$hide=mobile

PENZI ZITO SEHEMU YA SITA (06)

PENZI ZITO 6 SIMULIZI ZA JOSHUA / 3 weeks ago SIMULIZI: PENZI ZITO MTUNZI: Prosper Mgowe. MHARIRI JOSHUA SHAO 0713111547 WHATSAPP ...

PENZI ZITO SEHEMU YA NNE (04)

PENZI ZITO 6

SIMULIZI ZA JOSHUA / 3 weeks ago
SIMULIZI: PENZI ZITO
MTUNZI: Prosper Mgowe.
MHARIRI JOSHUA SHAO
0713111547 WHATSAPP


SEHEMU YA SITA​Bryan akaikumbuka barua yake aliyoificha kwenye mvua ambayo mpaka muda huo hakuwa akifahamu ilipotoka na wala aliyemuandikia. Bryan alitaka kukusanya mtihani kabla hajamaliza kufanya maswali yote ili akaiokoe barua yake. Lakini zilikuwa zimebakia dakika 4 na maswali alo' kuwa hajayafanya yaliyokuwa takribani kama 7 hivi. Kwa hiyo aliamua kungoja mpaka dakika ziishe.


**
Muda wa kufanya mtihani ulipokwisha wanafunzi wote walikusanya paper zao na mmoja baada ya mwingine kuanza kutoka nje kwa sababu mvua ilishapungua kwa muda huo. Bryan akili yake yote ilikuwa ni juu ya barua alo'tumiwa ambayo hakufahamu ilipotoka aliiendeea mpaka pale alipokuwa ameiweka. Alipofika na kuangalia barua yake ilipokuwepo nguvu zilimwishia kwani barua hiyo haikutamanika tena ilikuwa imelowa chapachapa. Akaichukua kinyonge na kuifungua lakini hakuambulia kiu kwani wino ulijichanganya changanya mno kiasi kwamba hata jina la muandishi akashindwa kulitambua.


Akiwa bado kasimama na barua yake hiyo mara Mercy akatokea na kumbusu shavuni Bryan akakwepesha
"Why Bryan?" Mercy aliuliza akionesha kusononeka.
"Hapana Mercy si unaona macho ya watu?" Mercy hakujibu zaidi ya kumtazama tu Bryan machoni.
"Enhe Vipi mtihani Mercy?"
"Ah kawaida tu sijui kwa wewe" " Ulikuwa mgumu kiasi chake" Alijibu Bryan " Sasa hiyo barua vipi mbona imelowana? Bryan akaanza tena kumpa kisa kizima mpaka ikawa vile.
"Mi nahisi aliyetuma hiyo barua ni Christer" Aliongea Mercy huku akicheka cheka.
"Hakuna kitu kama hicho" Bryan aliongea huku akijaribu kuamini huenda ni kweli lakini hakuwa na uhakika.


"Hivi Bryan naweza kukuuliza swali?. Uliza tu Mercy" Alijibu Bryan.
" Hivi ni kweli unanipenda" Aliuliza Mercy huku akimtazamaBryan kwa jicho la chati.
" Yaani mno, pengine ni zaidi ya unavyofikiria" Alijibu Bryan huku akimtazama Mercy kwa jicho lilelile la chati
"Mi nahisi kama vile nadanganywa" Aliongea Mercy huku akiwa kamkazia macho Bryan.
"Niamini Mercy" Bryan aliongea hivyo huku nafsi yake ikimnanga kuwa alikuwa akimghiribu Mercy.


* * *
Zilikuwa zimepita siku nyingi baada ya Bryan na Mercy kuhitimu O – level, kwa sasa kila mmoja alikuwa akiyasubiri matokeo ya kidato cha nne kwa hamu zaidi. Katika kipindi hicho chote Bryan na Mercy waliendelea kuishi kama wapenzi lakini hata siku moja hawakuwahi kupata nafasi ya kufanya mapenzi. Sio kwamba hawakupenda iwe hivyo, wote walipenda lakini kwa Mercy ilikuwa zaidi isipokuwa tu Bryan alikuwa akikwepa kwepa kutokana na sababu zake mwenyewe ambazo yeye anaamini ni za msingi.


Sababu ya kwanza hakupenda hata siku moja awe mlangai, asije akamkubalia Mercy ilihali penzi lake lipo deep kwa Chrster; japokuwa hafahamu pa kuonana naye ila imani yake ilimwambia ipo siku watakuja onana.


Sababu nyingine ilikuwa kwamba hakupenda kuwavunjia heshima wazazi wa Mercy ambao kwake yeye aliwachukulia kama wazazi wake wa kumzaa na hakujua awashukuru vipi kwa kumfikisha hapo alipo. Hizo ndizo sababu za kumkwepa Mercy. Isipokuwa alichokuwa akijaribu kukifanya Bryan ni kutomkwaza Mercy na kumfanya muda wote aonekane ni mwenye matumaini Fulani katika maisha yake.


Bryan alifanya hivyo kwa kuhofia kwamba angemuonyesha kwamba hamtaki angeweza kumuanzishia visa vya ajabu ajabu na kumfanya yeye kujihatarishia ajira yake. Bryan aliamini kuwa kwa sababu Mercy ndiye aliyemtafutia ajira pia huyo huyo anayeweza kumkosesha ajira. Hivyo ndio maana Bryan alimpa Mercy respect kwa kuhofia hilo.


Tembea yake, muonekano wake na ongea yake ni dhairi alionekana yeyeni champion. Akiwa ni mwenye makampuni kadhaa ndani ya jiji la Dar es salaam alikuwa na kila alichostahili kuwa nacho kigogo wan chi.


Huyo si mwingine bali ni yule yule Mr Enock Mwansasu, baba mzazi wa Bryan aliyemtelekeza mama yake. Mr Enock Mwansasu alikuwa ni tofauti na mwonekano wake kiundani, ingekuwa ndio kwanza unamuona ungeweza kusema ni mtu wa maana sana ni zaidi ya mstaarabu, mtu anayejali watu sana, kumbe vivyo aonekanavyo sivyo alivyo.
Alikuwa ni mwanaume mwenye kila sifa mbaya, mshenzi, Malaya tena tena asiye na haya. Hakuwa hivyo kabla isipokuwa hayo yote yalitokea baada ya kurejea kutoka masomoni Urusi.
Alishawachezea wanawake kibao tu na kuwatendea visivyo, wengine aliwaghiribu na kufanya nao mapenzi kisha kuwaacha kwa nyodo na matusi kibao, wengine aliwajaza mamba na kuwakana. Hakuwa na mapenzi ya dhati hata nukta na hakuwahi kuzijutia dhambi zake hizo hata siku moja na aliendelea kuvunja sheria kama kawaida, hiyo yote ni jeuri ya pesa.


Alikuwa kaegemea meza iliyo mbele yake. Daftari alikuwa kazifunga alikuwa hatamani tena kuendelea kujisomea. Sio kana kwamba alikuwa amechoka kusoma isipokuwa mawazo yalikuwa yamemtinga mno. Ni christer huyo ndiye alomwandikia Bryan barua ili kumweleza anavyojisikia juu yake lakini mpaka sasa hapakuwa na jibu lolote hicho ndicho haswa kilichomfanya Christer azame katika dimbwi la mawazo kwa muda huo ajiulize maswali mengi. Alijiuliza huenda Bryan hajampenda? Au kanichukulia mimi ni Malaya sana? Kama sivyo hivyo kwa nini sasa aunyanyase moyo wangu? "Lakini najua ipo siku tutaja onana tu" Christer alijifariji lakini aliumia sana moyo na hakujua afanye nini kwa muda huo.
"Dah Ama kweli penzi kizungumkuti" Alijisemea Christer.
Zilipita siku kibao, sasa hakutaraji tena kupokea barua kutoka kwa Bryan kwani alishasubiri vya kutosha na sasa ameshachoka.


Ilikuwa ni jumamosi Christer alikuwa akitoka katika majengo ya Library ya mkoa na kuelekea maeneo ya Zuny Ice cream kupoza koo, Alipofika zuny alitafuta sehemu moja ambayo haikuwa na mtu ndipo akakaa, akaagiza juice na keki mbili. Baada ya vitu vilivyoagizwa kuletwa akaanza kunywa juice kwa taratibu lakini mara kabla hajaanza kumega keki alijihisi kijasho chembamba kikimtoka na midomo ilibaki wazi huku akiwa ameshika kipande cha keki mkononi.
Akajihisi amefreeze kwani kila kitu mwilini mwake alikihisi akifanyi kazi kama kawaida. Hiyo yote ilisababishwa na kile ambacho alikuwa akikitazama mbele yake.
Alikuwa amemuona mvulana ambaye alikuwa amemtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio na hatimaye sasa amemuona pasipo kutarajia.
Ama kwa hakika akili ya Christer aliamini kabisa yule kijana aliyekuwa ametazamana naye, aliyekuwa amekaa mbele ya meza yake akinywa juice alikuwa ni Bryan, lakini cha ajabu na cha kushangaza huyo kijana ambaye christer aliamini kuwa ndiye Bryan alionekana kutomfahamu hata chembe binti aliyeko mbele yake.
Wakati Christer anatafuta pozi la kumuingia yule kijana, lakini hakuonekana kuwa na wazo lolote juu ya yule binti ambaye yeye hakumfahamu kabisa.
Christer akajiinua kutoka sehemu ambapo alikuwa amekaa na kwa hatua za hesabu akaanza kmuelekea yule kaka.
"Habari yako kaka" Christer alimsabahi kwa sauti ya utulivu.
"Safi tu dada'ngu karibu" alijibu yule kaka kwa sauti ya chini. Christer alimuangalia yule kaka usoni kwa sekunde kadhaa na kisha akakunja uso kidogo na kuachia hali ya kawaida kwa wakati huo kulikuwa na mawazo mawili katika kichwa chake yanayopingana. Wazo moja likikubali kuwa yule kaka alikuwa ndiyo Bryan halisi lingine likakataa kwamba yeye siye. " Sijui tunaweza kujumuika pamoja?" Christer aliuliza. " Hiyo tu haisumbui, unaweza mrembo ukakaribia" Alijibu yule kaka kwa sauti isiyo na kutetereka.
Christer alishukuru na kuhamishia vitu vyake kwenye meza ya yule kaka ambaye mpaka wakati huo hakujua anaitwa nani.
"Okey" may be nafikiri tungeanza kwa utambulisho, " Sifahamu mwenzangu unaitwa nani?" Alianza yule kaka kwa kumswali Christer. Naye Christer alimjibu kama ifuatavyo;
"Najua sura sio ngeni kwako hata ya kwako siyo ngeni kwangu lamda nikukumbushe tu, ni kwamba mimi naitwa Christerbey".
Yule kijana alimuangalia christer usoni kwa utafiti huku akijtahidi kuvuta kumbukumbu kama amewahi kumuona sehemu na kisha naye akasema
"Nashukuru kukufahamu christer kwa upande wangu mimi naitwa Lone"
Christer alishituka kidogo ni dhairi alikwishagundua ameingilia mlango wa kutokea, kwani alifananisha kwenye hamna. Kuanzia hapo Christer alianza kumtazama Lone kwa sura tofauti na kwa udadisi zaidi. Lakini kilichompa maswali na kumfanya achizike zaidi ni vipi Bryan na Lone wafanane kiasi kile?
"Na kuhusu kuonana kabla huenda ametufananisha" Lone aliendelea. " Oh, samahani ni kweli hatukuwahi kuonana kabla nilikufananisha tu." Alijihami Christer.
"Haina shida sana" Lone alimpoza kutoka muda huo kila mmoja aliendelea kunywa na kula pasopo kusema neno.
Zilipita takribani dakika 7 ukumya ukiendelea huku kila mmoja akimuangakia mwenzake kwa jicho la wizi na kisha Christer akavunja ukimya.
"Vipi Lone mbona kimya?"
"Ah, mi nakusikiliza wewe". Lone alijibu kwa kubabaika kidogo. "Hivi Lone unaishi maeneo gani?" Christer alimswali Lone.
Mimi nimefikia Bahi road kwa aunt yangu mmoja hivi lakini mimi ni mzaliwa wa Dar-es-salaam"
"Okey nashukuru kufahamu hivyo". Christer aliongea. Lone kwa ghafla bila hata yeye kutarajia alijihisi anahisia nzito sana za mapenzi juu ya Christer, tatizo ni jinsi ya kuanza kumueleza, je, aanze na step ipi, lakini alijiamini hawezi akamuacha kiumbe huyo wa uzao wa Eva hivihivi.
"Hivi ni kweli nimuache mtoto mzuri kama huyu hivihivi? No" haiwezekani.
Aliwaza Lone huku akimuangalia Christer usoni kwa macho yenye mng'ao.
Christer alipomuangalia Lone machoni alihisi moyo wake umelipuka kwa furaha, kwani alihisi ni kama nuru flani katika maisha yake na mara Christer akachana bonge la tabasamu. Lone alipomuangalia christer alijiuliza maswali mengi. "Huenda ameshayasoma mawazo yangu?" Au lamda ndo pozi lake? Lone alishindwa kupata jibu kamili. "Enhe Christer hivi unasoma wapi vile? "Lone alianza tena kumdodosa maswali" Nasoma Msalato Girls" alijibu Christer.
Kidoato cha ………."" Tatu" Alimalizia Christer
Lone alichukua glasi yake ya juice na kunywa funda moja wakati Lone akifanya hivyo Christer glas yake alikuwa akiigongesha gongesha kwa taratibu kwenye meno yake.
Wakati vitendo hivyo vikiendelea kila mmoja alikuwa akiwaza la kumwambia mwenzake
"Nikwambie kitu" kila mmoja alimwambia mwenzake kwa pamoja.
Pia wote wakacheka nakisha Christer akasema "ungeanza wewe kuniambia hicho kitu"
"Hapana nafikiri ungeanza wewe kwanza" Lone alimbishia Christer" Hapana ungeanza wewe kwanza kwa sababu baba ni kichwa katika ………….."


"A, ah Unafahamu kwamba Ladies first? Ukishalijua hilo nafikiri kutakuwa hakuna tena ubishi. Aliongea Lone.
Sawa umeshinda Lone, na nimekubali kushindwa" Aliongea Christer akikubali kushindwa, "Haya anielezee hicho kitu chenyewe" Aliongea Lone kwa usongo.


"Sa'skiza Lone nina vitu vingi sana vya kuongea na wewe" aliongea Christer na Lone akadakia " Ehne cha kwanza"" Ungeanza wewe" Na cha pili"" Si ukishamaliza wewe?" Alijibu Christer na wote wakacheka.
"Acha usanii wako Christer mimi niko serious aliongea Lone.
S'kiza Lone naona muda unatutupa mkono, sasa cha kufanya naomba kama bado upo Dodoma hii naomba Jumamosi unijie shule, nitakuwa free! Aliongea Christer.


Okey nitafanya hivyo kikubwa tuombe uzima" alisema Lone. Wote wakaamka wakainuka vitini na kabla ya kuondoka Lone aliongea.


"Naomba nikukiss kama hutojali" Christer aliguna kidogo kisha akasema" Okey you may" huku akicheka cheka.
Lone alimchumu Christer shavuni naye Christer alifanya hivyo.
"Thank you" alisema Christer
"You too" alijibu Lone"
Baada ya hapo wote waliagana kwa miada ya kuonana tena Jumamosi.


**
Ni siku nyingine tena baada ya siku nginyi kupita Bryan na Mercy walikuwa wakitokea maeneo ya Internet café kutazama matokeo yao na kila mmoja akilini mwake alikuwa anawaza lake na mara Mercy akaanzisha maongezi.
"Bryan" Mercy aliita.
"Sema Mercy" Alijibu Bryan akionekana kushtuka kidogo, hiyo inaashiria kwamba alikuwa katika lindi la mawazo.


"Matokeo ndio kama hivyo tulivyoyaona, sasa mwenzangu unashauri kitu gani?" Aliongea Mercy. "Ngoja kwanza Mercy tuyafikishe kwa wazazi ndipo tuyajadili iweje". Aliongea Bryan.
Kiukweli ni kwamba matokeo ya Bryan yalikuwa mazuri kuliko ya Mercy. Kwa sababu Mercy alipata 0 na Bryan alipata one ya point saba.
Walipofika nyumbani waliwaeleza wazazi wao yaliowajiri kwa siku hiyo.
Wazazi wao hawakufurahishwa na matokeo ya Mercy japokuwa walikuwa wakiamini binti yao ataendelea kusoma kwa njia moja au nyingine. Lakini pia walimpa pongezi nyingi sana Bryan kwa kufanya vizuri.
"Hongera sana Bryan, hongera baba" Walimpongeza baba na mama Mercy kwa kumpa mikono. Mercy akiwa na majonzi chungu mbovu na machozi kibao yakimtiririka kwa vile alivyouvurunda kwenye mtihani na asijue nini cha kufanya.
"Oooh, mwanangu Mercy usilie hivyo ni bahati mbaya tu, kwani hakuna mtu anayesoma kwa malengo ya kufeli. Isipokuwa ni bahati mbaya tu" Mama Mercy alijitahidi kumfariji mwanaye na kumuhaidi asivunjike moyo kwani ataendelea kusoma kwa namna yeyote ile.


Ilikuwa ni jumamosi ya kutimiza agano. Christer aikuwa nje kidogo ya maeneo ya shule akimngojea Lone. Mara baada ya nukta kadhaa akaona taksi moja ya kijivu ikimjia upande wake na kusimama pembeni yake kidogo na vioo vikashushwa. "Hi" ilisikika sauti ya Lone kutoka ndani ya gari.
"Hallow" alijibu Christer huku akichanua tabasamu.
"Ingia twende dada" Aliongea taksi driver. Christer alifungua mlango wa nyuma na kujitoma ndani na moja kwa moja safari ikaanza mpaka WIMPY wakashuka Lone na Christer na yule taksi driver akapewa chake na kupotea. Waliingia wimpy na kuchagua sehemu tulivu na kuketi. Waliagiza makulaji na mazungumzo yakaanza.
"Enhe za tangu kuachana" alianza Lone.
"Ah nzuri tu, sijui wewe" Alijibu Christer. Mimi heri tu"alijibu Lone. "Nimefurahi kukuona" hukuakimtazama usoni aliongea hayo Christer.
"Hunishindi mimi Christer" alijibu Lone. Christer alimuangalia Lone.
Christer alimuangalia Lone toka chini hadi juu nab ado isitoshe kummaliza, alirudia tena na tena mpaka na tena lakini bado aliona macho yake yakimdanganya nab ado alitamani aendelee kumuangalia hivyo tena na tena. " Vipi Christer mbona unaniangalia hivyo" Ilimbidi Lone aulize baada ya kushtukia kwamba vile aangaliwavyo sivyo.
"Unajua Lone kunamtu nakufananisha naye yaani hivyo ulivyo naye pia yuko hivyo hivyo ndio maana nakuangalia sana".
"Anaitwa nani huyo mtu?" Alizidi kuhoji Lone. "Kuna kaka flani anaitwa Bryan yaani mnafanana sana ama kweli nimeamini duniani wawili wawili"
"Lo aisee" Lone aliishia kuguna na kuyapuuza kwani hayo yalikuwa hayamuhusu sana na zaidi hayakuwa na faida kwake hivyo akayaacha kama yalivyo.
"Enhe" Christer nafikiri huu ni muda muafaka wa kuangalia kilichotuleta sasa nakusikiliza" Aliongea Lone.
"Unajua Lone katika maisha ya binadamu huwa anafanya au anatafuta kitu ambacho kitamfanya afarijike na ajisikie kujazika kama sio kukamilika alimradi ajisikie furaha". Aliongea Christer. "Yaani unamaanisha kwamba…….." Alidakiza Lone.
Kabla ya kuendelea Christer alinyamaza kwa muda na kumtafiti lone machoni ataupokea vipi ujumbe anaotaka kumwambia Lone.
"Nakusikiliza", aliongea lone. "Lone samahani kama nitakuwa nimeenda wrong na kile nitakachokwenda kukieleza kwako, lakini kiukweli mimi nafanya kama moyo unavyonituma"
"Enhe endelea" aliongeza Lone. "Ilove you Lone in a million reason" aliongea Christer huku sura yake ikiwa imevaa huzuni Fulani hivi.
"Wooooow so thanks u'r ma' sweet sex lady" Aliongea Lone na kumkumbatia Christer huku usoni mwake kukiwa na tabasamu la butwaa.
"I'll be your light shining bright "Aliongeza Lone. Baada ya hicho kikao cha dharula kwisha wote walinyanyuka na kwenda kituo cha taksi.
"Eh bwana suka tufikishe bahiroad" Lone alimwambia dereva.
"Okey buku mbili" "Haina shida" alikubali Lone.


Ilikuwa ni majonzi na simanzi mtimani mwa Mercy kwani alijua siku si nyingi Bryan ataondoka kwenda Tabora alipopangiwa kwenda kusoma masomo yake ya Adivance na kwa upande wa Bryan ni hivyo hivyo kwani alishindwa kuimagine maisha yake bila Mercy.
"Mercy usihuzunike sana kwani safari sio kifo naenda masomoni tu halafu nitarudi" Bryan alimfariji Mercy.
"Itanichukua muda mrefu sana Bryan mpaka nije kuizoea khali ya ukiwa" Aliongea Mercy huku machozi yakimlengalenga.
Alitamka Bryan alikuwa ndani ya taksi akielekea stendi kuu ya mkoa akisindikizwa na Mercy pamoja na mama Mercy.
Walipofika katika kituo cha basi Mizigo ya Bryan ikashushwa katika basi linalokwenda Tabora. Mama Mercy alimuaga Bryan kwa huzuni na kumtakia kheri katika masomo yake.


Muda wote ambapo mama Mercy alikuwa akiagana na Bryan Mercy alikuwa kasimama nyuma ya taksi huku machozi yakimtiririka pasipo kukoma. Huzuni alokuwa nayo haikumithilika alitamani sana aondoke pamoja na Bryan lakini haikuwezekana alishindwa kupata picha ya maisha yake bila Bryan, alihisi hayatokuwa maisha. Mercy akiwa katika hali hiyo mara honi ya basi analotakiwa apande Bryan ilipigwa.


"We Mercy njoo umuage kaka yako haraka, basi linaondoka" mama Mercy aliongea bila kufahamu mwanaye yupo katika mood gani kwani wakati ule na alipomuangalia usoni alimuona akibubujikwa na machozi.
"He we mwenzetu vipi?" Aliuliza mama Mercy.
"Unaumwa?" Alizidi kudadisi
"Mh mh?"
"Umeibiwa?"
"Mh mh?"
"Sasa tukuelewe vipi? Alizidi kuhoji mama yake.
"Mama Bryan, Bryan ananiacha mama peke yangu mama" Aliongea Mercy huku akilia kilio cha kwikwi
"He, kwa hiyo hutaki aende shule abaki na wewe tu"mama Mercy aliuliza na Mercy hakujibu.
"Mercy" aliita Bryan
"Abe" aliitika kama anadeka hivi
"Kwa heri Mercy , Aliongea Bryan kwa huzuni.
Mercy hakujibu lolote isipokuwa alizidi kumuangalia Bryan kwa macho yenye mjao wa machozi.


Umbali waliokuwa wamesimama kati ya Bryan na Mercy ni kama hatua nane hivi Bryan alitamani sana amkumbatie Mercy lakini alimuheshimu Mama yake Mercy.


Bryan akampungia mkono wa kheri Mercy na kugeuka kuanza kuielekea basi.
Kwa kasi ya ajabu Mercy alianza kukimbia kumuelekea Bryan alipo na alipomfikia alimkumbatia kwa nguvu zote pasipo kumuogopa mama yake.


Kichwa cha Mercy kilikuwa kifuani kwa Bryan, huku akikilowesha kifua cha Bryan kwa machozi ya huzuni.
"Bryan naomba usinitupe, popote uwapo naomba usinisahau" Aliongea Mercy kwa masikitiko.
"Siwezi kukusahau Mercy kwani wewe ndio mhimili wangu" Aliongea Bryan kwa sauti ya chini
"Nakupenda zaidi ya sana na nakutakia maisha mema" Naye Bryan alimaliza.


Waliachana na Bryan akamtazama kwa aibu mama aliyekuwa kaegemea taksi akiwatazama na kumpungia mkono wa mwisho mwisho.
Bryan alitoka mbio kuelekea basi ambalo lilishaanza kuondoka na kuingia ndani.
"Mr, naona ulishachizika na mtoto, ukasahau kabisa kama unasafari". Konda alimtania Bryan, Bryan hakujibu zaidi ya kucheka tu.


Alienda mpaka kwenye seat yake ya dirishani na kisha akaketi.
Basi lilizidi kujongea huku nje mama Mercy alizidi kumpungia Bryan mkono pamoja na Mercy aliyekuwa kakiuma kidole chake cha shahada cha mkono wa kushoto huku mkono wa kulia ukimpungia Bryan kwa taratibu mpaka basi lilipoondoka kituoni hapo. Baada tu ya basi kutoweka Mercy aliangua kilio kilichowashtua hata watu wengine waliokuwako kituoni hapo.


***BRYAN anaenda masomoni………umbali kati yake na Mercy unajengeka……..

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,149,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,196,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,110,FIFA.com - Latest News,15,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,11,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,207,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,39,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : PENZI ZITO SEHEMU YA SITA (06)
PENZI ZITO SEHEMU YA SITA (06)
https://1.bp.blogspot.com/-38NnJR4fR2E/XRUKwbDWnfI/AAAAAAAACm0/QH9EEAhZkwMkipb-s4U29lQb7ihHGZfdwCEwYBhgL/s640/PENZI%2BZITO.png
https://1.bp.blogspot.com/-38NnJR4fR2E/XRUKwbDWnfI/AAAAAAAACm0/QH9EEAhZkwMkipb-s4U29lQb7ihHGZfdwCEwYBhgL/s72-c/PENZI%2BZITO.png
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/penzi-zito-sehemu-ya-sita-06.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/penzi-zito-sehemu-ya-sita-06.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content