JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 02 | BongoLife

$hide=mobile

JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 02

JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU

       SEHEMU YA 2

             WHATSAPP 0655585220

           ZANZIBAR

ILIPOISHIA:
Ni pale yule mtu aliyekua amekaa kwenye kiti kunigeukia huku uso wake ukiwa ni wa paka!!!
TUENDELEE PAMOJA:
Kwa kweli nilipiga kelele sana ila cha ajabu sauti yangu ikawa haitoki, nilitamani kukimbia lakini miguu yangu ilishika ganzi, mwili wote unatetemeka kama nimeingiwa na baridi, nikajikuta nadondoka pale pale.
Yule paka akavuta kiti nyuma akasimama, kwakweli sijui nikuelezaje mpenzi msomaji, ila kama unamfahamu paka vizuri basi vuta picha.... Paka kavaa nguo halafu asimame kama mtu na mkia wake uko vile vile.
Nilitamani walau iwe ndoto kwa kujaribu kufumba macho na kufumbua lakini wapi!!!, yule paka akawa anazidi kunikaribia tu. Hadi akafika mbele yangu....
"Naombaa nsaa.... Nsameheeeeee, usiniumizee!!!", Nilijaribu kumuomba msamaha asiniue lakini sauti yangu ikawa haitoki kabisa, yani nilikatwa kabisa sauti.
Yule " paka mtu " akafungua mdomo wake...
Mungu wanguuu!!! Alikua ana meno mawili marefu yamechongoka sana, ile anataka kunishika tu!!!
"Njwiiiiiiii'iii!!"... Mlango ukawa unafunguliwa, sikujua ni wa chumba kipi, kumbe alikua ni dada wetu wa kazi (anaitwa Mwajuma).
Nilishkuru mungu, kwa kuhisi msaada utakua umenifikia, baada ya kufika pale, nlishangaa Mwajuma kutoshtuka wala nini kuhusiana na yule paka, badala yale alishaangaa kuniona mimi nikiwa katika hali ile pale chini.
" Naomi vipi mbona uko hapo??"...Mwajuma aliniuliza.
"Kuna paakaaa......" Nilijaribu kumuonesha Dada Mwajuma kuna paka mbele yangu lakini haikutoka sauti yangu wala mkono haukuinuka.
"Mmmmnh hebu ngoja nikamuite baba na mama!!!!"..... Dada baada ya kuona haelewi haelewi ikabidi awahi kumuita baba na mama.
Mimi macho yote kwa yule paka mtu, akaiwekea kidole mdomoni kuashiria nisongee kitu kisha....
" pyuuuuuuuh!!!!".... Akayeyuka pale pale.
"Vipi Naomi una nini?!!!". Baba alivyofika tu alianza kuniuliza, huku akiwa na wasiwasi mkubwa.
Sasa wakati nataka niinue mdomo nimjibu na kumueleza kilichonisibu, mdomo wangu ukawa haufumbuki, nikitaka niinue mkono, mkono hauinuki.... Yani sijiwezi hata kujisogeza.
" Naomi!! Una nini binti yangu, hebu niambie mwanangu!!!"
"Naomiii!!! Naomii!!!".... Baba alinitikisa kwa nguvu walau niongee, niliishia kumuangalia tu, nilitamani nimjibu baba yangu ila nilikua sijiwezi kabisa.
Baba akaniinua haraka haraka tukatoka nje ananipakiza ndani ya gari, wakati wote huo mama alikua hajashtuka kutoka usingizini.
Ilikua ni usiku sana ila ikawa haina budi kuwahishwa hospitali, nguvu ilikua inaniishia mwilini wakati tukiwa njiani mpaka nikapotewa na fahamu.
*
Nakuja kuzinduka niko kitandani, mazingira yakiwa ni ya hospitali, nachoweza kuzungusha ni shingo tu, si mdomo wala kiungo chochote kingine cha mwili wangu nilichoweza kukisogeza.
" Pole sana Naomi!!", Baba alinishika kichwa huku akiwa pembeni yangu, kwa muangalia tu usoni alikua ametandwa na huzuni nzito.
Nilishangaa kutomuona mama muda ule, kama ingekua ni mfanyakazi wa ofisini sawa!! Lakini baba ndiye anafanya kazi na mama yeye muda mwingi shughuli zake ni za nyumbani. Ila nikajipa matumaini itakuwa yupo.
Lakini kabla sijajibu chochote, nahisi baba alitambua mawazo yangu kwa haraka...
"Usijali mama yako yupo!!"....Baba alinipa matumaini huku, nafsi ikimsuta machozi yakimtiririka kwa uchungu.. Kilio cha kwikwi kikamshika hapohapo, kwa aibu aliinamia kwenye kitanda.
Ilinipa ishara kuwa kuna kitu kibaya tu kimetokea, nilijikuta nikitiririkwa na machozi, huku kilio kikali kikibubujika ndani kwa ndani kwa kua hata sauti sauti ilishindwa kunitoka.
" Ngoja nikwambie ukweli tu mwanangu maana haina jinsi!!"....Baba ikabidi anilieleze tu hali halisi.
Kwa kweli ni taarifa chungu nisiyo isahau kipindi chote cha maisha, mama yangu alikua amefariki na wadogo zangu wote wawili wana homa sana.... Huku mimi mwenyewe madaktari wakishindwa kutambua nina tatizo gani zaidi ya MWILI KUPOOZA TU, na nilipoteza fahamu takribani wiki mbili... Hivyo walishamzika mama yangu kipenzi.
Oooh!! inauma sana kwa kweli, walau kilio kingepunguza machungu yangu lakini ndiyo vile hakitoki!!!.
Nilichukuliwa nikawekwa kwenye kiti cha wagonjwa, kwakua muda wa kukaa hospitali umeisha inabidi nikamalizie matibabu tu nyumbani.
Nilikokotwa huku nkiwa sijiwezi, mpaka kwenye gari na safari ya kurejea nyumbani ikaanza...
"Tumehamia Kawe kwa mama mkubwa wako sasa hivi"... Baba alinieleza.
Nilihisi mwanga wa matumaini unaingia ndani yangu, kwa kua moja kwa moja matatizo yote haya ni kutokana na yule paka ila kwasababu tumehama.... Kutakua na ahueni kidogo.
.......
Si muda tukawa tumeshafika nje ya nyumba ya kifahari ya Mama mkubwa Frida, nikapokewa vizuri huku nikiwa ni mwenye kubebwa tu. Sijiwezi kwa chochote yani.
Nilipelekwa mpaka chumbani nikawekwa juu ya kitanda na mama mkubwa, alikua na upendo kweli yani, ingawa na machungu ya kufiwa na mama yangu mzazi nilihisi faraja kidogo.
Mama mkubwa Frida na mama, ni watoto wa baba mmoja mama mmoja, na wana ufanani kidogo kwa mbali...
" Ngoja nikulete walau chakula kidogo!!"..Mama mkubwa aliongea kisha akatoka kwenda kuniandalia chakula.
Huku mawazo yakiwa yamenijaa, nikiwaza ntawezaje kula na picha ikanijia kichwani ya kulishwa kama mtoto mdogo, vilevile roho inaniuma kila napomkumbuka mama... Mara mlango ukasogea kidogo kama mtu anaingia vile...
Nikasikia....
"Ng'waaaaaaaaaaauuuuuh!!!"
JE NINI KITAENDELEA???

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,146,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,192,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,110,FIFA.com - Latest News,13,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,203,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 02
JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 02
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/jinsi-paka-alivyomaliza-familia-yetu_25.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/jinsi-paka-alivyomaliza-familia-yetu_25.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy