KANYAGO SEHEMU YA TATU (03)

SIMULIZI:  KANYAGO
MWANDISHI: Dany benson
MAWASILIANO: 0656887460/ 0754051880 &0678520500

SEHEMU YA 03

Ilipoishia
haraka aliingia ndani kwake na kuchukua kisu kisha akatoka na kuelekea katika nyumba ya jirani yake yule na baada ya kukaribishwa aliingia na kunyoosha moja kwa moja mahali pale alipolala na kukichomeka kisu kile katika tumbo la mwanamk machungo ya kila siku mara ng'ombe akgeuka na kumjeruhi huyu tusaidien  basi...
_______

Sasa endelea

______

Licha ya kufurukuta Mara kadhaa lakini bwana yule ni wazi alikuwa amedhamiria jambo like kwakuwa aliufunga mdomo wake kwa kutumia kiganja kabla ya kusokomeza kisawasawa kisu kile bila hata kujari maumivu ambayo alikuwa akitlyapata hatimaye mwanamke yule akiaga dunia

Alitoka kama MTU aliyechanganyikiwa na haraka alinyoosha moja kwa moja nyumbani kwake na sasa hakuona hata haja ya usafi ule zaidi alisimama kidogo pembeni kisha akachukua simu yake na kupiga kwa MTU Fulani

"Yes boss"

"Sasa Mr. Wilison nakuachia jukumu LA kusimamia shughuli zote hapa pamoja na kundi hili kwakuwa naondoka kidogo kiziara nakwenda afrika kusini kusimamia biashara mpya huko sawa"

"Sawa mkuu ila mbona gafla sana hivyo na haukuwa umetoa taarifa!!!"

"Unapata wapi ujasiri wa kuhoji ikiwa Mimi ndio nimekuajiri...?"

"Basi mkuu nilihitaji kujua tu wala sikuwa namaana mbaya ila nitatekeleza uliyoagiza usijari"

"Na kesho nadhani mzigo utafika uwanja ule jomo Kenyatta jitahidi kuwahi kufika maana nimeshaulipia sawa"

"Ndio mkuu"

Alikata simu yake na  kisha akabonyeza vitufe kadhaa tena na akapiga kisha kuiweka sikioni kwa Mara ya pili

"Hellow naitwa Irene wakala wa usafirishaji katika shirika LA ndege LA fry Emirates naweza kusaidia tafadhari"

"Aaah shukran naitwa Mr kimera naweza kupata usafiri wa afrika ya kusini usiku huu?"

"Yes IPO ndege moja ya mwisho itokayo hapa SAA nne usiku na ndio ya mwisho"

"OK naweza book nafasi moja ili nisafiri Nayo!!?''

" yes! Ni laki tatu na sabini tu kwa bei zetu zimeshuka karibu sana"

"OK shukrani nita transfer muhamala soon then nami na come"

Hakuhitaji kusubiri wajibizano na sauti ile ya kike yenye kutokea katika shingo na niwazi kichujo chake wala hakikuwa na matundu makubwa ndio maana sauti ilitoka nyororo haswaa, Naye akaufanya mhamara haraka kama alivyopanga kisha akaikusanya mizigo yake katika begi na kuanza kuliburuta kuelekea katika gari lake na ndipo jambo Fulani likamjia kichwani

Haraka sana alirejea na kujaribu kutafuta kutu Fulani muhimu ambacho alikuwa amesahau aliyapepesa macho yake huku na Kule hakupata alijaribu kuzifungua droo za makabati yote yaliyokuwa ndani lakini hakupata hatima jasho likaanza kumvuja alirejea kutafuta Mara kadhaa lakini mambo yalikuwa kama mwanzo na ndipo tusi zito likamtoka mdomoni mwake kabla ya kulikanyaga kwa nguvu kabati ambalo bila hata kizuizi lilitua chini na kusambaratuka kutokana na kuwa na vioo upande mwingi

"Ina maana huyu nyang'au aliona na akahamisha ila mbona ni kipofu sema na ndio nimeshamua na sina wa kumuuliza hata yule alikuwa rafiki yake pia nimeshamfyeka daaah nafanyeje......??? Mmmmh ngoja nitajua huko huko wacha nilikimbie soo hili kabla halijaniweka matatani maana nisijedakwa kimbweha hapa nitakuwa mzembe"

Haraka alibeba begi lake lile na kutembea hatua kadhaa zilizomfikisha katika barabara kuu na akasimamisha moja ya tax iliyokuwa ikipita kando na kumuelekeza dereva kumfikisha uwanja wa ndege wa taifa lile LA Bantu

"Itakugharimu elfu kumi tu mzee wangu"

Alisisitiza dereva yule kabla ya kuliwasha gari lake ili tu safari ianze kuelekea Kyle mahali alikoelekezwa yote alikuwa ni kukwepa wa usumbufu ule wa sina au nipunguzie pindi afikapo mahali pale anapohitaji

"OK washa twende"

Safari ilisonga na story hazukuwa nyingi miongoni mwa watu wawili hawa kutokana na mzee yule kuwa na mawazo mengi sana juu ya kufanikiwa kwake kutoroka mjini hapa na akili yake yote alikuwa ikimtuma kufika afrika kusini na kuifikia ile mitaa ya Soweto ambapo nyumba zilikuwa kama vichuguu vywa mchwa huko alitambua hata isingekuwa rahisi kupatikana kwake hata kwa MTU ambaye angemfuatilia haraka asingempata,

Punde tu baada ya kushuka katika tax ile aliyokodishwa akalipia kiasi kile alichoambiwa akitoe na taratibu akasogea katika lango LA kuingia katika uwanja ule wa kimataifa akageuka na kutazama angani ambako kiza kilikuwa kimeanza kutanda na kujisemea kimoyomoyo

"Ubaya wangu ndio umefanya sasa nakuwa mkimbizi ili tu kunusuru maisha yangu kutoishia jela hakuna nilichokosa na hata wale wachache niliowaziba mdomo walisujudu lakini naapa nitarejea hapa nikiwa ni MTU huru kabisa baada ya kukamirisha mambo yangu na yakakaa sawia.."

Na hapa akageuka na kuingia ndani ambako walitazamana moja kwa moja na mhudumu yule aliyekuwa amewasiliana Naye na baada ya ukaguzi mdogo wa hati yake ya kusafiria walimsihi kupitisha mizigi yake katika mashine ya ukaguzi na wala hakukuwa na shida na akaruhusiwa kuelekea katika ndege na pindi anafuata korido ndogo ambayo ingempereka mpaka katika ndege alikutana na bwana mmoja mweusi mrefu mwembamba alikuwa amevalia miwani midogo iliyomfanya aonekane vyema katika USO ule wa mng'ao suti nadhifu iliyonyoosha vyema pamoja na tai iliyoyakwida mapambio ya kora ya shati yakakutana pamoja alikuwa akiingia nchini kutoka katika ndege iliyotua muda mfupi tu

Tafakari za wawili hawa waliotazamana kwa muda na hata pindi walipopishana kila mmoja aligeuka kumtazama mwenzake licha ya kuwa walikuwa hawafahamiani hata kidogo zaidi ni wazi kila mmoja alikuwa akihisi jambo Fulani kwa mwenzie pindi tu macho yao yalivyotazamana...

ITAENDELEA

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : KANYAGO SEHEMU YA TATU (03)
KANYAGO SEHEMU YA TATU (03)
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/kanyago-sehemu-ya-tatu-03.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/kanyago-sehemu-ya-tatu-03.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content