$hide=mobile

MWANACHUO SEHEMU YA KWANZA (01)

'CHOMBEZO YA MAPENZI'           'INAITWA'  -- MWANACHUO ?.-- MTUNZI;Isaack Kanyankole NO;0625915000 KUTOKA;DSM T...

MWANACHUO SEHEMU YA KWANZA (01)

'CHOMBEZO YA MAPENZI'

          'INAITWA'

 --MWANACHUO?.--

MTUNZI;Isaack Kanyankole
NO;0625915000
KUTOKA;DSM TZ
EPISODE;01

    ...UTANGULIZI...

  Hii ni simulizi ambayo itakuacha ukiwa umejifunza mambo mengi sana...na pia mwandishi wa chombezo hii anashauri yoyote atakayeisoma chombezo hii umri uwe ni kuanzia miaka 18+,,na pia soma huku ukijifunza..

    ...SONGA NAYO...

Nilishtuka kutoka usingizini baada ya kusikia mlio wa simu ukiita,,hivyo nilishika simu yangu na kutazama ni nani aliyekuwa ananipigia ila haikuwa simu yangu ilikuwa ni simu ya rafiki yangu ambaye tulikuwa tunaishi sote kwenye chumba hicho. Hivyo baada ya kuona sio simu yangu ilinibidi nimuamshe rafiki yangu aliyekuwa amelala fofofo.

"Thomaides,,,Thomaides,,Thomaides amka simu yako inaita". Nilimuita huku nikiwa namtisa kwa nguvu.

"Naam..vipi mbona unaniharibia usingizi". Thomaides aliamka huku akilalamika.

"Simu yako inaita na pia safari hii ni kama mara tatu inaita". Niliongea huku nikiwa nampatia simu yake na baada ya kumpatia simu Thomaides nilitoka chumbani na kuelekea maliwatoni,,na baada ya kufika maliwatoni nilianza kuwaza juu ya nasaha za wazazi wangu ambazo walikuwa wananipa kabla sijaja chuoni.

'Ina maana haya walikuwa wanayafahamu hama?'. Nilijiuliza nikiwa najimwagia maji usoni na hatimae mawazo hayo yalitoweka kichwani baada ya kusikia Thomaides akigonga mlango,,ilinibidi kutoka maliwatoni kwa haraka.

"Dah,,,yaani jana asikwambie mtu kuna shori fulani alijiingiza kwenye mkenge kipindi tukiwa tumekaa kwenye meza kama unakumbuka".

"Ndio nakumbuka ni vipi umempata". Nilimjibu nikiwa nimesimama kwenye mlango.

"Hebu toka kwanza nitakuja nakusimulia maana nasikia tumbo linang'uruma".

"Ok poa". Niliitikia huku nikitoka mlangoni na kuelekea chumbani na baada ya kufika chumbani nilijilaza kitandani na baada ya kujilaza kitandani usingizi ulinipitia..nilikuja kuzinduka baada ya kusikia mtu akiniita huku akinitisa.

"Hebu amka ujiandae twende chuo hama leo uendi". Thomaides alizungumza akiwa ananipiga na folonya kichwani ilinibidi niamke huku nikipecha macho yangu kwamaana nilikuwa bado nikihisi usingizi mzito kwenye macho yangu.

"Kwani,,,kwani,,,sasahivi ni saa ngapi?". Safari hii niliuliza huku nikiwa najinyoosha viungo vya mwili wangu.

"Kwasasahivi ni saa nne kamili hebu jiandae haraka kabla ya watu wengine kuamka na si unajua hapa ni uswahilini".

"Poa,,,poa yaani dah...jana tulifanya kufuru sana maana kila nikikumbuka nahisi kichwa changu kubabaika sana".

"We,,usiku natoka maliwatoni kuja kukusimulia nilikuta umelala hivyo ikanibidi nikuache na pia ulivyoniamsha usiku kwa jinsi nilivyokuwa nina usingizi hakika kama asingekuwa yule shori ambaye alijiweka kwenye mchoro ambao niliufanyia targeti hakika ungenikera sana".

"Ahaaa,,sawa bwana kwahiyo shori kakuelewa heti ehe?". Niliongea nikiwa naamka na baada ya kuamka nilijifunga tauro na kisha nilisimama mlangoni ili Thomaides aweze kunipa jibu.

"Hebu kwanza nenda uoge harafu tukiwa tunaelekea chuoni nitakusimulia kila kitu".

"Sawa". Nilitikia nikielekea bafuni na baada ya kufika bafuni nilioga harakaharaka na kisha baada ya kumaliza kuoga nilirudi chumbani na kujiandaa.

"Leo ujipulizii chibu parfume?". Thomaides aliniuliza akiwa ananipatia parfume.

"Ahaa!,,nilikuwa nimesahau". Niliongea nikiwa naipokea na kujipulizia na baada ya kujipulizia tulitoka chumbani na kisha nilifunga mlango..ufunguo niliuweka juu ya mlango.

"Ok,,tunaweza kwenda ila nafikiri twende kwa yule mwanamke ambaye anauza supu ya pweza si unajua tena kujiweka vizuri asubuhi".

"Na mimi ndo nilitaka nikwambie sasahivi hivyo twende na pia jana ambacho nilitaka nikwambie ni kuhusu suala la shori ambaye tulikutana nae kwenye club duh...shori huyo alikuwa ni bonge la demu ameumbika kwelikweli dah si unakumbuka wewe ndo ulitangulia kuingia kwenye club sasa kipindi na mimi nakufuata kwa nyuma  niligongana na shori huyo macho yangu yalibabahika baada ya kumuona mtoto huyo hivyo na mimi ambavyo siko mtu kuchelewa ikabidi nimvutie waya hapohapo kwa kumuomba namba ya simu lakini alikataa katukatu huku akidai ana mtu amekuja nae,,dah baada ya kuona shori huyo kakataa ikabidi nijikatae lakini nikajiapiza moyoni na kusema lazima nichukie namba yake leo hii?".

"Karibuni sana". Haikuwa sauti nyingine ilikuwa ni sauti ya Mama Jack  akitukaribisha.

"Asante vipi kuna supu ya pweza hama?".

"Supu ya pweza ipo?".

"Basi leta na pia leta chapati mbilimbili jumla ziwe nne".

"Sawa". Mama Jack aliitikia akiwa anaelekea jikoni kutuwekea tulichokuwa tumemuagizia atuletee.

"Ehe,,ikawaje maana mimi nakumbuka kipindi tukiwa mezani tunaendelea kunywa kuna binti ambaye ulimfuata kwenye meza".

"Naam ndo huyohuyo ujakosea,,ehe si nilimfuata na baada ya kufuata nikianza kumpiga sound za maana huku nikimlaghai kuwa mimi nafanya kazi benki na kweli binti akuweza kuchomoa yeye mwenyewe safari hii alinipatia namba na baada ya kunipatia namba...ilinibidi na mimi nimpatie namba yangu".

"Ndo Vaileth hama mwingine maana na wewe huko vizuri sana katika suala la kuchukua mademu".

"Ndo yeye Vaileth maana alivyonipatia namba tu alidai kuwa niondoke kwamaana kuna mtu ambaye alikuwa amekuja nae na alidai kuwa angenipigia usiku baada ya kuachana na mtu ambaye alikuwa amekuja nae na kweli jana usiku aliweza kuingia kwenye mchoro wangu ambao nilikuwa nimemchora akuweza kutoka alidai amenielewa ahaaaa,,,yaani wee acha tu na pia jumapili tumepanga kwenda kwenye club ambayo ipo kawe sijui ni club gani ila kadai ni club nzuri sana".

"Duh na wewe kwa mademu uachi je hao wengine ulionao".

"Ahaaa...kila mmoja ana muda wake na leo hii upo chuo usipofanya leo hii starehe utafanya lini hebu David acha utoto,,utoto kuwa na akili kama za mtu mzima achana na akili za shule hiki ni chuo".

"Poa bwana nimekuelewa Thomaides".

"Samahani kwa kuwacheleweshea supu,,,supu yenyewe ilikuwa imepoa ikanibidi niipashe". Mama Jack alizungumza akiwa anatuwekea supu mezani.

"Amna shida Mama". Thomaides aliitikia akiwa ananisogezea bakuri la supu.

  Nilichukua bakuri ambayo Thomaides alinisogezea na kuanza kunywa supu huku nikiwa nakula chapati na pia maongezi ya hapa na pale yaliendelea na hatimae baada ya kumaliza kunywa supu tulimpatia pesa Mama Jack na kisha tulitoka kwenye kwenye genge lake na kuanza safari ya kuelekea chuo kilipokuwa,,,chuo akikuwa mbali na sehemu tulipokuwa tunaishi.

"Supu ya leo imekuwa tamu sana". Niliongea nikiwa natazama magari kwa upande wa kushoto na kulia.

   Ila kipindi nikiwa naendelea kutazama barabarani,,nilishtuka baada ya kusikia kelele za watu wakiwa wanaomba msaada na mara kishindo kikubwa kilisikika katika eneo hilo mwili wangu wote uliishiwa nguvu baada ya kuona tukio ambalo sikutarajia kuliona kwa siku hiyo!?...

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,149,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,196,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,110,FIFA.com - Latest News,15,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,11,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,207,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,39,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MWANACHUO SEHEMU YA KWANZA (01)
MWANACHUO SEHEMU YA KWANZA (01)
https://1.bp.blogspot.com/-MaXus7taxCM/XRUR0tonoAI/AAAAAAAACm8/9D-mzJgFqAsKhlKUPsCtrD4S2A5s4pWWQCLcBGAs/s640/MWANACHUO.png
https://1.bp.blogspot.com/-MaXus7taxCM/XRUR0tonoAI/AAAAAAAACm8/9D-mzJgFqAsKhlKUPsCtrD4S2A5s4pWWQCLcBGAs/s72-c/MWANACHUO.png
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/mwanachuo-sehemu-ya-kwanza-01.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/mwanachuo-sehemu-ya-kwanza-01.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content