JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 3 | BongoLife

$hide=mobile

JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 3

JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU

         SEHEMU YA 3

      WHATSAPP 0655585220

         ZANZIBAR

ILIPOISHIA:
Ni pale nilipokua nimelazwa kitandani na mama mkubwa, yeye akatoka nje kwenda kuniandalia chakula, mara mlango ukawa unafunguliwa na ghafla nikasikia mlio wa paka!.
TUENDELEEE PAMOJA SASA:
Kwanza nilishtuka sana!, nikatamani niinuke niangalie ni yule paka wa kule nyumbani ama la!!, kabla sijawaza chochote zaidi....
Mara nikarukiwa na kitu kifuani!, kucheck hivi.. Daaaah!! Alikua yule yule paka wa nyumbani, safari hii alikuja katika umbile la paka na si mtu!!
"Nimekuja kukupa taarifa tu!!!".... Nilitahamaki sana baada ya yule paka kuchezesha mdomo wake na kutoa sauti ya kike iliyozungumza maneno hayo.
Kwa kuwa nilikua si mwenye uwezo wa kufanya chochote, mwili mzima umepooza, nikawa ni mwenye kumsikiliza tu.
Yule paka akaendelea kuzungumza, alizungumza kauli ambayo kwa namna moja au nyingine nilianza kuelewa dhumuni la matatizo yote anayotaka atufanyie...
" Nitawamaliza wote kama nilivyoagizwa, ili huyu baba yenu akaoe mwanamke wazazi wake waliomridhia.... Na kuthibitisha hilo, muda si mrefu naanza na mama yako mdogo, wewe nitakuweka wa mwishoni".
Kumbe huyu paka alikua amewekwa makusudi na bibi oili atumalize sisi pamoja na mama, kwa kua mama si mwanamke ambaye alitakiwa aolewe na baba!!!, Dah!!! Ukifikiria Mara mbili suala hili linauma sana mpenzi msomaji.
**
Yule paka akashuka chini, akaelekea mpaka mlangoni kisha akakojoa, sikuelewa nia yake ni nini, nikabaki kushangaa tu.
Muda si mrefu Mama mkubwa Frida akawa anaingia, mkononi kabeba bakuli la mtori, pamoja na kijipleti cha matunda na kisu.
Ile kashatua tu mguu wake kwenye ule mkojo, Mara akaanza kubadilika, kama mtu aliyechanganyikiwa au kurukwa na akili, akatupa bakuli kulee!!, lilikua la udongo likavunjika, akaotoka kisu AKAJIKITA TUMBONI!!!!
Daaaah!!!!, siwezi kuelezea maumivu niliyopata pale, mama mkubwa kioenzi, ambaye nilihisi angalau anaweza akachukua nafasi ya mama yangu aliyepoteza maisha wiki chache zilizopita, Leo paka yule yule anasababisha kifo chake.
Inabidi kushukuru mungu kwa kizuri alichokupa, ila nilijikuta natamani upofu kwa machungu ninayoyashuhudia, michirizi ya machozi ilianza kutiririka mashavuni mwangu. Maumivu niliyopata siku hii baki kuyasikia tu ndugu msomaji!!!
Wakati huo huo baba akaingia, hi ni baada ya kusikia kelele la kuvunjika like bakuli, kwasababu alilitupia dirishani na dirisha lenyewe ni la kioo.
Roho ya binadamu ni kazi sana kutoka katika kiwiliwili chake, pamoja na mkito wa nguvu aliyoupiga tumboni kwake, mama mkubwa alikua bado anagalagala chini, damu zikiwa zimetapakaa sakafuni.
"Shemeji Fridaaaaa!!! Kuna nini????"....Baba alishtuka sana kwa tukio lile.
Aliinama hadi miwani yake ikadondoka, hakujali kuhusu hilo, akambeba mama mkubwa mzima mzima, akiwa amelowa damu kisha akatoka nae nje, nahisi alitaka kumuwahisha hospitali.
**
Baada ya wao kutoka tu, yule paka akaingia tena chumbani, haraka haraka akaenda mpaka pale damu zilipokua zimemwagika akaanza kuzilamba!, alilamba kama paka wa kawaida alambavyo maziwa.
Nilifumba macho, sikutaka kuushuhudia kabisa unyama aliokua anaufanya paka yule, nilitamani niinuke nimpigilie mbali!!!
Ghafla akapanda tena kifuani kwangu, akaniongelesha tena kwa sauti yake ile ile ya kike....
" Nimeshammaliza mama yako aliyebakia, na Leo usiku nakuja na zawadi yako nzuri kabisa!!!!"
***
JE NI ZAWADI GANI HIYO PAKA MWENYE ROHO CHAFU ANATAKA AMLETEE NAOMI??
SEHEMU YA NNE SI YA KUIKOSA!!

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 3
JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 3
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/jinsi-paka-alivyomaliza-familia-yetu_55.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/jinsi-paka-alivyomaliza-familia-yetu_55.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy