PENZI ZITO SEHEMU YA SABA (07) MWISHO | BongoLife

$hide=mobile

PENZI ZITO SEHEMU YA SABA (07) MWISHO

PENZI ZITO SEHEMU YA NNE (04)

penzi zito mwisho

SIMULIZI ZA JOSHUA / 3 weeks agoSIMULIZI: PENZI ZITO
MTUNZI: Prosper Mgowe.
joshua shao
0713111547 whatsappSEHEMU YA MWISHO​Basi lilizidi kujongea huku nje mama Mercy alizidi kumpungia Bryan mkono pamoja na Mercy aliyekuwa kakiuma kidole chake cha shahada cha mkono wa kushoto huku mkono wa kulia ukimpungia Bryan kwa taratibu mpaka basi lilipoondoka kituoni hapo. Baada tu ya basi kutoweka Mercy aliangua kilio kilichowashtua hata watu wengine waliokuwako kituoni hapo.


Mama Mercy alimkumbatia mwanaye kwa nguvu na kumtuliza na kisha wakaingia ndani ya taksi na kurudi nyumbani.


Lone alikuwa ni mtoto wa Mr Enock Mwansasu (Baba yake Bryan) Isipokuwa yeye Lone alizaliwa na mama tofauti na mama yake Bryan.


Mimba ya Lone ilitungwa kipindi Mr. Enock alipokuwa Chuo Kikuu mwaka wa kwanza, kipindi hicho alipokuwa ameenda Sanawari Arusha pamoja na wanafunzi wenzake kufanya project. Ndipo siku moja alipokutana na Esnaty msichana mrembo ndipo Mr Enock alipomuelezea hisia zake naye Esnaty bila ajizi alimridhia na baada ya maridhiano ikawa kweli wakamake Love.


Kiukweli Mr. Enock hakumpenda Esnaty ile deepest zaidi isipokuwa alichokihitaji kutoka kwa Esnaty ni short time Love na baada ya Mr Enock ku make love na Esnaty alimbwaga na kuendelea na shughuli zake zilizomleta Arusha mpaka kurudi tena College. Hakuwahi kuonana tena na Esnaty hata alipoondoka na hakuna hata mmoja kati ya wao aliyekuwa na contact na mwenzake.


Mr. Enock hakumpenda kumpa nafasi Esnaty nafasi katika moyo wake kwa sababu alikuwa na mchumba huko Dodoma ambaye malengo yake ni kuja kuwa mke wake na mchumba huyo ndiye mama yake na Bryan. Hata hivyo Mr Enock alijutia sana tendo alilofanya na Esnaty kwa kujua alikuwa amemsaliti mchumba wake hata hivyo ilikuwa siri yake na alitubu moyoni mwake.


Kwa upande wa Esnaty baada ya masiku tele kupita akaanza kujihisi ni mjamzito na alipokwenda hospitali kupima kweli alikutwa ni mjamzito.


Siku, miezi ikazidi kukata na mara siku za kujifungua zikakaribia. Ni siku hiyo Esnatry alipougua uchungu nakukimbizwa Hospital na kufikishiwa wodi ya wazazi.
**
Katika vipimo vya daktari vilionyesha ya kwamba mtoto aliye tumboni ni mkubwa na hawezi kupita kwa njia ya kawaida kwani mlango wa uzazi wa Esnaty ni mdogo na hata wangejaribu kumzalisha kwa njia yabomba isingewezekana kwani wangemharibu mtoto na angeweza kuwa taahira au mgonjwa wa kifafa.


Hivyo njia mbadala walioiona madaktari ni kwenda kumfanyia Operation.
Operation ilifanyika na hatma ya yote mtoto alitoka salama ambaye ndiye Lone na kwa bahati mbaya Esnaty alipoteza maisha.


Hivyo Lone hakuwahi kumuona mama yake alilelewa na bibi yake pamoja na watu baki tokea udogo wake. Maisha waliyokuwa wanaishi katika Mji wa Arusha hayakuwa ya hali ya juu wala ya chini kabisa isipokuwa yalikuwa standard level.


Maisha yalizidi kwenda na umri wa Lone ulizidi kuongezeka alianza shule ya msingi na hata Sekondari.


Alipomaliza kidato cha nne matokeo hayakuwa mazuri na ndugu zake uwezo wa kumsomesha shule za private hawakuwa nao.


Siku moja usiku Lone alikuwa amepumzika chumbani kwake akaanza kukumbuka background ya maisha yake. Hakuelewa imekuwaje mpaka aanze kufikiria mambo yalopita katika maisha yake. Alijaribu kumImagine mama yake alifananaje lakini katu hakupata picha. Alijaribu kumkumbuka baba yake lakini wapi tena hakuwa hata na idea yake. Sio siri Lone aliumia sana na hata machozi yakamtoka na mwisho akapata wazo kuwa labda ajaribu kumtafuta kupitia vyombo vya habari kwani ilisadikika kwamba bado yuko hai.


Siku zote Lone alichokuwa akikiwaza ndicho alichokuwa akikifanya. Hivyo alisambaza matangazo magazetini na hata redioni na kisha yeye akatulia kusubiri matokeo ya matangazo yake.


Kwa bahati nzuri Lone alifanikiwa kumpata baba yake kwa kujulishwa kwa kupitia vyombo vya habari kwamba baba yake yupoDar –es – Salaam. Lone alifurahi sana kwa adhma hiyo kufanikiwa na alifurahi zaidi pale alipogundua kwamba baba yake aliishi Dar –es Salaam kwani toka zamani alikuwa akipenda kuishi Dar japokuwa hakupafahamu.


Ndugu zake walimchangia fedha kwa ajili ya nauli na zilipotimia Lone akasafiri kutoka Arusha kuja Dar –es Salaam. Mr. Enock alifurahi sana kukutana na mwanae na mwanae kadhalika. Lakini shughuli ilikuwa kwa mama"ke mdogo Lone. Damu zao zilikuwa tofauti hazikupatana hata nukta.


Kwa muda wa wiki mbili tu Lone alishachoshwa na visa vya pale kwao. Alishatukanwa sana, alishanyanyaswa sana, alishasingiziwa mambo kibao. Lakini hayo yote alipomwambia baba yake, wala hakuyatilia uzito wowote yeye jibu alilotoa ni kwamba huyo ndiyo mama yako na hivyo ndivyo jinsi alivyo kwa hiyo yakupasa umzoee.


Majibu hayo yalimnyong'onyeza Lone mpaka ikafika hatua akawa haipendi nyumba ile pamoja na waliomo humo japokuwa alikuwa na kila kitu ndani na hapo ndipo akawaza kutoroka kwenda Dodoma, kwa sababu aliwahi kusikia tetesi kwamba kuna shangazi yake yupo Dodoma; Lakini kabla hajaondoka alimuachia ujumbe Baba yake kwamba yeye ameondoka nyumbani na amekwenda Dodoma na hataki mtu yeyote amfuate kwani amechoshwa na maisha ya pale nyumbani kwake.


Na ilimuuma roho sana kwa sababu hakuwahi kufikiria kama kuna baba wa aina ile, tabia yake haieleweki wala hajali utu wa mtu licha ya mtu baki hata mwanae wa kumzaa alishindwa kuelewa yule ni baba wa aina gani.


Lone alipiga safari hadi Dodoma na kuanza kazi ya kumuulizia shangazi yake kwa bahati nzuri alimpata alikuwa akiishi bahiroad.


Kiuwezo shangazi yake huyo alijaliwa nyumba kubwa yenye kila kitu ndani na gari dogo moja kwa ajili ya kutembelea (yote hayo aliyafanya kwa juhudi zake binafsi) hakuwa na mume wala bwana.


Lone alipofika alipokelewa vizuri na shangazi yake huyo. Baada ya salamu na utambulisho. Lone alieleza mkasa mzima toka alipokuwa Arusha, Dar –es – Salaam mpaka wakati huo yupo Dodoma.


"Hilo ndio tatizo la kaka'ngu sijui ameshachanganjikiwa na maisha? Maana hashauriki wala haonyiki, dharau tu zimemjaa sijui anafikiri hiyo mimali atakufa nayo" Aliongea kwa uchungu shangazi yake Lone.


"Mwanangu Lone"
"Naam shangazi"
"Usiwaze sana hayo yote ni mapito tu ya maisha wewe kaa hapa kuwa huru nitaishi na wewe kama mwanangu"
"Asante sana shangazi"
Huo ndio ukawa mwanzo wa Lone kukaa kwa shangazi yake.


Walipokuwa njiani kuelekea Bahiroad Lone na Christer, mmoja wao akatoa kauli iliyomshangaza mwenzie.
"Dereva simamisha gari" Aliongea Christer, Lone alishangazwa na kauli ile.
"Kwani vipi Christer" Lone alihoji.
Samahani Lone huko Bahiroad sitoweza kwenda kwenda"
"Kwani vipi Christer?" Lone aliuliza kwa mshangao.
"Kwani huko bahiroad tunaenda kufanya nini Lone" He swali gani tena hilo Christer?"
"Hapana haiwezekani" Christer alijibu.
"Hapana nini" nitachelewa kurudi shule lamda tupange siku nyingine"
Lone hakuwa na lakufanya ilibidi amuamrishe dereva kwa shingo upande ageuze gari na amrudishe Christer shule.


Nyumbani kwa akina Mercy, Mercy alikuwa mwenyemajonzi tele mtimani pamoja na uchungu mwingi wa kuachwa pekee, Mercy aliona kama dunia imemgeukia kwani kilichokuwa chini ya jua kwake alikiona ni bure.
Hata rafiki zake walipokuja walomboa tu. Faraja pekee alokuwa akihitaji katika maisha yake ni Bryan tu. Takribani kama wiki tatu sasa tangu Bryan aondoke kwenda shule, Mercy alikuwa yupo katika hali mbaya mno. Kwani siku zote yeye alikuwa ni mtu wa kulia kucha kutwa na kulala tu. Kuna muda Mercy alighafirika hata kula yote hiyo ni sababu ya mawazo juu ya Bryan kiukweli Mercy alitia huruma sana.


Wazazi wake walipogundua binti yao yupo katika hali hiyo, Walifanya maamuzi ya kumtafutia sehemu yenye mchanganyiko wa watu tofauti ili kuchelea binti yao asije kuharibikiwa kisaikolojia. Hivyo walifanya hima katika hilo na kuamua Mercy akasomee mafunzo nursing huko Mvumi.


Taratibu zilifanywa na hatimaye Mercy akaenda Mvumi. Japokuwa Mercy alikuwa huko na akakutana na watu wa aina tofauti tofauti lakini Mercy alijihisi kumpenda sana Bryan na alihisi kutomsahau kamwe. Ilikuwa haipiti saa kwa Mercy pasipokumkumbuka Bryan.


Hali kadhalika kwa Bryan hali ilkuwa ni hiyo hiyo, hakuna saa linaloisha bila kumbukumbu za Mercy kupita ubongoni mwake, lamda akilala na hata hivyo alalapo, ndoto si chini ya ishirini katika usiku mmoja ziingiazo zinazomhusu Mercy. Ama kwa hakika watu hawa walipendana sana japokuwa mapenzi yao yalikuwa na utofauti.


Mr Enock baada ya kukuta ujumbe ulioachwa na Lone, aliusoma na kuupuza, "Ah, shauri lake" ndivyo alivyojisemea Mr Enock.
Lakini kila siku zilipozidi kukata alihisi kitu Fulani kikimhimiza kwamba amfuatilie Lone.
Ilikuwa imeshapita miezi takribani tisa hivi tangu Lone aondoke Dar-es- salaam.
Ni asubuhi moja tulivu. Mr Enock akiamka akiwa tofauti na siku zote. Aliingia bafuni akajimwagia maji chapchap na kisha kuingia chumbani kwake, alichagua suruale moja nyeusi na shati la bluu na viatu vyeusi vilivyobinuka mbele pamoja na miwani yake nyeupe.


Alivivaa na kisha akachukua koti lake jeusi na kuliweka begani funguo za gari mkononi. Alitoka chumbani kwake na kuelekea jikoni alipo mkewe.
"Hello mama watoto" Aliita Mr Enock,
"Sema Mr"
"Naenda Dodoma asubuhi hivi nimemkumbuka sana mwanangu Lone" "Halooooo unalo hilo utajiju mwenyewe na misafara yako ya ajabu ajabu eti nimemkumbuka mwanangu, katika watoto yule naye mtoto" Aliongea Mrs Enock.


"Usitake kunitibua asubuhi asubuhi we mwanamke unasikia? Yule mtoto ni damu yangu lazima nimfate huko aliko." Aliongea kwa jazba Mr. Enock.


"Mh mh" mkewe aliguna kishambenga" Umesikia we mwanamke nikirudi sitaki kukukuta humu ndani kuanzia muda huu kusanya kila kilicho chako halafu upotee, kwanza una bahati ya kuishi na mimi miezi yote hii "Aliongea Mr. Enock kwa jazba zaidi.


"Nisamehe …….."
"Hakuna ndo nimeshasema" Mr. Enock alisema na kufunga mlango kwa nguvu. Baada ya hapo aliingia ndani ya Lexas na kutia moto gari na kutoweka.


**
Lone alimsindikiza Christer hadi shuleni huku akilalama alivyomfanyia haikuwa fair. Walimshusha Christer kwa miadi ya kuonana tena wiki mbili mbeleni na wao wakageuza kurudi mjini. Ukweli ni kwamba kilichomfanya Christer aghaili safari ya kwenda Bahiroad ni kwamba alihisi dhamira yake ikimsuta kwamba alikuwa bado akimpenda Bryan kuliko Lone hiyo ndiyo sababu iliyomfanya aghaili.


Lone alipofika nyumbani kwao alihisi macho yake yakimuwasha na kutoa machozi pengine ni kwa ajili ya hali ya hewa ya vumbi la Dodoma lakini hakuwa na uhakika zaidi.


"We Lone" shangazi yake aliita. "Naam shangazi" Lone aliitika.
"Huko ndani unafanya nini sasa hivi?
"Nimelala" "Kisa?"
"Macho yananiuma shangazi"
"He mara hii, itakuwa vumbi la Dodoma kesho uende Mvumi ukapime yasije yakawa matatizo makubwa"
Sawa shangazi"
Asubuhi yake alimsindikiza Lone mpaka stendi ya mabasi ya Mvumi. Walipofika shangazi alimkabidhi kiasi cha fedha kwa ajili ya matibabu na chakula na baada ya hapo waliagana na kila mtu akatawanyika.


**
Lone alipofika hospital ya Mvumi alipata matibabu na kuandikiwa baadhi ya dawa. Macho yake aliambiwa hayahitaji miwani kwani matatizo hayakuwa makubwa sana. Lone aliwashukuru wahudumu wa pale na kuanza kuondoka. Alipofika kwenye lango la kutokea nje akakutana na binti mmoja aliyekuwa kavaa sare za kiuguzi. Lone hakuelewa kama yule binti ni Nesi kamili au mwanafunzi tu. Lone alipomuangalia usoni alikili ustadi wa Mungu. Kipindi chote hicho Lone alipokuwa akimtathmini mwanadada huyo yeye alikuwa akija upande wa Lone huku kichwa chake kimelazwa shingoni upande na macho yakiangalia chini.


Walipokaribiana huku dada huyo hajajua aliyeko mbele yake, Lone akajikuta akimshika mkono kwa vile walipishana kwa karibu mno.


"Hello mrembo mambo" Lone maneno yalimtoka. Mercy aliinua macho yake kumtazama aliyekuwa akimsalimu.


"Waoooow Brya…. "Aliyesema hivyo si mwingine bali ni Mercy na kisha kwa ghafla akasita na kumuangalia Lone kimkazo zaidi. Hakuna aliyeongea neno zaidi ya kumtazama tu, na mara baada ya nukta kadhaa Lone akavunja ukimya.


"Hallo baby naomba dakika chache tu nizungumze nawe kama hutojali" Lone alimwambia Mercy huku mikono yake akiwa ameikusanya pamoja hiyo ilimaanisha kumplease Mercy.


Mercy alishusha pumzi ndefu badala ya kujibu na hakujibu kitu zaidi ya kutingisha kichwa kuashiria kukubali ombi la Lone na kwa pamoja walibadili mwelekeo sehemu moja.


Walielekea sehemu moja iliyotulia yenye majani ya kijani kibichi pamoja na baadhi ya maua pamoja na miti mingi ya kivuli palivutia sana.


Walitulia chini ya mti mmoja wa kivuli wakiwa wamekaa ilihali kila mmoja kumface mwenzie Lone alianza kwa kusema.


"Naomba nikufahamu jina lako"
"Naitwa Mercy" Alijibu kwa kifupi"
"Nashukuru kukufahamu U-binti na jina lako ni zuri pia.
"Asante" Alijibu kifupi pasipo mazungumzo ya nyongeza.
"Naitwa Lone japokuwa hupendi kufahamu jina langu"
"Asante" Mercy alijibu.
Kiukweli Mercy alikuwa katika dimbwi la mawazo akimtafakari Lone. Alikuwa akijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu iweje Lone afanane na Bryan kiasi kile?
Pia Lone alishtuka pale Mercy alipotaka kulitaja jina lake kama Bryan japokuwa hakutaka kuonyesha mshtuko wake dhahiri.


Aliwaza huenda huyo Bryan ni mtu maarufu sana japokuwas hakufahamu huo umaarufu wake unatokana na nini. Huenda ni kicheche sana au anafedha zaidi au ni handsome kuliko, lakini potelea mbali mi hayanihusu sana.


Hayo yote Lone aliyawaza
Kwa pamoja wote wakarudi katika mood sawa. "Lone" Aliita Mercy kwa sauti ya upole.
"Naam Mercy"
"Bryan huwa mnawasiliana naye" Mercy aliuliza akiwa na uhakika Lone anafahamiana na Bryan.
"Bryan ndio nani?"Lone aliuliza. "Kwani wewe unaitwa Lone nani?"
"Mi naitwa Lone Enock Mwansasu" "Na ‘mi namuulizia Bryan Enock Mwansasu"
"He mi mbona sifahamu kama nina ndugu wa namna hiyo hebu naomba unipe historia yake angalau kwa ufupi". Mercy akamueleza kila kitu isipokuwa juu ya uhusiano wao. Na Lone akafanya vivyo hivyo kamueleza Mercy juu ya historia yake.


Kila mmoja alisikitishwa na stori ya mwenzake na kila mmoja alimpa pole mwenzake. Kwa sasa Lone alikuwa akifahamu Bryan ni nani japokuwa hakuwa akimjua lakini alitamani siku moja akutane nae na hilo aliamini itakuja tokea.


"Kwa hiyo wewe na Bryan nani senior na nani junior?"Mercy aliuliza.
"Mimi itakuwa ndiye senior" Alijibu Lone.
Kwa kila jicho la Mercy lililomtazama Lone hakika halikuona tofauti na Bryan.
"Samahani Mercy pamoja na hayo yote tulio yaongea bado kunakitu kinaitatiza akili yangu" Lone alizidi kuongea.
"Mercy" Lone aliita.
"Nakusikiza endelea" alijibu Mercy.
"Kiukweli ni kwa…………." Lone alishindwa kuendelea.
Kilichomfanya ashindwe kuendelea ni yale macho alokuwa akitazamwa na Mercy kwa muda wote Lone alokuwa akiongea Mercy alikuwa akimtazama yeye (Lone) Usoni pasipo kukopeza kope za macho yake.


Kwa hali hiyo alimfanya Lone aone aibu na kujidharau kwa kiasi Fulani huenda hayuko timilifu hajamfikia hadhi yake. Lakini kama mwanaume alijipa moyo naye ajaribu bahati yake. "Lone" Mercy aliita. Lone alijibu.
"Mbona kimya" Aliuliza Mercy.
"Nilikuwa bado natafuta maana ya hilo jicho nitazamwalo nalo" Lone alijibu.
"Usijali endelea mi nakuskiza"
"Mercy naomba unielewe kwa nitakayoyasema naomba usijibu kitu mpaka nitakapokwambia naomba unijibu" Lone alisema na Mercy alijibu kwa kutingisha kichwa.
"Kiukweli ni kwamba nikiweka hadharani kile kilichofichama ndani ya moyo wangu kwanza naomba uangalie mawingu".
Mercy aliinua kichwa chake na kutazama angani na kisha Lone akanyoosha mikono yake mbele kuashiria na Mercy ampe na mikono yake. Na Mercy alifanya hivyo pasipo ubishi. Hata yeye Mercy mwenyewe alijishangaa huo udhaifu wa kutenda kila aombwacho atende aliutoa wapi? Kwani tangu Bryan aondoke hakuwahi kuwaza kwamba atatokea mtu atakeye mfanya moyo wake uwe na impession naye zaidi ya Bryan.
Lone aliongea.
"The sky is blue, my love is true between me and you. Just belive me baby siyo kwamba naanzisha mimi kukupenda wewe, yalianza zamani sana toka Adamu na Hawa, toka enzi za mababu zetu na hata Ngoswe na Mazoea. Mercy ninavyokupenda huenda ikawa ni zaidi ya Romeo kwa Julieth naomba usadiki haya nikwambiayo" Aliongea Lone kwa hisia za mapenzi zaidi na huku kila neno alitamkalo likiishia na pumnzi zito.
Mercy pasip kutarajia akajikuta akimkumbatia Lone kwa nguvu na kumkiss kama mara tatu hivi non-stop.
"Naomba unijibu kwa maneno, Mercy" Lone aliongea.
Mercy alikaa kimya takriban dakika mbili hivi akionekana kama anakummbuka mambo Fulani yaliyopita ."Lone naomba unipe muda nifikirie nitakujibu kesho kutwa nikija Dodoma mjini"Mercy alimuomba Lone .
Lone alikubali japo kwa shingo upande .
Waliachana kwa miadi ya kukutana kesho kutwa ,Lone alipata lift ya taxi na kurudi na Mercy akaendelea na shughuli zake.


* * *
Christer siku hiyo alikuwa ametoka kwenda shopping mjini.
Alipokuwa katika mizunguko yake ya hapa na pale mara ghafla gari ikafunga breki miguuni mwake na alipogeuka kuangalia kilichokuwa kikiendelea .Sura yake ilikutana na sura mzee mmoja wa makamo ."Binti hujambo? "Ni Mr Enock kwa sauti nzito na yenye kukwaruza ."Naomba jumapili tuonane NAM hotel nina mazungumzo kidogo umesikia binti?"
"Hapana siwezi , sitokuwa na na ……………."
Wakati Christer akijing'atang'ata kuongea hayo, Mr Enock alichomoa kitita cha shilingi elfu hamsini na kumkabidhi..Christer alijiuliza apokee au asipokee,lakini aliona ni bora apokee kwani bahati kama hizo ni adimu sana .
"Hivi unaitwa nani mrembo?"
"Christer "
Mr Enock alichukua vidole vyake viwili na kuvielekeza mdomoni mwake na kumuonyesha tena Christer na kisha akamwambia afike saa 11 jioni bila kukosa .Mr Enock aliondoka kuelekea Bahi road kwa dada yake .Alipofika alibisha hodi, mlango ulifunguliwa na dada yake .Walisalimiana na dada yake kwa furaha kisha Mr Enock akaeleza kilichomleta.
Mda huo wote Lone alikuwa kesharudi ,aliposikia sauit ya baba yake alipita mlango wa nyuma na kuondoka na kwenda kwa rafiki zake aliapa hatarudi mpaka baba yake aondoke. Baba Lone aliagiza aitiwe Lone,Lone hakuwepo chumbani hivyo alisema atamsubiri mpaka arudi.
**
Ilikuwa ni jumapili Mercy aliporudi kwao kwa ajili ya likizo.
Alipofika tu sebuleni alimkuta Bryan katulia juu ya sofa yuko ndani ya suti ya cream ndani alivalia shati jeupe.
Baada ya Mercy tu kutokeza wote walipigwa butwaa na kufikisha macho ili yawape ukweli zaidi Baada ya kila mmoja kuamini kile alichokuwa akikiona alisema." Waaaoow!" Na kila mtu akimkumbatia mwenzie kwa nguvu akiyashirikisha machozi ya furaha .
"Kwanza umependeza "Bryan alimwambia Mercy aliyekuwa kavaa sketi ndefu nyeusi iliyomtight vema pamoja na blauzi nyeupe.
"Sikushindi Bryan" alijibu Mercy.
"Enhe mbona ghafla hivi"Mercy aliuliza huku akitabasamu.
"Si surprise nilitaka nije nikufumanie"
Wote wakacheka na kisha Mercy akaenda kuwasalimu wazazi wake waliokuwa bustanini na kisha akamrudia Bryan .Ama kwa hakika ilikuwa furaha isiyokifani ni hadithi na vicheko vilivyotawala .Jioni ya siku hiyo Bryan na Mercy walipanga kwenda kula chakula NAM hotel na kwa kweli wakaanza kujiandaa mtoko wa jioni hiyo.


**
"Ni siku ya pili sasa tangu Lone aondoke tangu juzi hajaonekana """Ah shauri zake bwana mimi jumatatu naondoka zangu Dar ila akija mwambie namhitaji arudi Dar tuje tuyamalize"Aliongea Mr Enock .
"sawa kaka"Alijibu shangazi yake Lone .
Muda huo ilikuwa ni saa kumi ,Lone alikuwa kwa marafiki zake akiongea na simu na Christer .Kwa hiyo njoo hapa stendi ya taxi halafu nitakwambia ninapotaka nikupeleke leo "Lone aliongea.
"Sawa"Upande wa pili ulijibu.
Muda si muda Christer alifika na kumkumbatia Lone na kumkiss "Vipi dear mzima wewe? Lone aliuliza.
"Wa afya hofu zaidi juu yako"
"Namshukuru mungu sijambo" Alijibu Lone wote wakaingia ndani ya taxi na kisha Lone akamwambia dereva awafikishe Nam hotel. Christer alishtuka kiaina ila akajikaza lakini wasiwasi ulimjaa mwili mzima ukijua leo ameunguza picha mpaka nega.
Safari ilianza taratibu kuelekea huko huko Nam hotel.
Kwa upande wa Mr Enock nako, "Dada mi sasa hivi, ntarudi usiku" Mr Enock alimuaga dada yake.
"Kaka na wewe bado hujatuliaga tu sasa wapi tena, usije ukagonganisha na wakwe zako huko," Aliongea shangazi yake Lone.
"Ah nshakuzoea na maneno yako" alitoka na kuingia garini moja kwa moja mpaka Nam hotel.


Bryan na Mercy walikuwa wamefika Nam hotel walikuwa sehemu moja hivi tulivu mno na tayari walikuwa wameshaanza kujichana huku stori zikiendelea.
Punde si punde Lone na Christer waliingia huku wameshikana mikono waliingia na kuelekea sehemu ile ile waliokuwako Bryan na Mercy. Hakuna aliyekuwa amemuona mwenzake hii ilitokana na kila mtu kufall kwa mwenzake.
Christer na Lone walichizika zaidi kiasi kwamba Lone akapamia meza ya akina Bryan na Mercy hapo ndipo kila mtu alizinduka kana kwamba walikuwa wamelala fofofo.
Lone kutazama anamuona Mercy yuko na mtu.
Bryan kutazama anamuona Christer yuko na mtu.
Kwa upande wa wale wasichana walitazamana kwa macho makali sana. Kisha Mercy "Hallo Lone mpenzi wangu hapa anaitwa Bryan" Huku akimkiss Bryan.
Kisha naye Lone akamtambulisha yule dada na kwamba ndiye mahabuba wake. Alionge huku akimkiss shavu.
Bryan na Christer walitazamana kwa shauku pasipo kusema neno kisha wakakonyezana.
Wakati wakiwa katika hali hiyo Mr Enock aliingia na kisha kupigwa na butwaa.
"Ha Christer?" Alishangaa Mr Enock.
"He, baba yangu" Aliduwaa Bryan.
Mr Enock alishangaa kusikia mtu akimuita baba ilihali pale hana mtoto zaidi ya Lone.
Kumuangalia usoni ni Lone vilevile. Mr Enock alikaa chini ili apewe full story.
Kwa upande wa Lone na Bryan walipotazamana kwa makini ilikuwa ni kama vile kila mmoja akijiangalia kwenye kioo kwani walifanana kupita kiasi.
Baada ya kila mmoja kupata full stori kutoka kwa mwenzake. Mr Enock alimaliza kwa kumtambulisha Bryan kama mdogo wake Lone.
Baada ya hapo Mr Enock aliomba afahamiane na upande wa wazazi wa Mercy na ikawa hivyo.


Sekunde ziliyoyoma, dakika zikakatika, saa zikasogea, siku zikaenda, umri ukaongezeka na mwisho kabisa Bryan alifunga ndoa na Mercy na Lone na Christer.
Miezi kadhaa baada ya ndoa yao Lone na Christer wakiwa katika nyumba yao yenye kila hitaji Lone alimkumbushia Christer siku ile hotelini.
"Oyaaaa mamaa" Lone aliita.
"Sema babaa"
"Unakumbuka ulivyotaka kutupanga na mdingi siku ile hotelini?"
"Ah, mkwe naye mapepe hajatulia hata kidogo" Christer aliongea na kisha wote wakacheka, na maisha yakaendelea.
Huku nako kwa akina Bryan na Mercy wakiwa wameyapatia maisha vilivyo nao walikuwa wanataniana.
"Unasikia dear?" Aliongea Mercy.
"Nakusikiliza laazizi" Alijibu Bryan.
"Nisingekomaa sasa hivi shemeji yako ndiye angekuwa analalia kitanda chako saa hizi."Aliongea Mercy huku akicheka.
"Duh, hata sielewi kipi kilichonichizisha kwa shem, ilhali mtoto mrembo kama wewe unang'aa kama hii silver yangu ulikuwepo"
Wote wakacheka na kugonga na maisha yakaendelea kuwa matamu.

MWISHO.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : PENZI ZITO SEHEMU YA SABA (07) MWISHO
PENZI ZITO SEHEMU YA SABA (07) MWISHO
https://1.bp.blogspot.com/-38NnJR4fR2E/XRUKwbDWnfI/AAAAAAAACm0/QH9EEAhZkwMkipb-s4U29lQb7ihHGZfdwCEwYBhgL/s640/PENZI%2BZITO.png
https://1.bp.blogspot.com/-38NnJR4fR2E/XRUKwbDWnfI/AAAAAAAACm0/QH9EEAhZkwMkipb-s4U29lQb7ihHGZfdwCEwYBhgL/s72-c/PENZI%2BZITO.png
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/penzi-zito-sehemu-ya-saba-07-mwisho.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/penzi-zito-sehemu-ya-saba-07-mwisho.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy