PENZI ZITO SEHEMU YA TATU (03)

PENZI ZITO SEHEMU YA TATU (03)


PENZI ZITO 3

SIMULIZI ZA JOSHUA / 4 weeks ago
SIMULIZI: PENZI ZITO
MTUNZI: Prosper Mgowe

SEHEMU YA TATU​


Hakika Mercy alipendeza kama sio kuvutia. Alijigeuza geuza pale kwenye drensing table baada ya kuridhika kuwa vile alivyo ndivyo atakiwavyo kuwa akaanza kupiga hatua za taratibu kuelekea mlango wa chumbani kwake ili aende sebuleni akawasikilize wito alioitiwa na babake.
"Shikamoo Dady"
"Fine how u doing" alijibu kwa umombo babake Mercy" "Well" aliitikia Mercy.
"Okey mama yako amenieleza juu ya matatizo yako"
"Ndio baba"alidakiza mercy
Nimekueleweni na nimekubali huyo kijana aje kuishi pamoja nasi, lakini ataishi kama houseboy"
"Woow" Asante sana baba endapo atakuwa hivyo" Lakini akija huyo kijana sitaki mambo ya upuuzi" akijaribu kwenda wrong na sheria zangu ataondoka mara moja.
"Sawa baba" Aliitikia Mercy kwa heshima zote.
Mercy alichukuwa biblia yake na kutoka kwenda kusubilia daladala ili kuelekea kanisa kuu, hiyo ni siku nzuri kwake.
Asubuhi ya kuamkia jumapili Bryan aliamka mapema kabisa na kuanza kufagia uwanja kuzunguka nyumba yao, baada ya kufagia aliingia chumbani kwake kufanya usafi, japokuwa chumba hicho kuta zake hazikuwa na rangi wala sakafu lakini yeye alikipenda sana na muda wote kilibaki nadhifu.

Wakati ananyunyizia maji aridhini katika chumba chake ili kuondoa vumbi mara ghafla akasikia mlango wake ukigongwa kwa fujo, fujo hizo zilifuatiwa na sauti kali na yenye hasira.

"Fungua we mbwa" alisema shangazi yake Bryan. Bryan kwa unyonge aliachilia shughuli aliyokuwa akiendelea nayo na kufungua mlango.
"Shikamoo shangazi"
Baada ya kupokea hiyo salamu, shangazi yake bryan alimkata jicho Bryan toka miguuni mpaka utosini na kasha akarudia halafu akamsonya msonyo mrefu na kasha akaukamata mkono wa Bryan kwa nguvu na kuanza kumvuta kuelekea nyumba ya nyumba yao.

"Nimekwambia hizi nguo ziishe, na ole wako usizimalize" Aliongea shangazi yake Bryan huku akimtolea macho Bryan.

"Lakini shangazi nitachelewa kanisani"
"Nitachelewa kanisani" shangazi yake alibana pua na kuigiza maneno yale.

"Sasa nasema hivi usipomaliza hizo nguo huko kanisani utapasikia ti". Na ukidiriki kwenda hapa nyumbani usirudi, Ufungashe kilicho chako na usirudi tena hapa" Aliongea shangazi yake.

Ulikuwa ni mlima wa nguo, nguo hizo zilikuwa ni za shangazi yake pamoja na mjomba wake. Bryan akageuza shingo akaangalia hizo nguo zenyewe. Alipoziona tu mpaka uvivu ukamwingia.

"Nimalize" na sizimalizi potelea mbali lakini saa tatu ikifika mimi najiandaa kwenda kanisani, mimi sijali hata wakinifukuza "Aliwaza Bryan baada ya shangazi yake kurudi kulala tena. Mpaka kufikia saa tatu zilibaki asilimia 25 kati ya asilimia 100 ya zilizokuwepo, Bryan aliamua aziache akaanza kujiandaa kwenda kanisani.

Akachukua maji kwenda kuoga alipotoka kuoga aliingia chumbani kwake na kuchukua kikopo chake cha mafuta aina ya rays na kuanza kujipaka kasha akafunua godoro lake la futi 3 kwa 6 na kutoa fulana yake aina ya form 6 pamoja na suruale yake ya shule.

Baada ya kuvaa fulana yake yenye mistari ya bluu na myekundu akavaa suruale yake na kisha akachukua soksi zake za pundamilia na kuzivaa pamoja na viatu vyake vya shule. Akachukua chanuo na kuanza kuchana nywele zake zenye urefu karibu na nchi moja na nusu. Akachukua kipande cha kioo chumbani humo. Baada ya kujitazama na kujiona yuko sawa alichukua kitabu cha Agano jipya na kutoka kwenda kusubiri daladala ili aende kanisani.

Mjomba ake Bryan alikuwa bado hajaamka kwa sababu ya pombe alizokuwa amekunywa jana alikuwa bado ana hang over.

Akiwa usingizini akahisi kama kuna mtu anampiga mgongoni. Akashtuka na kugeuza shingo kuangalia aliyekuwa akimpiga piga mgongoni.
"Za asubuhi dear" kumbe alikuwa mkewe
"Safi" Alijibu kichovu
Amka basi unafahamu sasa hivi ni saa ngapi? "kwani sa ngapi?"
"Saa si hiyo hapo juu ya droo, pembeni ya kitanda. Akanyoosha mkono na kupapasa juu ya droo na kuchukuwa saa yake aina ya Disco isiyo na mkanda.
"Aisee kumbe saa tatu" Mjomba wake Bryan aliongea huku akinyanyuka na kukaa kitandani mara na mkewe naye akanyanyuka na kukaa kitandani na kuanza kumsugua mabegani mumewe, Akiwa bado anaendelea na zoezi hilo mara mjomba ake Bryan alishangaa kusikia mkewe analia kilio cha kwikwi.

"Vip Darling"
"Si huyo Bryan" alijibu mkewe
"Bryan ?"
"Ndiyo huyo huyo Bryan"
"Kafanya nini?"
"Mume wangu yule si mtoto" Aliongea shangazi yake Bryan huku akijiliza kilio cha kwikwi.
"Enhe" mjomba'ke Bryan aliguna kuashiria mkewe aendelee na maongezi.
"Hivi Bryan anaweza kunichungulia bafuni mimi" Aliongea huku akizidisha kilio.
"Halafu ninamkanya na hiyo tabia yake eti ye ananitukana anasema eti siwezi kufanya chochote kwanza hapa kwa mjomba ake kwa hiyo ninaweza kuondoka muda wowote.

"Ha, ha, ha," Mjomba'ke Bryan alipigwa na butwaa na bila kufikilia wala kufanyia utafiti maneno yaliyosemwa na mkewe akachukua hatua ya moja kwa moja.

"Pole sana dear, usijali akija tu ataondoka nitamwambia aelekee anakojua" Aliongea mjomba wake Bryan huku akimpigapiga mkewe mgongoni kumtuliza.

Mkewe akatulia na moyoni mwake alifurahia sana kitendo cha Bryan kufukuzwa.
"Mme wangu utakuwa umefanya jambo la maana kwa sababu huyu Bryan anaweza kuharibu ndoa yetu.

"Usijali, Basi nenda kaandaye chai"
" Sawa mume wangu"
Shangazi yake Bryan alitoka na kwenda jikoni.

Bryan hakuwahi kusali kanisa kuu la mjini Dodoma kabla ya siku hiyo, lakini siku hiyo hata yeye alijishangaa kwa nini siku hiyo anajisikia kwenda kusali kanisa kuu lakini kuna roho iliyozidi kumwambia aende kwenye kanisa hilo.

Bryan aliamua kutii roho hiyo na kuingia kwenye daladala na safari ya kwenda kanisani ikaanza. Walipofika maeneo ya kanisa kuu Bryan aliomba msaada ashushwe karibu na kanisani.

Alilipa nauli na kushuka na kwa mwendo wa haraka akaanza kuelekea upande wa kanisani ili kuwahi ibada. Aliingia kanisani na kukaa benchi la nyuma ambalo lilikuwa limejaa watu.Ibada ilikuwa imeanza kama dakika 10 hivi kabla ya Bryan kuwasili. Ibada ikaendelea na ndipo ikafika wakati wa kutoa sadaka, ulianza upande wa wanawake.

Bryani alijikuta akimtumbulia macho binti mmoja aliyekuwa amempa mgongo. Alijikuta akimsindikiza kwa macho mpaka alipotoa sadaka mpaka alipokizunguka chombo cha kuwekea sadaka Bryan ndipo alipomtambua kumbe ni Mercy. Bryan aliendelea kumsindikiza kwa macho mpaka alipoenda kwenye sehemu yake.

"Kijana vipi? Ni zamu yetu sasa" Bryan alishtushwa na mzee mmoja aliyekuwepo pembeni yake ndipo akasimama tayari kwa kuelekea kwenda kutoa sadaka.

Bryan alipokuwa akirudi kutoka kutoa sadaka alimuangalia tena mercy kwa jicho la wizi lakini kwa bahati nzuri au mbaya macho yao yaligongana na wote wakatabasamu. Kutoka hapo kila mmoja alikuwa akitamani ibada iishe haraka au ikatishwe ili kila mmoja akaonane na mwenzake.

Baada ya ibada kuisha watu walitoka nje ya kanisa tayari kwa kwenda makwao. Aliyekuwa wa kwanza kutoka ndani ya kanisa kati ya Bryan na Mercy, Bryan ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka kwenda kujiegemeza katika mazingira ya kanisani, pale Bryan alipokuwa amesimama alimuona kila alitekuwa akitoka ndani ya kanisa na mara ghafla akatoka Mercy.

"Wooow" Mercy alipiga kelele huku akimkimbilia Bryan.
"Hallo Bryan mambo vipi?"
"Safi habari yaw ewe?"
"Swadakta"
"Nimefurahi sana kukuona aliongea Mercy. "Vipi kuna jipya? Bryan alimuuliza Mercy huku akicheka.
"Yapo mengi tu" Alijibu Mercy huku naye akitabasamu.
"Haya basi nipe hiyo michapo" aliongea Bryan huku akitoka nje ya kanisa.

Mercy alimueleza Bryan mikakati juu yake na pia alimueleza jinsi wazazi wake walivyokubali aende kuishi kwao. Bryan alifurahi mno kwenda kuishikwa akina Mercy na hakujua amshukuru vipi binti huyo kwa wema wake huo kwa maana alishachoshwa na matatizo ya kwa mjomba wake.

Bryan naye alimueleza Mercy matatizo aliyoyapata kwa mjomba wake na alimueleza jinsi shangazi yake alivyo mchimbia mkwara eti kwamba asirudi kama hatakuwa hajamaliza nguo alizopewa azifue. Mercy alimuone huruma sana na kwamba asijali kwani yeye yupo pamoja naye, kwa hiyo toka nukta ile alikuwa yupo huru kuhamia kwao.

"Nyumbani kwetu si unapakumbuka?" Mercy alimuuliza Bryan kama bado anapakumbuka nyumbani kwao kwa maana alishawahi kumuonyesha siku moja tu.
"Ndio bado napakumbuka" Alijibu Bryan.
"Okey nitakuwepo kukusubiri"
Baada ya hapo kila mmoja akaingia ndani ya daladala ya kwao na kuondoka.

Mjomba wake Bryan alikuwa anamaliza kufungasha kila kilichokuwa cha Bryan tayari kabisa kwa kumtimua na shangazi mtu alikuwa ni mmoja wa washiriki wa shuhuli hiyo ya ziada. Baada ya shughuli kuisha, virago vya Bryan vikaanza kutolewa nje ya nyumba yao, hii inamaana kwamba pindi Bryan atakaporejea toka kanisani afikie kubeba kila kilicho chake na apotelee anapokujua yeye mwenyewe.

Shangazi yake Bryan alifurahi sana moyoni kwani alishaona kuwa ndoto yake aliyotarajia sasa inakwenda kutimia.

"Vipi mjomba mbona unatoa vitu vyangu ndani kwangu?" Ilikuwa ni sauti ya Bryan baada ya kurudi kanisani. "Ishia hapohapo, Mwana haramu mkubwa wewe, Sasa nakwambiaje? Kuanzia nukta hii chakula kila kilicho chako na sitaki tena kukuona katika mboni za macho yangu"

"Kwani mjomba nimekukosea nini? Bryan aliuliza kwa uchungu.
"Anhaa kumchungulia na kumtukana shangazi yako unaona uko sahihi eeh?"
"Mbona sijafanya hivyo mimi?"
"Nimekwambia potea kabla sijakutolea panga", muda wote huo shangazi yake Bryan alikuwa dirishani akishuhudia jinsi mambo yalivyo huko nje.

Moyoni mwake alifarijika mno kuona ya kuwa Bryan anaondoka humo chumbani alikuwa akicheka cheka na kurukaruka peke yake mithili ya mwehu.

"Afadhali hili Ibilisi liondoke kwa maana lilikuwa likininyima raha" Alijisemea shangazi yake kimoyomoyo.

* * *

"Kama nimefanya hivyo Mungu anajua" Bryan alijisemea hayo huku akilia, kilichomliza si kuondoka kwa mjomba wake bali manyanyaso ya pale. Alikusanya kilichomuhusuna kuondoka zake.

* * *

"Hodi,hodi,hodi," Bryan alibisha hodi mbele ya jumba moja lenye geti jeupe, lakini hakuna aliyeitika wala kutoka.
Aliendelea kubisha hodi takribani dakika 10 nzima bila ya dalili ya mtu yeyote kuja kufungua.

Baada ya muda mfupi ulisikika mngurumo wa gari nyuma yake, wakati huo Bryan alikwisha kata tamaa kabisa kugonga hili geti kwani hakukuwa na dalili yoyote ya mtu kufungua.
Ile gari ilikuja moja kwa moja kwa karibu na miguu ya Bryan. Kisha milango ya ile gari ikafunguliwa kisha ndani ya ile gari akatoka mzee wa mmoja wa makamo.

"Shikamoo baba", Bryan alimsalimu mzee aliyeshuka garini.
"Oh Marahaba kijani habari yako?"
"Nzuri tu baba"
"Bila shaka wewe ndiye Bryan? Mzee Josephat alimuuliza.
"Ndio Baba"

Mzee Josephat alibonyeza kitufe cha kengele kilichokuwako pembeni kidogo ya geti na mara moja ya geti likafunguliwa aliyefungua alikuwa mamayake Mercy.

"Karibu" Alisema mama Mercy baada ya kufungua geti.
"Asante mama, shikamoo" Bryan aliamkia kwa nidhamu
"Marahaba mwanangu" Aliitikia mama Mercy
Mzee Josephati alirudi ndani ya gari na kuingia moja kwa moja car parking. Mama Mercy alimpokea mizigoyake nakuifikisha vyumba vya uwani na baada ya hapo akampeleka sebuleni

Baada ya Bryan kukaribishwa na kuketi sebuleni walianza kujuliana khali na kutambulishana wakati huo Mzee Josephat alikuwa ameshapaki gari yake na kujumuika pamoja nao. Pindi utambulisho ulipokuwa ukiendelea Mercy naye alikuwa akiingia sebuleni akitoka bustanini alipokuwa amepumzikia.

"Wooow Bryan karibu sana" Mercy alikuwa amefurahi sana baada ya kumuona Bryan alitamani amkumbatie ila kwa heshima ya wazazi wake aliishia kumpa mkono tu.

"Asante sana Mercy nishakaribia"Bryan aliongea kwa aibu kidogo akichekacheka.
Mercy akatoa utambulisho kamili kwa mara nyingine tena. Baada ya utambulisho kukamilika mzee Josephat alimueleza Bryan majukumu aliyotakiwa kuwa nayo katika nyumba hiyo.

Bryan alizidi kufurahi kwani hakuona gumu lolote ambalo angeshindwa kulitekeleza.
"Mercy kamwandaliye mwenzio chakula" alisema mama Mercy.
Mercy alifanya shashaa na baada ya muda kidogo Mercy alileta chakula na kwa pamoja wakajumuika kwa furaha.

Usiku wa usiku hiyo Bryan alipewa chumba cha upande wa upande wa uwani kilikuwa kizuri, ndani kilikuwa na rangi ya blue bahari na silingboard nyeupe, kilikuwa na kitanda cha 5 kwa 6, meza ya wastani pamoja na kochi moja watu wa tatu.

Bryan alipokuwa amepumzika katika chumba hicho ni mambo mengi yalikuwa yakipita katika ubongo wake.
Kwanza alikuwa akifikiria ni kitu gani ambacho Mercy aliwaza mpaka akaamua kumtendea wema kiasi hicho, na kwa nini asiwe mwingine isipokuwa yeye, hakuelewa angemlipa nini binti huyo kwa hakika alimuona ni kama mkombozi wake ila alijiapiza ni lazima ipo siku lazima atamlipa fadhila zake baada ya kuwaza hayo alipiga magoti na kumshukuru mungu kwa kumtuma mwakilishi wake kuja kumkomboa katika sakata alilokuwa nalo. Baada ya kumaliza sala zake alijitupa kitandani na kuvuta hayo yote yalikuwa ni kama ndoto lakini ni kweli.

Kwa upande wa Mercy alikuwa na furaha isiyokifani, furaha hiyo ilitokana na kuwa karibu na Bryan. Kwa Mercy aliamini ndoto zake za kummiliki Bryan zilikuwa zinaenda kutimia.

Mercy kwa kipindi hicho alikuwa amekaa juu ya kitanda chake, miguu yake akiwa ameikunja na mikono yake ikiwa imekumbatia mto wenye umbo la kopa.

Huku akisugua mto huo kwa taratibu fikra zake zikimpa kana kwamba yupo pamoja na Bryan.
Wakiwa wamesimama pamoja tofauti ya hatua moja.
"Bryan naomba nikumbie kitu"
"Kitu gani hicho Mercy?"
"Mmh, mmh?
"Mmh,mmh,kitu gani wakati umesema kuna kitu unataka kuniambia"Alihoji Bryan
"Naomba usinifikirie vibaya naheshimu hisia zangu ndo maana nimeamua kukuambia, Nafahamu mapenzi sio kitu rahisi, Lakini naomba unimiliki, NAKUPENDA SANA BRYAN". Kabla Bryan hajaongea kitu Mercy alinyoosha mkono ili kumkumbatia Bryan lakini huyo Bryan hakuwepo kwa Mercy yalikuwa ni mawazo tu ya kufikiria tu.

Akiwa juu ya kitanda chake alichanua tabasamu hafifu la kujifariji kwamba iko siku lazima mawazo yake aliyokuwa anayawaza nucta chache zilizopita ni lazima yatatimia.
Je! NDOTO ZITATIMIA???

Comments

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment