kwa sasa hakuwa na mapenzi na mimi.
Tarehe 14/02/2018 ikawadia, si siku ya mbali, ilikuwa juzi tu. Niliamua kuamka asubuhi na mapema na kisha kwenda Mlimani City kwa ajili ya
kununua maua kwa ajili yake kwani mara kwa mara siku kama hiyo huwa tunakaa pamoja nyumbani kwao au nyumbani kwetu.
Sikuwa nimewasiliana naye, nilitaka nimfanyie suprise moja ya nguvu. Nikanunua maua ambayo kila msichana aliyekuwa akiyaona, alitamani kama ningempa yeye. Ilipofika saa nane nikaelekea kwao, bahati mbaya, sikumkuta Prisca.
Nilimsubiri nyumbani kwao huku nikiletewa soda na kunywa, ikaingia saa tisa, kumi, kumi na moja, kumi na mbili mpaka saa moja, Prisca hakuwa amerudi nyumbani.
Nadhani utakuwa umepata picha ya kiasi gani nilikuwa nimeumia katika kipindi hicho. Nilikuwa mnyonge, sikuwa na raha, Prisca wangu ambaye nilikuwa nikimpenda kwa wakati huo alikuwa na rafiki yangu, Ahmed wakila maisha.
Muda ulizidi kwenda, mfuko wa kaki ambao uliyabeba maua yale bado ulikuwa pembeni yangu huku yakiendelea kutoa harufu nzuri ya pafyumu ya The Hiza ambayo ilikuwa ikiwavutia warembo wengi. Saa tatu ikaingia, saa nne mpaka saa tano lakini hali bado ilikuwa kimya kabisa. Kichwa changu kwa wakati huo kilikuwa kikitengeneza picha za ajabu ajabu, eti rafiki yangu Ahmed kwa muda huo alikuwa naye chumbani, kampandisha kitandani na kisha kuanza kuufanya mchezo ambao wala hautakiwi kuandikwa mahali hapa.
Wazazi wake wakashikwa na wasiwasi sana ila nadhani mimi nilikuwa na wasiwasi zaidi yao. Nikaanza kumpigia simu, simu yake haikuwa
ikipatikana kabisa. Hatukutulia, tulijaribu kuwapigia simu marafiki zake lakini wala hawakujua mahali walipokuwa.
Saa sita usiku, simu ya baba yake ikaanza kuita, alipopokea aliambiwa kwamba binti yake alikuwa amepata ajali ya boda boda na hivyo alikuwa amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili. Katika ajali hiyo, Prisca hakuwa peke yake, alikuwa pamoja na dereva na Ahmed ambao walikuwa wamepanda kwa staili ya mshikaki.
Huku tukionekana kuchanganyikiwa, usiku huo huo tukaamua kwenda hospitalini ambapo dokta alituambia kwamba miguu ya Prisca ilikuwa imesagika sana na hivyo ilihitajika kukatwa. Hiyo ilikuwa ni taarifa mbaya ambayo sikutaka kuisikia, miguu ya Prisca ambayo ilikuwa ikimvutia kila mwanaume ndiyo hivyo ilitakiwa kukatwa.
Kwa Prisca ilionekana kuwa kama bahati, kukaa katikati ya dereva na Ahmed ilionekana kumsaidia sana kwani wenzake wote walikuwa
wamefariki huku ni yeye tu aliyekuwa katikati akiwa amepona ila
miguu hakutakiwa kubaki nayo. Prisca wangu, mpenzi wangu ambaye nilikuwa namthamini ndiyo hivyo akakatwa miguu.
Ile ilikuwa kama ndoto maishani mwake ambapo baada ya muda alijiona kwamba angeamka na kujikuta yupo kitandani, haikuwa ndoto, lilikuwa ni tukio halisi ambalo lilikuwa limetokea katika maisha yake.
Mimi kama mimi, sikutaka kumuacha Prisca, nimeongeza mapenzi mara mbili zaidi ya nilivyokuwa nampenda kipindi cha nyuma. Kila siku amekuwa mtu wa kuniomba msamaha, nilichomwambia ni kwamba
nimemsahe na sasa tulitakiwa kusahau kila kitu kilichotokea katika maisha ya nyuma.
Leo ndiyo ilikuwa siku ambayo ameruhusiwa kutoka hospitalini, nipo naye, nampenda na kila siku nitaendelea kumpenda japokuwa miguu yake aliiacha hospitalini .Prisca ndiye mpenzi wangu, Prisca ndiye ninayemthamini, hakuna mwingine kama Prisca japokuwa yeye ni mlemavu anayetembelea kibaiskeli.
Mimi na Prisca mpaka kifo kitutenganishe.
**
Ujumbe huu ukufikie wewe unayemdharau mpenzi wako na kumuona si kitu. Nimechukua mfano wa Prisca, ila yawezekana wewe ukawa Prisca mwenyewe.


MWISHO.

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : SINTOISAHAU SIKU YA WAPENDANAO.
SINTOISAHAU SIKU YA WAPENDANAO.
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/sintoisahau-siku-ya-wapendanao.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/sintoisahau-siku-ya-wapendanao.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content