KUKARABATI NYUMBA YA KUPANGA HAKUKUFANYI KUWA MWENYE NYUMBA! | BongoLife

$hide=mobile

KUKARABATI NYUMBA YA KUPANGA HAKUKUFANYI KUWA MWENYE NYUMBA!


Nadhani ulishawahi kusikia mtu akilalamika, nimemsomesha halafu kaniacha, ukasikia nilimkuta hana kitu tumejichanga mpaka sasa kanunua kagari lakini kaniacha kaoa mwingine. Nilikua nawasiadia mpaka ndugu zake lakini wote wamenigeuka kapata mwamnaume mwingine kaolewa.

Nilimkuta hajielewi nikambadilisha sasa amekua mstaraabu anang’aa hataki hata kuniona anasema kua mimi si wa hadhi yake. Ndiyo inwezekana ni wewe, ulishamfanyia mwanaume ivyo, ukamfanyia mwanamke wako mambo makubwa, ukaosmesha na kuhudumia mpaka makaburi ya Bibi zake.

Lakini baada ya muda anakuacha anatafuta mtu mwingine, wewe unabakia kulia na kusema unamuachia Mungu, kana kwamba unataka kumpa kalaana hivi, nikuambie tu hembu acha kujipa laana wewe mwenyewe kwa kumlilia Mungu mambo ya kijinga, hakuna sehemu ambayo Mungu alisema ukawe mjinga na kukarabati nyumba ya kupanga.

Kama hajakuoa au hujamuoa kila unachompa ujue unahonga na huwezi kudai na hata kama ni kikubwa kiasi gani hakikufanyi kuwa mume au mke wake. Hii ni sawa na umefika nyumba ya kupanga, umekuta haina geti ukaweka, ukaweka umeme, ukaweka na bati la south na kuifanya kuwa mpya kabisa.

Ukishaifanya kua mpya basi jua watu wengine wataitamani na hata wale ambao awali walikuja na kuangalia wakaona haifai watataka kupanga pale na mwenye nyumba anaouhuru wa kukuambia ondoka na sikulipe chochote. Kwanza kwani alikuomba uikarabati, si ulikuta nyumba ya watu iko hivyo.

Wewe na kimbelembele chako ukataka geti tena hamkuelewana hata kuwa atakulipa, kwamba wakati unamsomesha binti wa watu kwani alikuambia kuwa nilazima umuoe au alikuambia kua mkiachana atakulipa. Si wewe ulitaka msomi kwani yeye alikuambia ana shida nahiyo shule.

Umekutana na Kaka wa watu hana kazi umemtafutia, anakunywa pombe umemshawishi kaacha na sasa kawa mstaarabu ana maendeleo, unaanza kusema kuwa umembadilisha kwani alikuomba. Ninachotaka kusema hapa nikua kama hajakuoa si mumeo na kama hujamuoa si mkeo.

Huna haki ki Mungu wala kishetani na kidunia kudai chochote ulichompa kipindi hamjaoana. Kwani si ulimpa huku unamtumia au ulimpa bure ndiyo hivyo, aliyehonga underwear na aliyehonga nyumba wote wamehonga.

Kama mtu ni mpenzi wako mauche awe mpenzi wako, hayo mambo ya maendeleo hembu fanya kivyako lakini kama utajitia kimbelembele ukishambadilisha wengi wanaachwa. Iko hivi inawezekana hata sababu ya kukubali nikwakua alikua anajiona ni wa viwango vya chini.

Hivyo baada ya wewe kumabdilisha basi anaona hana hadhi ya kua tena na wewe. Kuna watu ni kama kazi yao, kutafuta watu ambao wako chini yao wanawabailisha halafu wanaachwa, hembu tafuta mtu unayemtaka na kama utaamua kumbadilisha iwe unatoa sadaka tu na si kwasababu unawaza ndoa kwani utaliwa!

Badala ya kumshawishi mchumba wako mjenge, mkajikusanya mkajenga kwenye kiwanja chake ili baadaye muishi pamoja hembu jenga kwako na kama ikitokea mkaoana basi mtaishi huko. Lakini mkijenga pamoja tena nyumba jina lake akipata mwingine akikuacha jua kua huna chako, cha kua mjinga!

Watu wote waliodhulumiwa walioachwa walikua wanapendwa kama wewe, walikua na watu wanakaa na kupanga maendeleo ya pamoja lakini wakaja kuachwa. Hivyo mshauri mambo mazuri lakini hembu na wewe jishauri pia, wekeza kivyako na sio kwakua kashajitambulisha kwenu unajiona mke.

Yaani kajitambulisha tu na kuleta nusu ya mahari unamchukulia na mkopo mjenge au anunue gari! Acha ujinga huo, inawezekana hata kajitambulisha kwa watu kumi na kila mmoja akitoa milioni si ananunua gari na anakamilisha nyumba yake halafu ana watema wote au anachagua mmoja! Sasa wewe endelea tu kusema huyu hawezi kunisaliti kama huamini muulize X wake!

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : KUKARABATI NYUMBA YA KUPANGA HAKUKUFANYI KUWA MWENYE NYUMBA!
KUKARABATI NYUMBA YA KUPANGA HAKUKUFANYI KUWA MWENYE NYUMBA!
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/kukarabati-nyumba-ya-kupanga.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/kukarabati-nyumba-ya-kupanga.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy