JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 5 | BongoLife

JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 5

JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU

      SEHEMU 5

        MWISHO

        WHATSAPP 0655585220

             ZANZIBAR

ILIPOISHIA:
Tuliishia pale pale paka akiwa amenitokea na wale viumbe wawili wenye maumbo ya kipaka na kutakiwa niingiliane nao kimwili, ingali mwenyewe hata mwanaume wa kawaida tu sitambui yukoje!!!
TUENDELEE SASA!!!
Sikuwa na la kufanya kabisa, zaidi ya kuomba mungu, nilikua naona kabisa huo ndiyo utakua mwisho wa maisha yangu, mwisho wa matumaini yangu, nilihisi kuliona kaburi mbele yangu, maana kwa maumbo waliyokua nayo wale paka watu ilikua ni kunibaka mpaka kufa!!
Wale paka wakaanza kunipapasa mwili wangu, nilikua sihisi chochote zaidi ya manyoya yao mengi yakianza kupita katika maungio yangu nyeti ya mwili.
Kwa niliyokua nayo sikuweza kupiga kelele wala kujigeuza, nilikua kama gogo la nyanya yani, linalosubiri mnunuzi sokoni. Oh!! Mola wangu naomba hali ile usimpe msomaji wa mkasa huu!!
Punde nikaanza kuhisi nafunuliwa gauni langu, paka mmojawapo akaanza kufungua zipu yake ili atoe soseji na aanze kunishughulikia.
Kabla hajafanya kitendo kile, mlango wa chumba nilichokuwemo ulifunguliwa, alikua si mwingine bali ni baba yangu. Alikua ameongozana na viongozi wa dini.
Ghafla!!! Wale paka na vile viumbe vingine vilipotea. Baba alikuja moja kwa moja na wale viongozi wa dini mpaka pale nilipokua nimelala.
Akiwa mwenye kukatwa kabisa na tamaa baba yangu, aliwaelezea baadhi ya mikasa iliyokumba familia yetu..
"..............Nahisi nimshirikishe mungu juu ya hili, natumaini atanisaidia". Baba alimalizia kuongea maneno hayo huku kijasho kikiwa kinamtiririka usoni mwake, mwili wake ukiwa umechoka kwa pilika za kuchosha zisizomuisha, nguo aliyovaa ilikua ni siku ya tatu hajabadili.
"... Usijali bwana Salisala haya yote kwa mungu ni mambo madogo sana, maana kwake hakuna linaloshindikana!!"
Wale viongozi wakaanza kufanya maombi, walifanya maombi kama dakika tano hivi, mara ikaanza kusikika sauti ya paka pale chumbani.
Nilihisi naisikia peke yangu kama nilivyozoea, lakini nilishangaa kumuona baba na yeye anaisikia sauti ile. Alikua si mwenye kutulia na kutafuta tafuta wapi inatokea.
"Vuuuuuuup!!!!"
Yule paka alitokea pale mbele yetu kimaajabu huku akijikunja kunja kuonesha yale maombi yanamuingia.
Baba alishtuka sana na nusu akimbie, wale viongozi wa dini hawakushughulika naye na badala yake waliendelea tu kuomba.
**
Sikutaka kuamini nilichokua nakiona mpenzi msomaji, yule paka alijigeuza na kuwa na sura ya dada wetu wa kazi (Dada mwajuma!!)
"Iiiiiinhh iiiiinhh naombeni msiniumize, nisameheni jamani!!! Nisameheni!!!".
..Mara akaanza kulia na kuomba msamaha.
Muda wote huo baba alikua ameduwaa tu na hatambui la kufanya, Wale viongozi wa dini wakaacha kuomba na kuanza kumuhoji dada Mwajuma aliyegeuka kutoka katika umbo la paka.
" Wewe ni nani na unatokea wapi??"...Walimuuliza
"Ni ni ni dada wetu wa kazi huyo!!", Baba alidakia na kuwajibu.
Kusikia vile wale viongozi walipigwa na butwaa kidogo kisha wakaendelea kumhoji.
" Kwa nini unafanya unyama wa kiasi hiki?"
Dada Mwajuma hakujibu chochote zaidi ya kuinamia na kuendelea kulia, huku akiwa amevaa kanga yashingo tu na nywele zikiwa timutimu!!!
"Sasa kama hutaki kusema, sisi tunaendelea kuomba ili uzidi kupata maumivu!!"
Wale viongozi walimtisha kidogo, ndipo aliponyamaza na kuinua uso wake juu, akaacha kulia na kuanza kuzungumza.
"Subirini nitasema!!!, Mimi ndiyo nilimuua Mama Naomi, mimi ndiye niliyemuua dada yake Mama Naomi na mimi ndiye ninayefanya mpaka Naomi anateseka kiasi hiko".
Baada ya kuongea maneno yale, hasira zilinishika nikanyanyua mkono na kutaka kuinuka.
Nilistaajabu sana kwa kweli, baada ya muda mrefu, nilijikuta naweza kunyanyuka pale nilipo kitandani. Baba alifurahi kwa kushangaa kisha akanikumbatia huku kilio cha uchungu kikimtoka.
Wale viongozi bado walikua naye yule mbaya wetu, wakaendelea kumuhoji...
" Kwa nini umefanya uchafu wote wa namna hii lakini? Huoni kama hutakua na msamaha mbele ya mungu wako aliyekuumba??"
Dada Mwajuma aliacha kulia kisha akaanza kucheka kwa nguvu...
"Hahahahahhhah!!!..
"Huruma?!! Huruma gani kwa mfano??, labda niwape historia kidogo!!!"
**
"Miezi michache iliyopita, ilikua ni usiku sana huyu baba huyu mnayemuona huyu!!( Alimnyooshea kidole baba), mkewe alikua ametoka na wanawe, nikiwa nimebaki mimi na yeye nyumbani kule tegeta, aliingia chumbani kwangu na kunibaka!!! Niliumia sana!! Zaidi ya sana yani!!!, nilimpigia simu bibi yangu nikamueleza yote!!..
.....Bibi akanipa nguvu na kunielekeza ya kufanya!!! Nilitaka niwamalize mmoja baada ya mwingine na familia yao yote iishe huku nikiwa nimejenga chuki kubwa sana baina yao. Halafu wewe unaongelea kuhusu HURUMA!!! Huruma ipi labda haswa??"
Kwa kweli maneno yale yalinikata maini, baba aliingiwa na aibu na kuinana tu chini huku machozi yakimtiririka. Hakuwa na la kufanya zaidi kuomba tu ya kukiri kosa na kuomba msamaha.
Nilimchukia sana Mwajuma, kwa kuhukumu familia yetu kwa kosa la baba lakini sikuwa na la kumfanya zaidi alifukuzwa tu nyumbani na kurudishwa kijijini kwao.
Kutokana na vifo vya utata vilivyokua vimetokea kabla, baada ya ushahidi tuliohitajika kuutoa polisi, ilibidi Mwajuma aende kutafutwa mpaka kijijini kwao ila HAWAKUWEZA KUMPATA KABISA!!!
Tumebaki kumuachia mungu, ndiye atakuja kuhukumu juu ya hili!!!!

MWISHO!!!!!

Ulikua nami mtunzi wako wa mkasa huu AHMAD MDOWE nami kwa simulizi yangu ijayo!!!
AHSANTENI SANAAAAAAAAAH!!!!!

COMMENTS

BLOGGER

BIASHARA MTANDAONI $type=blogging$cate=2$count=4

Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,134,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,150,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,104,FIFA.com - Latest News,7,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,158,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 5
JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 5
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/jinsi-paka-alivyomaliza-familia-yetu_56.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/jinsi-paka-alivyomaliza-familia-yetu_56.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy