MADHARA YA KIAFYA YATOKANAYO NA KUVAA CHUPI KWA JINSIA ZOTE | BongoLife

MADHARA YA KIAFYA YATOKANAYO NA KUVAA CHUPI KWA JINSIA ZOTE

*USIVAE CHUPI TENA*

MADHARA YA KIAFYA YATOKANAYO NA KUVAA CHUPI KWA JINSIA ZOTE


By Dr BINGWA Emmanuel wa www.jamiihuru.com


Mpendwa bila shaka umeamka salama.


Leo naomba nikukumbushe somo la Afya ya uzazi. Somo hili litafafanua faida na hasara au madhara yatokanayo na uvaaji wa nguo za ndani hasa Chupi.


Uvaaji wa chupi kihistoria ulianza karne ya 19 baada ya uvumbuzi wa viwanda na mapinduzi yake yaliyoambatana na mapinduzi ya teknolojia.


Enzi za mama zetu na babu zetu uvaaji wa chupi haukuwepo hapa Tanzania. Uvaaji wa chupi uliletwa na wamisionari na wakoloni wakati wanaleta dini Africa. Kabla ya hapo waafrica hatukuwa na utamaduni wa KUVAA chupi.


Mtoto akizaliwa hakuvalishwa chupi kamwe kama ilivyo Leo.


Mwanamke pia enzi hizo alikuwa havai chupi. Mwanaume naye pia alikuwa havai chupi? Watu wote walikuwa hawavai chupi. Mwanamke alikuwa hachuchumai chini pindi akijisaidia kutokana na kwamba hawakuwa wanavaa chupi hivyo wakitaka kujisaidia haja ndogo walikuwa wanasimama tu na kupanua miguu na kuanza kukojoa.


Nyakati za leo ambapo uvaaji chupi kwa wanaume na wanawake uko juu sana kuanzia watu tunapokuwa watoto wadogo hali ya Afya ya viungo vya uzazi imeendelea kuwa mbaya sana. Yafuatayo ni baadhi ya madhara ya kuvaa chupi :


1. Magonjwa ya "Urinary tract infection" au UTI hayataisha kwako.


Hii hasa ni kwa wanawake wanavaa nguo nyingi kwa wakati mmoja na kwa muda mrefu zaidi ya saa kumi. Unavaa chupi, lakini tight, suruali ya jinzi, nk halafu unashinda na hizo nguo kuanzia asubuhi unapoenda kazini hadi saa mbili usiku unaporudi home. Hiyo ni hatari sana.


Mwanamke anayefanya kazi zinazompasa kuwepo kazini zaidi ya masaa 8 namshauri asiwe anavaa chupi kabisa. Chupi ivaliwe nyakati za hedhi tu. Kama hauko kwenye siku zako vaa suruali tu bila chupi. Au vaa underskirt pekee yake kwa ndani na ndoo uvae nguo yako ya kawaida. Hii itakuepusha na kuugua UTI. Ukiacha sababu za ngono UTI husababishwa na bacteria wanaopendelea mahali penye unyevu na joto. Kwa hiyo mwanamke akivaa nguo nyingi bacteria hao hujipatia joto la kutosha kuzaana.


Mwanamke ni vyema ukaepuka kuvaa nguo za kubana mwili sana ili kuepukana na uwezekano wa kupafanya ukeni pawe na joto sana na ikitokea bacteria mmoja tu akaingia humo atazaa haraka sana na kujikuta UTI inakuwa rafiki yako. Vaa sketi bila chupi au kama kuvaa suruali ni lazima hakikisha unavaa suruali peke yake. Jizoeze tu utazoea. Na ukizoea kuvaa nguo bila chupi utainjoi sana.


2. Magonjwa ya kuvu au fungus hayatakoma kwako.


Bado niko kwa wanawake, kama nilivyoeleza mwanzo hapo magonjwa ya fungus yanasababishwa pia na kuvaa chupi kwa muda mrefu. Chupi inayovaliwa kwa zaidi ya saa 8 lazima italeta ukungu au uvundo sehemu nyeti. Huo uvundo waweza kuleta fungus ukeni. Fungus za ukeni hazina tofauti na zile za miguuni kwa wanaume wanaovaa viatu kwa muda mrefu bila usafi miguuni wa kutosha.


Chupi inakuwa kama socks za wanaume. Mwanamke avaae chupi muda mrefu bila kuruhusu upepo upite ndani ni watapata fungus ukeni sawa na mwanaume anayevaa socksi zisizofaa kiafya. Chupi au socks zinazofaa ni zile za pamba au cotton.


Of course sababu za kupata ugonjwa wa fungus kwa mwanamke siyo tu kuvaa chupi inayobanaaaa kwa muda mrefu ni pamoja na kutawadha kwa kutumia maji.


Wanawake wengi hawajui kutawadha kwa kutumia maji. Wengi wamalizapo kujitawadha haja kubwa ndipo hurudi kujisafisha ukeni. Hii ni hatari sana kwani bacteria watokanao na kinyesi unawahamisha kutoka nyuma na kuwaleta mbele.


Mwanamke unapaswa kutawadha kwanza mbele kisha umalizie nyuma. 🐓🐕


Yaani hakikisha kuwa uchafu wa nyuma unaoweza kuwa umebakia kwenye vidole vyako usiuingize ukeni kwa namna yoyote. Tawadha pande zote lakini uhakikishe kuwa haviingiliani mbele na nyuma. Sawa dada yangu?? Uko poa hapo??


Kikubwa hapa ni usafi wa mbele na nyuma. Usafi wa chupi zetu. Uvaaji chupi wetu.


Kwa mfano uwapo safarini tena safari ndefu ya zaidi ya saa 8 ni vyema ukasafiri bila kuvaa chupi isipokuwa tu kama uko kwenye siku zile za adabu. Hata kama uko kwenye siku za adabu ni vyema ukasafiri bila kuvaa manguo mengi sana yanayobana mwili. Vaa chupi na sketi au suruali isiyoubana Jamaa General Manager:

sana mwili wako.


3. Chupi husababisha ugumba kwa wanaume.


Sababu nyingi za ugumba tunaweza ukizipata kutoka kwa madaktari wetu wa hospitali zetu. Lakini ukija kwangu mimi Daktari wa magonjwa ya tabia (Lifestyle Based Diseases Doctor) nitakuongezea sababu nyingine ya ugumba wa wanaume kuwa ni kuvaa chupi zinazobana sana.


Mwanaume shujaa havai chupi. Anavaa kaptura badala ya chupi. Tena havai kaptura inayobana sana. Anavaa isiyobana viungo muhimu kwa uzalishaji wa watoto. Mbegu za kiume huzalishwa kwa wingi wakati wa baridi. Kuvaa chupi inayobana kwa muda mrefu husababisha pumbu kuchemka sana na kushindwa kuzalisha mbegu nyingi. Mwanaume mwenye mbegu chache hushindwa kutungisha mimba kwani mbegu zake zinakwenda ukeni kwa uchache na kushindwa kuogelea ukeni.


4. Chupi husababisha miwasho sana kwenye mapaja ya mwanaume na mwanamke. Epuka kuvaa chupi zinazobana ili kuepukana na miwasho.


5. Chupi husababisha michubuko ya mapaja.


Ukivaa chupi kwa muda mrefu utajikuta umepata michubuko mapajani karibu na uume au uke .


6. Uvaaji chupi usiku huchelewesha tendo la ndoa.


Mwanaume anapohitaji vitu adimu usiku wakati mwingine anapaswa kujichotea tu kirahisi kwani ni mke wake halali lakini akikutana na chupi inakuwa kikwazo. Mwanamke usilale na chupi usiku. Unaogopa nini? Hakuna majambazi wala moto. Nani alikwambia ulale na chupi eti unajihami na ajali za moto usiku.?? Mbona tangu umelala na chupi usiku hakuna ajali ya moto iliyokwishatokea.


Acheni kuvaa chupi enyi wanawake ili ikitokea waume zenu tunahitaji naniii usiku tujipatie kwa wepesi!!! Au Siyo?


Tangu niache kuvaa chupi sijawahi tena kuwashwa mapajani wala mke wangu hajawa na taarifa za fungus na UTI kama zamani alipokea na kulielewa somo hili.


Na wewe pia nakushauri uache kuvaa chupi kuanzia leo Uwe na afya bora maeneo yote nyeti.


Nawatakia maandalizi mema ya kutokuvaa chupi!


WATUMIE HABARI HII KWA MARAFIKI

KWENYE MAGROUP WAEPUKANE NA MADHARA YA CHUPI. PIA DR BINGWA NAPATIKANA

www.jamiihuru.com NJOO NIKUELIMISHE MASWALA YA AFYA KILA SIKU


USIVAE CHUPI TENA

COMMENTS

BLOGGER

BIASHARA MTANDAONI $type=blogging$cate=2$count=4

Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,134,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,150,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,104,FIFA.com - Latest News,7,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,158,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MADHARA YA KIAFYA YATOKANAYO NA KUVAA CHUPI KWA JINSIA ZOTE
MADHARA YA KIAFYA YATOKANAYO NA KUVAA CHUPI KWA JINSIA ZOTE
https://lh3.googleusercontent.com/-4cs3yzg6kUs/XQduOoRJWAI/AAAAAAAACkg/62Ayi3JXsz0IT9aqoRSLX8Oa2Owc3sF-wCLcBGAs/s1600/IMG_1839.JPG
https://lh3.googleusercontent.com/-4cs3yzg6kUs/XQduOoRJWAI/AAAAAAAACkg/62Ayi3JXsz0IT9aqoRSLX8Oa2Owc3sF-wCLcBGAs/s72-c/IMG_1839.JPG
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/madhara-ya-kiafya-yatokanayo-na-kuvaa.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/madhara-ya-kiafya-yatokanayo-na-kuvaa.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy