SIKUKUOA ILI KUCHEZA NA WEWE

Imeandikwa na QiamEmaan_Official na kutafsiriwa na Kabuga Kanyegeri

--------------------------------------------------------------------------------------------------


Walioana baada ya simulizi tamu ya mapenzi yao, na baada ya wiki mbili mumeo aliamka asubuhi kwa lengo la kwenda kazini. Alielekea bafuni ili kunawa uso, na alipojitazama kwenye kioo akaona uso wake umejaa michoro ya rangi mbalimbali.


Mkewe alikuwa mchanga, mwenye mawazo ya ujana, na moyo usio na hatia. Aliuchora uso wa mumewe akiwa usingizini, na alifanya hivyo kwa mapenzi makubwa, ili akiamka asubuhi wapate kucheka.


Mume aliosha uso wake akiwa mwenye hasira na kuelekea jikoni ili kunywa kahawa ambayo alikuwa amezoea kuinywa kila asubuhi. Hakuikuta kahawa, akakasirika zaidi, akamwendea mkewe.


Mke alitabasamu kwa sababu alidhani kuwa mumewe atamchekea na kumwambia maneno matamu ya mahabba.


Lakini mume alimchapa kofi lililompeleka sakafuni, akamkoromea na kumwambia: “Sikukuoa ili kucheza nawe, mimi ni mwanaume sio mtoto mdogo. Nilikuoa ili kuanzisha familia na kuzaa watoto, ili niwe mwanaume mbele ya macho ya kila mtu. Unataka kuishi maisha ya simulizi za mapenzi ya filamu na simulizi za vitabu mapenzi ya vitabu unavyovisoma? Inuka, hizo simulizi hazijengi nyumba, hazileti chakula, hazilei watoto. Leo nitawaalika marafiki zangu kwa ajili ya chakula cha mchana, nikirudi nataka nikute kila kitu kipo tayari. Unanisikia?”


Aliondoka huku akijiona kuwa kidume wa nyumba. Alimuacha mkewe akiwa ameumia na kuvunjika moyo, alilia sana kiasi kwamba hakuweza kupumua vizuri.


Mke ni mgonjwa na anapolia hupoteza nguvu na kukaribia kuzimia.


Aliharakisha kwenda kuandaa chakula cha mchana kama alivyoagizwa na mumewe, lakini machozi hayakukatika mashavuni mwake.


Mume alienda na kumweleza rafiki yake kilichotokea huku akicheka:


"Wanafikiri kwamba ndoa ni mapenzi na simulizi za mahabba tu. Rafiki yangu, hivi ndivyo wanawake wanavyopaswa kushughulikiwa kabisa, vinginevyo hatojifunza majukumu yake. Hatakuwa mama mzuri. Anatakiwa kujua kwamba ndoa sio kama vile anavyoziona au kuzisoma. Hizo ni simulizi tu zinazoandikwa na watu ili kutengeneza pesa. Wanatakiwa kujua kwamba ndoa sio mchezo au simulizi."


Lakini kwa bahati nzuri rafiki yake hakuwa kama yeye, akusubiri amalize kuongea, alimkatisha na kumwambia: "Wewe ni mwanaume wa aina gani? Kwa nini umekuwa mkali sana kwa mkeo? Je, hivi ndivyo mume mwema anavyopaswa kuwa? Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alisema: “Kuweni wema kwa wanawake, kwani wao ni kama vioo.”


Unatakiwa kushughulika nao kwa uungwana na ulaini, na usizivunje nyoyo zao. Mtume wa Mwenyezi Mungu pia alisema kuwa: “Dunia ni starehe ya muda, na starehe bora ya dunia hii ni mwanamke mwema.”


Tahadhari sana na hicho ulichokisema kuhusu mambo ya kupika na kulea watoto. Hilo sio wajibu wake, lakini ukiwa mwema kwake utamfanya akupende zaidi na atayafanya yote hayo bila wewe kumkaripia. Unatakiwa kutambua kuwa yeye sio mtumishi wako wa ndani. Zinduka rafiki yangu na utubu kwa Mwenyezi Mungu. Nenda kwa mkeo ukamheshimu na usimuumize tena.”


Mume alijisikia huzuni na kujuta kwa aliyoyafanya.


Aliamua kumpigia simu mkewe ili kumtaarifu kuwa ameghairi suala la mwaliko wa marafiki zake kwenye chakula cha mchana, na aandae chakula chao peke yao.


Simu iliita lakini haikupokelewa.


Aliendelea nyumbani haraka na kugonga kengele ya mlango lakini hakujibiwa.


Alipotoka asubuhi alikuwa amesahau funguo ndani, kwa sababu alitoka akiwa na hasira.


Ghafla simu yake iliita, ilitoka kwa kaka wa mkewe.


Mkewe alimpigia kaka yake alipoanza kujisikia vibaya, ili ampeleke hospitali.


Shemeji yake akamwambia: "Shemeji, tuko hospitali."


Sauti yake ilikuwa imejaa huzuni, hali iliyomfanya moyo wa mume kukaribia kusimama kwa sababu ya khofu, na wazo la kwamba mkewe atakuwa amepatwa na jambo baya likamshtua.


Alichukua Taxi haraka akaelekea hospitali, na kuwakuta wanafamilia wote wa mkewe wakiwa huko.


Nyuso zao zilijaa huzuni.


Alidhani kuwa watakuwa wamemkasirikia, lakini ilionekana kuwa hakuwa wakijua kilichotokea.


Aliwasabahi na kumsubiri daktari.


Baada ya saa kadhaa daktari alikuja huku akiwa amekiinamisha kichwa chake na kuwaambia: “Kwa masikitiko makubwa moyo wake ulikuwa umedhoofika sana na alikuwa amechelewa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amrehemu.”


Kila mtu alilia, hasa mume. Alijuta na kujilaumu sana.


Mama wa mke alimuosha mwanaye kwa ajili ya mazishi na alizikwa siku hiyohiyo.


Wakati wa jioni mume alirudi nyumbani baada ya kuchukua funguo kutoka kwa shemeji yake.


Aliingia nyumbani na kukuta meza ikiwa imefunikwa. Aliondosha kitambaa na kukuta meza ikiwa imejaa vyakula vitamu, na akaona karatasi ikining’inia kwenye mlango wa friji.


Ilikuwa imiendikwa: 'Mpenzi wangu, niwie radhi kwa kosa langu la kutaka uachane na mila na desturi za jamii yako. Niwie radhi kwa kosa langu la kutaka uondokane na moyo mgumu kama jiwe, na kutaka nisikie maneno matamu ya mahabba kutoka kwako, kutaka unikumbatie na uniambie kuwa unanipenda. Nisamehe kwa sababu ya akili yangu ya utoto nilitaka uamiliane na mimi kama mtoto. Natumai marafiki zake watakipenda chakula niliwaandalia. Naahidi kuwa sitarudia tena kukuumiza au kukukasirisha. Nakuahidi. Nakupenda sana.”


Aliitazama meza na kuvitupilia mbali vyakula vyote, akakaa sakafuni, akalia na kulia huku akisema: “Jambo gani hili nililokufanyia mpenzi wangu? Nilikuua kwa ukatili wangu, nisamehe mimi.”


Siku hizi tunamdharau mtu anayeonesha mahabba kwa mkewe. Tumesahau kuwa utahesabika kuwa ni kidume iwapo utakuwa na huruma kwa mkeo, na hayo ni maamrisho ya Mwenyezi Mungu.


Mwenyezi Mungu anasema: “Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri.” (Qur’an, 30: 21)


Kumbuka kuwa mkeo anatokana na wewe, akiwa na furaha, utaishi maisha ya furaha.


*Tambua kuwa kujenga nyumba yenye furaha inahitajika subira, uaminifu na mapenzi .*

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : SIKUKUOA ILI KUCHEZA NA WEWE
SIKUKUOA ILI KUCHEZA NA WEWE
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/sikukuoa-ili-kucheza-na-wewe.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/sikukuoa-ili-kucheza-na-wewe.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content