PENZI ZITO SEHEMU YA TANO (05) | BongoLife

$hide=mobile

PENZI ZITO SEHEMU YA TANO (05)

PENZI ZITO SEHEMU YA NNE (04)


PENZI ZITO 5

SIMULIZI ZA JOSHUA / 3 weeks agoSEHEMU YA TANO​


MHARIRI JOSHUA SHAO

0713111547 WHATSAPPWakati Mercy alipokuwa chumbani kwake akiwaza hayo na Bryan pia alikuwa chumbani kwake akijipumzisha akiwa mawazo yake juu ya Crister. Alijiuliza na kwamba msichana yule alikuwa akimtazama vile, ni kwa nini yule msichana alimuuliza maswali mengi vile ilihali hawafahamiani.

Alikuwa katika mawazo hayo taratibu akajihisi Crister amemuingia moyoni alipokumbuka macho yake ya upole tabasamu lake tamu, midomo yake mipana, meno yaliyobanana hakuna pengo wala mwanya pamoja na uso wake wenye shepu ya kitoto, tayari Bryan alishahisi moyo wake kuzorota juu ya Crister. " Iwe isiwe lazima nitimize ndoto yangu juu ya Crister, sielewi nitampataje lakini naamini nitampata" Bryan alijikuta akiongea kwa sauti ili hali yupo peke yake chumbani humo.

Crister alikuwa yumo ndani ya Hice akielekea shuleni kwao msalato, akitokea mjini katika manunuzi yake ya vitu vidogodogo.

Akili yake ilijihisi haifanyi kazi vizuri toka waonane na Bryan. Kwa historia ya yeye hakuwahi kukutana na mvulana wa namna kama ya Bryan kwa upande wa Crister aliuchambua wasifu wa nje wa Bryan kanakwamba alikuwa mtanashati aliyestarabika, mwenye mvuto wa asili kwa wazungu wanaita Natural attract, mwenye nyusi nyingi, mwenye macho ya shape ya kungu, sio mazito wala mepesi ni saizi ya kati na pua ndogo iliyotulia katikati ya midomo na macho, hivyo vilitosha kumpa umajinuni dada wa watu naye pia alijikuta akimpa Bryan umaarufu mkubwa sana katika moyo wake,kwa kila hali alijipazia ni lazima awenaye.

Mercy alipofika shule kwao, aliendelea moja kwa moja bwenini kwake, akaweka vitu vyake kwenye tranker lake kasha akabadili nguo na kuelekea bafuni kwa ajili ya kuoga ili aondoe uchovu wa usiku mzima.

"Jamani sisi tunatoka kwenda kwenye matembezi yetu ya weekend" walikuwa ni Mr and Mrs Josephat wakiwaaga wasichana wao wa kazi pamoja na Mercy, mtamwambia na Bryan" waliongezea.

"Hamna shida" alijibu Mercy
" Halafu mtamwambia mlinzi asiruhusu watu wasioeleweka waingie humu ndani" Aliongezea mzee Josephat.

"Sawa baba" Alijibu Mercy kwa adabu.
Mr and Mrs wakatoka wakachukua gari na moja kwa moja wakaelekea mitaa ya Airport na kuingia katika baa moja maarufu iliyopo mtaani hapo.

"Bahati haiji mara mbili" Alijisemea Mercy kimoyomoyo baada ya wazazi wake kuondoka, kwa wiki nzima alikuwa akiombea hiyo nafasi iliyotokea kwa sasa Mercy aliapiza moyo ni lazima atekeleze azima yake ya siku nyingi juu ya Bryan.

Mercy aliingia bafuni kuoga kasha akaingia chumbani kwake akaufunga mlango wa chumba chake kwa ufunguo kisha akiwa ndani ya kanga moja akasimama mbele ya drensing table kasha akaiachia kanga kwa kuwa ilikuwa imefungiwa juu ya matiti ikashuka mpaka chini na kasha akabaki kama alivyoumbwa.

Hiyo yote ilikuwa ni kujithaminisha alikuwa analipa au? Baada ya kuridhika alifungua sanduku lake la nguo na kutoa nguo alizopanga kuvaa usiku huo.

Kwa chini alivaa miniskirt ya blue yenye kumeremeta juu alivaa top nyeupe isiyoshika mabega yenye mchoro wa kopa na maneno 4rever and 4 always nayo yalikuwa yakimetameta kichwani alivaa wigi la rangi ya kahawia na kasha akachukua uturi wenye nembo ya silver na kujinyunyizia hapo haikunoga akachukuwa na lipshine baada ya kujikubali akachukua sandals na kuzivaa na kuanza kutoka.

"He vipi da Mercy na we leo unatoka?"
Aliuliza kwa kejeli housegirl wao Paulina.

Hapana nipo kwa kaka Bryan tuna somasoma, siunafahamu mitihani inakaribia Mercy alijibu kwa kutojiamini kwani alishtushwa sana na swali hilo inamaanisha hakutazamia kwa wakati huo.

"Mh haya bwana mi naenda zangu kulala" Mercy alitoka bila kujali alifungua mlango mkubwa wa panel na kutoka kuelekea vyumba vya uwani mikononi akiwa na counter book la kuzugia na katikati aliweka card mahususi kwa ajili ya Bryan.

**
Kwa usiku huo huo wakati Mr and Mrs Josephat wametoka katika matembezi ya week end Bryan alikuwa ameingia bafuni kuoga. Baada ya kumaliza kuoga alirudi chumbani kwake na kuvaa trucksut yake nyekundu yenye mistari myeupe pembeni pamoja na singland nyeupe. Alipomaliza kuvaa alichukuwa remote control akawasha radio kwenye kona moja ya chumba chake, alifungulia sauti ndogo na kasha akaendelea bookshelves iliyoko chumbani humo na kutoa novel moja iliyokuwa bado hajamalizia kuisoma ya Chinua Achebe yenye title iliyoandikwa No Longer at easy, na kujilaza nayo kitandani na taratibu akaanza kuperuzi kurasa na hatimaye akapapata alipokuwa ameishia.

Hakufikisha hata kurasa kumi akasikia mlango wa chumba chake ukigongwa . Haikuwa kawaida kugongewa katika chumba chake usiku kama huo, na hakujua ni nani alokuwa akigonga. Alifikiria lamda ni Mercy lakini hilo wazo hakulipitiza moja kwa moja kwa sababu aliamini wazazi wake wapo sasa angetokatoka vipi usiku wote huo. Ingekuwa mchana wala asingeshangaa kwani alishazoea kumuona akiingia chumbani humo na kumfanyia vituko vingi tu.
Aliwaza ni housegirl lamda amekuja kumuita huenda kuna dharula.
"Lakini huyu housegirl mbona sina mazoea naye au lamda……Bryan hakuimaliza sentensi yake akaona ni upumbavu kujiumiza kichwa wakati jibu kamili atalipata pindi atapofungua mlango.

Taratibu akajiinua kuelekea mlango wa chumbani kwake ili aufungue amuone anayebisha mlangoni kwake.

Mercy alipoona amesubiri kwa muda kidogo bila mlango kufunguliwa akaamua kushika kitasa cha mlango na kujaribu kufungua kama ulikuwa wazi. Wakati Mercy alipokuwa akijaribu mlango wa chumba cha Bryan na Bryan naye ndipo alipokuwa akiufungua mlango.kwa pamoja wakagonganisha macho. Bryan akakutana na tabasamu lililochana usoni mwa Mercy pamoja na marashi yaliyozidi kumfanya Mercy aonekane kunukia zaidi pamoja na mazingira aliyokuwepo.

Mercy alimpa Bryan mkono bila kuongea neno zaidi ya kumuangalia Bryan machoni na kasha akakikunja kidole chake cha katikati na kumkuna Bryan katikati ya kiganja chake, na kasha Mercy akamuuliza Bryan.

"Are u okey? "alimuuliza kwa sauti ya taratibu.
"Yeah, of cuz" naye Bryan alijibu kwa sauti ileile ya taratibu. Kabla Mercy hajaendelea Bryan akamuwahi kwa swali.

"Kulikoni saa hizi ihali sio kawaida, halafu huogopi wazazi, na je, wakijua uko kwangu wakati kama huu? Bryan alimuuliza maswali mfululizo huku akiwa haamini ujio ule.
"Usijali Bryan leo baba na mama wametoka out. Au hufahamu leo ni weekend?.
Bryan hakujibu zaidi ya kwenda kukaa sehemu aliyokuwa amekaa awali. Alikuwa akisubiri kuona nini kitachofuata.

Mercy aliiendea sehemu aliyokuwa amekaa Bryan naye pia akaeti pasipo kukaribishwa.
"Sema nikusaidiye nini dadngu" Aliuliza Bryan kwa sauti ya upole yenye mikwaruzo kwa mbali.

Lilikuwa ni swali gumu kwa Mercy na pia ilimuwia vigumu zaidi pale ambapo Bryan aliongezea neno dadangu lakini alijipa moyo kwa kuwa alishaweka nadhiri lazima atekeleze azma yake.

"Bryan naomba uchuke hili counter book na kasha ufungue katikati na hicho ndicho kilichonileta namaanisha ni mzigo huo utakao ukuta humo"
Bila kusema kitu Bryan alichukuwa hilo daftari na kasha akafungua katikati na kukuta bahasha yenye jina lake, akaichukuwa bahasha hiyo na kufungua na kukuta card.

Alitoa card hiyo kwa juu ilikuwa na picha ya mishumaa mitatu mmoja ulikuwa umeungua mpaka kwisha, wa pili ulikuwa ukiwaka lakini upo nusu na wa tatu ulikuwa ndio kwanza unawake hiyo inamaanisha huo ulikuwa mzima, zaidi ya hayo kulikuwa na picha ya umbo la kopa lenye nyufa katikati yaani lilikuwa halijaunganika na pembeni yake kulikuwa na ua moja rose.

Juu kabisa katika card kulikuwa na maneno yaliyoandikwa kwa rangi ya njano yalisomeka kama "YOU ARE MY NUMBER ONE"
Baada ya Bryan kumaliza kusoma hayo pamoja na picha zilizomo juu ya card hiyo, alifungua ndani. Ndani ilikuwa na picha zilezile zilizokuwepo nyuma ya card lakini maneno yalikuwa tofauti, ni machache lakini yenye ujumbe mzito. Maneno hayo yalisomeka hivi : "My feelings fou you is more than the ward I LOVE YOU" Mwisho akamalizia na jina lake "Lots of love Mercy"
Ni kimya cha takribani dakika kumi, Bryan alikuwa akitafakari ujumbe uliyokuwamo katika card.

Bryan akashusha pumzi kwa nguvu kasha akamwambia Mercy;
"Nimeiona, nimeisoma na nimeielewa na nashukuru kwa hilo lakini napenda unijulishe umewaza nini mpaka umefikiria hatua hii na ni kipi hasa kilichokufanya uvutiwe na fukara mimi?"
"Usiseme hivyo Bryan, kwa sababu wewe ni mtu kama watu wengine na isitoshe mimi nimevutiwa na jinsi vile ulivyo, yaani sijui nikwambiaje, nafahamu siwezi nikakueleza ukanielewa, tuseme in short kama ujumbe wa kwenye card unavyoelezea" Aliongea Mercy akiwa anatazama vidole vyake alivyokuwa akivivunjavunja huku shingo yake akiwa kailaza upande wa bega lake la kushoto.

Bryan alinyamaza kwa dakika kadhaa akiyatafakari aliyoambiwa na Mercy, lakini kila alipojaribu kuyatafakari hayo, taswira ya Crister ikajitikeza katika ubongo wake, kiasi kwamba alijikuta akijipiga paji lake la uso kwa kiganja. Mercy alimtazama kwa jicho la kona halafu asijue la kufanya zaidi ya kusubiri matokeo ya ombi lake.

"Aisee Mercy umeniweka katika wakati mgumu" Aliongea Bryan huku akijifuta jasho handcarchief yake, hilo jasho hata yeye hajui lilipotokea kwa sababu chumbani humo kulikuwa na feni na ilikuwa imewashwa.

"Jamani Bryan naomba unielewe, kwa sababu inafikia wakati nashindwa kufanya shughuli zangu za kila siku na hiyo yote ni kwa sababu ya wewe, naomba unionee huruma" Mercy aliongea kwa huruma kiasi kwamba Bryan yalimuingia lakini pindi alipotaka kunyanyua mdomo amjibu Mercy, taswira ya crister ikatokea katika fikra za Bryan na kujikuta akishusha pumzi kwa nguvu na asiweze kuzungumza neno.

"Vipi Bryan" Mercy alimuuliza Bryan kwa sauti ya kukata tamaa lakini ilyokuwa na shahada ya uvumilivu.
"No,no,no, Mercy hilo swala kwangu litakuwa gumu" Bryan aliongea kwa sauti ya juu kidogo lakini hakuelewa uwamuzi huo alikoutoa

"Oh, Bryan kwanini? Kwanini unanifanyia hivi mimi? Kwanini mimi jamani? Mercy aliongea kwa sauti ya uchungu na machozi yalikuwa yamemuanza kumlengalenga. Bryan alimuangalia Mercy kwa macho ya huzuni bila kusema neno. Mercy alimuangalia Bryan kwa kwa macho yenye mg'ao wa machozi na kwa sauti ya taratibu akamwambia Bryan. "Bryan, najaribu kutafuta sana kosa, sioni japo kiasi, lakini kumbuka mimi ni binadamu, kukosea si ajabu, inawezekana siku moja niliwahi kukupa adhabu, kama basi ndivyo ilivyo sina budi kukuomba msamaha"

"Mercy hujanifanya baya lolote, kwanza mie ndio ninastahili kukuomba msamaha, kwa …….kabla hajamaliza sentensi yake fikra juu ya crister zikamjia tena, Bryan alinyamaza asijue la kufanya.
Mercy alimuangalia tu bila kutamka neno.Bryan akajitahidi kuzifuta fikra hizo juu ya crister na kujitahidi kurudisha fikra zake pale alipo. Pale alipofanikisha hilo ndio akaendelea.

"Unaona bwana" therefore I ‘m sorry for that" Kabla Bryan hajaendelea Mercy aliinuka na kuiendea CD iliyokuwepo mbele juu ya radio na kuiweka kwenye radio. Lakini kabla hajaweka play Bryan alimuuliza Mercy, Mercy u know what love is?" Bryan alimuuliza Mercy kwa kumpima, aliwaza may be ni foolish age inamsumbua anang'ang'ana na vitu ambavyo hata havielewi.

Mercy aligeuza shingo taratibu na kumtazama Bryan kwa macho yenye matumaini Fulani kasha akasema "Love an adiventure of the heart and a delight of the soul". Aliongea Mercy kwa kujiamini.

"Ofcourse that is right but ……………"Lakini kabla hajamalizia sentensi yake alinyamaza. Kipindi Bryan alipokuwa akiongea hayo, Mercy alikuwa akisoma nyimbo zilizokuwa zimeandikwa juu ya cover la CD na baada ya muda kidogo aliuona wimbo alo'kuwa akiupenda mno. Ulikuwa ni wimbo namba 6 katika Cover akachukua remote na kubonyeza, basi music ukaanza kwa taratibu, kwa hakika kila aliyekuwepo ulimpa hisia flani flani, ulikuwa umefunguliwa kwa sauti siyo ya chini sana wala ya ya juu sana. Nafikiri ndio sababu hata Bryan aliikatisha ile sentensi yake. Ulikuwa ni wimbo wa mwanamuziki mkongwe Phill Colins wimbo huo ulikuwa ukiitwa True colour. Baada ya wimbo kuanza Mercy hakurudi alipokuwa amekaa alienda katika moja ya kona za chumba hicho gemea ukuta huo mguu mmoja akiwa amekunjia ukutani na mkono yake yote mifukoni.

Wote walitazamana bila kukopeza kope za macho yao na wote wakashindwa kuzungumza neno huenda wote walivutiwa na mpangilio mzuri wa vyombo na sauti ya mwanamuziki huyo na mara ghafla kwa hatua za hesabu na za taratibu Bryan alianza kumsogelea Mercy, huku Mercy akiwa ametulia pale alipo naye alishtukia machozi yakitiririka juu ya mashavu yake. Kilichomliza hata yeye hakukijua, huenda music umemuingia na huenda music huo huo ndio uliomtoa Bryan sehemu aliyokuwepo na kusababisha amuendee Mercy.

Bryan alipomfikia Mercy alimtoa mikono yake mifukoni na kuizungusha katika kiuno cha Mercy huku chozi likimdondoka. Mercy naye bila kutaraji, alijihisi kama anaota naye akaichukuwa mikono yake na kuizungusha nyuma ya shingo ya Bryan huku mashavu yao yakiwa yamegusana.Kila mtu alijihisi kama anapaa pasipo mbawa. Mercy almtazama Bryan katika mboni za macho yake na Bryan akafanya hivyo pia.
"Weka midomo yako kama hivi" Bryan alimwambia Mercy huku akiwa ameachama midomo yake, Mercy alifanya kama alivyofundishwa na Bryan na mara midomo yao ikagusana na ndimi zao zikaanza kufanya kazi. Mpaka wimbo wa Phill Collins unaisha, wote wakaachiana na kila mmoja alikuwa anathema pasipo mfanowe.

"Mercy" Bryan alimuita huku akitweta. "Bee" Aliitikia kiuchovu.
"Naomba ugeuke unipe mgongo". Kwa taratibu Mercy katii amri.
Bryan akaanza kumtathimini toka juu mpaka chini. Bryan aliutazama mgongo wa Mercy ulionona kisha akashuka mpaka kiunoni akakwama. Kilikuwa ni chembamba kilichobebwa na mirindimo iliyojazia kama mjaluo, Bryan alijihisi akizidi kusisimka pindi alipoiona michirizi ya paja nyuma ya goti akazidi kuheuka. Alishuka kwenye mguu wa bia ambao ukijumlisha na kiuno unadaka kila aina ya nguo.

Bryan alishusha pumzi nzito na kisha kwa mara nyingine akamshika kiuno vivyo hivyohuku Mercy akiwa amempa mgongo akimkokota kuelekea mahala ambapo kitanda kipo.
Bryan akamsukumia Mercy kitandani, Lakini kabla Bryan hajafanya la kufanya mlio wa honi toka getini ulisikika.

"We Bryan wakina baba hao wamesharudi niache niende nikalale, wakijua nilikuwa huku kwako saa hizi, waweza wakakufukuza nyumbani".
Bryan akamuachia Mercy kiunyonge huku jasho likimtoka, Mercy aliondoka kwa mwendo wa haraka kuendea mlango ili atoke huku akisindikizwa na macho ya Bryan yenye kila aina ya shauku.

Mercy alitoka kwenye chumba cha Bryan na kuelekea chumbani kwake, alipofika ndani alijitupa kitandani, huku akivuta pumzi kwa awamu na mara wazazi wake waliingia ndani na moja kwa moja waliingia chumbani kwao hawakupata shida kufungua mlango kwa vile ulikuwa umerudishiwa tu.

Huku kwa Bryan toka Mercy atoke yeye alivuta shuka na kulala alichokuwa akiwaza kwa wakati ule alikifahamu yeye.


**


Ni asubuhi nyingine tulivu ya siku nyingine baada ya usiku uliopita wenye mkasa ambao haukufanikiwa kufikia tamati kwa sababu ya kukatishwa na honi ya gari la baba'ke Mercy.
Wanafunzi wote walikuwa wapo assembly walikuwa wakijiandaa na mtihani wa Taifa (NECTA) ambao ulikuwa ukitarajiwa kufanyika dakika chache baada ya hapo.
Bryan alikuwepo kaegemea kwenye mlingoti mmoja kati ya mingi iliyokuwepo pembeni ya korido mojawapo iliyokuwako shuleni hapo. Mikono yake ilikuwa katika mifuko yake ya mbele ya suruali macho yake yalikuwa yakitazama miguu yake. Kwa mtazamo wa haraka haraka hakuonekana kuwa katika mood ya kawaida kwani hakuonekana kushughulika na maandalizi ya mtihani kama wenzake. Akiwa katika hali hiyo mara akashtuliwa na sauti ya mtu "Ee bwana kuna barua yako hapa" Alikuwa ni kaka mkuu mkononi amebeba bahasha ya khaki.
Bryan akaipokea na kumshukuru yule head boy kabla hata Bryan hajaanza kuuchunguza ule mwandiko wa juu ya bahasha kengele ya kuingia katika chumba cha mtihani ikagonga.
Hapo Bryan akaanza kuelekea katika chumba cha mtihani
"Kijana unavifahamu vitu vinavyohusika katika chumba cha mtihani" Msimamizi alimuuliza Bryan.
"Ndiyo navifahamu" Alijibu Bryan." Sasa hiyo bahasha inahusikaje na mtihani?"
"Oh! Kumradhi mkuu" Bryan alimtaka radhi msimamizi huyo na kuipeleka barua kwenye maua yaliyokuwamo pembezoni mwa shule na kuiweka hapo na kasha yeye kurudi katika chumba cha mtihani.

Kwa upande wa Mercy alikuwa ni mtu mwenye furaha mno. Furaha yake ilitokana na ndogo yake kuwa na dalili zote za kutimia. Ingawaje ilikuwa bado haijatimia kabisa. Lakini aliamini kabisa ya kwamba ingetimia. Hata alipokuwa katika chumba cha mtihani tukio la jana usiku lilikuwa likimjia na kujirudiarudia katika ubongo wake kiasi kwamba alijikuta haupi tena umakini ule mtihani. Lakini kwa yeye aliamini yuko sahihi.

Mercy alitamani muda wa mtihani ungefupishwa amalize mtihani huo mapema ili apate kumuona tena farijiko la moyo wake kwani alijihisi amemmiss kuzidi maelezo.

Wakati wanafunzi wote wako busy katika vyumba vyao vya mitihani huko nje hali ya hewa taratibu ikaanza kubadilika.

Wingu zito lilitanda angani na hiyo ilimaanisha mvua inaweza kushuka muda wowote kutoka saa ile. Bryan alionekana yuko makini sana na mtihani kama mamba mtoni kiasi kwamba ukimuona utaamini hakosei. Kwa hakika hakufahamu yalo'tarajia kujiri huko nje. Mara akasikia kama harufu ya udongo ulioloweshwa na mvua. Akiwa bado hajapata uhakika juu ya ile harufu mara mvua kubwa ikaanza kunyesha.

Bryan akaikumbuka barua yake aliyoificha kwenye mvua ambayo mpaka muda huo hakuwa akifahamu ilipotoka na wala aliyemuandikia. Bryan alitaka kukusanya mtihani kabla hajamaliza kufanya maswali yote ili akaiokoe barua yake. Lakini zilikuwa zimebakia dakika 4 na maswali alo' kuwa hajayafanya yaliyokuwa takribani kama 7 hivi. Kwa hiyo aliamua kungoja mpaka dakika ziishe.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : PENZI ZITO SEHEMU YA TANO (05)
PENZI ZITO SEHEMU YA TANO (05)
https://1.bp.blogspot.com/-38NnJR4fR2E/XRUKwbDWnfI/AAAAAAAACm0/QH9EEAhZkwMkipb-s4U29lQb7ihHGZfdwCEwYBhgL/s640/PENZI%2BZITO.png
https://1.bp.blogspot.com/-38NnJR4fR2E/XRUKwbDWnfI/AAAAAAAACm0/QH9EEAhZkwMkipb-s4U29lQb7ihHGZfdwCEwYBhgL/s72-c/PENZI%2BZITO.png
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/penzi-zito-sehemu-ya-tano-05.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/penzi-zito-sehemu-ya-tano-05.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy