PENZI ZITO SEHEMU YA NNE (04) | BongoLife

$hide=mobile

PENZI ZITO SEHEMU YA NNE (04)

PENZI ZITO SEHEMU YA NNE (04)


PENZI ZITO 4

SIMULIZI ZA JOSHUA / 3 weeks agoSIMULIZI: PENZI ZITO
MTUNZI: Prosper Mgowe
MHARIRI JOSHUA SHAO
0713111547


SEHEMU YA NNE​Huku akisugua mto huo kwa taratibu fikra zake zikimpa kana kwamba yupo pamoja na Bryan.
Wakiwa wamesimama pamoja tofauti ya hatua moja.
"Bryan naomba nikumbie kitu"
"Kitu gani hicho Mercy?"
"Mmh, mmh?
"Mmh,mmh,kitu gani wakati umesema kuna kitu unataka kuniambia"Alihoji Bryan
"Naomba usinifikirie vibaya naheshimu hisia zangu ndo maana nimeamua kukuambia, Nafahamu mapenzi sio kitu rahisi, Lakini naomba unimiliki, NAKUPENDA SANA BRYAN". Kabla Bryan hajaongea kitu Mercy alinyoosha mkono ili kumkumbatia Bryan lakini huyo Bryan hakuwepo kwa Mercy yalikuwa ni mawazo tu ya kufikiria tu.

Akiwa juu ya kitanda chake alichanua tabasamu hafifu la kujifariji kwamba iko siku lazima mawazo yake aliyokuwa anayawaza nucta chache zilizopita ni lazima yatatimia.

Mercy alitamani sana muda huo awe na Bryan katika chumba chake hicho lakini sasa kwa muda huo hakuwa na ubavu kwani nyumba yao ilikuwa tofauti na vyumba vya uwani ambacho kimoja kati ya hivyo ndicho alichokuwamo Bryan na mbaya zaidi Mercy hakuwa na mazoea ya kutoka nje usiku kwani nyumba yao ilikuwa selfcontener, kwa hiyo angetoka wazazi wangestuka na kuhoji huko nje anaenda kufanya nini? Kwa hiyo basi Mercy wa watu alibaki humo chumbani kwake akizidi kuhangaika.

Laiti kama Bryan angemuona mtoto wa watu anavyoishughulika angemuonea huruma, Lakini kwa bahati mbaya hakuelewa kinachoendelea chumbani kwa Mercy. Baadae Mercy aliamua kulala baada ya kutopata ufumbuzi wa tatizo lake lakini aliombea pakuche haraka ili waonane tena na Bryan.

Mercy alilala hivyo hivyo tu usingizi wa mang'amung'amu mpaka pakakucha.

**

Bryan aliwahi kuamka, ilikuwa asubuhi ya kuamkia Jumatatu. Alimshukuru Mungu kwa kuiona siku hiyo pia akiwa salama baada ya hapo alipiga push up kama 30 hivi na kasha akafungua mlango wa chumba chake. Alitoka akiwa amevalia bukta yake nyeusi yenye mistari myeupe pembeni huku akiwa kifua waz na moja kwa moja alielekea lilipokuwa bafu la nje, aliingia bafuni na kufungulia bomba la mvua tayari kwa kuoga. Alitumia kama robo saa tu akawa ameshamaliza kuoga.

**

Ilikuwa ni asubuhi, kipindi Mercy alipokuwa ameshtuka kutoka usingizini, mtu wa kwanza kumfikiria katika fikra zake alikuwa ni Bryan. Mercy alijikuta akitabasamu tu, bila sababu ya msingi ambayo hata yeye hakuifahamu pengine hiyo ndiyo ilikuwa siku nzuri kwake.

Mercy aliamka na kukaa kitandani na kupiga mwayo mrefu huku akijinyoosha. Alijitoa kitandani akiwa amevalia night dress, alilielekea pazia la dirisha la chumba chake na kasha akalifungua pazia hilo kwa kupitia vioo vya dirisha hilo. Mercy alionekana kama kutoamini kitu alichokiona kupitia kwenye dirisha hilo kwani alifikicha macho yake mara mbilimbili.

Mercy alikuwa ameduwaa kama sio kubung'aa yaani alishangaa. Kilichomsataajabisha sio kingine Mercy alimuona Bryan akiwa anatoka bafuni, alipagawa na kifua chake kilichojengeka vizuri na zaidi yale majimaji yalokuwa bado hayajakauka vizuri kwa muonekano huo Mercy alijikuta akizidi kumpenda Bryan. Mercy alimwemwesa midomo yake asijue la kufanya huku mikono yake akiwa amejitwika kichani. Butwaa likiwa bado halijamuisha mara akasikia hodi kwenye mlango wa chumba chake ndipo hapo akashtuka na fahamu zake kumrudia katika hali ya kawaida.

**

Bryan alikuwa chumbani kwake akivaa uniform zake za shule alipomaliza kuvaa alichukua kitana na kuisogelea dressing table na kuanza kuchana nywele. Bryan alijiangalia kwenye kioo dakika mbili, tatu na kasha kutabasamu na nyusi zake nyingi na nyeusi zilimfanya Bryan azidi kuvutia, hata yeye alikubali hilo. Bryan alichana na kioo na moja kwa moja alichukua mfuko wake wa daftari tayari kwa kwenda kuwajulia khali alioachana nao jana na kisha aende shule.

**

"Karibu" Mercy alimkaribisha aliyekuwa anagonga kumbe alikuwa ni msichana wao wa kazi amekuja kumuamsha baada ya kuona siku hiyo Mercy amechelewa kuamka.
"Vipi da Mercy mbona leo umechelewa kuamka" aliuliza msichana wa kazi aliyekuwa akiitwa Paulina. Paulina hakuwa mdogo kiasi cha kumuita Mercy dada, hii yote ilisababishwa na uwezo wa kifedha waliokuwa nao akina Mercy.

"Ah leo nilipitiwa ndo maana nimelala mpaka saa hizi" Alijibu Mercy huku akifikicha macho yake kana kwamba ndo anatoka kuamka.

Mercy alichukua mswaki wake pamoja na taulo na kuelekea bafuni kwa ajili ya kujisafi. Alikoga upesi upesi na kisha kurudi na kuvaa uniform zake pamoja na viatu alipomaliza kujiandaa alitoka moja kwa moja kwenye vyumba vya uwani, na mara akaufikia mlango wa chumba cha Bryan na mara akakishika kitasa cha mlango huo wakati Mercy akitaka kufungua mlango wa chumba hicho na Bryan alikuwa ameshakishika kitasa alipofungua na Bryan alifungua na Bryan alipotaka kutoka Mercy naye alikuwa anaingia.

Mra Mercy na Bryan wakakumbana.
"Waooooh" Mercy alimlaki Bryan kwa kumkumbatia Bryan.
Bryan alihisi msisimko wa ajabu, alibaki amesimama tu asijue la kufanya zaidi ya mihemo kuanza kubadilika.

Kwa upande wa Mercy ni hivyo hivyo, ilivyo kama Bryan. Alihisi damu ikisisimka yaani kamwe haikuwahi kumtokea kabla ya hapo. Kwa nukta kadhaa wakabaki wamekumbatiana hivyo bila hata mmoja wao kusema neno.

Mercy aliuvunja ukimya, wakiwa nyuso zao zinatazamana kwa karibu zaidi.
"Mambo vipi Bryan?
"Safi tu" Bryan alijibu kwa sauti ndogo ikifuatiwa na pumzi kubwa.
"Twende tuka shaftahi ili tuwahi shule" Aliongeza Mercy.
"Okey, lakini kumekucha salama?" Aliuliza Bryan
"Bila shaka" kwa ufupi Mercy alijibu.

Waliachiana mikono na wote wakatoka kuelekea dining room ili kupata kifungua kinywa.

Walikuta Paulina keshatenga chai na chapatti walisali kwanza kabla ya kula ndipo wakaanza kula waliendelea kula bila kusemeshana

"Vipi wazee bado hawaja amka" Bryan alivunja ukimya
"Unadhani hao wanaamka sasa hivi?" Mercy alitoa jibu linaloambatana na swali
"Mbona tumechelewa sana zimebaki dakika 15 kengele igonge. Bryan aliuliza swali jingine.
"Usijali Dereva atatuwashisha na gari ya baba"
Muda flani Mercy alipokuwa akimuangalia Bryan alikuwa akitabasamu sababu iliyomfanya Mercy atabasamu hata mimi sijui. Bryan aliposhtukia khali hiyo akawa anaangalia chini akawa anahofia labda amekosea kitu Fulani ndio maana Mercy alikuwa akimcheka. Walipomaliza chai Bryan alishukuru kwa chai hiyo kwani ni kitambo sana hajakutana na chai ya namna hiyo.

Mercy naye alijibu Asante kushukuru.
Safari ya kwenda shule ilianza. Bryan na Mercy walikuwa ndani ya gari aina ya Range rover walikuwa wamekaa Backseat.

**

Eh bwaneeeh! Mshikaji wetu siku hizi anamiliki toto la nguvu" aliongea Bakari ambaye wengi hupenda kumwita Baker. Hiyo ni baada ya Bryan na Mercy Kushuka ndani ya Range rover milango sita.

" Mtoto gani huyo? Aliuliza John
"Si Mercy huyo" Alijibu Baker
Hawa wote walikuwa wakisoma darasa moja na Bryan.

Bryan na Mercy waliendelea kuishi kwa upendo na amani, Bryan aliendelea kuwa kama house boy katika nyumba ya Mzee Josephat lakini alichukuliwa kama mmoja wa watoto wa Mzee wa Josephat kwani kila alilohitaji alitimiziwa na hata ada alikuwa akilipiwa na Mzee Josephat, pia na hata nguo alizokuwa nazo sio kama zile alizokuja nazo.

Bryan na Mercy walikuwa wameshafanya Mtihani wa Taifa kidato cha pili kuingia kidato cha tatu na wote walifaulu vizuri. Kwa kufaulu kwao kuliongeza furaha na upendo ndani ya familia yao. Walizidi kufanya vizuri katika upande wa masomo, walimaliza kidato cha tatu na sasa wameingia kidato cha nne.
Katika kipindi cha kidato hicho Mercy alijitahidi kuziwakilisha hisia zake kwa muhusika yaani Bryan lakini ilimuwia vigumu, kwani kila alipotaka kumwambia anavyohisi juu yake, alijikuta akishindwa kumwambia kwaajili ya aibu aliyokuwa nayo Mercy.Na alipojaribu kutumia lugha ya mwili (Body language) alijikuta akiambulia patupu. Kwani pamoja na kutumia ishara hizo Bryan hakuwa na muelekeo wowote.

Mercy hakuelewa kuwa Bryan hakumuelewa au alifanya kusudi. Kwa Mercy yalikuwa ni mateso bila chuki kwani alizidi kukonda moyo na asijue la kufanya kwa kuwa Mercy alishaapia ya kwamba iko siku yeye na Bryan watakuwa pamoja kwa hiyo hakukata tamaa aliamini iko siku malengo yake yatatimia, kwa sasa Mercy alikuwa akipanga mikakati mipya ya kumuingia Bryan kwani ameshachoka kuumia moyo.

Kwa upande wa Bryan ilikuwa ni tofauti na Mercy, kwa fikra zilikuwa ni kupanga maisha yake ya baadaye, sio kwa maana hisia za mapenzi zilikuwa hazimjii, La hasha ila alikuwa akijitahidi sana kuondokana na hali ile kwa kufanya mazoezi na shughuli ndogondogo ambazo zilizopelekea umbile lake kuzidi kuhamasisha na kufanya warembo wengi wajigonge kwa yeye, lakini Bryan hakuwa na mpango na hata mmoja kati ya hao, kitu ambacho kilipelekea wasichana wengi wahisi kuwa Bryan sio rijali kamili. Lakini hisia zao kwake hazikumpa presha.
Mercy kwa Bryan alichukulia kama dada wa tumbo moja. Vituko vya Mercy kwa Bryan vilionekana isipokuwa Bryan hakutaka kupitisha jibu la moja kwa moja katika ubongo wake kuwa alikuwa akitakwa au ndo'mapozi yake yalivyo. Bryan alijiuliza maswali mengi sana kichwani mwake bila ya kupata jibu la maana.

"Hivi endapo Mercy atakaponitaka na nikamkubalia itakuwaje? Ili hali wazazi wake nawaheshimu kama wazazi wangu na sipati picha pindi watakapogundua mimi na Mercy tunamahusiano ya kimapenzi, duh, sijui itakuwaje? Na ukizingatia wema wote walionitendea na kufanya niwe mimi leo, na niwe na heshima kama watu wengine, bila ya wao sasa hivi na hisi ningekuwa chokoraa na hiyo shule ningekuwa naisikia kwenye bomba tu, kwa kweli si kuwahi kuwaza kama kama kuna siku ningekuwa katika maisha ya hali hii, kwa hakika namshukuru huyu binti pamoja na wazazi wake kwa kunifanya niwe moja kati ya wao, nawaombea kwa mungu awtangfulie. Akiwa katika mawazo yake hayo mara ghafla mlango wa chumba chake ukagongwa, Bryan akajiinua mahala alipokuwa ili akafungue mlango.

Aliyekuwa akigonga mlango wa Bryan alikuwa si mwingine zaidi ya Mercy. Bryan alifungua mlango wa chumbani kwake kisha Mercy akaingia alipoingia moja kwa moja alimuendea Bryan na kumshika mikono yake miwili na wakatazamana nukta kadhaa bila kusemezana.

Baada ya Mercy kusema kilichomleta altabasamu kidogo kisha akampiga Bryan kikofi cha uwongo na kweli kisha akamwambia kwa taratibu.
"Bryan unaitwa na baba"
Bryan huku akimuangalia Mercy miguuni alitingisha kichwa kuashiria amekubali
"Haya nakuja" alisema Bryan kwa sauti hafifu.

Mercy alipiga hatua chache ili kutoka chumbani humo lakini hajatoka nje Mercy alisimama na kugeuza shingo na kumtazama kwa macho ya upole bila kusema kitu na kisha Mercy akatoka nje. Baada ya Mercy kutoka Bryan alicheka kidogo naye akatoka kwenda kuitikia wito.

Bryan aliingia sebuleni na kumkuta mzee Josephat kakunja nne.
"Shikamoo baba" Bryan alimsalimia mzee Josephati
"Marahaba habari za mchana kutwa"
"Nzuri tu baba"

Lengo langu la kukuita ni kutaka kukupongeza kwa utendaji wako wa kazi na kwa kuweza kumsaidia Mercy katika masomo yake, kwani siku izi namuona maendeleo yake kitaaluma yanaridhisha tofauti na zamani kwa hiyo pokea bahasha hii na mwisho wa wiki mtaenda na Mercy kufanya shopping na lingine la ziada nawaombea mitihani mwema kwani bado wiki mbili tu"
"Nashukuru sana baba naomba mungu akuzidishie yaani sijui nikushukuru vipi?"
"Ishalah" sas unaweza kuendelea na kazi zako"

Bryan alipewa bahashishi ya shilingi ishirini Elfu, kwa kweli alikuwa anafuraha sana na wala hakutegemea kupata fedha kama hizo kwa kipindi hicho.

Ilikuwa ni Week end Bryan na Mercy walikuwa kati ya duka moja maeneo ya Oneway, walikuwa wakichagua nguo pamoja na viatu na vitu vingine walivyoona vinafaa. Wlitoka One way na kuelekea maeneo ya sabasaba, baada ya kufika katika banda moja kati yam engine yaliyokuwepo hapo Bryan alichagua fulana moja nyeupe isiyo na neno hata moja yenye kola ya V, pamoja na jeans nyeusi na raba nyeupe, hapo tayari walikuwa wameshakidhi mahitaji.
Wakiwa pamoja Bryan na Mercy wakibadilishana story za hapa na pale walikuwa wapo bado maeneo ya sabasaba mara ghafla Bryan alijikuta amempamia mtu mmoja aliyekuwa mbele yake.

Mtu huyo alikuwa ni binti apataye takribani miaka 18, mrefu wa kadri mwenye umbo namba 3, machoni alikuwa amevaa miwani ya bluu katika mkono wake wa kulia alikuwa amebeba mfuko wa karatasi wa rangi ya kaki. Baada ya kupamiwa na Bryan mfuko huo ukadondoka.

"Oh samahani sister" Bryan aliongea huku akiinama ili aokote mfuko.
" Hamna shida kaka'ngu wala usijali" alisema binti aliyeamgushiwa mfuko. Bryan hakujali akauokota ule mfuko na kumkabidhi yule binti.

Yule hakuuopekea mara moja alimtazama Bryan machoni kwa nukta kadhaa kana kwamba anadadisi kitu katika macho ya Bryan kisha akaupokea.

"Okey thanx, sijui unaitwa nani?"
"Bryan, sijui mwenzangu?"
" Mie naitwa Christer na ni mwanafunzi wa kidato cha tatu Msalato Girls"
" Na mie nasoma Dodoma Sekondari"
" Eti umesema unaitwa Bryan nani vile?
" Mwansasu" alijibu Bryan.
Waliaga na kupeana mikono na kila mmoja kuelekea upande wake.

Kwa upande wa Bryan na Mercy walikuwa wameshamaliza kununua mahitaji yao kwa hiyo walikubaliana kurudi nyumbani kwao na ikawa hivyo.
Kitendo cha Bryani kuongea na Crister kilimuumiza moyo Mercy kwani alihisi tayari keshazidiwa na Christer.
" Haiwezekani mwenyeji kama miye nizidiwe na mtu kama yule tena mpita nje tu" Aliongea Mercy kwa hamaki.
Hapa ni lazima nifanye kitu, hatakama akiniona mimi Malaya kimpangowake' Aliongea Mecy kwa kujiamini.

Wakati Mercy alipokuwa chumbani kwake akiwaza hayo na Bryan pia alikuwa chumbani kwake akijipumzisha akiwa mawazo yake juu ya Crister. Alijiuliza na kwamba msichana yule alikuwa akimtazama vile, ni kwa nini yule msichana alimuuliza maswali mengi vile ilihali hawafahamiani.

Alikuwa katika mawazo hayo taratibu akajihisi Crister amemuingia moyoni alipokumbuka macho yake ya upole tabasamu lake tamu, midomo yake mipana, meno yaliyobanana hakuna pengo wala mwanya pamoja na uso wake wenye shepu ya kitoto, tayari Bryan alishahisi moyo wake kuzorota juu ya Crister. " Iwe isiwe lazima nitimize ndoto yangu juu ya Crister, sielewi nitampataje lakini naamini nitampata" Bryan alijikuta akiongea kwa sauti ili hali yupo peke yake chumbani humo.

***MERCY anaamua kujivika ujasiri ili asizidiwe kete na CRISTER…..je atamuwahi??? Na BRYAN anaanza kuhisi kitu juu ya CRISTER……Nini kitaendelea&

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : PENZI ZITO SEHEMU YA NNE (04)
PENZI ZITO SEHEMU YA NNE (04)
https://1.bp.blogspot.com/-38NnJR4fR2E/XRUKwbDWnfI/AAAAAAAACm0/QH9EEAhZkwMkipb-s4U29lQb7ihHGZfdwCEwYBhgL/s640/PENZI%2BZITO.png
https://1.bp.blogspot.com/-38NnJR4fR2E/XRUKwbDWnfI/AAAAAAAACm0/QH9EEAhZkwMkipb-s4U29lQb7ihHGZfdwCEwYBhgL/s72-c/PENZI%2BZITO.png
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/penzi-zito-sehemu-ya-nne-04.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/penzi-zito-sehemu-ya-nne-04.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy